Wednesday, September 21, 2011

MAONYESHO YA PICHA YA "AMRIK" YAFANA JIJINI DAR

 Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya "AMRIK" yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Brazil, Taasisi za nchi za Kiarabu  na Aga Khan. Ambapo Balozi huyo amewapongeza walioshiriki maonyesho hayo. Maonyesho hayo yenye lengo la kuhamasisha ushirikiano kati ya Wabrazil na Waarabu yalitarajiwa kufanyika wiki iliyopita lakini yakaahirishwa kufuatia ajali ya kuzama kwa Meli ya MV SPICE ISLANDER iliyotokea huko Zanzibar.Katikati ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu na Kushoto ni Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani.
 Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu akisoma hotuba kwa wageni waalikwa katika maonyesho ya Picha yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan Bw. Navroz Lakhani ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo akizungumza machache katika hafla ya ufungaji wa maonyesho hayo.
 Kutoka kushoto pichani ni Balozi wa Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Bw. Mallalla Mubarak Al-Ameri na kiongozi wa Mabalozi wa Kundi la nchi za Kiarabu, Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz na Makamu wa Balozi Bw. Ronaldo Vieira wakisikiliza hotuba kutoka kwa Mwakilishi wa Mtandao wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Aga Khan (hayupo pichani).
 wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali nchini, Taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali wakifuatilia picha zilizokuwa zikionyeshwa katika maonyesho hayo jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Balozi wa Brazil nchini Mama Luz akibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa.
 Afisa Ubalozi Lucy Mwambungu akiwa katika picha ya pamoja na msanii wa siku nyingi wa michezo ya Kuigiza maarufu kama Sinta pamoja na Makamu wa Balozi wa Brazil nchini Ronaldo Vieira.
 Balozi wa Marekani nchini Alfonso E. Lenhardt akiangalia picha zilizokuwa zimetandazwa katika maonyesho hayo.
miongoni mwa wadau mbalimbali kutoka sehemu na Idara Tofauti za ndani na nje ya nchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla hiyo ya maonyesho ya picha yanayoelezea ushirikiano wa nchi  ya Brazil na zile za kiarabu katika nyanja mbalimbali.

No comments: