Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia baadhi ya Wananchi hawapo pichani
alipokuwa akiwasili katika uwanja wa Tawi la CCM Matarumbeta katika
jimbo la Jang'ombe,ambapo Ndugu Kinana alikabidhi vifaa vya michezo kwa
vijana,alikabidhi vifaa vya mradi wa maji safi,pia alikabidhi hati kwa
kikundi cha vijana Jang'ombe
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi bati kwa ajili ya ujenzi wa msikiti
kwa mmoja wa wananchi kwenye uwanja wa Tawi la CCM Matarumbeta
katika jimbo la Jang'ombe,ambapo Ndugu Kinana alikabidhi vifaa vya
michezo kwa vijana,alikabidhi vifaa vya mradi wa maji safi,pia
alikabidhi hati kwa kikundi cha vijana Jang'ombe.
Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukiwasili katika tawi la CCM
Mikunguni (shehia ya Mikunguni),kushiriki katika shughuli za uchimbaji
na utandazaji wa mabomba ya maji na salama.
Mbunge wa Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza mbele ya wakazi wa Shehia ya Mikunguni (hawapo pichani),wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyoianza leo wilaya ya mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi na wanachama wa Shehia ya Mikunguni ,wakati wa ziara yake aliyoianza leo wilaya ya mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na
Mbunge wa Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akishiriki
uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama kwa wakazi wa Shehia ya
Mikunguni ,katika jimbo la Kwahani.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mbunge wa
Jimbo la Kwahani,Mh.Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakishiriki katika shughuli
za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya maji safi na salama kwa wakazi
wa Shehia ya Mikunguni ,katika jimbo
la Kwahani.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Shehia ya Makadara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana alipotembelea jimbo la Rahaleo,ambapo alishiriki katika
ujenzi wa Taifa za uchimbaji wana utandazaji wa Mabomba ya maji safi na
salama.
Wananchi wa mji wa Shehia ya Makadara na wanachama wa CCM,wakishangilia jambo Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Kinana akiwa
Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya tawi la CCM-Mwembeladu katika jimbo la Rahaleo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Balozi Ali Karume alipowasili katika Shehia ya Miembeni,katika
jimbo la Kikwajuni,ambapo Ndugu Kinana alipokea taarifa fupi ya mradi
wa Zahanati na kushiriki katika ujenzi wa Taifa wa Ukarabati wa
Zahanati ya Miembeni (Nyumba ya Yasu).Pichani kulia ni Muwakilishi wa
jimbo la Kikwajuni,Mh.Mahamoud Mohamed Mussa pamoja na Mbunge wa jimbo
hilo la Kikwajuni Mh.HamadiYussuf Massauni
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na Balozi Ali Karume walipokutana leo katika Shehia ya Miembeni,katika jimbo la Kikwajuni
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ya mradi mkubwa wa
kisasa alipokwenda kutembelea Tawi la CCM Vikokotoni katika jimbo la
MjiMkongwe
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi ya mradi wa maduka kwa
vijana wajasiliamali katika Shehia ya Kilimani,ambapo Ndugu Kinana
alishiriki shughuli za uchimbaji na utandazaji wa mabomba ya mradi wa
maji safi na salama na ujenzi wa Maskani ya Fishamen,katika jimbo la
Mjimkongwe..
Katibu
Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana pamoja na wanachama wa CCM wakiwemo na
Wananchi kwa pamoja wakishiriki katika shughuli ya za uchimbaji na
utandazaji wa mabomba ya mradi wa maji safi na salama katika shehia ya
Kilimani,kwenye jimbo la Mjimkongwe.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya chumba cha
kufundishia Kompyuta katika kituo cha Vijana (Tanzania Youth Icon),cha
kuwaendeleza na kuwawezesha katika masuala mbalimbali ikiwemo
elimu,Ajira na Michezo kilichopo Shehia ya Miembeni,Mwembemadema katika jimbo la Kikwajuni.
Mwenyekiti
wa Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman
akisoma hotuba Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na
mambo mbalimbali yahusuyo kituo hicho cha huduma rafiki kwa Vijana
kilichopo Muembemadema ndani ya jimbo la Kikwajuni sambamba na
changamoto wazipatazo juu ya kituo hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza mbele ya wanachama wa chama hicho
pamoja na Wananchi nje ya Kituo cha Tanzania Youth Icon (TAYI),ambapo
mlezi na mhamasishaji wake ni Mbunge wa jimbo la Kikwajuni,Mh.Hamad
Yusuf Masauni.Kituo hicho cha TAYI ni Taasisi ya vyama visivyokuwa vya
kiserikali,ambayo ina muelekeo wa kuwasaidiana na Wadau mbalimbali
katika kufanikisha shughuli za maendeleo.Mwenyekiti wa Kituo cha
Tanzania Youth Icon (TAYI),Bwan.Abdullah Miraji Othman amesema kuwa
Taasisi hiyo hivi sasa ina ina wanachama wasiopungua 500 ambao tayari
wameandikishwa na kuwepo katika rekodi na kumbukumbu za ofisi,Bwana
Abdullah aliongeza kuwa kituo hicho kinawajenga vijana kiuchumi na pia
kuwapa taaluma ya uongozi ili waje kuwa viongozi wazuri ,''kituo hiki
kimekuwa kiwanda kizuri cha kuzalisha vijana wazuri kwa Taifa'',alisema Bwan.Abdullah .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikabidhi piki piki kwa mmoja wa makatibu wa CCM.
Mmoja wa Mabalozi akifurahi mara baada ya kukabidhiwa baiskeli yake na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,kwa
shughuli mbalimbali za kichama,baiskeli hizo ilikuwa ni ni moja ya
ahadi alizoahidi kutoa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mh Masauni,ambapo
pia alitoa piki piki kwa makatibu wa chama.
No comments:
Post a Comment