Na
Ally Daud-WAMJW DODOMA
SERIKALIi imedhamiria kuboresha kiwango bora vyoo mjini na vijijini kutoka asilimia 35 hadi asilimia 55 kufikia
mwaka 2025 ili kujenga taifa lenye afya bora na lisilo na maambukizi ya
magonjwa yatokanayo na uchafu wa vyoo.
Akizungumza hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo
kama “NIPO TAYARI” Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imepania kufikisha asilimia ya ubora wa vyoo
mpaka kufikia 2030.
“Hatua hii itafikiwa endapo kwa pamoja tutasukuma
mbele ajenda ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa
katika ujenzi wa vyoo bora,utupaji salama wa taka ngumu,upatikanaji wa maji
salama kwa mikono miwili” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa yapo mafanikio
yaliyofikiwa katika kupunguza kasi ya watu kujisaidia ovyo tabia ambayo ni
kisababishi cha maambukizi ya magonjwa mengi katika jamii.
Mbali na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wanasiasa
wenginekushirikiana na wananchi katika majimbo yao ilikusukuma kwa vitendo
ajenda ya Usafi wa Mazingira nchini .
Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa watanzania wa wa mijini na vijijini wawe
mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatumia vyoo bora kila kaya ili kuepuka
magonjwa ya kuambukiza.
Naye Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwelwe amesema kuwa ili kuendana na kasi hiyo wamejipanga kuhakikisha
shule zote za msingi na sekondari nchini zinapata maji safi na salama kwa
wakati sahihi.
No comments:
Post a Comment