Monday, October 31, 2016

WAZEE WILAYA YA ARUSHA WAMUOMBA RASI MAGUFULI NAFASI MOJA YA UWAKILISHI BUNGENI KATIKA NAFASI ZAKE KUMI



MKUU wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro, amemugiza afisa Usitawi wa Jamii wa halmashauri ya jiji la  Arusha kuhakikisha wazee wote wa jiji hilo wanapatiwa vitambulisho kabla ya mwisho wa mwaka huu ili waweze kupata huduma mbalimbali ikiwemo matibabu mahospitalini.

Mhe. Daqaro ametoa agizo hilo kwenye mkutano na wazee wa jiji la Arusha uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa (AICC), ulikuwa una lengo la kusikiliza kero zao ili zipatiwe ufumbuzi na pia kufahamiana.

Mkuu huyo wa wilaya ameiagiza Idara hiyo kuhakikisha vitambulisho vinapatikana kabla ya mwisho wa mwezi ujao, sanjari na kuwataka watendaji wa serikali, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali za serikali katika jiji la Arusha kuhakikisha kuwa zinatoa kipaumbele kwa wazee ambao wamekuwa hawapati huduma zao kwa wakati.

Aidha amewataka wenyeviti wa mitaa,kata na tarafa kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha wanaimarisha usalama kwenye maeneo yao ili kuwezesha wazee kuishi kwa usalama bila kubughudhiwa na kuhakikisha wanasimamia maadili.

‘’Mumepewa madaraka ya kuimarisha ulinzi. Yatumieni ili wazee wasibughudhiwe...Tambueni kuwa wazee ni watu muhimu na ndio waliotufikisha hapa. Sasa sitaki kusikia kuwa wanasumbuliwa... sitaki kusikia malalamiko  ya kuporomoka kwa maadili ””alisema Daqarrro.
Wakichangia  kwenye mkutano huo wazee wamedai kuwa taasisi za fedha pamoja na halmashauri ya jiji haziko tayari kuwakopesha wazee kwa hofu ya kuwa watakufa karibuni na  kutaka dhana hiyo iondoke kwa kuwa kuzeeka sio kufa .

Wamesema nao wana mahitaji mbalimbali ya kuendesha sghuhuli zao za kiuchumi hivyo wanayo haki ya kupewa mikopo kama yalivyo makundi mengine ya jamii.

Wazee hao pia ameomba kushirikishwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi halmashauri ili wawe na wawakilishi wao ambao watawasilisha kero zao kwenye vikao vya maamuzi vya serikali na baraza la madiwani. Pia wameomba wapate uwakilishi bungeni kama yalivyo makundi mengine ya walemavu, vijana na wanawake.

Wamelalamikia kukosa Vitambulisho ambavyo vingeliwawezesha kupata huduma za haraka kwenye taasisi mbalimbali za serikali,ikiwemo dawa kwenye hospital za serikali, pia wamelalamikia lugha za kuwadharirisha zinazotolewa na baadhi ya wahudumu wa hospital za serikali na vituo vya afya.Wamelalamikia hatua ya Zahanati kutokutoa huduma siku za mwisho wa wiki hali ambayo inawasababisha kukosa huduma za matibabu.Aidha wamelalamikia TASAF kutoa fedha kwa ajili ya watu wasiokuwa na uwezo kwa upendeleo ambapo walengwa wamekuwa hawanufaiki na mpango huo wa TASAF.


Katikati Ni mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha Bw. David Mwaiposa na kushoto ni mwenyekiti wa baraza la wazee wilaya Arusha Mzee Mhina Sezua wakati wa mkutano na mkuu huyo wa wilaya kubaini changamto mbali mbali wanazokumbana nazo wazee wilayani hapa

Meza kuu wakifuatilia hoja mbali mbali zilizokuwa zinatolewa na wazee leo jijini Arusha

Sehemu ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya Gabriel Daqarro

Katibu wa wazee akiongea katika mkutano huo

WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KWENYE KIKAO HICHO

Katibu Tawala wilaya ya Arusha David Mwaiposa akiwa anamkaribisha mkuu wa wilaya kuongea na wazee ilikujua kero zinazowakabili

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea na wazee wa jiji la Arusha ambao wamemuomba mkuu huyo kuwafikishia salamu zao kwa viongozi wakuu wa serikali akiwemo raisi dkta John Magufuli kuwa wakifika Arusha waweze kuonana na baraza la wazee kama wanavyoonana na wazee wa Dar es salaam

Mwakilishi wa OCD nae akijibu maswali ambali mbali kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha

Mwenyekiti wa baraza la Wazee wilaya ya Arusha mjini Mhina Sezue akiongea katika mkutano huo ambao aliiomba serikali wilayani hapa kuwapa uwakilishi wazee kwenye mabaraza ya serikali kuanzia ngazi ya kijiji kata hadi Taifa huku wakimuomba raisi kuwapa nafasi moja katika zile kumi za uwakilishi wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Hata sisi hatupo nyuma kama walivyokutwa na kamera wakiingia ndani ya ukumbi wa Simba kwenye kituo cha mikutano cha AICC Leo Jijini Arusha

WAZEE HAWA NAO WALIKUWEPO KATIKA KUTOA MICHANGO YAO YA MAWAZO KUBORESHA HUDUMA ZAO

wakifuatilia mkutano huo kwa umakini

Bibi akifuatilia mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Arusha na wazee wa jiji la Arusha leo jijini Arusha

Sehemu ya wakifuatilia mkutano huo

Mandari ya muitikio wa wazee kwenye mkutano huo wakiwa katika ukumbi wa simba hall

wazee wakifuatilia mkutano huo kwa umakini na kueleza kero mbali mbali kwa mkuu wa wilaya ya Arusha

WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KAMA HAPA WAKIFUTILIA MKUTANO HUO. Picha zote na Mahmoud Ahmad,Arusha





DK. SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA NCHI OFISI YA RAIS,TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakati wa kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud akisoma kazi za Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ ACP Sida Muhamed Himid na (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija,[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika kikao cha robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.
Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Mhe,Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,akiuliza suala wakati wa kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 cha Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti weke Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Balozi Seif Ali Iddi,na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd, Radhiya Rashid [Picha na Ikulu] 31/10/2016.
Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakiwa katika mkutano wa siku moja unaozungumzia Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Mhe,Mwinyiussi Abdalla Hassan (kushoto) akisisitiza jambo wakati akiwa na Wakuu wa Wilaya nyengine katika mkutano wa siku moja unaozungumzia Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 31/10 /2016.

MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHANDISI MATHEW MTIGUMWE AKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA PAMBA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa wa Singida.
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa pamba Mkoa wa Singida
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Choro Tarimo akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo
 Moja ya wakulima wa Kilimo cha pamba Wilayani Ikungi Timoth S. Nkulu akimuomba Mkuu wa Wilaya kuzisimamia Wilaya zote kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uzalishaji wa kilimo hicho.
 Wadau wa kilimo cha pamba wakihakiki maazimio waliyoyapitisha

Na Mathias Canal, Singida

Zao la Pamba ni miongoni mwa mazao ya kipaombele ya biashara yanayozaliswa Mkoani Singida kwa kuwa linastahimili hali ya hewa ya Mkoa ya uwepo wa mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo ambapo kutokana na hali hiyo Mkoa unaendelea kuhimiza wakulima kuzalisha zao hilo kwa kiasi kikubwa ili waweze kuongeza kipato na usalama wa chakula.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati akifungua Mkutano huo iliokuwa na dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa huo.

Mhe Mtigumwe amesema kuwa Katika Mkoa wa Singida Kampuni ya Biosustain Ltd inayojishughulisha na Kilimo cha Mkataba imeweza kusaidia zao la Pamba kwa kuanzisha kiwanda cha kuchambua Pamba chenye uwezo wa kuchambua Tani 16,000 kwa mwaka ambapo kupitia kilimo cha mkataba wakulima wa Mkoa wa Singida wamepata pembejeo, Mafunzo ya kilimo bora na soko la uhakika ambapo katika utekelezaji wa kilimo cha mkataba msimu wa mwaka 2015/2016 wakulima 4,204 wamepatiwa mafunzo.

Kwa msimu huu wa Mwaka 2016/2017 Mkoa umepata mgao wa mbegu za Pamba kutoka Bodi ya Pamba jumla ya Tani 120 (Wilaya ya Iramba na Mkalama Tani 80, Wilaya ya Manyoni Tani20 na Wilaya Ikungi na Singida Tano 20) ambazo zinaendelea kusambazwa kwa wakulima.

Imeelezwa kuwa zao la Pamba linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tija ndogo katika uzalishaji (200 kg/ekari) kutokana na wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo cha pamba, matumizi ya viuatilifu ambavyo havina uwezo wa kudhibiti wadudu waharibifu wa zao la pamba (Feki), Matumizi ya mbegu zisizoota vizuri (Feki), Kubadilika kwa bei ya pamba mwaka hadi mwaka, Mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo kwa mfano maeneo ya Bonde la Ufa ya Iramba, Mkalama na Manyoni.

Rc Mtigumwe amesema kuwa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba ni fursa nzuri ya kuwakutanisha wadau muhimu wa zao la pamba na kujadiliana mafaniko, Changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kufanikisha kuongeza kwa tija na faida katika uzalishaji wa zao la pamba.
Ameeleza malengo ya kimkoa kulima zao hilo kwa kiwango  kikubwa cha Hekta 8,510 kwa Mwaka 2016/2017 na matarajio ni kuzalisha Tani 8,075.

Katika Mkutano huo kwa umoja wao wadau wa kilimo cha Pamba wamepitisha maazimio 17 kama ifuatavyo:

  1. Wataalamu wa kilimo wa ofisi ya mkuu wa Mkoa na halmashauri za wilaya  watafute ufafanuzi wa deni kwakushilikiana na Biosustain kumpatia Katibu Tawala wa Mkoa ndani ya mwezi mmoja.
  1. Katibu Tawala wa Mkoa awaandikie barua uongozi wa Kampuni ya Quton kuitwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuja kutoa maelezo kwanini hawahudhurii vikao na walete ufafanuzi wa deni wanalodaiwa na namna ya kulilipa.
  1. Halmashauri ya Wilaya ya Singida inatakiwa ilejeshe fedha za ushuru  wa Pamba  kwa halmashauri ya Ikungi iliyolipwa kwao kwa makosa ndani ya miezi sita (6). 
  1. Elimu juu ya Matumizi ya mizani iendelee kutolewa ili kuongeza uelewa na ufanisi kwa wakulima.
  1. Kila halmashauri itoe taarifa ya maendeleo ya zao la Pamba kwenye eneo lake kwenye vikao vya wadau wa Pamba.
  1. Bodi ya Pamba ilete wakaguzi wa Pamba wasiopungua  wawili kwa Mkoa wa Singida ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.
  1. Wakurugenzi wapitie na wasimamie mikataba inayoingiwa kati ya Makampuni na wakulima ili kuepuka malalamiko yasiyo yalazima wakati wa utekelezaji.
  1. CDTF wawe ni wajumbe kwenye kikao hiki  na waalikwe kuanzia kikao kijacho ili watoe mchango wao kwa maendeleo ya Pamba katika Mkoa wa Singida.
9)      Bodi ya Pamba iangalie uwezekano wa kuwahusisha watafiti watoe mbegu bora inayostahimili ukame na kutoa mazao mengi.

10)   Katibu Tawala wa Mkoa aiandikie Wizara ya Kilimo kuikumbusha kuimarisha udhibiti wa ubora wa viuatilifu.

11)   Wakurugenzi wa halmashauri, Bodi ya Pamba na kampuni ya Biosustain waendelee kutoa Elimu stahiki ili kukuza uzalishaji wa Pamba.

12)   Kila kaya lazima ilime ekari mbili za Pamba ili tupate Pamba yakutosha kuanzisha kiwanda cha nguo. 

13)   Kila shule ya msingi na sekondari lazima iwe na ekari mbili (2) za zao la Pamba ili zitumike kama shamba darasa kwa wanafunzi na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani. 

14)   Wakurugenzi wahakikishe vitabu vya mwongozo wa kilimo na mifugo vinapatikana na kuwafikia wakulima, kila kijiji kipate nakala tano (5) kabla ya Januari, 2017.

      15) Jalada la usajili lenye orodha ya wakulima na ekari zao kiujumla na mazao wanayoyalima     kuanzia ngazi ya Kitongoji, Kijiji, Kata na Wilaya lifunguliwe na lianze kutumika kuanzia msimu wa 2016/2017.

      16) Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote ziwe na mashamba darasa ya kilimo cha Pamba.

17) Katibu Tawala Mkoa amwandikie katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo kujua matokeo ya uchunguzi   uliofanywa na TPRI wa Viuatilifu ambavyo havikufanya kazi msimu wa 2015/2016 na hatua zilizochukuliwa.


Wakiwasilisha taarifa ya Kilimo cha zao la Pamba kwa mkataba wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Singida kwa pamoja wamesema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi zilizosababisha kupata mavuno machache ya kilimo hicho ikiwemo ubora hafifu wa uzalishaji wa uzalishaji hivyo wameeleza mikakati katika kutimiza malengo waliyojiwekea kwa Mwaka 2016/2017 kuwa ni pamoja na Usimamizi wa karibu wa maafisa ugani, Kusimamia kwa karibu zoezi la ugawaji wa mbegu za pamba, kufanya ziara za hamasa katika maeneo ya wakulima wa zao la Pamba, Kuhamasisha wakulima wengi kulima zao la pamba na kuongezwa vituo vya ununuzi wa pamba.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Suingida Mhe Elias Choro Tarimo amesema kuwa ili kukabiliana na uzalishaji duni wa zao la pamba ni vyema watafiti wakaanza mapema kufanya utafiti juu ya mbegu bora za pamba zenye uwezo wa kuhimili ukame.

Tarimo Amependekeza Kampuni zote zinazoingia mikataba ya kusambaza dawa za pamba na kusambaza dawa feki wafutwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ili kudhibiti dawa feki.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amependekeza kila Halmashauri Kupitia upya ukubwa wa uzalishaji wa kilimo cha pamba ili kuwa na malengo ya kuzalisha zaidi tofauti na mapendekezo yaliyotolewa na Wakurugenzi wa Halmashauri kwani bado yapo kwenye kiwango cha chini cha uzalishaji.

Atoa taarifa ya Kampuni ya BIOSUSTAIN alisema kuwa kampuni hiyo imejipanga kulifanya zao la pamba kuwa zao muhimu kwa wakulima wa mkoa wa Singida kwa msimu wa mwaka 2016/2017 kwa kutoa elimu na kuongeza uzalishaji kutoka kilo 300 hadi kilo 600.

Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni hiyo ni kuanzisha kiwanda cha nguo endapo kutakuwa na uzalishaji Mkubwa.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI NCHINI KENYA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS UHURU KENYATTA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Kenya.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyeji wake, Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta, alipowasili Ikulu ya Kenya, Jijini Nairobi leo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Rais wa Kenya, Mh. Willam Ruto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya kaburi la Muasisi na Rais wa Kwanza wa Kenya Maremu Mzee Jomo Kenyatta mara baada ya kuweka shada la maua katika eneo la katikati ya jiji la Nairobi nchini Kenya mara baada ya kuwasili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati wa dua katika eneo la kaburi hilo la Muasisi na Rais wa Kwanza wa Kenya Maremu Mzee Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikiwa zinapigwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima aliloandaliwa na Jeshi la Kenya mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na ujumbe wake katika Ikulu ya Nairobi.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mbalimbali wa Kenya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya. PICHA NA IKULU.