Monday, June 11, 2012

MASHINDANO YA MISS UTALII TANZANIA YAGAWANYWA KIKANDA

Bodi ya Taifa ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania, katika kutekelezaa mpango mkakati wake wa kuimarlisha na kuboresha zaidi mashindano hayo, imegawanya mikoa yote ya Tanzania na Vyuo Vikuu katika kanda maalumu za mashindano hayo.
 
Kwa lengo la kuimalisha utekelezaji wa malengo ya mashindano na usimamizi , Kuanzia mwaka huu kutakuwa na jumla ya kanda 14 za mashindano ya Miss Utalii Tanzania , zikiwemo saba (7) za kawaida na saba (7) kanda maalumu za Miss Utalii vyuo Vikuu. 

Hatua inalenga pia kufikisha mashindano ya Miss Utalii Tanzania hatika Ngazi za chini zaidi , mijini na vijijini, ambapo kwa kuanzia mashindano haya sasa yataanzia katika Ngazi za kata, Majimbo ,Wilaya,mikoa, kanda, taifa na hatimaye Dunia, hiku mpango mkakati ni kuanza kufanyika katika mgazi za vijiji ifikapo mwaka 2014.

 Huu ni mpango wa lazima kwetu kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya, ambayo pamoja na malengo mengine yanalenga pia kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa sekta ya Utalii kiuchumi na kijamii,hivyo kuwa fulsa pekee ya kufanyika kwa mashindano haya katika Ngazi za vijiji kufikia mwaka huo 2014.
 
Mgawanyo wa kanda hizo na mikoa yake katika mabano ni:
A: KANDA ZA KAWAIDA NI:
1.      Miss Utalii Tanzania –Kanda ya Mashariki  (Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara, Zanzibar)
2.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi (Simiyu, Shinyanga na Mara)
3.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Ziwa (Mwanza, Geita, Kagera na Kigoma)
4.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Arusha)
5.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kati  (Tabora, Dodoma, Singida na Morogoro)
6.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya  Kusini Nyanda za Juu  (Mbeya, Rukwa na Katavi)
7.      Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Kusini  (Ruvuma, Iringa na Njombe)
B: KANDA MAALUM ZA VYUO VIKUU NI:
1.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kati  (Dodoma, Kigoma, Tabora, Singida)
2.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini (Iringa, Ruvuma, Njombe)
3.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Pwani  (Dar es Salaam, Zanzibar , Lindi na Mtwara)
4.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu- Kanda ya Magharibi (Mwanza, Geita, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga na Singida)  
5.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kusini Nyanda za Juu  (Mbeya, Rukwa, Katavi)
6.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Kaskazini ( Arusha,Kilimanjaro,Manyara)
7.      Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu – Kanda ya Mashariki (Morogoro, Mtwara na Lindi)
Mgawanyo huu wa kanda umezingatia , maeneo ya kijografia, mwingiliano wa tamaduni, uwepo wa vivutio vya Utalii katika kila kanda, urahisi wa kutangaza Utalii na kuhamasisha Utalii wa ndani,pia kutoa fulsa kwa mabinti wengi zaidi kushiriki mashindano haya katika Ngazi zote.
 
Aidha mfumo huu, utasaidia kuwachuja washiriki katika Ngazi za kanda, hivyo kuwa na washiriki wenye viwango na ushindani unaokibalika kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano haya na mengine yahusuyo kitaifa na kimataifa.
 
Kwa mwaka huu, kanda ya ziwa ndiyo itakayo kuwa ya kwanza kufanya Fainali zake za Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012 na kushirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Geita na Kigoma. Shindano hilo linalo andaliwa na Fania Hassani ambaye ni Mkurugenzi wa Miss tourism Tanzania Organisation kanda ya Ziwa na Fania Beauty Saloon ya limepangwa kufanyika Juni 30, 2012 katika ukumbi wa Monarch Hotel Mwanza na kudhaminiwa na Gold Masters, Monarch Hotel, Garrett Security Items na Solar Power MSP – H na magazeti ya Gazeti la Jambo Leo, KIU Investment.
 
(picha zilizo ambatanishwa na Taarifa hii ni za washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Ziwa, wakiwa wamepozi katika hoteli ya Monarch ambako kambi ya Mazoezi inaendelea, tayari kwa Fainali itakayo fanyika hotelini hapo 30-6-2012.
 
Asante,
 
Mr. George Ntevi  - Katibu wa Bodi ya Taifa ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania .
 
Miss Tourism Tanzania  Symbol Of National Heritage -Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"
Regards,
 Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.

No comments: