Monday, September 7, 2015

ZOEZI LA KUWAPOKEA WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI LAENDELEA VIZURI KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU MKOANI KIGOMA

 Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
 Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.
 Mtoto Jamine Nibetanga(14), kutoka nchini Burundi akiandaa chakula   katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli.
 Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
 Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda.  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ili kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
 Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
 Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
 Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake  katika kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa  mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katika kambi ya Nyarugusu.
 Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira kama walivyokutwa jana na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni.
 Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara  katika kambi hiyo.
Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

1 comment:

Anonymous said...

NA SISI WATANZANIA TUKIVURUGA AMANI TUTAKUA KAMA HIVI. TUSHUKURU TUPO MAJUMBANI KWETU TUNAKULA NA KULALA