Saturday, October 1, 2016

Waziri Nnauye azindua Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China Jijini Dar es Salaam

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Sanaa na Utamaduni umekuwa chachu kubwa katika kuwajengea uwezo wasanii wetu na kutekeleza shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na wataalamu kutoka pande hizi mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizindua wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China katika Ukumbi wa Utamaduni wa watu wa China leo jijini Dar es Salaam.

 “Kwa miaka mingi Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano uliotoa fursa kwa watu wake kujifunza shughuli za sanaa na kiutamaduni zilizoko katika kila nchi hivyo kuendeleza na kuuenzi ushirikiano uliopo katika sekta za Sanaa na Stamaduni” amesema Mhe. Nnauye

Mhe. Nnauye amesema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili umeweza kukua, kuboresha na kuendeleza wasanii wetu hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ambapo hutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni na kuwapa wasanii wa hapa nchini fursa ya kufanya maonyesho kama haya nchini China.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa Maonyesho ya Utamaduni wa China hapa nchini yanatoa fursa nzuri kwa wananchi wa Tanzania kuelewa na kujifunza utamaduni na sanaa ya China, kuimarisha ushirikiano wa utamaduni wa China na Tanzania pamoja na kukuza urafiki wan chi hizi mbili.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin amesema kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu kwa sekta ya Sanaa na Utamaduni na kujifunza mambo mapya ili kuendeleza Utamaduni, ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili.

Wiki ya Maonyesho ya Utamaduni wa China itakuwa na maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya sarakasi ya Kichina, maonyesho ya picha, hadhara za opera za China, Udaktari wa kijadi wa China na Utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. (katikati mbele) ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akikagua picha mbalimbali za kiutamaduni wa China wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei.

 Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni wa China wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto waliokaa ni Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong
 Kikundi cha Utamaduni na Sanaa cha Jiangxi kikionyesha sarakasi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Msanii kutoka China akionyesha mchezo wa utamaduni wa mazoezi maalumu yanayojenga afya yaitwayo Qigong wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (wapili kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha China nchini Bw. GAO Wei na wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin

Washiriki wa Maonyesho ya wiki ya Utamaduni wa China kutoka Chama cha Mchezo wa WUSHU Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akimsikiliza Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong (kulia) wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Utamaduni wa China leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni kutoka Jiangxi China Bw. Chen Hongmin.

DC ARUSHA MH. GADRIEL DAQARRO AZINDUA UTAFITI WA SAUTI ZA VIJANA JIJINI ARUSHA ULIOFANYWA NA BRITISH COUNCIL

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini,kulia ni Meneja Mradi wa British Council Tanzania,Elizabeth Nkanda. 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini. 
Mtaalamu wa sera za ufugaji, Carolyn Kandusi akiongoza shughuli nzima iliyofanyika jijini Arusha. 
Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana. 
Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana. 
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo. 
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo. 
Mtaalamu wa masuala ya Mitaji,Baraka Megiroo akiwapa mbinu vijana wenzake namna ya kutumia fursa zinazojitokeza kujikwamua kiuchumi. 
Mtaalamu wa masuala ya kijamii,Hadija Hassan akizungumza na vijana umuhimu wa
kujiamini na kuzikabili changamoto mbalimbali,kushoto ni Mtaalamu mwenzake Gladys Mmari na Mary Bird 
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo.

WAFANYAKAZI WA MANISPAA YA UBUNGO WAUNGANA KUPANDA MITI KATIKA MANISPAA YAO JIJINI DAR LEO.

Kaimu Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo, Joseph Alute akipanda mti katika kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipowataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kupanda miti kwaajili ya kutunza mazingira pamoja na kupendezesha mazingira ya jiji.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari wakipanda mti jijini Dar es Salaam leo.

 Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dkt. Sivila Mwanisi akishirikiana na mfanyakazi wa manispaa ya Ubungo Kupanda miti ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam za kupanda miti  jijini Dar es Salaam leo.
 Wanafunzi wakiwa wamebeba miti kwaajili ya kupanda.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wakipanda miti jijini Dar es Salaam leo.

baadhi ya wafanyakazi wa manispaa ya Ubungo akipanda  miti jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Yasir Adam.

MASAUNI AZITAKA TAASISI ZA KIDINI NCHINI KUPAMBANA NA MAOVU, AFUNGUA MKUTANO WA 47 WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia meza kuu) akimsikiliza Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakati alipokuwa anatoa hotuba yake katika Mkutano wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry wakati Naibu Waziri huyo alipomaliza kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo wa 47 unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 47 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

BRITISH COUNCIL WAZINDUA UTAFITI WA SAUTI ZA VIJANA JIJINI ARUSHA

Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini,kulia ni Meneja Mradi wa British Council Tanzania,Elizabeth Nkanda. 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini. 
Mtaalamu wa sera za ufugaji, Carolyn Kandusi akiongoza shughuli nzima iliyofanyika jijini Arusha. 
Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana. 
Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana. 
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo. 
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo. 
Mtaalamu wa masuala ya Mitaji,Baraka Megiroo akiwapa mbinu vijana wenzake namna ya kutumia fursa zinazojitokeza kujikwamua kiuchumi. 
Mtaalamu wa masuala ya kijamii,Hadija Hassan akizungumza na vijana umuhimu wa kujiamini na kuzikabili changamoto mbalimbali,kushoto ni Mtaalamu mwenzake Gladys Mmari na Mary Bird

Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo.