Wednesday, May 25, 2011

MKE WA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MAMA ASHA BILAL, AZINDUA MFUKO WA PAMOJA TUSHIKAMANE WA KUSAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza wakati akisoma hotuba yake ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa kusaidia Wazee wasiojiweza wa ‘Pamoja Tushikamane’ ulio chini ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
Mmoja kati ya wageni waalikwa, Bi. Eshe Sururu, akizungumza kutangaza kiasi alichotoa kuchangia mfuko huo jana, ambapo alitangaza kuchangia Sh. 500.000.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (katikati) na Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tushikamane Pamoja Faundation, Rose Mwapachu (kulia) wakipiga makofi kuwashangilia watu waliojitolea kuchangia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana Mei 24.
Baadhi ya wageni walioalikwa kuhudhuria hafla hiyo.
Mtunza hazina wa mfuko huoakionyesha kidani cha Silver alichonunua kwa Sh. 750,000 baada ya kupigwa mnada, ambacho thamani yake halisi ilikuwa ni Sh. 150,000.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu, baada ya kuzindua rasmi mfuko wa Tushikamane Pamoja Faundation, iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini dare s Salaam.
Mama Asha Bilal (kushoto) akiongozana na Mwenyekiti wa mfuko huo kuingia ukumbini baada ya kuwasili kwenye Hoteli ya New Africa.
Mmoja kati ya wafanyakazi wa mfuko huo akibofya kitufye cha Kompyuta kuonyesha baadhi ya picha za watu waliofanikiwa kuwatembelea.
Baadhi ya Masister waliohudhuria hafla hiyo walioongazana na mmoja kati ya wazee wasiojiweza wanaomlea katika kituo chao Msimbazi.
Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wanaojitolea kufanya kazi katika mfuko huo wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni walioalikwa kuhudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya wageni waalikwa.


Baadhi ya wageni waalikwa.

No comments: