Saturday, October 1, 2011

DK KAWAMBWA AFUNGA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTAFITI WA USHIRIKA BARANI AFRIKA.

 Umakini katika kufuatilia hotuba ya mgeni rasmi
 Washiriki katika hafla hiyo
 Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk Shukuru kawambwa akiongozwa na mwenyeji wake mkuu wa chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara,Moshi,Prof Faustine Bee wakielekea ukumbini.
 Mkuu wa chuo cha MUCCoBS akifanya utambulisho kwa mgeni rasmi wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la utafiti wa ushirika barani Afrika lilifanyika chuoni hapo.
 Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk Shukuru Kawambwa aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano la kimataifa la utafiti wa ushirika barani Afrika lililofanyika chuoni hapo akitoa hutuba wakati wa kufunga kongamano hilo.
 Viongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara,Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mara baada ya kufunga kongamano la a kimataifa la utafiti wa ushirika barani Afrika.
Wataalamu wa IT katika chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara (MUCCOBS) waliofanikisha mawasiliano katika kongamano hilo kutoka shoto ni Johnes Mwita,Germinus George,George Matto na Abswaidi Ramadhani.


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

Serikali imesema imeanza kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazozikabili sekta mbali mbali za kiuchumi, kwa kuhakikisha inawawezesha watafiti kuzibaini changamoto hizo na kuainisha njia zitakazosaidia kuzikabili.

Rai hiyo imetolewa leo na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipokuwa akizungumza kwenye ufungaji wa kongamano la kimataifa la utafiti wa ushirika barani Afrika, lililofanyika kwa siku tatu katika chuo kikuu cha Ushirika na biashara-MUCCoBS mjini Moshi.

Dk. Kawambwa amesema katika utekelezaji huo serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kwa ajili ya shughuli za utafiti, zitakazoiwezesha Tanzania kupiga hatua kiuchumi na kijamii.

Katika hatua nyingine waziri Kawambwa, ameupongeza uongozi wa chuo kikuu cha Ushirika kwa kuwakutanisha wadau wa masuala ya utafiti wa ushirika kutoka nchi mbali mbali barani Afrika ambapo wameweza kubadilishana uzoefu na kuainisha njia za kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Naye mkuu wa chuo hicho Profesa Faustine Bee, amesema kongamano hilo pia ni sehemu ya maandalizi ya maazimio kwa ajili ya kongamano la ushirika la Umoja wa Mataifa litakalofanyika mwakani, kuandaa mipango
ya kuendeleza sekta ya ushirika barani Afrika kwa kuzitumia tafiti mbali mbali.

Kongamano hilo la kwanza kufanyika barani Afrika limehudhuriwa na washiriki wapatao 200, kutoka nchi za Afrika.

No comments: