Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akikabidhi kadi ya bima ya Afya kwa mmoja wazee waliokatiwa bima ya afya na Naibu Waziri huyo, Salehe Mgonza katika Mkutano uliofanyika Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa chama na serikali akikabibidhi mikokoteni kwa kikundi cha Umoja waendesha mikokoteni wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza juu ushirikiano katika ulinzi na usalama pamoja na kuwapeleka shule wanafunzi wa kuanza darasa la kwanza.
Mganga mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo (kushoto)akijibu swali mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega picha na Emmanuel Massaka,Globui ya jamii.
Baadhi ya Madiwa wani kwakiwa katika mkutano huu
sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano huu.
ZAIDI ya shilingi bilioni 1.2 zimetengwa na Wakala wa barabara nchini TANROAD kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara kutoka Ulanga hadi Kurungu wilayani mkuranga katika Mkoa Pwani.
Akizungumza na wananchi wilayani humo jana katika mkutano wa hadhara wa kufunga mwaka 2017 na kukaribisha 2018 Mbunge wa Jimbo hilo Abdalla Ulega ambaye pia ni Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi,alisema tayari serikali imeshatenga fedha hizo.
Ulega aliwaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa katika miaka miwili ya uongozi wake yapo mambo mengi ambayo ameyafanya, lakini barabara ni kero kubwa kwa wanamkuranga hivyo katika juhudi zake amefanikiwa kupata fedha hizo kwa ajili ya kuaza ujenzi huo.
"Ndugu zangu wanamkuranga mwanenu napambana kwelikweli kwa maana najuwa niliahidi na nyie mlinituma na mmeendelea kunituma nami staki kuwaangusha, hivyo kuazia January hadi Februari mwaka huu 2018 ujenzi wa barabara hii ambayo nimetaja itaaza ujenzi. "alisema Ulega
Pia aliongeza kuwa anajuwa kwamba changamoto ya barabara imekuwepo kwa muda mrefu na viongozi mbalimbali wamepita lakini aliwaeleza wasubiri utekelezaji wake kuanzia miezi hiyo. Akizungumzia eneo la afya wilayani humo,Ulega aliwaeleza wananchi hao kuwa kwa muda mrefu hospitali ya wilaya ilikuwa haina kipimo cha X-ray lakini kwa jitihada zake amefanikisha kupata kipimo hicho na kitakabidhiwa hospitalini hapo hivi karibuni.
Alisema mbali na hilo lakini pia hospitali hiyo ilikuwa na kero karibu tatu hadi nne ikiwamo na ukosefu wa madawa, huduma ya maji, lakini hivi sasa kero hizo zimeondoshwa kwa kiwango kikubwa.
"Wazee bila shaka sasa mambo yanakwenda vizuri ukilinganisha na tulikotoka na tunaendelea kuboresha huduma hii ikiwamo na kufungua vituo vya afya kwa lengo la kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya. "alisema Waziri Ulega
Pia alisema kuna ongezeko kubwa la Zahanati kutoka 35 hadi kufikia 40 katika vijiji vyote 125 ndani ya wilaya hiyo, nakudai kuwa lengo kufikia 2020 zifikie zahanati 50.
Akizungumzia Elimu Ulega aliwataka wazazi kusimamia suala zima la watoto kwenda shule ambapo alidai kutokana na hamasa ya elimu bure Wilaya ya mkuranga imefanikiwa kutoa mtoto aliyeshika nafasi ya pili kitaifa.
Aliongeza kuwa kutokana na juhudi zinazofanywa na wazazi kwa lengo la kuhakikisha elimu wilayani humo inastawi, ameweza kuchangia saruji mifuko 100 na mabati 100 katika kuunga mkono katika ujenzi wa madarasa Katika shule ya msingi mkuranga mjini
Kwaupande wake Mkuu wa wilaya hiyo Firbeto Sanga akizungumza katika mkutano huo aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano ndani ya wilaya hiyo ili kukomesha vitendo vya kiharifu.Aliwataka kuwatambua wageni wanaongia kwenye wilaya hiyo nakutoa taarifa sahihi lakini huku akiwakumbusha kupeleka watoto shule wenye umri wa kusoma na kamwe wasisubiri kusukumwa na serikali.
No comments:
Post a Comment