Tuesday, July 5, 2011

TBL yazindua kampeni ya Jivunie Utanzania leo

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania,Robin Goetzche akizungumza leo katika uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager ikiwa ni harakati ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Kampeni hii imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,katikati ya Jiji la Dar na kuhudhuriwa na wageni mbali mbali.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),David Minja akifafanua jambo juu ya Kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi leo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Mawasiliano na Mambo ya Nje wa TBL,Emma Oriyo,akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania iliyofanyika leo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,jijini Dar.
 MC Taji Liundi akiongoza shughuli hiyo.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche, Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo, Mjumbe wa Bodi Geoggrey Msella, Mkurugenzi Masoko TBL, David Minja na Maneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio wakiwa wameshika bia za Kilimanjaro Premium Lager kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya ‘Kili Jivunie uTanzania uliyofanyika katika Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo.
Wakongwe wa Muziki wa dansi nchini pia walikuwa ni sehemu ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Wachezaji wa zamani wa timu za mpira wa miguu wa timu za Yanga na Simba pia walikuwepo.toka kushoto ni Salvatory Edward,Kenneth Mkapa,Mohamed Mwameja na Edbil Jonath Lunyamila.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo.
Wadau wa InterGrated wakiwa na Mwanariadha wa Siku nyingi,Suleiman Nyambui (mwenye koti).
Suleiman Nyambui akiwaeleza jambo waandishi wa habari.
Wakuu wakizungumza.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),David Minja akiagana na Mkongwe King Kikii.katikati ni Kiongozi wa bendi ya Kilimanjaro wana Njenje,Waziri Ally.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu.

No comments: