Thursday, February 7, 2013

MAMA SALMA ATOA MSAADA WA VIFAA VYA HOSPITALI YA SOKOINE-LINDI

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9 Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
Kikundi cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya kukabidhi vifaa vya tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine,na wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi rasmi vifaa vya tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013 huko Lindi Mjini. Waliokaa kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ambaye pia ni Meya wa Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa mwisho ni Mwakilishi wa Project C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe Kimario.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete kwa furaha akiagana na wafanyakazi wa hospitali ya Mkoa wa Lindi,Sokoine, viongozi na wananchi waliohudhuria sharehe za kukabidhi vifaa vya hospitali hiyo tarehe 6.2.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments: