Wednesday, April 27, 2016

Heart Marathon yafana jijini Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na wadau wa riadha wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Half Marathon zilizofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kongamano la Afya Tanzania na Mratibu wa mbio hizo Dkt. Omary Chillo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chakao Khalfan akizungumza na waandishi wa Habarai mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jana jijini Dar es Salaam. Heart Marathon hii imejumuisha mbio za urefu wa 21Km, 10Km, 5Km, mita 700 kwa ajili ya watoto, Baiskeli Kilomita 21 na Baiskeli walemavu.
Wanariadha washiriki wa Heart Marathon wakichuana katika mbio za urefu wa kilomita 21 jana jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa mbio za Heart Marathon kwa waendesha Baiskeli wakiwa katika mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
Watoto wakiwa katika mashindano ya Heart Marathon mbio za urefu Mita 700 jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanaume mbio za Kilomita 21 Bw. Dickson Marwa wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akimvalisha Medali mshindi wa kwanza kwa wanawake mbio za Kilomita 21 Bibi. Failuna Abdi wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Marathon zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akikabidhi Tuzo kwa mdhamini mkuu wa mbio za Heart Marathon, Taasisi ya Tindwa Medical and Health Services wakati wa ufungaji wa mbio za hizo jana jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilikuwa na kauli mbiu ya “Kuwa huru katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza”. Picha na: Frank Shija, WHUSM.

No comments: