Wednesday, November 30, 2016

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL NAJEM ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE


Na Anna Nkinda - JKCI

Serikali ya Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine  na vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika katika chumba cha upasuaji.

Ahadi hiyo imetolewa leo na  Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem Al Najem alipotembelea  Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia ni  jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa  tiba.

Mhe. Balozi Al Najem alisema vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu vitapatikana kabla ya kumalizika  kwa mwaka huu ambapo vifaa  pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017.

“Serikali ya nchi yangu inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii pamoja na Taasisi zingine zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini ili watanzania waweze kupata huduma bora”, alisema Mhe. Balozi Al Najem.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi  alishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na mashine  zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa moyo.

“Tuna vyumba vitatu vya upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina vifaa, kupatikana kwa vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait kutatufanya tuwe na vyumba vya upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia  kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .

Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kutoa  zawadi kwa watoto waliolazwa.
Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili kuona namna gani nchi yake inaweza kusaidia vifaa tiba.

Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya mdoli Mtoto Furaha Mwechi ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ajili ya kuziba tundu la moyo na kufungua mshipa wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu. Mhe. Balozi Najem alitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia vifaa tiba.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Prof. Ayoub Magimba na Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.

Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait mara baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya katika Taasisi hiyo. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia Taasisi hiyo. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi. Picha na Anna Nkinda – JKCI.

SERIKALI KUFANYA MALIPO KWA MFUMO WA KIELEKRONIKI NCHINI

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

Wizara ya Fedha na Mipango imekamilisha ujenzi wa mfumo wa malipo moja kwa moja kupitia akaunti za walipwaji katika mtandao wa malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (Tanzania Interbank Settlement System – TISS), katika mkoa wa Morogoro, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa miamala mbalimbali inayofanywa na serikali

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amezitaja Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Mvomero, Kilosa na Ulanga, kwamba zitaanza kufanya malipo hayo kwa mfumo huo wa TISS kuanzia mwezi Desemba mwaka huu.

“Nia ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwezi Desemba, 2016 Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Morogoro ziweze kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa malipo wa TISS” alisema Dotto James.   

Amesema kuwa malipo hayo yatafanyika kwa kutumia mfumo wa malipo wa TISS uliojengwa katika mikoa yote Tanzania Bara ikiwemo Ofisi za Hazina Ndogo na Sekretariati za Mikoa, Wizara, Idara za Serikali zinazofanya malipo yake kupitia Ofisi Kuu ya Malipo (CPO) iliyopo Hazina, malipo ya Pensheni kwa wastaafu, Kitengo cha Kupambana na Fedha Haramu, Mfuko wa Bunge, Mfuko wa Mahakama na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

“Hivi karibuni mfumo huu wa malipo umeunganishwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mfumo huu umeunganishwa katika Halmashauri za Wilaya  ya Ukerewe, Magu, Sengerema, Kwimba, na Misungwi” alifafanua Katibu Mkuu huyo.

Ameongeza kuwa katika mkoa wa Mbeya, mfumo huo umefungwa katika Halmashauri ya jijini la Mbeya, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Kyela, Mbarali, Chunya, Mbeya, Mbozi na Ileje wakati mkoani Arusha maeneo yanayohusika ni  Halmashauri ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Longido, Meru, Monduli, Karatu, Ngorongoro.

Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma mfumo huu umeunganishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, na Kondoa wakati mkoani Tanga, Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Pangani, Muheza, Handeni, Kilindi, Korogwe, Lushoto na Mji wa Korogwe zimeunganishwa katika mfumo huo.

Kuanzia Julai, 2010 hadi katikati ya Mwezi Novemba, 2016 mfumo huu ulikuwa tayari umeunganishwa katika Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo katika Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Songwe, Arusha, Dodoma na Tanga ambapo umeonesha mafanikio makubwa” Alisema Bw. Dotto James.

Katibu Mkuu huyo amewataka wadau wote wanaofanya biashara na maeneo yaliyofungwa mfumo huo mkoani Morogoro, kuwasilisha taarifa muhimu ili ziweze kuingizwa katika Mtandao wa malipo wa Serikali [Intergrated Financial Management System (IFMS)] ili uanze kutumika kuanzia Mwezi Desemba mwaka huu kufanya malipo.

Taarifa hizo zinahitajika kwa kuwa ni muhimu ili kuwezesha malipo kufanyika kwa mlipwaji, ikiwa ni pamoja na Namba ya akaunti ya benki, Namba ya tawi la benki, Jina la akaunti, Aina ya akaunti, Namba ya kuandikishwa biashara, Namba ya kuandikishwa Kampuni, Namba ya Mlipakodi, Jina la benki na Jina la Tawi la benki.

“Hivyo Makampuni na watu wanaofanya biashara na  Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Halmashauri za Wilaya  ya Kilombero, Morogoro, Mvomero, Kilosa, na Ulanga wanashauriwa kuwasiliana na Halmashauri husika ili waweze kupatiwa fomu maalum za kujaza taarifa hizo muhimu” Alisisitiza Dotto James.

Amesema kuwa  zoezi hilo ni endelevu ambapo Serikali itaendelea kufunga mfumo huo kwenye mikoa na Wilaya zote zilizobaki upande wa Tanzania Bara. 

KIGOMA MJINI WAMPONGEZA LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YAO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi anaendelea na ziara ya siku tatu katika mkoa wa Kigoma ambapo amefungua rasmi Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoa wa Kigoma pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ya wananchi wa Kigoma. 

Wananchi hao wamempongeza Mhe. Waziri kwa hatua anazozichukua katika kumaliza migogoro yao ya ardhi na kuwajengea Baraza la Ardhi na Nyumba ambalo jipya na lililo na viwango kushinda mengine yote hapa nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akifungua Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma, Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe.Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
Jengo jipya la Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
Samani mpya za Baraza la Ardhi na Nyumba la Mkoani Kigoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi akiongea na wananchi wa Kigoma Mjini na kutatua migogoro yao ya ardhi.
Wananchi wa Kigoma Mjini wakiwasilisha malalamiko yao ya migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willim Lukuvi ili yaweze kutatuliwa.
wananchi wa Kigoma mjini wakimsikiliza Waziri wa Ardhi.

UN NA EU YAWANOA MABALOZI 50 WA MALENGO YA DUNIA IRINGA

UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini Tanzania. Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao, vijana 50 wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo hayo (Global Goals Champions). Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya Tanzania. 

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa
Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akimkabidhi cheti Rais wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa Athman Waziri aliyehitimu kuwa balozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champion).
Picha juu na chini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na zoezi la kutunuku vyeti kwa mabalozi wa malengo ya dunia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champions) baada ya kuhitimisha semina maalum iliyoshirikisha vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU), Muazarau Matola
Baadhi ya Global Goals Champions katika picha ya kumbukumbu na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Mkufunzi wa Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na wahitimu wa semina malengo ya dunia (Global Goals Champions) mara baada ya kuhitimisha semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa ambapo imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).

MAGAZETI YA LEO JUMATANO,NOV 30