Tuesday, May 29, 2012

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akizungumza machache wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kuwa leo tunatoa heshima kwa Walinda Amani zaidi ya 2900 ambao wamepoteza maisha wakiwa kazini katika miaka iliyopita na kuahidi kuendeleza kazi yo kurejesha Amani katika nchi zenye vita.Amesema katika siku hii ya Umoja wa Mataifa ya Walinda Amani tuitumie kukumbuka jinsi watu walivyojitolea maisha yao, na tuahidi kuimarisha ushirikiano wa kidunia ambao unawafanya hawa wavaa kofia za Bluu waonekane kama alama ya Amani duniani kote.
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani 2012 ambapo amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu imelenga kuunganisha majeshi yote ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na Amani na Utulivu.
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa. 
Brass Bendi ikiingia katika Uwanja wa Mashujaa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei.
Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).
Baadhi ya Wanajeshi wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa ya jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).
"Mungu Ibariki Afrika, Wabariki Viongozi Wote.......!!!
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akijongea na kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka walinda Amani wa Afrika.
General Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.
Usia Nkhoma-Ledama kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) ambao ndio waandaaji wa maadhimisho hayo hapa nchini.
Zainab Abdalah kutoka Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania akighani Mashairi wakati wa Sherehe za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania wakitoa burudani za nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo.Picha zote na MO BLOG.

Monday, May 28, 2012

Pamvu ya Lt Abdu Manambi Choka na Amina Shaaban Sato Bl 41 Kinondoni

 Ankal habari !
 Ukoo wa Manambi Choka  unaendelea na libeneke la harusi kwa kwenda mbele. Safari hii ni  Luteni Abdulkadir Manambi Choka ni mpwa wangu amemposa Bi Amina binti Shaban Sato! Jumamosi Mei 26, 2012 tuliwasilisha mahari kwa Bi Harusi mtarajiwa  BL 41 Kinondoni ambapo baada ya kutoa mahari ikafuatiwa na mnuso wa nguvu halafu Adfande Abdul akamvisha pete ya uchumba Bi Harusi mtarajiwa .
Muihtasari wa habari katika picha ni:
Mjomba  wa Bwana Harusi Mtarjiwa Mzee Issa E.C.Manambi akitoa dibaji ya ulipaji mahari ambapo aliwaambiwa Wazazi wa Bi Haruisi Mtarajiwa kuwa unalipwa mzigo kamili, picha inafuatiwa Mzee Issa Maanambi anakabidhi 'mzigo' kamili kwa Baba Mdogo wa Bi harusi Mtarajiwa Mzee Yahya Sato , mzigo huo baadae unahakikiwa na Mjomba wa Bi Harusi Mtarajiwa nakuonekana umetimia.
Mnuso uliofuata na halafu Bi Harusi Mtarajiwa analetwa katika hadhara na Afande Abdul Choka anamvisha pete ya uchumba 'rasmi'! Picha nyingine ni za ukumbusho Mama Mzazi wa Bwana Harusi Bi Mwajellah Manambi Choka na Mama Mdogo wa Bi Harusi Mtarajiwa Bi Simtovu Bakari Msonde ( mwenye mikongojo) na Maharusi Watarajiwa na nyingine za upande wa Bwana Harusi Mtarajiwa na  Bi harusi Mtarajiwa.
Ankala usinichoke naomba uchapishe kwa usanifu wako picha hizi katika blog yako.
Shukran !
Wasalaam
Mdau - Midladjy Manambi Maez
Mei 28, 2012
Dar es Salaam.
 Mzigo ukihesabiwa
 Mnuso wa hafla
 Hapa tonge nyama
 Bw Harusi Mtarajiwa aingia
 Akutana na mtarajiwa mwenza
 Baadhi ya mashuhuda
 Mtarajiwa apiga goti kuomba chanda cha pete
 Abusu chanda kilichorembwa pete yake
 Hii hapa....
 Chereko chereko...
Wazaa chema wafurahia
 Picha ya pamoja



SIMBA SC WALIVYOSHEREHEA UBINGWA WAO DAR LIVE

Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam jana.

TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE. Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live. Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba.
Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika msafara kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao jana.
Mashabiki wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za ubingwa.
Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana.
Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).
Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo,Mh. Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani.
Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda apokea mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Spika wa Bunge akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd kwa kuiwezesha Halmashauri ya Mji wa Njombe kupata Mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo Mwandamizi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mhandisi Juma Hamsini alipokuwa akielezea ubora wa mitambo ya kampuni hiyo kabla ya kumkabidhi rasmi Mhe. Spika kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mitambo hiyo imenunuliwa kwa gharama ya zaidi ya Milion 700 za Kitanzania kwa makubaliano ya mkopo usiokuwa na riba kutoka Mfuko wa Halmashauri ya Mji wa Njombe. Kulia kwa Mhe. Spika ni Mwenyekiti wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mehboob Karmali na walioko kushoto ni watendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wakiongozwa na George Mkindo (mwenye koti)Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo akitoa pongezi zake kwa kampuni ya uuzaji wa mitambo ya ujenzi ya GF Trucks & Equipment Ltd baada ya kukubali kuizia Halmashauri yake Mitambo ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine katika Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa Mkopo usio kuwa na Riba wa kiasi cha Million 700 za Kitanzania.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokea mfano wa Ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kamapuni ya GF Trucks & Equipment Ltd ya jijini Dar es Dar es Salam Bw. Imran Karmali baada ya makabidhiano ya Mitambo ya Kisasa ya kutengeneza Barabara na miundombinu kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Mitambo hiyo imenunuliwa kwa gharama ya Tsh. Million 700 kwa makubaliano maalum ya mkopo nafuu usiokuwa na riba. Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd Mehboob Karmali na aliye kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akijaribu mojawapo ya mitambo hiyo mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Njombe. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kamapuni ya uuzaji mitambo hiyo ya Jijini Dar es Salaam ya GF Trucks & Equipment Ltd Bw. Imran Karmali.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifurahia mojawapo ya mitambo ya kisasa ya kutengenezea barabara na miundombinu mingine iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji wa Njombe kutoka Kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Imran Karmali, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw. Mehboob Karmali na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe George Mkindo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Mitambo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Njombe George Mkindo mara baada ya kuipokea kutoka kampuni ya GF Trucks & Equipment Ltd ambayo ndio walioiuzia Halmashauri hiyo mitambo hiyo.
Mhe. Makinda akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kupokea mitambo hiyo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.