Tuesday, January 2, 2018

MFANYABIASHARA AJENGA ZAHANATI YENYE VIFAA VYA KISASA NA KUIKABIDHI SERIKALINI

 Mfanyabiashara, Emmanuel Mallya (katikati) akisaini hati na mkataba wa zahanati EB, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila kwenye hafla hiyo ya makabidhiano. Kushoto ni mke wa Bw. Mallya, Bi. Marry Mallya akishuhudia makabidhiano hayo.
 Mfanyabiashara, Emmanuel Mallya (kushoto) akimkabidhi hati na mkataba wa zahanati EB Zahanati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.

Na Mwandishi Wetu, Moshi.

MFANYABIASHARA na mzaliwa wa Kijiji cha Uchau Kaskazini wilaya ya Moshi Vijijini, Emmanuel Mallya, ameikabidhi serikali zahanati ikiwa na vifaa vya kisasa vikiwamo vitanda vya wagonjwa vinavyotumia nishati ya umeme.

Zahanati hiyo inayojukana kwa jina la EB zahanati, imejengwa na mfanyabiashara huyo kwa kutumia nguvu zake mwenyewe bila kuhusisha msaada kutoka Halmashauri ya wilaya ya Moshi wala serikali kuu.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuikabidhi zahanati hiyo kwa serikali, mfanyabiashara huyo alisema wazo la kujenga zahanati hiyo lilitokana na kuwepo na changamoto za umbali wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo.

Alisema changamoto hiyo ilipelekea kuwepo na vifo vya watu wengi vilivyochangiwa na umbali wa upatikanaji wa vituo vya afya na kwamba changamoto hizo ndizo zilizomsukama kuona haja ya kujenga zahanati hiyo.

Alitoa wito kwa mamlaka husika kuitunza zahanati hiyo pamoja na vifaa vitakavyotumika katika kuwahudumia wagonjwa huku akitoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kujitolea katika kuwahudumia wananchi wasio nacho.

“Utajiri unatokana na moyo wa mtu alionao, unaweza ukawa na utajiri na usiwe na moyo wa kuwasaidia wengine, kila mtu amepewa karama na mwenyezi Mungu, muhimu hapa ni namna ya kuzitambua hizo karama,” alisema.

Kabla ya ujenzi huo ulioanza julai mwaka 2013, familia iliyokuwa ikishi mahali ilipojengwa shule hiyo iliridhia ombo la mfanyabaishara huyo la kuachia eneo hilo na kupelekwa kwenye eneo jingine kwa ushirikiano wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Kimasio.

Aliwapongeza familia hiyo kwa kukubali ombi lake la kuliachia eneo hilo na kuongeza kuwa, bila familia hiyo kuridhia kuondoka katika eneo hilo ndoto zake za kujenga zahanati katika eneo hilo zingeishia ukingoni.

Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu alihimiza usimamizi wa karibu wa zahanati hiyo kwa wale watakakuwa wasimamizi baada ya aliyeijenga kuikabidhi kwa serikali.

"Mhehsimiwa Mkuu wa Wilaya, uzoefu unaonyesha kuwa, miradi mingi inayojengwa na wafadhili imekuwa ikiharibika kutokana na kutokuwepo na usimamizi wa karibu, ni rai yangu kuwa tuitunze zahanati hii isijekuwa mazalia ya popo kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya,” alisema.

Alisema mfanyabiashara huyo ametenda wema wa hali ya juu kwa wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini na Vunjo kwa ujumla  na kwamba wema huo kamwe hautafutika ndnai ya mioyo ya wananchi hao. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila, alitoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo kuchangishana kwa kile kidogo walichonacho ili wanunue gari la wagonjwa ambalo litahudumia zahanati hiyo kwa muda wa saa 24.

Alisema uwepo wa gari la wagonjwa katika zahanati hiyo utarahisisha kuwapeleka wagonjwa katika Hospitali kubwa ikiwamo ya Kibosho, Mawenzi na KCMC kwa wale ambao watahitaji kupewa rufaa.

Alisema maendeleo yanahitaji umoja na mshikamano na kuonya kuwa maendeleo hayana itikadi yoyote ya kisiasa kwani zahanati hiyo itahudumia wananchi wote bila kujali huyu ni wa chama gani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alipongeza moyo ulioonyeshwa na mfanyabiashara huyo wa kusaidia watu wenye mahitaji. Pia alitoa wito kwa serikali ya kijiji hicho kuanza mazungumzo na wananchi wanaoishi karibu na zahanati hiyo kuachia maeneo yao ili zahanati hiyo ipanuliwe na kufika hadhi ya kituo cha Afya.


Alitoa wito kwa kila mtu kuchangia chochote alichonacho ndani ya jamii na si lazima iwe pesa na kuwapongeza walioachia eneo ilipojengwa zahanati hiyo wametoa mchango mkubwa sana kwa jamii.

DK. MNDOLWA AKABIDHIWA RASMI OFISI LEO, AAHIDI KUUNDA KAMATI KUTAFUTA UFUMBUZI DHIDI YA KUMOMONYOKA KWA MAADILI KATIKA JAMII YA KITANZANIA

 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo Seif Shabani Mohamed alipowasili Makamo Makuu ya Jumuiya hiyo kwa ajili ya makabidhiano hayo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa  akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Najma Giga wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Mndolwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Makamu Menyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wqzazi Tanzania Abdallah Bulembo akionyesha Katiba ya Jumuiya hiyo kabla ya Kumkabidhi Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hizo Zanzibar Abdallah Haj Haidar
 Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Abdallah Bulembo (kushoto) akikabidhi nyaraka zenye orodha ya mali za Jumuiya hiyo, kwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo, Dk. Edmund Mndolwa, leo Januari 2, 2018, Makao Makuu ya Jumuiya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Zanzibar  Abdallah Haj Haidar. 
 Bulembo akiendelea kukabidhi nyaraka
 Dk. Mndolwa na Bulembo wakisaini nyaraka za makabidhiano
 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania  Zanzibar  Abdallah Haj Haidar na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Seif Shabani Mohammed wakisaini nyaraka upande wa mashahidi
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi
 Dk Mndolwa na Bulembo wakifurahia jambo baada ya makabidhiano ya ofisi
Watumishi wa Jumuiya ya Wazazi Makao Makuu wakiwa kazini wakati wa makabidhiano hayo ya ofisi baina ya Dk Mndolwa na Bulembo PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Na Bashir Nkoromo.

Mwenyekiti mpya wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuunda Kamati ya  kutathmini namna Jumuiya hiyo inakavyolishughulia kwa ufanisi tatizo la kuporomoka kwa maadili katika jamii hapa nchini.

Dk. Mndolwa ametoa ahadi hiyo leo, hayo wakati akikabidhiwa rasmi Ofisi na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mstaafu Abdallah Bulembo, hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania jijini Dar es Salaam.

"Katika hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli alitutaka sisi viongozi wa Jumuiya hii tusikae kimya wakati vitendo vya kuporomoka kwa maadili katika jamii ikiwemo wasanii wa kike kuonyesha sehemu za miili yao zinazotakiwa kusitiriwa. Sasa hili ni agizo lazima mimi na viongozi wenzangu tulipe kipaumbele katika kulifanyika kazi.

Kwa hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi leo hii, miongoni mwa mipango yangu Kama Mwenyekiti ni Kuunda Kamati itakayojikita kwa undani kuhakikisha tunapata njia bora za kudhibiti kuporomoka kwa maadili katika jamii ya Watanzania", alisema Dk Mndoldwa. Alisema, pia atahakikisha katika zama za uongozi wake, Jumuiya ya Wazazi inainuka na kujitegemea vya kutosha kiuchumi ili iondokane na adha ya kuwa ombaomba.

"Jumuiya hii ianazo mali nyingi, kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha fedha zinazotokana na mali au miradi hii zinaingia kwenye hazina ya Jumuia badala ya kupotelea mifukoni mwa wajanja wachache, tukifanikiwa kuthibiti bila shaka tutakuwa na fedha za kutosha", alisema Dk. Mndolwa.

Akimzungumzia Bulembo, Dk Mndolwa amesema, alikuwa kiongozi bora ambaye ameisaidia kwa kiasi kikubwa Jumuiya ya Wazazi, na kwamba katika jitihada zake ameiboresha Jumuia hiyo kwa karibu asilimia tisini.

"Nimejifunza mambo mengi kwa Bulembo, mojawapo ni uvumilivu, huyu ni mvumilivu kiasi kwamba itanibidi kuiga uvumilivu wake ili na mimi nistaafu kwenye Jumuiya hii nikiwa safi kama yeye," Alisema Dk. Mndolwa.

Kwa Upande wake Bulembo aliwataka viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kuthamini sana Waaandishi wa habari kwa kuwapa ushirikiano kila unapohitajika na kwamba yupo tayari kutoa ushauri pale utakapohitaji.

Aliwaasa viongozi wapya kuendeleza mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita huku wakiachana na mabaya yaliyofanyika wakati huo.

"Namna nzuri ya kuongoza ni kuwa karibu na unaowaongoza, msikae nao mbali mnaowaongoza na ikiwa kutakuwa na jambo miongozi mwenu viongozi ambalo haliendendi vizuri utatuzi wake uwe kwenye vikao si kwingineko", Alisema Bulembo.

WAZIRI MKUCHIKA ATEMBELEA TPSC TAWI LA MTWARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (kushoto) akiwasili chuo cha Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Tawi la Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea matawi ya chuo hicho nchini kulia ni Mkurugenzi wa TPSC Tawi la Mtwara Dkt. Emmanuel Shindika,ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (katikati) akipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa TPSC Tawi la Mtwara Dkt. Emmanuel Shindika (kushoto) akiwa katika moja ya madarasa ya chuo hicho tawi la Mtwara ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kutembelea matawi ya chuo hicho nchini, ziara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki.Wengine pichani ni watumishi wa chuo hicho.
Kwaya ya TPSC tawi la Mtwara ikitoa burudani mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Hayupo pichani), aliyefanya ziara fupi chuoni mwishoni mwa wiki sambamba na kupokea taarifa ya tawi na kusikiliza changamoto za watumishi na wanachuo.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Utumishi wa Umma TPSC tawi la Mtwara, wakimsikiliza kwa makini waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika (Hayupo pichani), aliyefanya ziara fupi chuoni hapo mwishoni mwa wiki sambamba na kupokea taarifa ya chuo na kusikiliza changamoto za watumishi na wanachuo.

ZAIDI YA BILIONI 1.2 ZIMETENGWA NA WAKALA WA BARABARA NCHINI TANROAD KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA KUTOKA ULANGA HADI KURUNGU


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akikabidhi kadi ya bima ya Afya kwa mmoja wazee waliokatiwa bima ya afya na Naibu Waziri huyo, Salehe Mgonza katika Mkutano uliofanyika Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa chama na serikali akikabibidhi mikokoteni kwa kikundi cha Umoja waendesha mikokoteni wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ushirikiano katika ulinzi na usalama pamoja na kuwapeleka shule wanafunzi wa kuanza darasa la kwanza.


Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo (kushoto)akijibu swali mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega picha na Emmanuel Massaka,Globui ya jamii.
Baadhi ya Madiwa wani kwakiwa katika mkutano huu
sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano huu.

ZAIDI ya shilingi bilioni 1.2 zimetengwa na Wakala wa barabara nchini TANROAD kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara kutoka Ulanga hadi Kurungu wilayani mkuranga katika Mkoa Pwani.

Akizungumza na wananchi wilayani humo jana katika mkutano wa hadhara wa kufunga mwaka 2017 na kukaribisha 2018 Mbunge wa Jimbo hilo Abdalla Ulega ambaye pia ni Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,alisema tayari serikali imeshatenga fedha hizo.

Ulega aliwaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa katika miaka miwili ya uongozi wake yapo mambo mengi ambayo ameyafanya, lakini barabara ni kero kubwa kwa wanamkuranga hivyo katika juhudi zake amefanikiwa kupata fedha hizo kwa ajili ya kuaza ujenzi huo.

"Ndugu zangu wanamkuranga mwanenu napambana kwelikweli kwa maana najuwa niliahidi na nyie mlinituma na mmeendelea kunituma nami staki kuwaangusha, hivyo kuazia January hadi Februari mwaka huu 2018 ujenzi wa barabara hii ambayo nimetaja itaaza ujenzi. "alisema Ulega

Pia aliongeza kuwa anajuwa kwamba changamoto ya barabara imekuwepo kwa muda mrefu na viongozi mbalimbali wamepita lakini aliwaeleza wasubiri utekelezaji wake kuanzia miezi hiyo.  Akizungumzia eneo la afya wilayani humo,Ulega  aliwaeleza wananchi hao kuwa kwa muda mrefu hospitali ya wilaya ilikuwa haina kipimo cha X-ray lakini kwa jitihada zake amefanikisha kupata kipimo hicho na kitakabidhiwa hospitalini hapo hivi karibuni.

Alisema mbali na hilo lakini pia hospitali hiyo ilikuwa na kero karibu tatu hadi nne ikiwamo na ukosefu wa madawa, huduma ya maji, lakini hivi sasa kero hizo zimeondoshwa kwa kiwango kikubwa.

"Wazee bila shaka sasa mambo yanakwenda vizuri ukilinganisha na tulikotoka na tunaendelea kuboresha huduma hii ikiwamo na kufungua vituo vya afya kwa lengo la kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya. "alisema Waziri Ulega

Pia alisema kuna ongezeko kubwa la Zahanati kutoka 35 hadi kufikia 40 katika vijiji vyote 125 ndani ya wilaya hiyo, nakudai kuwa lengo kufikia 2020 zifikie zahanati 50.

Akizungumzia Elimu Ulega aliwataka wazazi kusimamia suala zima la watoto kwenda shule ambapo alidai kutokana na hamasa ya elimu bure Wilaya ya mkuranga imefanikiwa kutoa mtoto aliyeshika nafasi ya pili kitaifa.

Aliongeza kuwa kutokana na juhudi zinazofanywa na wazazi kwa lengo la kuhakikisha elimu wilayani humo inastawi, ameweza kuchangia saruji mifuko 100 na mabati 100 katika kuunga mkono katika ujenzi wa madarasa Katika shule ya msingi mkuranga mjini

Kwaupande wake Mkuu wa wilaya hiyo Firbeto Sanga akizungumza katika mkutano huo aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya wilaya hiyo ili kukomesha vitendo vya kiharifu.Aliwataka kuwatambua wageni wanaongia kwenye wilaya hiyo nakutoa taarifa sahihi lakini huku akiwakumbusha kupeleka watoto shule wenye umri wa kusoma na kamwe wasisubiri kusukumwa na serikali.