Leo,
waMarekani wameadhimisha miaka 50 tangu kufanyika kwa maandamano
makubwa ya kudai haki za watu weusi. Katika maadhimisho hayo, kamera ya
swahilivilla blog iliegeshwa kando ya mlango wa kuingila na kushuhudia
watu maarufu hapa nchini wakipekuliwa kwa sababu za usalama kabla ya
kuingia ndani sherehe hizo ambazo ambazo zimehudhuriwa na maelfu ya watu
kutoka sehemu mbali mbali nchini hapa.
Tuliobahatika
kuwanasa katika kamera hiyo ni pamoja na muigizaji Jamie Foxx, pale
alipotolewa ndani ya gari na maofisa kuanza kupekua gari alilolipanda
kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln Memorial Washington DC.
Muigizaji
wa filamu Jamie Foxx akishuhudia gari lake likipekuliwa kabla ya
kuingia ndani ya tukio la maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington
DC
Mwigizaji
wa filamu Angelha Bassett Evelyn alipotolewa kwenye gari lake na
maofisa kuanza kulipekua kabla ya kuingia ndani ya eneo la Lincoln
Memorial Washington DC
Mshangao
mkubwa watu walioupata ni pale mtoto wa Rais wa zamani nchini Marekani
John F. Kennedy, Caroline Kennedy ambae ni balozi mteule Nchini Japani,
alipoingia na Cab (Taxi). cha kuchangaza pia ni pale gari lake
lilipopekuliwa bila ya kujali ukubwa au cheo alichonacho na kufata
sheria ya upekuzi kama wengine magari yao yalivyopekuliwa.
Muigizaji
maarufu wa filamu nchini Marekani Forest Whitaker nae pia gari lake lilifanyiwa
upekuzi na maofisa wa usalama baada ya kuwasili katika endeo la Sherehe
za miaka 50 ya March on Washington DC
Forest Whitaker akikionyesha tabasamu baada ya kutolewa ndani ya gari lake na kufanyiwa utaratibu wa kupekuliwa kabla ya tukeo kuanza rasmi.
Vile
vile kamera ya swahilivilla blog imemnasa Rajiv “Raj” Shah American
Economic development specialist, alipotolewa nje ya gari lake na
kufanyiwa upekuzi wa lazima siku ya Jumatano Aug 28, 2013 Washington DC
Watu
tupo kazini..: Ofisa Usalama akifanya upekuzi wa magari ya watu maarufu
yanayoelekea katika maadhimisho ya miaka 50 ya March on Washington DC
siku ya jumatano Aug 28.
Mwanasheria
Mkuu wa jimbo la California Kamala Harris pia alishushwa ili kuruhusu
upekuzi wa gari kabla ya kuingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka
50 ya March on Washington
Kamala
Harris aliamua kusogea na kusalimiana na baadhi ya watu waliokua karibu
yake pamoja na kamera ya swahilivilla wakati gari yake ikipekuliwa
kabla ya kuingia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya March on
Washington
Ni
Oprah Gail Winfrey pekee ambaye hajatoka kwenye gari lake ambalo
lilipekuliwa na kuruhusiwa kuondoka bila ya kutolewa ndani ya gari hilo
alilokua amalipanda
Oprah
Gail Winfrey akishangaa kwa mbali flash ya swahilivilla wakati
anaelekeaa ndani ya Lincoln Memorial Washington Washington DC
Chief wa swahilivilla Abou Shatry akiwa katika 50th anniversary March on
Washington DC Siku ya Jumatano 28, 2013
Rais Barak Obama, leo ametoa changamoto kwa kizazi kilichopo kuwaenzi
mashujaa walioandamana mwaka 1963 kudai haki sawa kwa watu wa rangi zote
nchini Marekani. JAMII RADIO ina ripoti kamili.Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment