Friday, August 30, 2013

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI UHOLANZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Holland..Rais Shein yupo nchini Holland kwa ziara ya kikazi. 
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh: Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanzania wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein hapo jana katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag. 
 Mwenyekiti wa Tane nchini Uholanzi ndugu Kweba Bulemo akimkabidhi zawadi ya kitabu maalumu Mheshimiwa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kama kumbukumbu alipofanya mazungumzo na Watanzania hao hapo jana nchini Uholanzi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa ufafanuzi wa maswali yote aliyokuwa akiulizwa na baadhi ya Watanzania kuhusu mustakabari wa Kisiwani Zanzibar
 Pichani ni mahudhurio ya watanzania waliojitokeza kuzungumza na Mh:Rais Ali Mohamed Shein hapo jana katika ukumbi wa hotel ya Hilton
 Kati ya Watanzania waliouliza maswali ndugu Omary Abbas alikuwa mmoja wapo..pichani akiuliza moja kati ya maswali yake hapo jana.
 Baadhi ya Watanzania wakiwa makini kabisa kusikiliza nini Rais anazungumza.
 Wake kwa waume walijitokeza kwa wingi katika mkutano huo na Mheshimiwa Rais wakiwa makini kusikiliza 
 Maganga One Blogger akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hapo jana.
Maganga One Blogger akiwa na Mheshimiwa Balozi Diodorus Kamala hapo jana katika mkutano wa wa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi[Picha zote na maelezo toka http://magangaone.blogspot.com/ .. Kwa picha zaidi bonyeza habari zaidi/read more

Thursday, August 29, 2013

EU Members of Parliament visit Tanzania

Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation welcomes Hon. Hannes Swoboda, Member of the European Parliament (MEP) and President of the Social Democrats in the European Parliament.  Hon. Swoboda paid a courtesy visit earlier today to discuss matters of regional integrations, promotion of good governance and accountability, areas of cooperation that includes piracy, oil and gas.
Ambassador Gamaha greets H.E. Filberto Cerian Sebregondi, Head of Delegation the European Union. The EU delegation arrived in Dar es Salaam earlier today from Brussels, Belgium.
Ambassador Gamaha welcomes Hon. Norbert Neuser, Member of the European Parliament (MEP) and Social Democrats Coordinator.
Ambassador Gamaha welcomes Hon. Ricardo Cortes, Member of the European Parliament and Social Democrat Coordinator for Development. 
Ambassador Gamaha explains about the progress of the custom union in the East African Community (EAC) and the success of the free trade area in the Southern Africa Development Community. 
THe European Delegation during the meeting. 
Tanzania delegation that include Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas and Mr. Frank Mhina, Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 
The meeting continues.
On a separate meeting, Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation took time to meet with H.E. Filberto Cerian Sebregondi, Head of Delegation the European Union.  
Ambassador Gamaha listens to Head of the EU Delegation Filberto Cerian Sebregondi during their meeting. Also in the photo is Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. All photos by Tagie Daisy Mwakawago from the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

taswira mbalimbali za Maadhimisho ya miaka 50 ya March in Washington

Leo, waMarekani wameadhimisha miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano makubwa ya kudai haki za watu weusi. Katika maadhimisho hayo, kamera ya swahilivilla blog iliegeshwa kando ya mlango wa kuingila na kushuhudia watu maarufu hapa nchini wakipekuliwa kwa sababu za usalama kabla ya kuingia ndani sherehe hizo ambazo ambazo zimehudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali nchini hapa.
Tuliobahatika kuwanasa katika kamera hiyo ni pamoja na muigizaji Jamie Foxx, pale alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC.
Muigizaji wa filamu Jamie  Foxx akishuhudia gari lake likipekuliwa kabla ya kuingia ndani ya tukio la maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC
Mwigizaji wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial  Washington DC
Mshangao mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani John F. Kennedy, Caroline Kennedy ambae ni balozi mteule Nchini Japani, alipoingia na Cab (Taxi). cha kuchangaza pia ni pale gari lake lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani Forest Whitaker nae pia gari lake lilifanyiwa upekuzi na maofisa wa usalama baada ya kuwasili katika endeo la Sherehe za miaka 50 ya March on Washington DC
Forest Whitaker akikionyesha tabasamu baada ya kutolewa ndani ya gari lake na kufanyiwa utaratibu wa kupekuliwa kabla ya tukeo kuanza rasmi.
Vile vile kamera ya swahilivilla blog imemnasa Rajiv “Raj” Shah American Economic development specialist, alipotolewa nje ya gari lake na kufanyiwa upekuzi wa lazima siku ya Jumatano Aug 28, 2013 Washington DC
Watu tupo kazini..: Ofisa Usalama akifanya upekuzi wa magari ya watu maarufu yanayoelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC siku ya jumatano Aug 28.
Mwanasheria Mkuu wa jimbo la California Kamala Harris pia alishushwa ili kuruhusu upekuzi wa gari kabla ya kuingia  katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington
Kamala Harris aliamua kusogea na kusalimiana na baadhi ya watu waliokua karibu yake pamoja na kamera ya swahilivilla wakati gari yake ikipekuliwa kabla ya kuingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington
Ni Oprah Gail Winfrey pekee ambaye hajatoka kwenye gari lake ambalo lilipekuliwa na kuruhusiwa kuondoka bila ya kutolewa ndani ya gari hilo alilokua amalipanda
Oprah Gail Winfrey akishangaa  kwa mbali flash ya swahilivilla wakati anaelekeaa ndani ya Lincoln Memorial Washington Washington DC 
Chief wa swahilivilla Abou Shatry akiwa katika 50th anniversary March on Washington DC Siku ya Jumatano 28, 2013 Rais Barak Obama, leo ametoa changamoto kwa kizazi kilichopo kuwaenzi mashujaa walioandamana mwaka 1963 kudai haki sawa kwa watu wa rangi zote nchini Marekani. JAMII RADIO ina ripoti kamili.Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)

Ziara ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein nchini Uholanzi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,alipotembelea katika bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano na ujumbe wake, nchini Uholanzi, {Picha na Ramadhan Othman Uholanzi].
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake waliokaa wakipata maelezo kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake wakipata maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Bandari na Mpango mzima wa utendaji kazi kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,  alipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano  nchini Uholanzi na ujumbe aliofuatana nao.
Baadhi ya Meli za Mizigo kutoka Nchi mbali mbali ikiwemo China,ni miongoni mwa Meli zinazotia nanga katika Bandari ya Rotterdam, Nchini Uholanzi kama inavyoonekana pichani ikiwa imesheheni makontena yenye Bidhaa mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa na wawakilishi wa Makampuni yanayotaka kuwekeza Zanzibar wakiwa katika mazungumzo ya kujadili nanama ya kufikia hatua za kuwekeza  Nchini,wakati alipokuwa katika ziara Nchini Uholanzi itakayochukua siku tano,ambapo atatembelea sehemu kadhaa za kimaendeleo katika nchi hiyo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wawakilishi wa Makampuni wakati alipowasilim katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Famili ya Mfalme panoja na makampuni nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya siku tano nchini humo.