Wednesday, September 5, 2018

KESI ZINAZOHUSU MASUALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KUSIKILIZWA MFULULIZO: DKT. ELIEZER FELESHI

MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa mahakimu wakazi wa wilaya na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 iliyoanza Septemba 5, 2018 mkoani Morogoro. Semina hiyo imeratibiwa kwa ushirikiano wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Paul F. Kihwelo (kulia) na Mkurugezni Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba.
Na K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema hategemei kesi zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi zikichelewa pindi mashauri yake yanapofika mahakamani.

Dkt. Feleshi ameyasema hayo Mjini Morogoro Septemba 5, 2018 wakati akifungua mafunzo kwa mahakimu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Morogoro yanayoratibiwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kuendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo.

“Sitegemei kesi za namna hii ziingie kwenye kundi la njoo kesho… njoo kesho, mashahidi wake ni wangapi? Kesi za namna hii zikiingia zisikilizwe mfululizo, kumbukeni inamuhusu mtu aliyeumia, inagusu uhai, inahusu ulemavu wa kudumu kwa hiyo nyuma kuna wategemezi na yeye mwenyewe kwa hiyo inahusu maisha ya mtu, pia ushahidi wake uko wazi na adhabu zake ziko bayana” Alifafanua Dkt. Feleshi.

Aidha Mhe. Jaji Kiongozi alisema, kila mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anayo haki ya kupata fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria na kwa yule atakayefariki katika mazingira hayo basi wategemezi wake nao wanapatiwa haki zao zilizoanishwa kisheria.

Alisema huduma ya Hifadhi ya Jamii ni haki inayotambulika na kulindwa na Katiba, ibara ya 11 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mambo mengine inatamka kwenye ibara ndogo kwamba Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi, au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi, na bila kuathiri haki hizo Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.

“Hayo ni maneno ambayo yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo ni haki ambayo imetamkwa na inalidwa na Sheria na kwa kuzingatia matakwa hayo ya kikatiba ndio maana ilitungwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyoanzisha Mfuko huu wa WCF.” Alifafanua Dkt. Feleshi.

Alisema Mafunzo hayo kwa Mahakimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, yana manufaa makubwa na ndio maana yameratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambacho ndio chenye jukumu la kutoa elimu kwa watumishi wa mahakama.

“Katika sheria ya sasa kwa mujibu wa vifungu vya 22 (1) 46 na 48 na majedwali ya 2,3 na 4 ulipaji wa fidia unazingatia zaidi uhalisia wa tukio, kiwango cha hasara na madhara ambavyo vinafanya fidia inayolipwa ikokotolewe kwa kufuata asilimia ya vigezo hivyo na malipo ya ujira wa mwezi au malipo ya mwisho ya mhusika.” Alibainisha Dkt. Feleshi.

“Takwimu zinaonyesha kuwa Mfuko umekwishalipa Fidia kiasi cha Shilingi bilioni 4.4 tangu ulipoanza kulipa fidia hadi Julai 31, 2018, na hii inaonyesha umuhimu wa Mfuko huu kwa jamii, taifa lakini hata sisi wenyewe kama watumishi.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mshomba alisema kwa sasa Mfuko umeweka kipaumbele kwenye utoaji elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mahakimu ili na wao waelewe vizuri shughuli za Mfuko na jinsi ya kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko.

Kwa sasa Mfuko umekwisha wafikia wadau wengi na kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika uelewa wa kutekeleza sheria hii na ni wachache sana ambao bado wanakuwa wazito kutekelza sheria, alisema Bw. Mshomba.

Washiriki wa mafunzo hayo wanatarajiwa kujifunza sheria inayosimamia shughuli za Mfuko, lakini pia muundo na shighuli za Mfuko na taratibu za utoaji Fidia.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wahwshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka.
Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Bi.Elizabeth S. Missana, akipitia kipperushi chenye maelezo kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Hakimu Mfawidhi wa Mahaka ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mheshimiwa Elizabeth Nyembele, akizungumza kwenye semina hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kibaha, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akishauriana jambo na Mkuu wa Huudma za Sheria wa Mfuko huo, Bw.Abraham Siyovelwa
Bw. Mshomba (katikati), akimtambulisha Dkt. Feleshi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, wakati akiwasili ukumbini.
Dkt. Feleshi akisalimiana na Bw. Siyovelwa.
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, wakiwa na furaha baada ya Dkt. Felishi kufungua mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa wa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu namba 5 [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] kwa mahakimu Wakuu Wakazi wa Mikoa na Wilaya kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara. Semina hiyo iiyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Cha Uongozxi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeanza Septemba 5, 2015 mjini Morogoro. 
Kutoka kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, Mhe. Dkt. Feleshi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Jaji Paul Kihwelo, Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia zinazosimamia Mfuko huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada 
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, akiongoza semina hiyo. 
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akisalimiana na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Dkt. Paul F. Kihwelo, (kulia), akisindikizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe.Elizabeth Nyembele, (kushoto) na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor. 
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe.Lamek Samson akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence.

DC TANGA AZINDUA KAMPENI JUMUISHI YA UPIMAJI WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI MKOANI TANGA

 MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa Furaha Yangu uliokuwa na lengo la Pima,Jitambue ambapo kwa mkoa wa Tanga imezinduliwa leo kwenye viwanja vya Tangamano kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu 
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florance Temu
MKURUGENZI wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu akizungumza katika uzinduzi huo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella anayefuata ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha Mahita
 Mwakilishi wa JWTZ akizungumza katika uziunduzi huo
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella   kulia akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO) Dkt Asha mahita wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo kulia ni Suleimani Zumo Afisa Tarafa,nyuma waliokaa aliyevaa miwani ni Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati mwenye koti la suti akikagua mabanda mara baada ya kufanya uzinduzi huo
Mgenii rasmi kwenye uzunduzi huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita
Wasanii wa kundi la Tanga Kwanza wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo

NA MWANDISHI WETU,TANGA.

KATIKA kuendeleza kuchangia juhudi za Serikali kuimarisha huduma za Afya ikiwemo huduma za Ukimwi,Shirika la Benjamini Mkapa kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Amref chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) inatekeleza mradi wa miaka mitatu 2018-2020 Desemba.

Mradi huo wenye kufanya upimaji Jumuishi wa Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Jamii na Kuhamasisha Jamii kubadili tabia hatarishi ili kuweza kusaidia kupunguza maambukizi hayo kwa jamii .

Hayo yalisemwa na Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi Dkt Anastazia Masanja wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwenye viwanja vya Tangamano mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu  na Mkurugenzi wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la  Benjamini Mkapa Foundation Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo

Alisema kupitia mradi huo wa kupambana na kifua kikuu na Ukimwi ambao utekelezaji wake umeanza mwezi Juni 2018,Taasisi imepewa wilaya mbili ambazo ni Kilindi na Pangani kwa Mkoa wa Tanga .

"Kwa kipindi hiki Shirika la Benjamini Mkapa linatarajia kufikia kata zote 35 ambapo kati ya hizo 21 ni za wilaya ya Kilindi na 14 ni za wilaya ya Pangani lengo la upamaji kwa kila kati ni kuweza kupima watu 2081(Jumla 72,839 kwa kata 35).

Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na uchunguzi wa awali wa kifua kikuu ambapo watu wote 7082 waliohudhuria waliweza kuchunguzwa ambao watu 220 walikutwa na dalili za kifua kikuu na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

"Kwa upande wa shinikizo la damu ambapo jumla ya watu 5269 walipimwa kati yao 182 walikutwa na shinikizo la damu lisilokuwa la kawaida "Alisema.

Afisa Mradi huyo alisema pia huduma za uzazi wa mpango zilitolewa ikiwamo vipandikizi,sindano,vidonge ambapo jumla ya wakina mama waliopata huduma hiyo walifikia 188 na ugawaji wa kondomu ambapo jumla ya kondomu 5000 zimegawiwa.

"Lakini pia tuliotoa elimu ya mfuko wa Afya ya Jamii ikiwemo ya mabadiliko ya tabia kupitia sinema na vikundi vya ngoma "Alisema

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 5, 2018

Tuesday, September 4, 2018

MAMA AMMWAGIA MWANAYE MAFUTA YA TAA NA KUMCHOMA MOTO

Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa) ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.

Binti huyo amelazwa katika hosptali ya St, Joseph Mbweni katika wodi ya watoto akiwa hawezi hata kutoa maelezo  vizuri.

Akizungumza jinsi mtoto huyo alivyofikishwa hospitalini hapo, Dkt,  Valentino Francis Bangi amesema, mtoto alifikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Agosti 31 kuamkia Septemba Mosi mwaka huu akiwa katika hali mbaya, alikuwa ameunguzwa na moto sehemu ya mbele ya  kifua na usoni.

Dkt, Bangi amesema, mtoto huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa hawezi kupumua wala kuongea, lakini walimpatia huduma ya kumuweka katika hali nzuri na kuanza kurudi katika hali ya ubinadamu .

Dkt. Bangi amesema moja ya huduma waliyoifanya ni kumuoongezea maji pamoja na kumpatia huduma nyingine ya kumfanya apumue.

‘kwa sasa hali ya mgonjwa, anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa kwa sababu alikuwa hawezi hata kuongea, lakini sasa hivi anazungumza ambapo amelazwa wodi ya watoto hospitalini hapa.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii, wa Hospitali hiyo,  Angela Isingo ambaye anashughulikia masuala ya watoto, amesema tukio hilo linasikitisha , kwani wamemuhoji  binti huyo amesema aliyemfanyia kitendo hicho ni mama yake mzazi.

Isingo amesema mtoto huyo ameeleza chanzo cha tukio hilo kwamba, “binti alirudi usiku kutoka shule, mama yake akamuuliza kibubu cha pesa kiko wapi?, kwa sababu ndani kulikuwa na vibubu viwili havionekani kwa hiyo akaenda moja kwa moja kwa huyo mtoto na kumuuliza, anasema mtoto alimjibu kuwa hafahamu kibubu kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji tena kuwa akitafute hadi akipate, akasema akazunguka akapata kibubu kimoja, na pale  ndani haishi peke yake ana baba yake na  ndugu zake wawili na dada yake mkubwa mmoja.

Akasema licha ya kumjibu mama yake kuwa hafahamu kibubu hicho kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji kuwa, lazima aseme kibubu kilipokwenda ndiyo mama yake akachukua mafuta ya taa akamwagia na  kisha  akachukua kiberiti kumuwasha.

Amesema, baada ya kumuwasha ndiyo alihisi maumivu.

Hata hivyo, Isingo amesema, hali ya binti huyo ni nzuri kwa sasa tofauti na mwanzo alivyofikishwa hospitalini hapo alikuwa amevimba kwani kwa sasa maumivu ya ndani yamepungua. 

"Kitendo alichofanyiwa mtoto huyu cha kinyama na cha kikatili sana, nina amini vyombo vya dola vitafanya kazi yake kama nilivyosikia mama yake yupo polisi.

"Ninaamini sheria itashika mkondo wake na mimi nitasimamia kesi hii hadi inafika mahakamani, kwa sababu kesi nyingi za watoto huwa zinaishia njiani wanasema familia ikakae ielewane," amesema Isingo 

Ofisa huyo alisema lazima wasimame kidete kuhakikisha jambo hilo linakomoshwa na anaweza huyu akawa mfano kwa wamama wengine ambao wanawafanyia watoto wao au watoto wa kuwalea.tuwe walinzi wa watoto na si wa kuwafanyia vitendo vya kikatili.

Blogu ya jamii imefanikiwa kufika nyumbani kwa binti huyo na kufanikiwa kuzungumza na mdogo wa binti aliyechomwa moto (jina limehifadhiwa), anayesoma darasa la tatu hapa jijini, 

Akisimulia mtoto huyo ambaye ndiye aliyekuwa ameachiwa nyumba bada ya dada yake mkumbwa kwenda kupeleka chakuila Hospitali amesema, 
“Mama ndiyo alinituma nikanunue mafuta ya taa ya sh 300 pale dukani, (akionyeshea kwa kidole duka hilo), amesema, hakujua mama yake alitaka kufanyia nini mafuta yale, kwa usiku huo.

Alipoulizwa na Diwani wa kata ya bunju  mahali alipo mama yake, amesema, “mama yupo polisi na dada Angel ameenda hospitali kumpelekwa mgonjwa chakula (dada yake).

Amesema,mgonjwa aliunguzwa na mama,sababu alikuwa anachukua hela za mama ndani anaenda kuzila. Amesema wakati dada yake anachomwa yeye na mdogo wake walikuwa humo humo ndani lakini dada yao mkubwa Angel alikuwa nje, 

“Mama  alimuunguzia ndani sisi tukiwa humo humo tulipiga kelele. Nikamshuhudia dada anawaka moto kifuani, wakati huo baba hakuwepo,,baba alipokuja alimkuta Dada yupo ndani hajapelekwa hospitali, baba akauliza mama yake huko kuna nini, hapo sasa sijui mama alimjibuje baba. Tupo watoto wa nne dada Mary ni wa pili.

Amesema,baadae mama yao alimmwagia maji dada yake na kumzima moto ule sisi hatujafurahishwa na kitendo alichokifanya mama.Mama” amesimulia mtoto huyo.

Kwa upande wake, Alex John, Mjumbe na Katibu wa Shina namba tatu, kata ya bunju, ameelezea  tukio hilo la kusikitisha 

Amesema, aliamshwa majira ya saa tano kasoro usiku na dada mmoja ambaye ni jirani yake, aliyemtaja kwa jina la Maria Clement, amesema alimueleza kuwa jirani yangu kamuunguza mtoto na wanapiga makelele 

Nilipopata hiyo taarifa tukaongozana hadi nyumbani kwa mtoto huyo, bahati nzuri tukamkuta mama yake yupo, mume wake na watu wengine nikamuuliza kulikoni? Nipewa taarifa na jirani yenu kuwa mtoto wenu ameungua moto na nyinyi ndio mmemuunguza, wakaniambia kuwa yule ni mwizi.

Ameongeza, Nikawaambia hata kama ni mwizi yuko wapi? Sasa wakati wanataka kunipa maelezo ya kina akaja jirani yangu ambaye ni Abiti Njau akasema kuna nini mbona yule mtoto ameungua namna ile, nikamuuliza yuko wapi? akasema yupo kule kwangu Yale mazungumzo yakaishia pale, kwa hiyo sikupewa maelezo ya kina 

Ikabidi kuongozana na yule jirani yangu ili tuweze kumuona huyo mtoto kuona jinsi gani ambayo tunaweza kumsaidia, tulipofika tukaambiwa tena amekwenda bondeni kwa sababu alikuwa anapiga makelele huku analalamika, yaani alikuwa kama vile ukimchinja kuku halafu ukamuachia si anaweza akakimbia basi ndiyo kitu ambacho kilimtokea huyo mtoto

Wakati tunarudi tena eneo la tukio tukakuta wamemkata. “Kwa kweli nilivyomuona nilihisi kuumia sana, mtoto alikuwa ameungua kupita kiasi. Ili tukio kwa mujibu niliyopewa na dada Maria aliniambia mama mtu ndiye aliyehusika, muda huo sikujua baba mtu yuko wapi. Tulifanya utaratibu na kumpeleka mtoto hospitali baada ya kupata Fomu namba Tatu ya Polisi (PF3) kutoka polisi Mbweni.

Nilipowaeleza watoto kuhusiana na tukio hilo wakataharuki baada ya kumuona mtoto alivyounguzwa ,wakaniuliza nani alifanya hivyo, nikamwambia kwa taarifa ambazo ninazo Mimi hadi sasa mama yake ndiyo alimfanyia kitendo hiki, askari wakamchukua huyo mama wakamuweka chini ya ulinzi wakamuingia ndani.

Akizungumzia suala la baba wa mtoto huyo kuwa ana undugu na mkubwa mmoja wa Jeshi la Polisi kutaka kumaliza suala hilo mezani, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bunju, Ibrahimu Mabeo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya usalama amesema wamesikia kuwa baba wa mtoto yupo uraiani, wataenda polisi yeye pamoja na Diwani kuhakikisha na baba mtu naye anachukuliwa hatua kwa sababu kama na baba naye anatetea jambo hilo la kinyama basi kama viongozi wa kata hatuwezi kulifumbia macho. 

Nae Diwani wa kata hiyo, Elly Nassoro ameeleza kusikitishwa kwake na tukio hilo, kwani kitendo kilichofanywa na  wazazi wa binti huyo ni cha aibu na kibaya. 

“Binti ameungua sana hali yake hatujui itakuwaje tunaomba Mwenyezi Mungu amsaidie ili apone. Kitendo ni cha kinyama kama tulivyomuhoji mtoto akasema mama ndiyo alimtuma kununua mafuta, halafu akachukua kiberiti akamuwasha”.

"Tumefikia hivi Watanzania kweli, kwa kweli inasikitisha sana wito wangu tuzidi kukemea maovu haya ambayo ya anaendelea kutokea kama vile mzazi mwenyewe anaweza kufanya hivi ni jambo la kutisha, tubadilishe," alisema Msingi 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni , Murilo Jumanne Murilo amedhibitisha kutokea tukio hilo ambapo mama wa mtoto huyo wanamshikilia na wakati wowote watampandisha mahakamani.
“Taarifa hii ni ya kwali na mhusika tumeshamkamata na tumemuweka mahabusu na wakati wowote atapandishwa mahakamani kwa tuhuma hizo”amesema Murilo  
 Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa )ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.