Tuesday, January 17, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU REGIA MTEMA KARIMJEE DSM LEO, KUZIKWA KESHO IFAKARA

 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshma zake za mwisho kwa Marehemu Mhe. Regia Mtema katika viwanja vya Karimjee leo
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
 Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga. 

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.
 Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Salaam Kutoka kwa Katibu mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia,  wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa,  pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia,  wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na baadhi ya ndugu wa Marehemu.
 Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mh. Jaji Fredrick Werema.
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick. 
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Sadick Meck, Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe wakimsubiri makamu wa Rais leo katika viwanja vya karimjee kuaga mwili wa Mbunge wa Chadema Viti Maalum Marehemu Regia Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari Jumamosi tarehe 14, 2012 
Baadhi ya Waheshimiwa wabunge wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu,Mh. Regia Mtema iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.Picha na Muhidin Sufiani wa OMR na Owen  David wa BUNGE.

2 comments:

Anonymous said...

Nimempenda Hawa Ghasia kwa heshima ya kitanzania ya kwenye msiba na wa kinamama na kinadada waliofunika nywele zao, sio wengine hapo kama wamenda kwenye fashion show.

Anonymous said...

R.I.P SUPER LADY REGIA E. MTEMA, UMETUTANGULIA TU KATIKA HAKI, KWA MUNGU TUMETOKA NA KWAKE SOTE TUTAREJEA.

TUTAKUKUMBUKA NA KUKUENZI KWA MEMA YOTE ULIYOYAFANYA.

Malisa A.