Wednesday, October 19, 2011

22 comments:

sud said...

nimemsifu mzee luwasa kwa ujasili wake wa kuongea ila cha kushangaza mbona amezungumzia kashfa moja tu juu yake mbona kwenye magazeti tumeziona kashfa nyingi tu zinazomhusu? kama vile richmond, tunamuomba azungumzie maswala yote kwa uwazi asifiche kama kweli yeye ni mwadilifu

Anonymous said...

Kaka tunashukuru kwa kutuletea hotuba hii kwa wakati,ila ni nachoweza kusema hotuba yake ni nzuri lakini bado hajasema yale mambo ambayo watanzania wengi walitaka kuyajua kama mfumu mzima wa Richmond na Dowans na anaonaje kuhusu serikali yetu kulipishwa deni hilo kupitia tanesco nk.

Anonymous said...

hi

kwa suala la wanasiasa na waandishi kujikita kwenye masuala yatayoiletea tija taifa letu nakubaliana nae. Kila mtu atekeleze wajibu wake

Anonymous said...

WATANZANIA TUACHE KULUMBANA,TUFANYE KAZI....MUDA WA MALUMBANO KTK DUNIA YA SASA UMEKWISHA.

Anonymous said...

mkubwa mbona la kujivua gamba hujaliongelea????????

Anonymous said...

Ukiwa mwadilifu huna haja ya kujisafisha kwa maandishi. Waadilifu tunawajua na ndo maana huwaoni magazetini wala huwasikii kwenye vinywa vya watu. Kufanya maswala sahihi ni wajibu wa kila mtu, kufanya maswala ya kijinga na kipumbavu lazima yasemwe na yeyote aliye na akili timamu. Kutumia muda wa watanzania na vyombo vyao vya habari kwa nia ya kujisafisha ni kutukana watanzania.

Anonymous said...

Hongera Mh. kwa kuongea bila kunyoosha vidole kwa wenzako kwa majina japo umetamka tu "viongozi", "uhuru wa vyombo vya habari" na "hatua unazofikiria kuchukua juu ya hivyo vyombo". Mimi nadhani usijikite sana kwamba wanakuchonganisha na mwenyekiti wa CCM, uwachukulie hatua pia kukuhusisha na ufisadi ili tujue vema uhusiano wako na richmond na dowans. Hili litakuepusha na uhujumu uchumi ambalo ni kosa kubwa kiusalama kitaifa kuliko hata hilo la usalama wa viongozi maana usalama wao unatokana na wananchi kuridhika na huduma za jamii.

Anonymous said...

ni kweli wanasiasa wengi tulionao wamezoea mamjungu na kuacha kufanya kazi kwa uadilifu,tunaipeleka pabaya TANZANIA...

Anonymous said...

Watanzania tuache uzushi usio na msingi, hivi kweli mtu akiambiwa athibitishe kuhusika kwa Mheshimiwa Lowasa na hayo maovu yazushwayo ataweza kufanya hivyo? Naomba nieleweke vizuri sina maana ya kumtetea ila ninachochelea ni kumhukumu mtu kwa kudhani si vizuri.

Jambo lingine la msingi ni kufikiria kwa undani, hivi umaskini wetu unasababishwa na Lowasa? au ni uzembe wetu wenyewe? Mimi kwa mtazamo wangu hakuna hata mbunge mmoja anyeweza kunishawishi kuwa yeye ni msafi kwani wote walikuwepo wakati wa Richmond, Kagoda, Dowans na vituko vinginevyo na vimepitia bungeni humo humo lakini leo kwa sababu watu tumefunguka macho wanataka kumtumia Lowasa kuficha kutokuwajibika kwao kwa kupitisha mikataba ya hovyo n.k. Tuamke na kujadili mambo ya msingi badala ya kusaidia kusafisha uchafu wa watu wengine kwa kuangalia Lowasa na kuwasahau wao.

Anonymous said...

mmh mwenzenu nilizani ndo anajivua gamba afuate nyayo za rostamu .....uongozi mtamu

Anonymous said...

Mkuu is beating around the bush. Wapi maamuzi magumu? unatu cost?

Anonymous said...

Taarifa ya mh. Lowasa haina maelezo ya kina na haikidhi haja yoyote. Kwanza ni vigumu kuelewa kiunagaubaga hasa lengo la mkutano wake na waandishi wa habari lilikuwa kuvitisha vyombo vya habari ama kukanusha tuhuma dhidi yake. Kama angelikuwa anataka kukanusha tuhuma angezichambua kwa kina kila tuhuma alizopata kutuhumiwa nazo. Ametumia muda mwingi kuvilaumu vyombo vya habari kuliko hata kuingia kwa undani dhidi ya wazushi wake mfano alianza kwa kusema 'kukutana nanyi leo haina makusudi kuzozana na vyombo vya habari'. Nilitarajia kuona neno kukanusha tuhuma linakuja mwanzo kabisa hasa za Richmond, EPA, kujiandaa kuwania Urais 2015. Lakini kwa muonekano huu alikuja na lengo la kuvitisha vyombo vya habari zisiendelee kuandika juu ya tuhuma dhidi yake kwa maana atavishughulikia kama alivyosema ' nimeanza kuwasilisha malalamiko yangu kwa kuwasiliana na msajili wa magazeti na Baraza la habari Tanzania'na 'nimeshaanza kujipanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi na wahariri'Lakini kikubwa zaidi ni kama mh. Lowasa anajaribu kuvilalamikia vyombo vya dola kwa kushindwa kudhibiti habari (uzushi) juu yake na anavitaka viwadhibiti waandishi na 'wengineo', mfano anasema uzushi wa viongozi 'unadhalilisha vyombo vya dola ambavyo vinafanyakazi kubwa kuhakikisha hujuma dhidi ya viongozi zinadhibitiwa'. Hii ni sawasawa na kusema jamani polisi, jeshi na usalama dhibitini hao wabaya wangu watu wasijue, wasiniumbue, jamani nisaidieni kuwadhibiti hawa.
Lakini pia Mh. Lowasa hajaeleza kama yeye amepewa ruhusa ya kuongelea chama chake, viongozi na wanachama wake ya kuwaongelea nje ya vikao vya CCM, kwa kuwaita wazushi na wasio masaidia rais katika kutekeleza majukumu ya serikali. Lakini hili naona amelikebehi kwa kusema 'najua kwenda kinyume na UTAMADUNI wa kimaadili wa ndani ya ccm'. Kwa hiyo hapa haoni kama ni kanuni au sheria ya ccm bali ni Utamaduni au kwa lugha nyingine ni mazoea tu. Kwa maana hiyo anaona hajakiuka kanuni au maadili yoyote ya ccm.
Pia ziara zake za siku au wiki nje ya nchi hazimfanyi akaelewa vizuri utendaji kazi wa vyombo vya habari vya nchi hizo katika kuandika habari za maendeleo, walau angesema amepata kusoma au kufanyakazi katika nchi hizo ningemwelewa zaidi. Mh. Lowasa anataka kusema waziri wa ulinzi wa Uingereza Liam Fox aliyeandamwa na vyombo vya habari kwa kutembea na rafiki yake katika ziara za kidiplomasia vilikuwa vizushi pia? Mbona alikanusha hapo awali na sasa amekubali kujiuzuru baada ya mambo mengi kuibuliwa?
Mh. Lowasa ametaja changamoto zinazolikabili taifa lakini hajajikita hata katika mojawapo kuongelea jinsi zinavyotusumbua watanzania na namna ya kutatua, mbali ya kuziacha kabisa changamoto za umeme,mafuta, maji, ufisadi n.k
Mimi sijaelewa pia kwanini Mh. Lowasa ameamua kumsemea Rais Kikwete kuwa 'hajashawishiwa na propaganda chafu' si angemwacha kikwete akasema hivyo?

Anonymous said...

Kweli kaka mkubwa hapo hajaongea kitu kama kweli ni msafi atuambie mambo ya richmond kwa nini alituingiza kwenye mkenge. mbona hilo amekaa kimya?

Anonymous said...

we mh. lowasa mbona unaongelea issue za urafiki wenu na JK badala ya kuongelea issues zinazoweza kuimarisha urafiki kati yako na wananchi??? kwani ukikosana na JK kwa maslahi ya wapiga kura wako utakufa?? huoni aibu kuumia kwa ajili ya uswahiba wako na JK badala ya kuumia kwa ajili ya Richmond, Dowans na EPA??? Mbona unachekesha wewe???

Anonymous said...

Huwezi kusema tufanye kazi, wakati tumepoteza ethics, hatufuati code of conducts, hizo kazi hazitaleta manufaaa mfano ni ufisadi umetawala vichwani mwa viongozi, tunataka strategic viongozi watoe mikakati, siyo kusema fanyeni kazi,

Anonymous said...

Ah!! Mimi nilidhani anamfuata Rostam Azizi.. kumbe kawachana waandishi. Sasa watu wataongeleaje kupolomoka kwa shilingi, ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira wakati wao wanachukua kila kitu na kutuacha watupu. Waandishi waendelee kuongea mpaka wachukie na kuachia madaraka hao...

Anonymous said...

Sioni la maana zaidi ya Kujitetea na kujibu kisiasa zaidi. Nimependa conclusion yake kuwa waandishi acheni kushabikia matukio andikeni habari zinazoweza badilisha maendeleo ya nchi hii

Anonymous said...

Sawa kabisa naungana na mhe huyu mkono. Kuna gazeti moja la kila wiki ambalo kila siku lazima litoe picha za huyu jamaa na habari zile zile zinazojirudia na siku nyingine hata picha na kichwa cha habari haviendani na story yenyewe. Wana habari hakikisheni habari kabla hamjatupatia sidi wananchi. Mnaturusha nyuma kwa kutuchapishia habari za baa na kitaani hambazo hazina tija kwetu wananchi.

Anonymous said...

ha ha haa.hapana kujisafisha kwa sasa,ashaharibu saaana tu

Anonymous said...

annonymous
bado hajakata kiu yangu kabisa hilo sio niliotaka kulisikia toka kwake nilitaka nisikie kuhusu "rich(man from)mond(uli), na sio hilo kwa maana ya kukanusha hoja ndo ku-prove kutohusika na kashfa husika ina maana kama hajakanusha ishu ya richmond thats means anahusika nayo isipokua hiyo ya kumhujumu kikwete tu ndo hahusiki

Anonymous said...

hongera kwa kuamua kuwa wazi waandishi wa habari tuwe makini

Tuntu said...

Wapendwa Watanzania;
Napenda kumshauri Mzee Lowasa; WATANZANIA WA SASA SIO WA ENZI YA UHURU. Wanajua kila kitu; wamechoka kuibiwa, na kudangagywa kila kukicha.
Mali nyingi imepotea kipindi ambacho yeye alikuwa Waziri Mkuu. Akiwa kama mtendaji mkuu serikalini, alipaswa kuwa makini kwa maamuzi yote nyeti, kulinda maslahi ya mtanzania maskini. Nadhani angewaomba radhi Watanzania kwa haya yanayotokea. Amemponza hata Mheshimiwa Rais Kikwete.

Mi namshauri mzee "taulo likikudondoka, haraka chuchumaa au keti uliokote".