Saturday, July 23, 2011

Mashindano maalumu ya pool mjini Dodoma leo

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imedhamini mashindano maalum ya pool mjini Dodoma ambapo kumefanyika mchezo kati ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na viongozi wa Tbl,Chama cha Pool na Integrated Communication Ltd.
Michezo hiyo imefanyika katika ukumbi wa Tiger Motel mjini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi ni Mh Mathius Chikawe –Waziri wa nchi ofifi ya Rais utawala bora.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Meneja wa Bia ya safari Oscar Shelukindo alisema TBL imekuwa ikiendeleza mchezo wa pool nchini kwa muda mrefu ambapo kwa sasa lengo ni kuhakikisha idadi ya mikoa inayoshiriki mashindano hayo inaongezeka toka kumi na nne ya sasa hadi 21 ndani ya Tanzania bara.
Nae Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania,Bwana Steven Kilindo alisema mafanikio yaliyofikiwa na Bia yaSafari katika kukuza na kuendeleza mchezo wa pool nchini kwa kiwango kikubwa unatokana na ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali kwa kuweza kutambua umuhimu wa michezo nchini ukiwepo mchezo wa pool,Mheshimiwa Waziri TBL inatambua kwa undani umuhimu na mahitajio ya watanzania walio wengi kuwa wanapenda michezo nasi TBL kwa kutambua hilo tumeona tutumie kiasi fulani tunachopata kwenye mauzo ya vinywaji vyetu na kuvirejesha kwa Watanzania kupitia michezo mbalimbali ukiwepo huu mchezo wa pool,Kipekee tunafarijika kuona mchezo huu umeweza kukua kwa kasi kubwa na hata kuwa kati ya michezo iliyo katika kiwango cha juu kwa kupendwa nchini
Tulianza na timu chache ,kisha ukakua na hatimae kuingia katika vyuo vikuu nchini na chuo Cha usimamizi wa Fedha IFM kufanikiwa mabingwa wa kitaifa kwa vyuo kwa mara ya kwanza na sasa tupo nanyi wabunge ni mafanikio makubwa sana,Alisema bwana Kilindo.
Kwa Upande wake Mgeni rasi Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi utaala bora Mh Mathius Chikawe alisema mwanza serikali ikuwa ikidhania mchezo wa pool ni mchezo wa kijiweni na wawahuni lakini kupitia TBL na bia ya Safari imeweza kuukuza na kuwa sehemu ya ajira kwa watanzania
Kwetu kama serikali tulikuwa na tafasiri tofauti mwanzoni lakini sasa TBL kupitia bia ya Safari wameweza kuleta mapinduzi ya kweli kwenye huu mchezo na sisi kama wabunge na serikali tunawajibu wa kupokea na kuundeleza katika majimbo yetu na taasisi mbali,bali kama ambavyo bunge limeanza kwa sasa.
Tunaahidi kuendeleza katika sehemu mbalimbali ilio kuweza kuja kupata timu nzuri ya Taifa na hatimae kuweza kuleta sifa kwa Taifa letu la Tanzania.
Huu mchezo wa leo uwe ni changamoto kwa waheshimiwa wabunge kuweza kuanzisha club mbalimbali za pool katika majimbo yao, Nimepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wachezaji waliopo hapa na wameambia kuwa kwa sasa wameweza kujiajiri kupitia fedha mbalimbali wanazopata kwenye usajili,zawadi na hatimae kuendesha maisha yao, haya ni mafanikio na mfano wa kuigwa kupitia hii kampuni ya bia ya Tbl.
Na mwisho napenda kuwaambieni wazi kabisa mawazo kuwa mchezo wa pool ni mahsusi kwaajili ya walevi ni imani potofu na hapa waheshimiwa wabunge wamedhihirisha hilo kupitia mchezo wa leo.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha pool nchini Bwanba Fred Mushi alisema Tbl imekuwa mfano wa kuigwa kwa kuweza kuleta ,mapinduzi ya dhati katika mchezo wa pool nchini, Tbl imeweza kuwa nasi kwenye kipindi chote cha kuasisi mchezo huu nchini na hatima sasa umeweza kuwa katika kiwango cha juu sana na juma lijalo tuanaanza fainali za kitaifa kwa kushirikisha mikoa kumi na nne ya Tanzania bara ,kupitia mashindano hayo sehemu kubwa ya watanzania wameweza kufaidika kwa njia moja au nyingine.
Mchezo huo maalu timu ya Bunge imefanikiwa kufungwa kwa tabu sana kwa jumla ya fremu kumi kwa tisa.
Wachezaji wa Bunge ni.
George Simbachawene
Stephen Ngonyani
Dr Kiziba
Shaffih Sumara
Khamis Kingwalangwala
Jitu Son
Timu mchanganyiko TBL,TAPA INTERGRATED COMMUNICATION
1.Steve Kilindo –TBL
2.Oscar Shelukindo-TBL
3.Fred Nthiga-Integrated Communication
4.Issack Togocho-TAPA
5.Fred Mushi-TAPA
6.Amos Kafwinga-TAPA
7.Zahoro Ligalu-TAPA

No comments: