NA MWANDISHI WETU,TANGA.
KATIKA kuendeleza kuchangia juhudi za Serikali kuimarisha huduma za Afya
ikiwemo huduma za Ukimwi,Shirika la Benjamini Mkapa kupitia Shirika
lisilo la Kiserikali la Amref chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa
Kupambana na Ukimwi Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) inatekeleza
mradi wa miaka mitatu 2018-2020 Desemba.
Mradi huo wenye kufanya upimaji Jumuishi wa Maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi katika Jamii na Kuhamasisha Jamii kubadili tabia hatarishi ili
kuweza kusaidia kupunguza maambukizi hayo kwa jamii .
Hayo yalisemwa na Afisa Mradi wa Mkoa wa Tanga wa Kifua Kikuu na Ukimwi
Dkt Anastazia Masanja wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanywa na
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwenye viwanja vya Tangamano
mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Dkt Asha Mahita,Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha
Salim,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu na
Mkurugenzi wa Mpango wa Furaha Yangu kutoka Shirika la Benjamini Mkapa
Foundation Rahel Sheiza akizungumza katika uzinduzi huo
Alisema kupitia mradi huo wa kupambana na kifua kikuu na Ukimwi ambao
utekelezaji wake umeanza mwezi Juni 2018,Taasisi imepewa wilaya mbili
ambazo ni Kilindi na Pangani kwa Mkoa wa Tanga .
"Kwa kipindi hiki Shirika la Benjamini Mkapa linatarajia kufikia kata
zote 35 ambapo kati ya hizo 21 ni za wilaya ya Kilindi na 14 ni za
wilaya ya Pangani lengo la upamaji kwa kila kati ni kuweza kupima watu
2081(Jumla 72,839 kwa kata 35).
Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa ni pamoja na uchunguzi wa awali wa
kifua kikuu ambapo watu wote 7082 waliohudhuria waliweza kuchunguzwa
ambao watu 220 walikutwa na dalili za kifua kikuu na kupewa rufaa kwenda
Hospitali ya wilaya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
"Kwa upande wa shinikizo la damu ambapo jumla ya watu 5269 walipimwa
kati yao 182 walikutwa na shinikizo la damu lisilokuwa la kawaida
"Alisema.
Afisa Mradi huyo alisema pia huduma za uzazi wa mpango zilitolewa
ikiwamo vipandikizi,sindano,vidonge ambapo jumla ya wakina mama
waliopata huduma hiyo walifikia 188 na ugawaji wa kondomu ambapo jumla
ya kondomu 5000 zimegawiwa.
"Lakini pia tuliotoa elimu ya mfuko wa Afya ya Jamii ikiwemo ya
mabadiliko ya tabia kupitia sinema na vikundi vya ngoma "Alisema
No comments:
Post a Comment