Thursday, February 7, 2013

Wama yakabidhi vifaa kwa Hospital ya mkoa wa Lindi

Na Abdulaziz Video, Lindi 
 Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)Katika kusaidia sehemu kubwa ya Jamii na makundi yenye kuhitaji msaada hususan Wanawake,watoto na wasio na uwezo ufadhili wa Taasisi mbalimbali Nchi Za Nje ili Kuboresha Huduma za Afya hapa Nchini Imetoa msaada wa Vifaa tiba kwa Hospital ya Mkoa wa Lindi 

Hayo yamebainika katika Hafla fupi ya kukabidhi Vifaa tiba kwa Vyenye thamani ya Milioni 700 vilivyotolewa na Shirika la Project Cure la Marekani baada ya Taasisi hiyo kuchangia na leo kukabidhiwa kwa Vifaa hivyo kwa Mkoa huo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ambae Pia ni Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete kueleza kuwa licha kukabidhi msaada huo misaada zaidi ya WAMA ipo katika nyanja za elimu, afya pamoja na maendeleo ya wanawake katika mikoa yote Nchini. 

Aidha alibainisha kuwa pamoja na taasisi ya WAMA kupata mafanikio katika kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto, mapambano dhidi ya Malaria na UKIMWI, chanjo kwa watoto ikiwemo ya ugonjwa wa Nimonia, mimba kwa wanafunzi wa kike pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wa kike hapa nchini Pia ametoa wito kwa Wakazi wa Lindi kusimamia Elimu ya Watoto. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Project Cure la Marekani.Bw Abdu Kimario ameipongeza taasisi ya WAMA kwa mchango wake katika jamii hasa kuboresha elimu, huduma za afya pamoja na mapambano dhidi ya mimba za udogoni kwa wanafunzi wa kike na kuwaendeleza wajasiriamali wa kike nchini na kubainisha kuwa Vifaa kama hivyo vilivyokabidhiwa leo pia vitakabidhiwa katika mikoa mingine nchini 

Hivi Karibuni Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Dr Richard Boniface alieleza jinsi msaada huo utakavyosaidia kufuatia kutowepo kwa huduma ya X-ray kwa zaidi ya mwaka mmoja hata hivyo pamoja na msaada huo pia aliomba ufadhili zaidi wa Elimu kwa watumiaji wa Vifaa tiba hivyo Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na Mashine ya X-ray pamoja na vifaa vyake vyote,Mitambo ya kitanda maalum cha ICU Kwa ajili ya wagonjwa mahututi,Mitungi ya gesi ya Oxygen ambayo itasaidia kutoa huduma ya dharura hasa wakati Umeme umekatika,Vifaa na mitambo kwa ajili ya huduma za kinywa na meno,Vifaa vya upasuaji mdogo na mkubwa,Ultra sound machine,Taa,meza na mashine ya Usingizi
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi 
Mama Salma Kikwete akibeba kichanga katika wodi ya wazazi
Waliohudhuria sherehe wakifuatilia kinachoendelea
Ngoma ya utamaduni ikitumbuiza
Mama Salma Kikwete akiongea kwenye hafla hiyo
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa na WAMA
Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi vifaa hivyo
Askari wa usalama barabarani wakijipanda kuwajibika

No comments: