Friday, May 6, 2011

Tuzo za Wanamichezo bora 2010 zafana sana usiku huu

Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo bora mwaka 2010,Makamu wa Rais,Dr. Mohamed Gharib Bilal akitoa hotuba kwa wageni waalikwa waliohudhulia hafla hii katika ukumbi wa hoteli ya Movenpic,jijini Dar usiku huu.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin W. Mkapa akizungumza usiku huu wakati akitoa shukrani kwa tuzo maalum aliyoipata kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya michezo hasa kwa kujitoa kwake kwa hali na mali kufanikisha ujenzi wa uwanja wa taifa iliyotolewa na Chama cha Michezo nchini,Taswa.
Makamu wa Rais,Dr. Mohamed Gharib Bilal akipiga makofi ya pongezi mara baada ya kumkabidhi tuzo maalu na ya heshima,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa aliyoipata usiku huu.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimpatia tuzo yake Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL,Teddy Mapunda mara baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Rais,Dr. Mohamed Gharib Bilal usiku huu katika ukumbi wa hoteli ya Movenpic,jijini Dar.
Mwenyekiti wa Chama cha Michezo nchini,Juma Pinto akizungumza usiku huu katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanamichezo bora wa mwaka 2010 katika ukumbi wa hoteli ya Movenpic jijini Dar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za wanamichezo bora 2010,Masoud Saanan akizungumza usiku huu na baadae kuitambulisha kamati yake iliyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa na hatimae kufikia hatamu usiku huu.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL,Teddy Mapunda akimkabidhi tuzo ya Mwanariadha bora wa Mwaka 2010,Marco Joseph.
Boss wa TSN,Mkumbwa Ally akikabidhi tuzo


































No comments: