Saturday, September 30, 2017

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM- Taifa) RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM-TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) kabla ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe. Dkt. John Magufuli akijadiliana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Rodrick Mpogolo kabla ya kufungua mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)   jijini Dar es Salaam.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam. 
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam.

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) wakipiga makofi mara baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli kuwasili ukumbini hapo jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Taifa) Rais Mhe Dkt. John Magufuli akipiga makofi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es Salaam.


 Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiendelea na Kikao jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. 

PROF. MAGHEMBE AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTALII DUNIANI MKOANI IRINGA

Na Hamza Temba-WMU
...............................................................
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe jana tarehe 30 Septemba, 2017 amefungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na Serikali katika kupambana na Majangili kwa kutoa taarifa za siri zitakazoweza kuwaibaini na kuchukuliwa hatua.

“Ili kulinda uwepo wa rasilimali za utalii zilizopo kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ni lazima wananchi kushirikiana pamoja na Serikali katika mapambano dhidi ya ujangili, mkiona mtu ananyemeleanyemelea huko porini tuambieni tutamshukia kama mwewe, hizi rasilimali na zetu sote” alisisitiza Prof. Maghembe.

Alisema changamoto ya ujangili bado ipo katika baadhi ya maeneo hapa nchini, alitaja maeneo hayo kuwa ni upande wa Pori la Rugwa na Selous karibu na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo watu huingiza mifugo hifadhini kwa kisingizio cha kutafuta malisho wakati huo huo wakifanya uhalifu wa kuua tembo.

Prof. Maghembe alifungua maadhimisho hayo pamoja na Maonesho ya Karibu Kusini na maonesho ya wajasiariamali wa viwanda vidogo SIDO yaliyoshirikisha wajasirimali kutoka mikoa ya nyanda zajuu kusini kwa lengo la kuonesha bidhaa zao zitakazoweza kutumiwa na watalii pamoja na watoa huduma hiyo. 

Akifungua maadhimisho hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Prof. Maghembe alisema, kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu kwa upande wa Siku ya Utalii Duniani ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo wakati ile ya Maonesho ya Karibu Kusini ikiwa ni “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.

Alisema sekta ya utalii imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi kwa kuchangia asilimia kubwa ya mapato ya Serikali, kuongeza ajira, kipato cha jamii na kuchochea ukuaji wa sekta zingine. 

"Utalii ndio ndio sekta pekee inayoongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa asilimia 25, Aidha, inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na asilimia 11 ya ajira zote nchini" alisema prof. Maghembe. 

Alisema mapato yanayotokana na utalii yameongezeka kutoka Dola za Kimarekani milioni 1,353.29 mwaka 2011 hadi Dola za Kimarekani milioni 2,131.57 mwaka 2016.

Alisema mchango huo umechagizwa na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi ambao waliongezeka kutoka 867,994 mwaka 2011 na kufikia 1,284,279 mwaka 2016.

Hata hivyo, alisema mafanikio hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za Serikali katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali, utangazaji, mazingira bora ya uwekezaji na ushirikiano madhubuti baina ya sekta ya umma na binafsi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani alisema Serikali imekusudua kuhakikisha kuwa utalii wa nyanda za juu kusini unakua juu zaidi uweze kutoa mchango stahiki kwenye pato la taifa. Alitoa wito kwa wananchi kutunza vivutio vya utalii vilivyopo, kuhifadhi mazingira na kupiga vita ujangili.

"Kwa upande wa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla natoa witoe washirikiane na Serikali kuweka mazingira bora na ya kuvutia katika maeneo yenye vivutio  vya utalii ikiwemo hoteli za kisasa kwa ajili kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutia hivyo" alisema Mhandisi Makani.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina masenza alisema katika kuunga mkono azma ya Serikali ya kukuza na kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini Serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na wadau wa utalii wameandaa Mpango Makakati wa kukuza sekta hiyo mkoani humo. Mpango huo umezinduliwa jana na Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe.

Kila mwaka nchi wanachama wa Shirika la Utalii Duniani huadhimisha Siku ya Utalii tarehe 27 Septemba kwa lengo la kuhanasisha umuhimu wa sekta hiyo katika kuleta maendeleo ya jamii, utamaduni, kukuza demokrasia, kutunza na kuhifadhi mazingira, kujenga uchumi na kuimarisha mahusiano ya kitaifa na kimataifa. Kilele cha Maadhimisho ni siku ya jumanne tarehe 2 Oktoba, 2017.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (katikati),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 2, Oktoba. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani akizungumza katika maadhimisho hayo mkoani Iringa jana.
Mkuu wa Wilaya ya Iirnga, Richard Kasesela akiratibu shughuli nzima ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mkakati wa Utalii wa Mkoa wa Iringa ambao umeandaliwa kwa lengo kuunga mkono azma ya Serikali wa kufungua utalii wa Nyanda za Juu Kusini katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Amina Masenza na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakionesha Mkakati wa Utalii na Jarida la Iringa baada ya uzinduzi rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akiwa na baadhi ya washiriki wengine kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya Machifu wa Iringa waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo.
 Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatila ufungunguzi wake.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini. Nyuma yao ni mabanda ya maonesho hayo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakielekea kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya Kichangani Mkoani Iringa jana.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akipimwa afya katika banda la MSD wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. KKauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni  “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto), akikagua bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa pili kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza moja ya bidhaa za wajasiriamali wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia). Kauli Mbiu za maadhimisho hayo yatakayofikia tamati tarehe 2 Oktoba ni “Utalii Endelevu” – Ni chombo cha maendeleo na “Utalii endelevu ni nguzo ya Uchumi wa Viwanda”.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akikagua kifaa maalum cha kuwashia umeme katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (kushoto). 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto),  Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) wakipata maelezo katika banda la Sido kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini yanayoendelea Mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto), akikagua gari maalum kwa ajili ya mafunzo katika banda la VETA wakati wa zoezi la kukagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. Wanaoshuhudia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatno kulia). 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia), Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kulia kwake) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza wakikagua vifaa vya mfumo wa umwagiliaji vilivyotengenezwa na VETA katika maadhimisho hayo.
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto), akisalimiana na Machifu wa Kabila la Wahehe katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani na Maonesho ya Karibu Kusini mkoani Iringa jana. 
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akionesha picha za nyayo za Zamadamu wa Laetoli na Engaresero zilizogundulika Ngorongoro mkoani Arusha takribani miaka milioni 3.6 iliyopita kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa muda mrefu.
Katika maadhimisho hayo kuna fursa za kuwaona wanyamaori mbalimbali ikiwemo Simba kama wanavyoonekana kwenye banda lao maalum. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, Oktoba 1, 2017

Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri
Makamu Mwenyekiti 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote duniani katika kuadhimisha siku ya wazee duniani. Wakati dunia inaadhimisha siku hii, Tume inatoa wito kwa jamii ya Watanzania kuondoa vitendo vyote vya unyanyasaji dhidi ya wazee ili kuhakikisha kuwa wanaishi katika kutekeleza kauli mbiu ya taifa inayosema “Kuelekea uchumi wa viwanda: Tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.

Uzee na kuzeeka havikwepeki; hivyo ustaarabu wa jamii au nchi yoyote duniani si wingi wa raslimali na mazingira mazuri bali katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya kulinda na kutetea haki za makundi maalum yanayohitaji ulinzi wa jamii husika. Kwa kulitambua hilo Desemba 14, 1990, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Azimio lake Na. 45/106 ulipitisha tarehe 01 Oktoba, ya kila mwaka kuwa siku ya wazee Duniani. Vipaumbele katika Azimio hilo ni pamoja na suala la uhuru wa wazee, wazee kushiriki na kushirikishwa katika shughuli za maendeleo, kutunzwa na kuheshimiwa.

Hivyo siku hii ya tarehe 01 Oktoba, dunia inawapa nafasi wazee kukutana pamoja na kubadilishana mawazo juu ya nini cha kufanya kuhusiana na mustakabali wa haki zao kwa ujumla, katika kuleta maendeleo ya Taifa tunapoelekea Tanzania ya viwanda.

Katika kutambua, kulinda kukuza na kutetea haki za wazee serikali imeridhia Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, yaani “The African Charter on Human and People’ Rights (ACHPR)” pamoja na Itifaki ya kusimamia haki za wazee ’’Protocol to the African Charter on Human and People’ Rights on the Rights of elder persons in Africa”.  Kadhalika kuna Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, yaani The International Convenant on Civil and Political Rights (ICCPR), na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, yaani The International Convenant on Economic, Social and Cultural Rights (ICESCR).

Kitaifa, kuna Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake ibara ya 12 (2) na ibara ya 14 ambazo zimeeleza juu ya wazee kupewa heshima na kupata hifadhi kutoka kwa jamii wanamoishi.

Aidha, kuna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo ni Idara huru ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 129 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, na Sheria Na. 7 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya mwaka 2001 ambayo ni kitovu cha kulinda, kutetea na kukuza haki za binadamu nchini.

Takwimu za wazee kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, Tanzania ilikuwa na wazee 1,952,041 (sawa na wanaume 940,229 na wanawake 1,011,812) na katika sensa ya mwaka 2012 idadi ya wazee iliongezeka hadi kufikia 2,507,568 (wanaume 1,200,210 na wanawake 1,307,358) sawa na 5.6% ya wananchi wote. Hivyo, kwa kadiri idadi ya wazee inavyoongezeka ndivyo changamoto zinazowakabili zinavyoongezeka. Hivyo jitihada mahsusi lazima zifanyike kukabiliana nazo.

Tume kama taasisi ya kitaifa yenye jukumu la kulinda, kukuza na kutetea haki za binadamu imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kuwa wazee wanapata haki zao. Jitihada hizo ni pamoja na:
i)      Kushughulikia malalamiko yanayohusu uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa wastaafu hasa katika suala linalohusu mapunjo na wastaafu kutolipwa stahiki zao kwa wakati.

ii)     Tume imekuwa ikitoa elimu ya haki za binadamu ikiwemo haki za wazee kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo taasisi za serikali, asasi za kiraia na wadau mbalimbali wa haki za binadamu na umma kwa ujumla.

iii)   Tume imeshiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga sheria ya wazee kwa kutoa maoni yanayohakikisha kuwa haki za wazee zinalindwa na kuhifadhiwa. Pia inashiriki katika mchakato wa mpango wa pensheni jamii.

iv)   Tume imetoa matamko mbalimbali kulaani mauaji ya wananchi wakiwemo wazee yanayotokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Tume inapongeza sana jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia masuala ya wazee. Jitihada hizo ni pamoja na:
i)        Kuimarisha Wizara inayoshughulikia masuala ya wazee kwa kutaja neno “wazee” katika jina la Wizara.

ii)       Kuimarisha huduma za afya kwa kuongeza bajeti ya Afya inayoiwezesha Serikali kununua dawa na vifaa tiba kwa wakati.

iii)      Kuweka madirisha ya wazee katika hospitali na vituo vya afya.

iv)     Kuanzisha mchakato wa mfuko wa Afya ya jamii.

v)       Kuanzisha mchakato wa malipo ya pensheni kwa wazee wote.

vi)     Kuanzisha mchakato wa kupambana na mauaji ya wazee.

vii)    Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanzisha mpango wa malipo ya pensheni jamii kwa wazee wenye umri  wa miaka 70+.

viii)   SMZ pia imo katika mchakato wa kutoa vitambulisho maalum kwa wazee vitakavyowawezesha kupata huduma mbalimbali.

ix)     SMZ imeimarisha huduma za wazee kwa kuanzisha idara ya wazee.

Pamoja na jitihada ambazo zimefanywa na Serikali, Tume, Asasi za Kiraia, Mikataba, Maazimio na Itifaki za kikanda na kimataifa, bado wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kimsingi huvunja haki. Changamoto hizo ni pamoja na:
i)     Ukosefu wa Sheria maalum inayoweka ulinzi na kuzitambua haki za wazee.

ii)    Wazee walio wengi kutofaidika na mafao mbalimbali ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Pensheni jamii) licha ya kwamba maendeleo yaliyofikiwa na nchi hii ni matokeo ya mchango wa wazee kwa kazi zao walizofanya.

iii)  Umaskini wa kipato miongoni mwa wazee.

iv)  Usalama mdogo kwa wazee kutokana na ukatili na manyanyaso wanayofanyiwa, hususani vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake, walemavu na mauaji ya wazee kutokana na imani potofu. Kwa mfano, takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani (2016) zinaonyesha kuwa wazee wameendelea kuuawa katika sehemu mbalimbali nchini. Kwa mfano, mwaka 2014 waliuawa wazee 557, mwaka  2015 wazee 190 na katika kipindi cha mwezi  Januari hadi Oktoba 2016 wazee 119 waliuawa. Mikoa  inayoongoza kwa mauaji  ya wazee kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2016 ni: Tabora (49), Shinyanga (17), Mbeya (15), Geita (11), Rukwa (9), Njombe (9) na Simiyu (7).

Kutokana na changamoto hizo, na ili kuhakikisha kuwa haki za wazee zinalindwa, zinadumishwa, zinakuzwa na kuendelezwa, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inatoa mapendekezo yafuatayo kwa Serikali, wadau na jamii kwa ujumla:
i)        Elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora itolewe kwa wananchi wote. Hii itasaidia katika kujenga jamii inayoheshimu haki za binadamu nchini.

ii)       Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikamilishe kutunga Sheria ya Wazee ili kurahisisha utekelezaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003.

iii)      Serikali iendelee kuboresha huduma za afya na zitolewe bure kwa wazee wote, ikiwa ni pamoja na kukamilisha mpango wa afya ya jamii.

iv)     Serikali ikamilishe mpango wa malipo ya pensheni jamii (Social Pension) kwa wazee wote.

v)       Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama ihakikishe panakuwepo ulinzi madhubuti kwa wazee ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahusika wa mauaji ya wazee na kuwafikisha katika vyombo vya dola kwa wakati na jamii ijitokeze kutoa ushahidi.

vi)     Kamati za ulinzi za Kata na Vijiji ziimarishwe ili kulinda maisha ya wazee.

vii)    Kupitia mkakati wa kunusuru kaya maskini unaosimamiwa na TASAF, kipaumbele kitolewe kwa wazee kote nchini.

viii)   Mabaraza ya wazee yaanzishwe na kuimarishwa ili kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa wazee katika maendeleo ya nchi.

Mwisho, Tume inatoa rai kwa Serikali na wananchi wote kwa ujumla kulinda na kutetea haki za wazee. Aidha, tuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa.

“Uzee na kuzeeka havikwepeki”

Imetolewa na: 
Iddi Ramadhani Mapuri
Makamu Mwenyekiti 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA 

Oktoba 1, 2017

BETTER HEALTH, WATER AND FOOD FOR TANZANIA WITH THE HELP OF NUCLEAR TECHNOLOGIES AND INTERNATIONAL PARTNERS

Science and technological innovations play a fundamental role in assisting African leaders to root causes of poverty, hunger and climate change. 

It is therefore no surprise that nuclear science and innovative nuclear technologies are playing a major role in providing viable solutions to help achieve these targets. It is well known globally that nuclear technologies have much to offer in the fight against poverty, hunger, dread diseases, and water shortages, not to mention its ability to provide sustainable and environmentally friendly electricity. 


Let’s take a closer look these various applications.

Nuclear medicine helps millions of people across the globe to successfully fight cancer and has reducedthe mortality rate of non-communicable diseases by one third. Moreover, nuclear science centers and research facilities are indispensable in the production of radioisotopes which are used in complex medical treatments. African countries have already made significant steps in nuclear science development under the guidance of the United Nation’s International Atomic Energy Authority (IAEA) and its key member states.

For example, in Zambia “people can access treatment locally for a fraction of the cost they would pay by travelling outside the country. More than 17,000 new cases of cancer have been diagnosed and treated over the last 10 years,” said MulapeKanduza, Chief medical physicist of the Cancer Diseases Hospital (CDH) in Lusaka.“Without the assistance of the IAEA, it would have been very difficult for us to set up a highly technical centre like this one and care for so many patients,” said Dr Lewis Banda, the CDH’s Senior Medical Superintendent.

IAEA provides training and seminars to improve cancer management across the globe.With the help of nuclear technologies Tanzanian doctors can now deliver more precise radiation treatment to patients with oncological diseases using modern scanning methods previously not available in the region. These new methods make it possible to treat more patients than before with more accuracy.

“We now have the skills to more fully understand the extent of a tumour and ultimately plan better and more precise treatment for our patients,” said Dr Mark Mseti, a radiation oncologist at the Ocean Road Cancer Institute in Dar es Salaam, which receives technical support and equipment through the IAEA. Previously, DrMseti participated in IAEA training on 3D planning for target volume definition and contouring for radiotherapy.

Another issue is water supply. As the population continues to grow rapidly in emerging countries, the availability of potable water remains one of the most pressing issues for the mankind. Innovativenuclear technologies can be used to desalinate ocean wateror to reducecontaminants in contaminated water, making it safe to use.

Water purification and desalination can be of huge benefit to Tanzania, where it is difficult for many people in arid regions to access clean water. Implementation of these technologies is of high importance for the East African country where nearly 23 million people don’t have full access to safe potable water. 

And there is a huge issue of food supply. For decades African nations have suffered the devastating consequences caused by the tsetse fly. According to the United Nations (UN) Food and Agriculture Organization the bloodsucking insect kills more than three million head of livestock in sub-Saharan Africa every year, resulting in more than US $4 billion in losses in region. With the help of nuclear technologies Tanzanian island of Zanzibar have already won the battle against the tsetse fly thanks to the nuclear based sterile insect technique (SIT).

Since the eradication of the tsetse fly in 2014 socio-economic studies have shown that the total number of all cattle breeds have increase by roughly 38%.Milk production has nearly doubled from 4.6 to 10 liters after the introduction of nuclear based techniques. Radiation has proved to be an effective solution for the eradication of many infectious insects on almost every continent on Earth. SIT has been applied to hundreds of species of fruit flies, moths, mosquitoes and screwworm flies.

And neighboring Zambia has drastically increased its maize and other crop varieties productivity using nuclear techniques to make them more resistant to external factors. Moreover, nuclear technologies not only made it possible to increase crop productivity but at the same time reduced negative environmental effects of other agricultural practices. Now Zambian farmers enjoy better harvests despite previous downfalls due to climate change and severe droughts.

It is worth noting that Zambia is well on the way of building its own multipurpose nuclear scientific center with the help of foreign partners like IAEA and Russian nuclear corporation Rosatom.Viktor Polikarpov, Rosatom Regional Vice President for Sub-Saharan Africa, notes: “Radiation treatment of food products is one of the various applications of the state-of-the-art radiation technologies offered by Rosatom to its foreign partners. Today about 515 radiation facilities created with the use of Russian technologies are in operation in 22 countries worldwide, including the UK, France, Germany, Finland, Japan, China, South Korea and India”.

DC WA KAKONKO KANALI NDAGALA APIGA MARUFUKU UNYANYASAJI KWA WAZEE,KUWATUHUMU WANAZUIA MVUA

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaagiza Wananchi wa Wilaya ya Kakonko kuacha tabia ya kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa Wanazuia Mvua na kutaka kuwaondoa ikiwa ni pamoja na kuwauwa kwa kwa imani za kishirikina , na vikundi vitakavyo gundulika vinawatuhumu watachukuliwa hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Akizungumza na Wananchi jana katika maadhimisho ya siku yaWazee Wilayani humo katika kijiji cha Kasanda ,Ndagala alisema kumekuwa na tabia ya Wananchi wengi kuwatuhumu baadhi ya wazee kuwa wanazuia mvua, jambo ambalo ni imani za kizamani na zilizopitwa na wakati.
 
 "Kwa hiyo mimi nawaomba tuendelee kushirikiana na wazee wetu hawa kwa kuwa pia wana mchango wao mkubwa katika jamii,ni vyema tukawafanya wazee wetu waishi kwa amani na kuachana na imani hizo zinazoweza kuleta chuki na uhasama mkubwa baina yetu",alisema Ndagala.

Alisema vitendo kama hivyo vilijitokeza mwaka jana, baadhi ya wazee walitaka kuuwawa kwa tuhuma hizo,aliema na kuongeza kuwa imani hizo zinapaswa kupuuzwa kwani zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani Kwa Wazee hao ambao ni hadhina kubwa kwa jamii. 
 
"Niwaombe wananchi mshirikiane na Wazee waliopo katika maeneo yenu, tumeona mchango wao ni mkubwa sana katika jamii na Taifa kwa ujumla Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni thamini mchango wa wazee kwa maendeleo ya Nchi yetu, na serikali inalitambua hilo ndio maana inatoa kipaumbele kwa Wazee kwa kuhakikisha wanakuwa na Afya njema kwa kupatiwa matibabu bure kutokana na mchango wao", alisema Ndagala.
 
Aidha Ndagala alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuandaa watumishi watakao kuwa wakishughulikia masuala ya Wazee na kuhakikisha jamii ina tambua na kuthamini mchango wa wazee na kuihamasisha jamii kutambua umuhimu wa wazee na kuihamasisha jamii kuwathamini wazee na kuwapenda kwa kuweka mipango shirikishi kwa wazee na jamii ilikuweka usawa kati yao.

Alieleza kuwa Serikali inaendelea kuwajali wazee kwa kutoa huduma ya afya bure,Wilaya imeamua kuwatambua wazee na kutoa huduma za Afya bure kwa wazee 1700 wamepatiwa vitambulisho vya msamaa vya matibabu vya muda na kumuagiza Mkurugenzi kuandaa utaratibu mzuri wa wazee kupatiwa vitambulisho vy a kudumu.

Nao Wazee hao katika risala yao iliyo wasilishwa na Mwenyekiti wa chama cha wazee Wilaya ya Kakonko Mbonipa Kisama, waliishukuru Serikali ya awamu ta tano kwa kutambua umuhimu wa wazee na kuwapa kipaumbele kwakuwapatia matibabu bure na kuiomba serikali kuanza kutoa petion jamii waliyo ahidiwa kwa muda mrefu kwa Wazee iliwaweze kufanya shughuli ndogo ndogo za kujikimu katika kipindi hicho na kuondolewa tozo za kijamii kwa wazee.

Alisema Wazee wanamahitaji yao ya ziada iliwaweze kuishi bila wasiwasi wilaya ina wazee 7103 ambapo wazee wanawake ni 3135 na wanaume ni 3975 ambao ni Wanachama wa chama cha Wazee ambapo kupitia chama hicho serikali imeweza kitumia Wadau kufanya sensa ya kuwatambua wazee na mahitaji yao na kuweza kutoa msaada kwa Wazee wasio jiweza.

Aidha Wazee hao waliyashukuru mashirika ya Help age international na shirika la TCRS kwa kutoa misaada kwa wazee wasio jiweza na kuomba kuendelezwa kwa misaada ya kisheria na haki za wazee kuishi na kutoa mchango wa huduma za kijamii kwa Wazee na wanaamini maombi waliyatoa serikali itatue changamoto hizo ilikuondokana na changamoto hizo.

Hata hivyo katika maadhimisho hayo yaliadhimishwa kwa Wazee kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, uvutaji wa kamba na ukimbizwaji wa kuku ambapo mshindi alikabidhiwa mbuzi na kiasi cha shilingi 20,000/= na Mkuu huyo kuomba michezo hiyo kwa wazee kuendelezwa katika kila kata ili kuimarisha Afya za wazee hao .
 Baadhi ya Wazee wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho hayo
 Mkuu Wawilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi zawadi ya Mbuzi kwa timu ya wazee wa kijiji cha Kasanda iliyofanya vizuri katika michezo wakati wa maadhimisho hayo ya Wazee.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabizi vitambulisho vya matibabu kwa baadhi ya wazee wilayani Kakonko.
 Baadhi ya wazee wakicheza ngoma katika maadhimisho ya siku ya wazee.