Thursday, June 1, 2017

BENKI YA KCB TANZANIA INAFANYA ZIARA KATIKA MIJI MIKUU NCHINI MAREKANI


Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi, Dismas Assenga.
Raisi wa Jumuiya ya watanzania waishio Houston Marekani Bw. Daudi Mayocha (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mijini Houston.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (aliyesimama, wapilikushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki ya KCB kwa baadhi ya watanzania (pichani) wanaoishi katika mji wa Houston.
Raisi wa jumuiya ya watanzania waishio Dallas Marekani Bw. Ben Kazora (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mjini Dallas.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi. Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas. 

 Benki ya KCB Tanzania kupitia dawati lake la Diaspora Banking inafanya ziara katika miji waishio watanzania nchini Marekani. Ziara hii imeanza tarehe 26 Mei na kutegemewa kumalizika tarehe 7 Juni. Miji inayotembelewa ni Washington Dc, Houston, Tx, Dallas, Durham Raleigh, Nc Boston, Ohio, Minnesota Na Chicago. 

Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Shose Kombe akizungumza kuhusiana na ziara hii, alisema “Kuna watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi na wanahitaji kuwekeza na kupata huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania, hivyo Benki ya KCB inatembelea miji ya Marekani yenye watanzania wengi ili kuwapatia huduma bora kwa haraka, usalama na bila usumbufu”. 

Huduma za kibenki wanazopatiwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni; akaunti za akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi nchini Tanzania. 

“Huduma hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani” alisema Bi. Kombe. 

Akizungumza na Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi, Bi. Kombe na watanzania wanaofanya kazi ubalozini, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Dismas Assenga alifuraia ujio wa benki ya KCB nchini Marekani. 

“Watanzania wanaoishi Marekani wanahitaji sana kuwekeza nyumbani hivyo tutafurahi mkifikia watanzania wote kutoka miji tofauti ya Marekani” alisema Kaimu Balozi. Bi. Kombe alimaliza kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo, mteja anahitaji kua na nakala ya Pasi ya kusafiria, Leseni ya udereva au risiti ya huduma za umeme au maji (utility bills). 

No comments: