Tuesday, June 28, 2011

ziara ya nape nnauye mkoani mtwara

 Nape akiongoza wanachama wapya wa CCM kula kiapo, baada ya kuwakabidhi kadi za CCM, wanachama 30 wwalijiunga wakiwemo kutoka chama cha CUF.Kushoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa CUF, Rukia Panyota, aliyeamua kurejea CCM wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
 Mashabiki wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tandahimba mkoani Mtwara,
 Nape akicharaza ngoma baada ya kuwasili katika Tandahimba mkoani Mtwara
kwa ajili ya mkutano wa hadhara,
 Viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wao wa ndani na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara.
 Nape akisalimia wazee wa Newala alipokwenda kufanya mkutano wa ndani na  viongozi wa mashina na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM kwenye ukumbi wa Chama Cha Akiba na Mikopo (SACCOS) mjini Newala mkoani Mtwara
 Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake na Nape, wakiwa njiani kwenda Mjini Liwale.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa wilaya ya Newala mkoani Mtwara walipoupokea msafara wake akiwa njiani kwenda Mjini Liwale
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimjulia hali Somoye Ismaili (70) aliyekuwa akisubiri matibabu kwenye chumba maalum cha kuhudumia wazee, katika hospitali ya Wilaya ya Lindi mjini, juzi. Nape alitembelea hospitali hiyo, mwishoni kwa ziara yake ya siku mbili mkoani Lindi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah juma

No comments: