Wednesday, December 14, 2011

Mbowe asherehekea jubilei ya miaka 50 kwa harambee ya ujenzi wa kanisa na msikiti jimboni kwake

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh.Freeman Mbowe akimkaribisha mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mh. Godbles Lema kuchangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa KKKT usharika wa Nshara Moshi.
Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi akichangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
Meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael akichangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa.
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Bw. Reginard Mengi akimueleza jambo Mh Mbowe kabla ya kuanza kwa harambee.
Mh Mbowe akipongezwa na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Bw Reginard Mengi.
Mh Mbowe akipongezwa na baba yake mdogo mzee Manase Mbowe.
Mh Mbowe akipongezwa naibu waziri wa TAMISEMI,Mh. Aggrey Mwanry ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Siha.
Mh Mbowe akipongezwa na Gavana wa kwanza wa benki kuu ,Bw Edwin Mtei.
Mh Mbowe na familia yake wakiwa wamesimama kwa ajili ya kupongezwa na viongozi mbalimbali waliokuwepo kanisani hapo.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini,Martin Shao akimuwekea mikono Mh Mbowe ikiwa ni sehemu ya ibada ya jubilei ya kutimiza kwake miaka 50.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini,Martin Shao akiongoza ibada ya jubilei ya kutimiza miaka 50 ,mh Freeman Mbowe.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya Arusha,Thomas Laizer akiongoza ibada .
Mh Mbowe akiteta jambo na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Bw Reginard Mengi,katikati ni mke wa Mh Mbowe,Dk Lilian Mbowe.
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kulia kwake ni Meya wa manispaa ya Moshi ,Jafary Michael wakiwa katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Nshara iliyoenda sanjari na jubilei ya miaka 50 ya mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Mh Mwanry akiteta jambo la Askofu Laizer muda mchache baada ya kuchangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa.
Mbunge wa jimbo la Siha na mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Kilimanjaro Aggrey Mwanry akizungumza kabla ya kuchangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Nshara.
Mh Mbowe akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Rambo uliopo Machame wilayani Hai.
Wabunge wa viti maalumu Chadema pia walikuwepo.
Mh Mbowe akimtambulisha Meya wa manispaa ya Moshi mstahiki Jafary Michael wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti huo.
Mh Mbowe akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Rambo uliopo Machame wilayani Hai.
Mh Mbowe akiotesha mti katika eneo la msikiti wa Rambo wilayani Machame kama kumbukumbu ya kufika msikitini hapo.
Waumini wa dini ya kiislamu wakimsikiliza Mh. Mbowe (hayupo pichani) wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Rambo uliopo Machame wilayani Hai.
Waumini wa msikiti wa Rambo na wageni mbalimbali.
Waumini wa msikiti wa Rambo na wageni mbalimbali.
Mh Mbowe akisalimiana na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi wakati wa harambee ya kuchangia msikiti wa Rambo.


Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

2 comments:

Anonymous said...

NI MFANO WA KUIGWA KATIKA NCHI AMBAYO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO NYINGI.MWINGINE ANAWEZA PIA KUFANYA KAMA HIVYO LAKINI KATIKA SECTOR NYINGINE,KAMA VILE ELIMU,MIUNDOMBINU N.K,hongera sana...mh.

Anonymous said...

je? watazameni jamii hii ya wachagga, wanavyosahau itikadi zao za kidini na kuamini MUNGU ni mmoja mapokeo tofauti. je ingewezekana hili hapa dar au pemba au lindi nkadhalika, na ndio maana hawa ndugu wana maendeleo yasio na mzaha, DINI nini? wenzetu wana maji,vituo vikubwa vya afya maji barabara n.k why not nchi nzima?

william mbeya