Friday, July 31, 2015

VIJANA WAJASILIAMALI ZAIDI YA 650 WAKWAMLIWA KIUCHUMI NA AIRTEL FURSA

 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akiwakaribisha wageni katika semina ya kuhamasisha makampuni mbalimbli  kukabiriana na ukosefu wa ajira hapa nchini ili kumwezesha kijana mjasiliamali kujikwamua kiuchumi katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
 Wageni kutoka makampuni mbalimbali wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna katika mkutano wa ajira kwa vijana wajasiliamali wanaothubutu kujikwamua kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Meneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi kampuni la airtel  hapa nchini linavyoendelea kukomboa vijana wajasiliamali wanathubutu kujikwamua kiuchumi hasa kwa kutumia Aitel Fursa inayoendelea kuwawezesha vijana wengi hapa nchini wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ikiwa Aitel fursa imeshasaidia vijana wajasiliamali zaidi ya 650 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ikiwa inaendelea kwa mikoa mingine hapa nchini.katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikilizaMeneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi AIRTEL FURSA ilivyokwamua changamoto mbalimbali kwa vijana wajasiliamali hapa nchini waliokua na malengo ya kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa vifaa pamoja na kuwasaidia kimasoko.
 Mwenyekiti wa kampuni ya  Roots and Shoot, Ray Kiliho akichangia maada katika mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks baada ya mtoa maada kutoka kampuni ya simu za mkononi Airtel Hawa Bayuni kuhusiana na changamoto zinazomkuta kijana mjasiliamali wakati wa kuendeleza biashara yake, katika mkutano uliofanyika katika hoteli hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Solution Bloks, Msomisi Mbenna akiuliza swali kwa Meneja huduma za jamii wa Airtel  hapa nchini ,Hawa Bayuni katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa kampuni ya Popular lines, Neserian Alexander akichangia maada mara baada ya mtoa maada kumaliza kuelezea jinsi Airtel Fursa inavyoendelea kukwamua vijana kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa hoteli ya Colossem, Tanya Visser akitoa zawadi kwa washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks uiofanyika jana jijini Dar es Salaam. 




Washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks  wakiwasikiliza watoa maada kutoka Airtel  na kampuni ya Solution Blocks  katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

RAIS YOWERI MUSEVEN AFUNGUA MKUTANO WA MARAIS WASTAAFU KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR

????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda akifungua rasmi mkutano wa Marais wastaafu wa Afrka AFRICA LEADERSHIP FORUM unaofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Mkutano huo unaojumuisha marais wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania , Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Festus Mogaye wa Botswana, Bakili Muluzi wa Malawi na Jerry Rowlings wa Ghana unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika bara la Afrika na Changamoto zinazokabili barahilo na umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
????????????????????????????????????
Marais wastaafu Bakili Muluzi wa Malawi kulia na Jerry Rawlings wa Ghana wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kushoto na Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu Mstaafu wa AU na Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki KuuProf. Beno Ndulu wa tatu kutoka kulia na wageni mbalimbali wakihudhuria katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Marais wastaafu kutoka kushoto ni Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia,Benjamin Mkapa wa Tanzania na Festus Mogaye wa Botswana wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin Mkapa akitoa mada katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda kulia akiwa katika mkutano huo pamoja na marais wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu wa Nigeria Mh. Olusegun Obasanjo.

KIDOTI :VIJANA WA JIJI LA ARUSHA CHANGAMKIENI FURSA ZA KIJASIRIAMALI



 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo  (kidoti) akiwa na mabalozi wake aliwapata ndani ya mkoa wa Arusha tayari kwa kwenda mtaani kutangaza bidhaa zake zake za kidoti zilizoingia jijini Arusha kwa mara ya kwanza 



 warembo wa Kidoti wakiwa wako katika pozi wameshikilia baadhi ya bidhaa za Kidoti 


 mmoja wa mabalozi wa kidoti  aliyejulikana kwa jina la Anolia Agustino akiwa anaongea na waandishi wa habari


 Meneja masoko wa kampuni ya kidoti Peter Kasija akiwa anaongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya triple A hii leo wakati walivyokuja jijini Arusha kutangaza bidhaa za kampuni yao
 mabalozi wa kidoti   wakiwa kazini
 baadhi ya bidhaa zinazosambazwa nakidoti jijini Arusha
 hizi ndizo ndala za kidoti
 mawigi ya kidoti ndio haya


Na Woinde Shizza 
wa libeneke la kaskazini blog

Wito umetolewa kwa vijana ndani ya jiji la Arusha kujitokeza katika
kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza
kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya
jamii kukosaa thamani.
Wito huo umetolewa na Joketi Mwigelwa (kidoti) wakati akichagua vijana
wajasiriamali ndani ya jiji la Arusha katika ukumbi wa triple A jijini
hapa ambapo anatarajia kuwapata wajasiriamali vijana ambao
hatawaingiza katika fursa ya wajasiriamali kwa kupitia kampuni yake ya
kidoti.

Alisema  kuwa amevutiwa  kuja kuwekeza ndani ya jiji la Arusha  katika
nyanza za ujasiriamali kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Arusha
hususa ni wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la
ujasiriamali na maendeleo binafsi.



Aidha alibainisha kuwa katika  mchakato huo wanatarajia kupata
wajasiriamali wapatao 13 ambapo tofauti na kujiingizia kipato cha
ujasiriamali pia watakuwa mabalozi wa kutangaza bidhaa zilizo chini ya
kampuni ya kidoti.
“ndugu mwandishi unavyowaona hawa wote hapa ni vijana kutoka mkoa
mzima wa arusha na mikoa ya jirani tunawafanyia usaili na kupata
vijana ambao wanakithi vigezo vya kuingia katika ujasiriamali ,utakao
wapelekea wao kufanya kazi na kampuni ya kidoti pamoja na kujiajiri
binafsi” alisema kidoti

Pamoja na hayo alisema kuwa kampuni hiyo kwa mwaka huu imeamua
makusudi kusogeza huduma za  ikiwemo bidhaa zake katika mikoa ya nje
ya jiji la Dar Es Salaam ili kuwapa furusa watu wa mikoani ambao
walikuwa hawazipati huduma za kidoti.

Kwa upande wa mmoja wa washiriki waliojitokeza katika mchujo huo
Anolia Agustino  alimpomgeza kidoti kwa hatuqa aliofikia ya kuwaajiri
vijana haswa wasiochana kwani   ,jambo hili litawasaidia wanasichana
wengi kupata ajira pamoja na kujiajiri binafsi.

Aidha alisema kuwa  mbali na kupata ajira pia kampuni hii itawasidia
kujifunza ujasiriamali pamoja na kujiajiri binafsi kwani ,bidhaa za
kidoti ni za bei na fuuu na unaweza kuanza kujiajiri kwa kutumia mtaji
mdogo.
Kwa upande wa mshiriki mungine ambaye teari alikuwa amenufaika na
kampuni ya kidoti aliyejitaja kwa jina la Anjela Mushi alisema kuwa
kampuni hii imemsaidia sana kwani alikuwa anakaa nyumbani bila kazi
lakini alivyoona kwenye mtandao wa kijamii aliamua kujitafuta
mawasiliano na kuanza  na mtaji mdogo na kwasasa ivi mtaji wake
umekuwa.

“mimi nilianza kuona bidhaa za kidoti katika mitandao ya kijamii kama
intagramu  nikaamua kutafuta mawasilano kwakeli nilipata na nilikuwa
na mtaji mdogo kwani nilianza na mtaji wa shilingi laki moja na sasa
na shilingi laki nne na biashara yangu nilianza mwezi wa tano na sasa
ni mwezi wa saba  kwa hadi sasa nina mienzi mitatu nashukuru mungu
mtaji wangu umekuwa”alisema Anjela.
Alimalizia kw akumpongeza kidoti na kumsihi aendelee kuwasaidia
wasichana kwani hivi sasa kumekuwa na changamoto ya ajira kwani ajira
imekuwa ni ngumu.

Simu TV - Habari mbalimbali kutoka vituo vya Luninga.

SIMUtv: Watuhumiwa 25 wa kesi ya ugaidi wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kujibu mashtaka huku wakisindikizwa na ulinzi mkali. http://youtu.be/yDBpF3JAsQs
SIMUtv: Mkuu wa mkoa wa Dodoma awataka viongozi kuwajibika ipasavyo katika mradi wa ujenzi wa bwawa katika bonde la Farkwa.  http://youtu.be/ASbycQxK4ZI
SIMUtv: Taasisi isiyokua ya kiserikali inayojihusisha na utafiti wa teknolojia yawakutanisha watafiti kutoka vyuo vikuu mbalmbali nchini kujadili tafiti za maendeleo. http://youtu.be/xHMLVg_3cbc
SIMUtv: Baadhi ya wafanya biashara mjini Moshi waiomba taasisi ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na Kusini kuwasaidia kupata mikopo ya bei nafuuhttp://youtu.be/93qKcHdZFq4
SIMUtv: Shirika la madini la taifa STAMICO lasema mapato yake yatokanayo na uwekezaji kupitia kampuni zake tanzu umepanda kutoka Mil 282 hadi Bil3.http://youtu.be/IujLu1dAVM8
SIMUtv: Serikali yasema mfumo wa soko la bidhaa unaotarajiwa kuanza hapa nchini hivi karibuni utawasaidia wakulima kutatua changamoto za masoko.http://youtu.be/jQ-54JNkLDo
SIMUtv: Tume ya taifa ya uchaguzi NEC yaongeza siku nne katika zoezi hilo ambalo liligubikwa na changamoto nyingi zilizozuia maendeleo ya tukio hilo.http://youtu.be/Ao4DNolup5I
SIMUtv: Mkurugenzi wa elimu ya walipa kodi awataka wanasheria nchini kuijua kwa ndani sheria mpya ya kodi la ongezeko la thamani VAT.http://youtu.be/xmLN5LG3FnM
SIMUtv: Michuano ya KAGAME yaendelea kuelekea hatua ya nusu fainali timu nne zilizobaki zitaanza mtanange huo kesho huku Azam ikitarajiwa kupeperusha bendera. http://youtu.be/ju1ktyCfDOA
SIMUtv: Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu awataka viongozi wa vyama vya mbalimbali kuweka kando maswala ya kisiasa katika utekelezaji. http://youtu.be/7zR00wxX204
SIMUtv: Bondia Thomas Mashali atamba kumpiga mpinzani wake Ibrahim Tamba kwa knockout katika pambano lisilokua la ubingwa litakalofanyika agosti 29. http://youtu.be/SUCD3DdJBmo
SIMUtv: Makamu wa rais DK Maalim Bilal aisindikizwa na DK John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kutoka kia hadi mererani. http://youtu.be/V243ieYYQdc
SIMUtv: Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amekuwa mtu wa kwanza kuchukua fomu mapema leo ya kuwania Urais kupitia tiketi ya CHADEMA. http://youtu.be/zUiJH3PAHoA
SIMUtv: Mfanyabiashara mmoja afikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji baada ya kuwaua wenzake wawili kutokana na kutoelewana kibiashara Mkoani Mwanza.  http://youtu.be/SPv3ggaPDSc
SIMUtv: Tume ya taifa ya uchaguzi yaongeza siku nne katika zoezi hilo ambalo liligubikwa na changamoto nyingi zilizozuia maendeleo ya tukio hilo. http://youtu.be/D61rsC2BEHk
SIMUtv: Uongozi ulioko sasa barani Afrika waelezwa kua ndio changamoto kuu inayokwaza utangamano kamili wa bara la Afrika.http://youtu.be/5T8g4pR57Yo
SIMUtv: Idara ya uhamiaji nchini yatoa onyo kwa watu wasio watanzania na wanajiandikisha  kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2015 kuacha tabia hiyo. http://youtu.be/2EDZK5dZMqc
SIMUtv: Idara ya uhamiaji yatoa onyo kwa watu wasio watanzania na wanajiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu2015 kuacha http://youtu.be/2EDZK5dZMqc
SIMUtv: Waziri wa zamani Edward Lowassa asema kamwe hatayumbishwa na maneno ya watu kuhusu kuihama CCM wakati  akichukua fomu Leo.http://youtu.be/udp89ECsU8A
SIMUtv: Idara ya uhamiaji imebaini kuwa raia wa kigeni zaidi ya 2048 wamejiandikisha katika daftari la wapiga kura kinyume na sheria.http://youtu.be/tI_0okUoA70
SIMUtv: Baadhi ya Wagombea nafasi za Ubunge Jimbo la Nzega walalamikia kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi yao wanaotaka kushinda katika kura za maoni. http://youtu.be/XbNRNCdZThQ
SIMUtv: Wanafunzi wa vyuo Vikuu wamesema wataendelea kuwa watiifu wa chama cha CCM licha ya Mkongwe Edward Lowassa kukihama.http://youtu.be/1lq1iOM5awA

Thursday, July 30, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo.
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
  Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
  Magufuli, akikabidhiwa fimbo ya heshima ya kabila la Kimasai.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwashukuru wananchi wa zawadi ya vazi la Kimasai, baada ya kuvishwa wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR

Wednesday, July 29, 2015

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa  msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho. 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
PICHA NA IKULU.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Sehemu ya umati wa wanachuo na wageni waalikwaa waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle .
  Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Kikwete akimpongeza Bi. Bernadette Mathias ambaye kwa kushirikiana na mpiga piano mumewe Profesa Philip Mathias walitumbuiza kwa wimbo wa "Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote" kwa ufasaha na kusisimua waliohudhuria sherehe za Rais Jakaya Mrisho Kikwete kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle
 Rais Kikwete na msafara wa wanachuo wakiondoka jukwaa kuu huku wakishangiliwa na waliohudhuria ikiwa ni pamoja na Mama Salma Kikwete na mwana wao Ali Kikwete na ujumbe wa Rais Kikwete kwenye msafara huo.
 Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania na Waganda waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete akipongezwa na raia wa Burundi waishio Australia baada ya kutunukiwa shahada.