Wednesday, December 21, 2011

Heka Heka za Mafuriko katika eneo la Jangwani jijini Dar leo

Hii ndio hali halisi kwa wakazi wa eneo la Jangwani leo mara baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha jijini Dar es Salaam leo na kuyafanya makazi ya wakazi wa eneo hili kuwa namna hii kama zinavyoonyesha picha hizi.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo akijaribu kupita kwenye maji hayo ili afike barabari kwa kujiokoa na mafuriko hayo.
Nyumba zote zimezungukwa na maji huku mengine yakiwa yamejaa ndani ya nyumba hizo.
Kwaambaali anaonekana mmoja wa wakazi wa eneo hilo akiwa kapanda juu ya paa la nyumba yake ili kujirusuru na mafuriko hayo ambayo yameenea katika kila kona ya eneo hilo la Jangwani leo.
Mmoja wa wakazi wa eneo la Jangwani Jijini Dar akiwa amekaa juu ya godoro mara baada ya kuokolewa na waokoaji waliofika katika eneo hilo leo.
Yaani ni kama bahari ilikuwa imeamia hapa maana maji yalienea kila kona.
Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia wakijaribu kuwazua watu waliokuwa wakiitumia barabara ya morogoro rodi kutokana na kujaa maji kwa barabara hiyo leo.
Wakazi wa Jangwani wakiwa juu ya mapaa yao wakisubiri kupatiwa msaada.

Askari wa Jeshi la Wananchi wakiwa na mtumbwi wakisaidia kuwaokoa wananchi ambao wamekubwa na Mafuriko hayo katika eneo la Jangwani jijini Dar.
Yaani hali ni mbaya sana kwa wakazi wa eneo hili maana mambo ni kama yanavyoonekana pichani hapa.
Helkopta ya Polisi ikiendelea na doria ya kuona kama kuna yeyote anaehitaji msaada kwa wakati huo.
Wengi walilazimika kutembea kwa miguu leo kwani hakuku na gari iliyokuwa ikiruhusiwa kupita katika eneo la Jangwani leo.
Wananchi wakisaidiana kushusha mtumbwi katika eneo la jangwani tayari kwa kazi ya kuokoa waliokwama kwenye mafuriko hayo.
Gari la wagonjwa likipita huku na kule kuona kama kuna yeyote anaehitaji msaada.

14 comments:

Anonymous said...

GREAT Photos, they TELL the STORY VERY WELL!

Anonymous said...

Serikali ili kuokoa maisha ya watu na mali zao iache porojo na kusimamia utawala wa sheria, kila mtu apate haki yake kama ulijenga kwenye eneo lisiloruhusiwa wabolewe bila fidia, waliojenga pia kwenye mitaro, vinginevyo huu utakuwa wimbo wa kila siku.

jen said...

Hii ni mvua kubwa haijawai tokea kwa miaka ya karibuni. Manake walioadhirika sio wa mabondeni peke yao. Kweli ajali haina kinga

Anonymous said...

“Woe to us Tanzanians. These are the fruits of our labour"

Anonymous said...

YULE ALIYEKUWA ANAFUNGUA KINYWA KWENYE PAA PICHA YAKE IKO WAPI

Anonymous said...

Eeee Mwenyezi Mungu naomba uwanusuru ndugu zetu.

Anonymous said...

Well it is true they tell every thing,but all in all we should put prayers ahead of every thing,God can change his creations in a second,let us pray please.The only almight God can do what he wants when we upset him.only prayers realy from our heart can make him reduce or take away the punishment.We should all together go to prayers,no matter what belive you have for him is all ok.
See in one second he can change the world to anything he wants.

Anonymous said...

Dah kwakweli hali ni mbaya, hii yote ni sababu ya miundo mbinu, inauma sana kuona nchi yetu haijali vitu vya umuhimu ili kuepukana na majanga kama haya

fadhila said...

it's very pain jamani daah

Anonymous said...

poleni Watanzania wenzangu

Anonymous said...

This is what we call KUBWA KULIKO!

Anonymous said...

hivi ingenyesha wiki 1 uchumi wa tz ungeshuka up to negative

Anonymous said...

rais anapoanza kuwalaumu watendaji wake inamaanisha kipindi anaingia madarakani alikuwa haioni hiyo hali na nyumba nyingine zimejengwa yy yupo madarakani,rais wetu aache usanii ktk huu uzembe naye anahusika

Anonymous said...

Kama ukiangalia wakazi TABATA KINYEREZI,wameachwa katika mazingira magumu sana kwani hakuna barabara ya kuingia wala kutoka kinyerezi,madaraja yote yamepasuka,lakini what makes me sad ni kwamba hata ungozi hamna unaojali watu hawa hata kuweka kivuko katika daraja karibu na gereza la segerea na kuwaacha wahuni na vibaka kujifanya kuvusha watu na kuwaibia,na wanaopata shida ni akina mama,watoto na wazee.....