Thursday, February 27, 2014

Mhe. Membe alipokutana na Makamu wa Rais wa China mjini Beijing

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao alipokutana nae kwa mazungumzo kwenye Jumba la Mikutano la Kitaifa la China maarufu kama People's Great Hall mjini Beijing, China. Mhe. Membe yupo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 24 hadi 28 Februari, 2014.
Mhe. Membe na Mhe. Yuanchao wakiendelea na mazungumzo.
Mhe. Membe akiagana na Mhe. Yuanchao mara baada ya mazungumzo yao.

....Mhe. Membe alipokutana na Makamu Waziri wa Usalama wa Raia wa China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Wang Hanning, Makamu Waziri wa Usalama wa Raia wa Jamhuri ya Watu wa China alipokutana nae mjini Beijing wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Membe nchini China tarehe 26 Februari, 2014.
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Hanning huku Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Abdulrahman Shimbo (kulia kwa Mhe. Membe) na wajumbe waliofuatana na Mhe. Hanning wakisikiliza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Li Jinzao, Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China kabla ya kufanya mazungumzo rasmi na Waziri huyo wakati wa ziara yake nchini China.
Mhe. Membe (kulia) na Ujumbe wake wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na Mhe. Jinzao (kushoto) na ujumbe wake.

President Kikwete attends last protocol proceedings for the late Chancellor of the University of Dar es salaam

 President Jakaya Mrisho Kikwete is received by the Vice Chancellor of the University of Dar es salaam Professor Rwekaza Mukandara as he joins UDSM's Last Protocal Proceedings for the late Chancellor of the university Ambassador Fulgence Kamuzora held today at the Mlimani campuse's Nkrumah hall in Dar es salaam
 The ever present media was there to record the sombre event
 Former Prime Minister Hon Frederick Sumaye and the Minister for Education and Vocational Training Dr Shukuru Kawambwa 
 President Kikwete sandwiched by the Vice President Dr Mohamed Ghalib Bilali and the UDSM Vice Chancellor Prof Rwekaza Mukandala
 CCM Secretary General Ndugu Abdulrahman Kinana sits with UDSM dons
 Chief Secretary Omebni Sefue (right) and Dar es salaam Regional Commissioner Hon Said Meck Sadick
 The bereaved family members
 Former Prime Minister Judge Joseph Sinde Warioba reads his eulogy 
 A bird's eye view of the Nkrumah hall during the proceedings
 UDSM members and other mourners
 Dons and other members of the academia
 The guest list reads like the who-is-who in the academia
 Sombre mood everywhere
 Members of the academia follow closely the Last Protocal Proceedings
 Members of the bereaved family
  Members of the bereaved family
  Members of the bereaved family
 The ever busy Nkrumah hall during the proceedings  President Kikkwete, Vice President Dr Mohamed Ghalib Bilali with other VIPs

 President Kikwete consoles members of the bereaved family
 President Kikwete consoles members of the bereaved family
 President Kikwete takes his leave
President Kikwete says kwaheri to UDSM Vice Chancellors Prof. Rwekaza Mukandara

UONGOZI KILWA WATOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MCHANGO WA RASILIMALI ZA WILAYA HIYO

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna wilaya hiyo inavyoendelea kuboresha huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.Kushoto ni diwani wa kata ya Kikole Mwl.Haji Mulike na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Ali Mohamed Mtopa.
Ramani ya hospitali ya kisasa yenye hadhi ya kimataifa itakayojengwa wilayani kilwa kwa nguvu za halmashauri na wadau wa Maendeleo. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es salaam.

Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa umesema kuwa utahakikisha   rasilimali zote zinazopatikana katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na gesi asilia zinatumika kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.

Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, watendaji na baadhi ya Madiwani  wanaohudhuria kikao kazi jijini Dar es salaam,  Bw. Mapunda amesema kuwa halmashauri hiyo imejipanga kupunguza utegemezi wa fedha toka serikali kuu kwa kupanua wigo wa mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Amevitaja vyanzo hivyo kuwa vyanzo hivyo vipya ni pamoja na ushuru wa zao la Ufuta ambalo sasa mapato yake yamefikia milioni 595, mauzo ya viwanja na ushuru wa Gesi asilia inayozalishwa katika kijiji cha Songosongo ambayo sasa inatoa asilimia 0.3 ikiwa ni ushuru wa tozo la huduma.

Akifafanua kuhusu mapato hayo Bw. Mapunda amesema kuwa katika zao la ufuta asilimia 20 ya pato hilo inarudishwa vijijini na halmashauri hiyo na kuongeza kuwa mapato ya ushuru wa huduma unaolipwa kwa halmashauri kutokana na shughuli za gesi za kampuni ya PAN AFRICAN ENERGY katika eneo la Songosongo huchangia 20% kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo.

“ Kuanzia mwezi Septemba 2012 Baraza la Madiwani lilipendekeza tuanze kupeleka asilimia 20 kwenye kijiji cha Songosongo kutokana na malipo ya kampuni ya PAN AFRICAN ENERGY kiasi cha shilingi milioni 811ambapo hadi sasa tumeshapeleka jumla ya shilingi milioni 139 na tunajiandaa kupeleka kiasi kingine kilichobaki cha shilingi 22” ameeleza Bw. Mapunda.

Akitoa ufafanuzi kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii mkurugenzi huyo amesema kuwa wilaya ya kilwa inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Maji Safi, Umeme, Elimu, mkakati wa kukuza ajira, kuimarisha ulinzi na usalama kwa kujenga kituo cha polisi cha kisasa kitakachogharimu shilingi milioni 625 na uboreshaji wa huduma za afya.

Ameongeza kuwa katika kuboresha huduma za afya wilaya hiyo imeshatenga eneo la hekari 30 kwa ajili ujenzi wa hospitali ya kisasa yenye hadhi ya kimataifa itakayotoa huduma ya afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.

“Mradi huu wa hospitali ya kisasa utaanza haraka iwezekanavyo ndani ya mwaka huu hii ikiwa ni mchango wa rasilimali za eneo letu pia kwa kushirikiana na kampuni inayochimba gesi, pia tunajiandaa kwa ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kimataifa utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.8”

Aidha katika hatua nyingine Bw. Mapunda ameeleza kuwa halmashauri ya Kilwa inaendelea na mikakati ya kuimarisha miundombinu ya barabara ili kuimarisha usafiri wa ndani wa wilaya hiyo, kufanya juhudi ya ukamilishaji wa miundombinu ya ulinzi na usalama ili kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wa miundombinu iliyopo.

BODI YA FILAMU: UWASILISHAJI FILAMU WAONGEZEKA

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo (kulia) akieleza jambo wakati alipokutana na mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana. Pancras Mayala (kushoto) leo katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam.

Na. Benedict Liwenga-Maelezo

Bodi ya Filamu Nchini imekiri ongezeko la uzingatiaji wa Sheria ya Filamu na Kanuni zake unaofanywa na watengenezaji na wasambazji wa filamu wa ndani na nje ya nchi. Aidha imethibisha kuwa uwasilishaji wa filamu Bodi umeongezeka kwa kiwango cha kuridhisha baada ya wengi wa wadau kuitikia wito wa kuwasilisha kazi zao ili ziweze kukaguliwa na kupewa madaraja stahiki.

Vile vile Bodi imefafanua kuwa filamu na muziki iliyo katika video isiyofungiwa kwa kukosa maadili na zinazoendelea kurushwa ama kuonyeshwa bila kuzuiwa haimaaninishi ni halali isipokuwa zinapaswa kuwasilishwa Bodi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kabla ya kwenda kwa walaji.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds Media Group ofisi kwake jijini Dar Bi. Fissoo amesema kuwa Bodi ya Filamu ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza namba 4 ya mwaka 1976 Sheria ambayo ilitanguliwa na Sheria ya Picha za Sinema ya mwaka 1930 jambo linalodhihirisha ukongwe wa tasnia ya filamu nchini. Bodi inafanya kazi zake kwa kujielekeza katika kusimamia Sheria ya hiyo na Kanuni zake .

Akijibu swali toka kwa mtangazaji wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Bwana Pancras Mayala lililotaka kujua filamu ngapi zilizofungiwa na Bodi ya Filamu na sababu za kufungiwa kwa filamu hizo, Bi. Fissoo amesema kuwa mpaka sasa ofisi yake imepoke na kushughulikia jumla ya kazi zipatazo 1059 kutanzia 2011 hadi Januari 2014 ikiwa ni kwa maana ya majina.

“Mwaka 2011 mpaka sasa tumepokea na kushughulikia filamu 1059 ikiwa ni kwa maana ya majina, lakini ukienda kwa maana ya Part 1 na Part 2 maana yake ni jumla ya filamu 2118 ambapo kati ya hizo filamu 123 sawa na asilimia 5.8 zilielekzwa kufanyiwa marekebisho na filamu 7 sawa asilimia 0.33 hazikuruhusiwa kati ya mwaka 2011 hadi juni 2013 ambazo ni za ndani na za nje 2.4 hazikuruhusiwa.

Aidha kati ya Julai 2013 hadi 2014 jumla 570 zilipokelewa zikiwemo filamu 263 zilizokuwa zimeshaingia sokoni na kati ya hzo filamu 16 zilielekezwa kufanyiwa marekebisho. Tayari filamu zilizoelekezwa kufanyiwa marekesho 14 zimekwisha wasilishwa na kupewa kibali na filamu mbili za MV Spice na Nimekubali Kuolewa hatuajapokea marekebsho. Hakuna filamu iliyofungiwa kati ya julai 2013hadi Januari 2014”. Alisema Bi. Fissoo.

Aliwapongeza wadau wa filamu kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa filamu zisizoendana na maadili na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora na viwango. Kwa upande wake mtangazaji wa Clouds Media, Bwana Mayala alitaka kujua ni vigezo gani vinavyotumika katika kuzuia filamu zisiende kwa walaji ambao ni watazamaji, Bi. Fissoo alifafanua kuwa Bodi ya Filamu inazuia filamu kwa mujibu wa sheria na vipo vipengele mbalimbali vitumikavyo katika kufanya zoezi hilo aidha alimpitisha mtangazaji huyo aktika vifungu hivyo vya sharia na kanuni .


vile vile alieleza kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo maneneo yote yanayoshauriwa kurekebishwa au kuondoshwa hupitiwa kwa pamoja kati ya Bodi na wenye kazi na kufikia muafaka. Katika eneo hilo tumeendelea kupata ushirikiano mkubwa sana.

Aidha, Bi. Fissoo amewaasa wadau mbalimbali wa filamu Tanzania kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza mambo yaliyoelekezwa kwa mujibu wa sheria, na kwa wasanii amewasisitizia kuwasilisha miswada ya kazi zao ili iweze kupitiwa na Bodi na baadae filamu iwezwe kutengenezwa. Alisisitiza kuwa ofisi za Bodi ziko wazi kwa wadau wote na wakati wowote wanapohitaji ufafanuzi wanakaribishwa kwa bodi kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote

KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI LAMALIZIKA MKOANI MTWARA

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akizungumza na viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara katika siku ya pili ya kongamano la viongozi hao kuhusiana na rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania. Kongamano ambalo lilifanyika leo katika ukumbi wa VETA, Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagani akitoa mada juu ya Mipango ya Matumizi ya gesi asilia Lindi na Mtwara katika siku ya pili ya semina ya siku mbli ambapo leo ndio kilele cha kongamano hilo lililowahusisha viongozi wa dini katika mikoa hiyo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris Mtwara Padre Dkt. Aidan Msafiri akitoa mada ya Tunu na maadili katika rasilimali za gesi, mafuta na madini leo katika ukumbi wa VETA Mtwara kwa viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo alisisitiza kuwa mwanadamu amepewa jukumu la kuwa meneja wa rasilimali ikiwemo gesi. Kongamano ambalo lilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa VETA, Mtwara na kuwashikisha viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Baadhi ya wanakongamano wakimsikliza Padre Dkt. Aidan Msafiri katika siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara juu ya matumizi bora ya tunu za kimaadili, kiroho, akili, utashi, imani, haki na elimu adilifu ambapo mwanadamu amepewa jukumu la kuwa meneja wa rasilimali vitu ikiwemo gesi asilia, mafuta na madini.
Makam wa Askofu wa Kanisa la Kanisa la Anglikana Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Newalaa Oscar Mnung’a (wa kwanza kushoto) akifuatilia kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara lililofanyika katika ukumbi wa VETA Mtwara. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia.
Baadhi ya viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa katika ukumbi wa VETA, Mtwara katika siku ya pili ya kongamano la viongozi hao kuhusiana na rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madinikwa amani na maendeleo ya Tanzania.
Mkuuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akiwa miongoni mwa washiriki katika siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini yeye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Lindi.
Mmoja wa wananchi walionufaika na ziara na mafunzo ya elimu ya gesi nchini Thailand Hsasan Gobossi akitoa ushuhuda mambo aliojinea katika mafunzo yao wakiwa nchini humo ikiwemo kiusalama katika miradi ya gesi na kiuchumi leo katika ukumbi wa VETA, Mtwara wakati wa kongamano la siku mbili la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mrs Pendo Mshiba wa kanisa la Wadventista Wasabato Mtwara akiuliza swali juu ya kundi kubwa la vijana ambao hawaendi kanisani au msikitini ambalo wao wanajiita kundi la “wanaojishukuru” akimaanisha ni kundi lililosahaulika katika jamii na maisha yao kubakia kukata tamaa. Pia alitoa ushauri kwa Serikali nini kifanyike ili kulinusuru kundi hili ambapo alisihi wapatiwe elimu juu ya gesi ili nao wajue nini kina fanyika ndani ya nchi yao washirikikatika kujiletea maendeleo yao na taifa. 
Picha ya pamoja ya viongozi wa dini na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya siku ya pili ya kongamano lililohusu raslimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania. Kongamano ambalo lilifanyika leo katika ukumbi wa VETA, Mtwara.(Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mtwara).

Na Eleuteri Mangi- Maelezo, Mtwara

Serikali imeahidi kuangalia uwezekano wa kuwafadhili wanafunzi wapatao 20 kutoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara wanaosoma katika chuo kikuu kishiriki cha Stella Maris Mtwara (STEMUCO) ambao hawana uwezo wa kulipa ada ya masomo yao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi alipokuwa akijibu ombi lililotolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha STEMUCO Padre Dkt. Aidan Msafiri alipokuwa akiwasilisha mada yake ya Tunu na maadili katika rasilimali za gesi, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania wakati wa siku ya pili ya kongamano la viongozi wa dini kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.

Katibu Mkuu Maswi alisema kuwa serikali ipo tayari kuhakikisha inawapatia elimu hiyo ili waweze kihudumia jamii ya wanalindi na Mtwara katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla.

Lengo kubwa la kongamano hili lilikuwa ni kutoa elimu zaidi kwa viongozi wa dini kuhusiana na rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima kwa ujumla.

Elimu hiyo ililenga kuwaelimisha viongozi hao wa dini ambao wanaushawishi mkubwa kwa waumini wanaowaongoza ambapo mada mbalimbali zilitolewa ili kuwajengea uwezo wa kuwaelimisha waumini wao juu ya masuala ya gesi asilia, mafuta na madini.

Mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo ili kufanikisha uelewa wa pamoja kwa viongozi wa dini ni pamoja na Mtazamo wa Kitheolojia/Kidini juu ya rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini iliwasilishwa na Sheikh Abubakar Zuberi, Maelezo ya jumla ya Wizara ya Nishati na Madini kuhusu za gesi asilia, mafuta na madini iliwasilishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Eliakim Maswi, Tunu na maadili katika za gesi asilia, mafuta na madini iliwasilishwa na Padre Dkt. Aidan Msafiri, Ushuhuda wa mwakilishi aliyehudhuria mafunzou ushirikishaji mang’amuzi ya uchumi wa gesi nchini Thailand iliwasilishwa na Hssan Gobbosi.

Mada nyingine ni Mipango ya matumizi ya gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara iliwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagane, Uzoefu wa ushiriki wa wazawa  katika masuala ya gesi asilia iliwasilishwa na Sultan A. Sultan na Maelezo ya Wizara yaliyowasilishwa na Mwara Shoo na Ally Samaje. 

Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeridhia kuendelea kuwapeleka vijana wa mikoa hiyo kusoma VETA kwa muda wa miaka mitatu ili waweze kutumia fursa ya kugunduliwa kwa rasilimali mbalimbali katika mikoa hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Yona Killagane akiwasilisha mada juu ya mipango ya matumizi ya gesi asilia Lindi na Mtwara alisema kuwa zipo faida nyingi za mradi wa gesi kwa wananchi.

Killagane alizitaja faida hizo kuwa ni kujenga shule za chekechea, wanafunzi wanapata udhamini wa kusomeshwa shule za sekondari, kujengewa hospitali, kuwapatia maji safi, ajira na kupata umeme unaotokana na gesi aktika maeneo yao. 

Kongamano hili la siku mbili la viongozi wa dini wa mikoa ya Lindi na Mtwara liliandaliwa na viongozi wa dini wa mikoa hiyo ikiwa ni muendelezo wa kongamano la kitaifa la viongozi hao lililofanyika mwezi Januari mwaka huu jijijni Dar es salaam.


Makonamano haya yote mawili yaliongozwa na kauli mbiu ya “Rasilimali zetu za gesi asilia, mafuta na madini kwa amanina maendeleo ya Tanzania.
 Jaji wa Mahakama Kuu Mstaafu Mh. Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi wa uzinduzi wa Rasimu ya pili ya Katiba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Haki za Binadamu Bi. Helen Simba akieleza kuhusika kwa haki za Binadamu katika Rasimu ya Pili katiba kwa wananchi.
 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akitoa hotuba kabla ya uzinduzi Rasmi wa kampeni ya Taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa Wananchi

 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu  akizindua Rasmi Kijitabu kidogo kilicho andikwa Rasimu ya Pili ya Katiba Inasemaje? Chapisho la Lugha nyepesi
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu  akizindua rasmi vipeperushi vilivyo andikwa , Mambo Saba makubwa ya kuungwa mkono na wananchi katika Rasimu ya Katiba pamoja na mambo makubwa matano yanayokosekana katika Rasimu ya Katiba na Kipeperushi cha pili kinacho sema 'Taifa ni letu na Katiba ni yetu Husika tupate Katiba Bora.
 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akigawa vipeperushi hivyo kwa ishara ya uzinduzi rasmi.
 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi Jarida la Rasimu ya Pili ya Katiba 
 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Flash Disk maalum zenye Rasimu ya Katiba ambazo zitagawiwa kwa waendesha Bodaboda ili abiria akipanda nae apate kusikiliza Rasimu hiyo.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi, DVD, VCD pamoja na AUDIO CD kwa ajili ya walemavu.
Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu akizindua Rasmi Tovuti 'Blog' inayo itwa Taifa ni letu  www.taifaniletu.blogspot.com ambayo ni maalumu kwa ajili ya Rasimu ya Pili ya Katiba.

 Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Tume za haki za Binadamu Bi. Maafudha Hamidu  akitoa pongezi kwa jinsi mchakato unavyokwenda ikiwa ni pamoja na kutumia Teknolojia ya hali ya juu ili kila mtu afikiwe na Rasimu ya Pili ya Katiba
 Kundi la watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwa wamefika katika uzinduzi wa kampeni ya taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wananchi wote
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani wakiwa katika uzinduzi wa kampeni ya taifa ya kusambaza uelewa wa Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wananchi wote,ambapo pia kulikuwa na shule zengine Kama Azania ,Mazimbwi na Chamazi.
 Kwaya kutoka Haki za Binadamu wakitumbuiza kwa moja ya nyimbo zao
Sehemu ya watu waliohudhuria katika Uzinduzi huo.

Picha na Dar es salaam Yetu Blog