Thursday, May 26, 2011

KAMATI YA MIUNDOMBINU YA BUNGE LA TANZANIA YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA AIRTEL LEO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor akitoa ufafanizu wa Kampuni yake kwa Wabunge wa Kamati ya Miundombinu (hawapo pichani) waliotembelea leo makao makuu ya Kampuni hiyo ili kufahamu mambo mbali mbali yafanyikayo hapo.Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Peter Selukamba akizungumza na Mkurugunzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel,Beatrice Singano mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliowakutanisha viongozi wa Kampuni hiyo na Kamati ya Miundombinu leo katika makao makuu ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel,Sam Elangallor pamoja na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni hiyo,Beatrice Singano wakizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini,Eng. Rambo Makani (kulia) mara baada ya mkutano wao uliomalizika mchana huu katika ukumbi wa mikutano wa Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Sam Elangallor akionyesha moja ya picha zilizokuwa zikionyeshwa kwenye Screen (hapo pichani) kwa Wabunge wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliotembelea leo makao makuu ya Kampuni hiyo.
Waheshimiwa Wabunge wakifatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel pindi walipotembelea leo.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Miundombuni.
Wafanyakazi wa Airtel wakifatilia mkutano huo kwa makini.
Waheshimiwa Wabunge.
Mkutano ukiendelea.

No comments: