Tuesday, September 16, 2014

KAGERA SUGAR WAIFUATA MGAMBO JKT MJINI TANGA

Na Faustine Ruta, Bukoba
Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari  kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na  viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.Viongozi wa Kagera Sugar
Ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu msimu huu.
WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wakijifua kwenye Uwanja wa Kagera Sugar hivi karibuni tayari kwa Ligi kuu Vodacom sep 20 mwaka huu. Kagera Sugar wataanza ufunguzi wa Ligi kuu Vodacom Ugenini na timu ya Mgambo JKT mkwakwani Mjini Tanga wikiendi hii.
Kocha huyo alisema: “Tuna imani na vijana wetu kuwa wanaweza kutufikisha tunapotaka, japokuwa ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu, lakini tutajitahidi kupigana ili kuweza kushika nafasi za juu”.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakifaya mazoezi yao kwenye Uwanja wa Kaitaba Hivi karibuni.



Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa Uwanjani Kaitaba wakishuhudia mazoezi ya Vijana wao. Wakijifua kujiandaa na Ligi Kuu Vodacom msimu mpya 2014/15 inayotarajia kuanza hivi Karibuni sep.20 mwaka huu.
Kikosi cha Kagera Sugar
Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar (kulia) tayari amebainisha kuwa mapungufu waliyokuwa nayo katika kikosi chao kuwa wameishayafanyia marekebisho na wako tayari kupambana na Mgambo JKT ya Mjini Tanga.
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar (kulia) Bw. Jackson Mayanja akiangalia vijana wake wakati w mazoezi yao kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Kaitaba hivi karibuni.

No comments: