Monday, February 27, 2012

Kampuni ya Simon Group yanunua mabasi 30 ya UDA

Meneja Biashara wa Kampuni ya TATA, Srinivas Nemalapuri akionesha baadhi ya mabasi ya UDA yaliyonunuliwa na Kampuni ya Simon G.

Na Oscar Mbuza

HATIMAYE Kampuni ya Simon Group imeanza mikakati ya kulifufua Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) baada ya kununua mabasi 30 yenye uwezo wa kubeba abiria 40 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji jijini Dar es Salaam .

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa UDA kununua magari mengi kwa wakati mmoja tangu kuanzishwa kwa shirika hilo zaidi ya miaka 38 iliyopita.

Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group, Robert Kisena aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba kampuni yake imejizatiti katika kuifufua UDA kama ilivyoahidi wakati iliponunua hisa za kuliendesha shirika hilo.

“Tayari yamewasili nchini ili kusaidia kuboresha hali ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam. Kwa sasa mabasi hayo yamehifadhiwa kwa ajili kupigwa nembo ya UDA.”

Hatua hiyo ya Kampuni ya Simon Group kuagiza mabasi mengi kwa wakati mmoja ina badili taswira na mitazamo iliyokuwepo kwamba kampuni hiyo ya Tanzania haina uwezo wa kuweza kuhimili kikamilifu changamoto zilizopo kwenye sekta ya usafirishaji.

Baadhi ya Wabunge wa Jiji la Dar es Salaam walipokuwa wakichangia bungeni mwishoni mwa mwaka jana walieleza wasiwasi kwa kampuni hiyo kuweza kuliendesha Shirika la UDA kwa ufanisi kwa madai kwamba haina uzoefu wa masuala ya usafirishaji.

“Kimsingi ni kwamba kampuni yetu imejizatiti katika kuleta mageuzi makubwa sana katika sekta ya usafirishaji abiria hapa nchini, tunayo mipango mikubwa ni suala la kupewa muda wa kutosha na tutaweza kuthibitisha na kuondoa wasiwasi kwa abiria pamoja na watanzania wenzetu,” alisema Kisena

Kisena alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita Kampuni ya Simon Group imeweza kuingiza kati ya Sh. bilioni 2.7 na Sh. bilioni 3 katika uwekezaji ndani ya UDA.

Alisema kiasi hicho cha fedha ni zile za kulipa mishahara ya watumishi wa UDA, kununua vipuli vya magari pamoja na kununua magari mapya ikiwa ni fedha kutoka kwenye vyanzo vingine vya mapato kutokana na akaunti za UDA kusitishwa ili kuweka sawa baadhi ya kasoro zilizojitokeza wakati shirika hilo lilipokuwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Wakurugenzi ya zamani, chini ya uenyekiti wa Idd Simba.

Kisena alisema anashindwa kuendelea na harakati nyingine za kuwekeza zaidi katika UDA hasa kutokana na ukiritimba katika kutatua tatizo lililopo. Lakini mwekezaji anasema kwamba ameambiwa kwamba katika kipindi cha mwezi mmoja ujao Serikali itakuwa imekamilisha masuala yake.

“Kazi iliyobaki kwa Serikali ni namna ya kujiondoa ili sasa Simon Group iweze kuwa na udhibiti wa kampuni pamoja na uendeshaji wake…ninaamini kazi hiyo itakamilika katika kipindi hicho cha mwezi mmoja ambacho kinakadiriwa,” alisema Kisena

Anasema kama kampuni hiyo itakabidhiwa Shirika la UDA analenga kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi kutokana na wingi wa mabasi makubwa ya kubeba abiria jijini Dar es Salaam. “Tunataraji kutoa ajira nyingi zaidi kwa Watanzania, maana tunao mpango wa kuingiza nchini mabasi zaidi ya 1,000,” alisema Kisena

Aidha taratibu za ukaguzi wa mahesabu ya UDA zimeshakamilika na pengine Serikali inasuburi dokezo hilo ili taratibu nyingine za kumkabidhi mwekezaji mpya Simon Group ziweze kufuata.

Mapema mwezi huu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovick Utouh alisema kuwa ripoti hiyo imewasilishwa Makao Makuu ya Kampuni ya KPMG nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuihakiki na kuangalia ubora wa ukaguzi wenyewe ndipo waikabidhi kwake aweze kuipitia.

Utouh alisema anatarajia kuipata ripoti hiyo wakati wowote ili aweze kuipitia na kuiwasilisha serikalini kwa ajili ya hatua zaidi. Alisema kwamba ripoti hiyo ilitakiwa kuwasilishwa Januari mwishoni, lakini kinachofanyika sasa ni kuhakiki zaidi ili iwe kwenye kiwango kinachokubalika.

Utouh alisema kuwa KPMG ni miongoni mwa kampuni zinazoanya vizuri kwenye kazi hiyo na kwamba, hakuna mashaka yatakayoweza kujitokeza juu ya utendaji wa kazi zao, bali kinachotakiwa kufanyika ni kusubiri wakati wa kuiwasilisha serikalini.

Kabla ya ubinafsishaji huo, UDA ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Serikali Kuu, kupitia Hazina, wakiwa na jumla ya hisa 15 milioni ambapo kila hisa moja ilikuwa na thamani ya Sh100.

Kwa mchanganuo, Halmashauri ya Jiji ilikuwa inamiliki asilimia 51 ya hisa hizo, huku Hazina ikimiliki asilimia 49. Februari 11, Bodi ya Wakurugenzi ya UDA, chini ya Idd Simba, ilikutana na uongozi wa Simon Group ikiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji Kisena na kusaini mkataba, ambao ulithibitisha kwamba UDA ilikuwa imeiuzia Simon hisa milioni 7.8 sawa na asilimia 52.535 ya hisa zote.

Mkataba huo ungeifanya Simon Group kuwa mwanahisa mkubwa katika umiliki wa UDA kwa vile Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Hazina, wangebaki na hisa milioni 7.7, ambazo ni sawa na asilimia 47.465.

Baada ya mkataba kusainiwa, kipengele cha kwanza kiliitaka Simon Group kulipa asilimia 25 ya fedha za ununuzi wa hisa za UDA (Sh bilioni 1.142) ambazo ni sawa na Sh milioni 285.669, ndani ya siku 14, tangu kusainiwa ili kuufanya mkataba utambulike kisheria, na Simon Group ililipa fedha hizo siku hiyo hiyo.

Saturday, February 25, 2012

Dkt Shein Rais awaalika chakula cha Mchana askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama visiwani Zanzibar leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono Maaskari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakati alipowaalika chakula cha mchana katika kambi ya Bavuai huko Migombani nje ya Mji wa Zanzibar leo,(kulia) Waziri Nchi Ofisi ya Rais Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Makame.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi .Ali Shein,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Balozi Seif Ali Iddi,wakati alipowasili katika kambi ya Bavuai huko Migombani nje ya Mji wa Zanzibar leo,wakati alipowaalika Maaskari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika chakula cha Mchana.
Makamo wa Pili wa Rais wa Balozi Seif Ali Iddi,akisalimiana na Brigedia Jenerali wa JWTZ Farah Abdi Mohamed,wakati alipowasili katika kambi ya Bavuai huko Migombani nje ya Mji wa Zanzibar leo,wakati hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa Maaskari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Brigedia Jenerali wa JWTZ Farah Abdi Mohamed,wakati alipowasili katika kambi ya Bavuai huko Migombani nje ya Mji wa Zanzibar jana,wakati alipowaalika Maaskari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika chakula cha Mchana leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, aakisalimiana na Mkuu wa JKU Kanali Sudi Haji Khatibu,wakati alipowasili katika kambi ya Bavuai huko Migombani nje ya Mji wa Zanzibar leo,wakati alipowaalika Maaskari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,katika chakula cha Mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Shein,(katikati) pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Balozi Seif Ali Iddi,na Viongozi wengine wakiwa wamesimama Wimbo wa Taifa Ukipigwa na Vikundi vya Brassband vya Vikosi vya Ulinzi wakati wa Sherehe za Kuwapongeza wanajeshi hao kwa kuwaalika chakula cha Mchana,kwa kushiriki kwao katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,huko katika Kambi ya Bavuai,Iliyopo Migombani Nje ya Mji wa Zanzibar leo.
Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein,leo katika Kambi ya Bavuai,Migombani Nje ya Mji wa Zanzibar,kwa ushirikiwao katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatiwa na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki 101KV Brigedia Jenerali Farah Abdi Mohamed,Makamo wa Pili wa Rais wa Balozi Seif Ali Iddi,na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Mwinyihaji Makame,wakichukua chakula cha mchana, walichoandaliwa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,kwa ushirikiwao katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,huko katika Kambi ya Bavuai,Migombani Nje ya Mji wa Unguja
leo.
Baadhi ya maaskari walioshiriki katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar,wakichukua chakula walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,katika Kambi ya Bavuai,Migombani Nje ya Mji wa Unguja leo.
Baadhi ya maaskari walioshiriki katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Zanzibar,wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ali Mohamed Shein,katika Kambi ya Bavuai,Migombani Nje ya Mji wa Unguja leo.
Baadhi ya Makamanda wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,wakiwa katika hafla ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein,leo katika Kambi ya Bavuai,Migombani Nje ya Mji wa Zanzibar,kwa ushirikiwao katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar,awaalika chakula cha mchana washiriki wa Halaiki Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono watoto walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakati alipowaalika chakula cha mchana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli jana,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Mwinyihaji Makame,na Waziri wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe.Mohamed Aboud Mohamed.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Walimu wa Halaiki katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar jana, wakati alipowaalika watoto walioshiriki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika chakula cha mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,wakati wa ghafla ya chakula cha mchana,walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Walimu wa Halaiki wakiwa katika picha wakati wa kutambulishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,wakati wa hafla ya chakula cha Mchana walichoandaliwa watoto walioshiriki Halaiki katika maadhimisho ya miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotelm Mjini Zanzibar.
Watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakiwa wamevalia sare,wakisubiri kuanza kwa shuhuli hiyo ya chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Baadhi ya watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakichua chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,pia wakiwa wamevalia sare maalum.
Baadhi ya watoto walioshiriki katika Halaiki ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakila kwa utulivu chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar,pia wakiwa wamevalia sare maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Mwinyihaji Makame,(wa pili kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahya Mzee,wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya wa ghafla ya chakula cha mchana, walichoandaliwa watoto walioshiki katika Halaiki wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa kufundisha Halaiki ya watoto,baada ya hafla ya chakula cha Mchana walichoandaliwa watoto walioshiriki Halaiki katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar,hafla hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotelm Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman IKULU.

Friday, February 24, 2012

VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU KWA MARA YA KWANZA TANGIA KIJENGWE MWAKA 1967

Mkuu wa Polisi Jamii wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Issaya Doya akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa VodacomTanzania Mwamvita Makamba, wakati wa sherehe ya kakabidhi rasmi kituo hicho kilichakarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation kwa thamani ya shilingi Milioni 17,tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akipongezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika katika kukarabati kituo hiuchi. Kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini.Nguvu Kamando.
Mkuu wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Arusha.(INSP)Amilton Matangi akiwaonyesha moja ya chumba cha mahabusu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kulia na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho,Jumla ya shilingi Milioni 17 zilitumika kukikarabati kituo hicho tangia kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, Jumla ya shilingi Milioni17.zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC).Thobias Andengenye akipanda mti wa ukumbusho wa uzinduzi wa kituo cha polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17, wakishuhudia ni Mkuu wa Kituo hicho INSP Amilton Matagi ,Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba ,Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Nguvu Kamando.
Hichi ni Kituo cha Polisi Cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kikionekana katika muonekano mpya baada ya kukarabatiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kiasi cha shilingi Milioni 17 kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.
Baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wakishuhudia Makabidhiano rasmi ya Kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo mara baada ya kukarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 17.
Waandishi wa habari wakiwa kazini kama kawa wakati wa Makabidhiano rasmi ya Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Foundation, tangu kujengwa kwake mwaka 1967,Maboresho hayo yamegharimu kiasi cha shilingi milioni 17.

Saturday, February 18, 2012

JK AONGOZA MATEMBEZI YA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI YA KINAMAMA YA BAOBAB ITAYOENDESHWA NA CCBRT

 Rais Jakaya Kikwete wa nne akiwasili kushiriki matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Wadi ya akina mama katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo ya kilomita mbili na nusu yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT katika kampeni hiyo inayotwa Find your Moyo. Pichani Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali hiyo Dr Wilbroad Slaam akimtambulisha JK kwa  Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT.
 Wafanyakazi wa CCBRT wakimlaki JK ambaye kaongozana na Dr Wilbroad Slaa
 JK akipokea zawadi ya picha yenye kuonesha mama na mtoto
 JK akipata maelezo ya mafanikio ya CCBRT katika kupambana na Fistula
 JK akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa CCBRT
 JK akitmbulishwa kwa mmoja wa viongozi wa hospitali hiyo
 JK akisalimiana na balozi
 JK akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi juu ya juhudi za kupambana na Fistula
 JK akipelekwa kutembelea wodi
 JK akisalimiana na watoto wenye matatizo mblaimbali































 Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa (Finde your Moyo).
Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.


 Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa (Finde your Moyo).
Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.

 Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa (Finde your Moyo).
Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.