Wednesday, July 2, 2014

taswira mbali mbali za sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi  wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa wakati wa Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu wa Jimbo la Tabora,Mhasamu Paul Ruzoka akizungumza machache wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiwa na wasaidizi wake wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa akiongoza ibada maalum ya Jubilei hiyo.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,Mhashamu Severini Niwemugizi akizungumza katika sherehe hizo,wakati alipokuwa akitoa salamu za Baraza hilo kwa Serikali.
Mh. Lowassa akiwapungua mkono Waumini wakati alipokuwa akitambulishwa.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa wakati wa Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono kwa kuwasalimia waumini waliofika kwenye Sherehe za Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa,Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa,iliyofanyika Julai 01,2014 kwenye Kanisa Kuu la Katolini Mjini Iringa.
Halaiki ya vijana.
Sehemu ya Waumini walioshiriki kwenye Jubilei hiyo.

Tuesday, July 1, 2014

Balozi Seif Ali Iddi atembeela Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitolea na kujizatiti katika kuwaondoshea usumbufu wa upatrikanaji wa huduma muhimu wananchi wake katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Alisema kipaumbele kimewekwa zaidi katika kuhakikisha huduma za  maji safi na salama pamoja na umeme zinapatikana ili kuwapatia fursa nzuri wananchi hao kuelekeza nguvu zao katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni kiliopo Shehia ya Kidoti ndani ya Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuwapa matumaini kwamba Transfoma inayofungwa  hivi sasa katika kijiji hicho iliyotolewa na Serikali kuu ni hatua za awali za kuwaondoshea usumbufu huo.
“ Huduma ya umeme katika Kijiji cha Mvuleni imeshafika. Kilichopo hivi sasa ni kutakiwa muwe na subra kwa ajili ya kusogezwa kwenye maeneo yenu ili mpate kuutumia”. Alisema Balozi Seif.
Aliwaomba Wananchi hao kuendelea kuwa wastahamilivu katika kipindi hichi ambacho Serikali imeamuwa kuwapatia huduma za maji safi na salama  wananchi hao kwa njia ya mgao kwa kutumia magari ya Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } hasa katika kipindi hichi kigumu cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Alisema Serikali Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } na Shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } itaendelea kuimarisha miundo mbinu ya miradi ya maji na umeme ili huduma zote mbili zipatikane na kuwafaidisha wananchi katika muda wote kijijini hapo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatahadharisha Wananchi hao wa Mvuleni kuwa macho na baadhi ya watu wanaojinasibu kwamba huduma za miradi ya maji ndani ya eneo hilo imetekelezwa chini ya ufadhili wao.
“ Mradi wa Maji uliomo ndani ya Jimbo la Nungwi umeanza tokea awamu ya Sita ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoongozwa na Mheshimiwa Amani Karume na baadaye Rais wa sasa Dr. Sheni akauzindua Mradi Mkubwa wa Tangi la Maji ndani ya Jimbo hilo. Sasa anapokuja mtu akasema huduma hizo kaleta yeye wakati hata hajaingia madarakani na mradi huo upo tayari, mjue huyo kwa kweli anakuongopeni mchana “. Alieleza Balozi Seif.
Akitoa ufafanuzi wa miradi mbali mbali ya maji ndani ya jimbo la Nungwi   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar  { ZAWA } Dr. Mustafa Garu alisema Jimbo hilo linatarajiwa kufaidika na mradi wa maji ulioanzishwa na Serikali kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kiislamu { BADEA }.
Dr. Garu alisema  wahandisi wa Mamlaka hiyo hivi sasa wako katika hatua za kukamilisha ujenzi wa tangi kubwa la kuhifadhia maji liliopo katika eneo la Mwanguo ambalo linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.
Alisema Wataalamu wa Mamlaka hiyo wamekuwa wakiendelea  kuchimba idadi  kubwa ya visima katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba  ili kujiepusha na athari ya kutumbuka kwa maji ya chumi katika vianzio vya maji.
Wakitoa Taarifa yao fupi Wananchi hao wa Kijiji cha Mvuleni wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua inayoendelea kuchukuwa ya kuwapunguzia matatizo yanayowakabili zikiwemo huduma za Maji safi na Umeme.
Hata hivyo Wananchi hao walisema visima vinavyosambaza huduma za maji katika maeneo ya fukuchani kutoka  Kiashange na Kigongoni kwa wakati huu havikidhi kabisa mahitaji  ya wanajamii wa eneo hilo kikiwemo kijiji chao.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis aliiomba Serikali kupitia Mamlaka inayohusika na huduma za maji safi na salama kufanya utafiti  ili kujua tatizo linalosababisha usumbufu wa maji katika Jimbo la Nungwi.
Mh. Pembe aliafiki na kuunga mkono hoja ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji ya kutaka kufanywa uchunguzi huo kutokana na  uwepo wa zaidi ya Visima 13 ndani ya Jimbo la Nungwi wakati uwezo wa upatikanaji huduma hiyo umekuwa na mashaka.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/7/2014.

NSSF YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA 38 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ‘SABASABA’

Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mrs Eunice Chiume (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa uhusiano wa shirika hilo katika maonyesho ya Sabasaba  yanayoendelea katika viwanja ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Meneja Kiongozi, Uhusiano na huduma kwa wateja Mrs Eunice Chiume wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii akifafanua jambo kuhusu Bima ya Afya kwa mwanachama alietembelea Banda hilo katika maonyesho ya Sabasaba.


MADEREVA WA BODA BODA WILAYANI SIMANJIRO MKOANI MANYARA WAANDAMANA

Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ASP Lwitiko Norman Kibanda, akizungumza na madereva wa pikipiki za kubeba abiria ambao juzi waliandamana hadi kwenye kituo hicho wakipinga kutozwa fedha sh22,000 na maofisa biashara wa wilaya hiyo, waliodai kuwa tozo hizo ni amri ya Mamlaka ya Usafirishari wa vyombo vya usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra).


Madereva wanaoendesha pikipiki 800 wa kubeba abiria, maarufu kama bodaboda wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiaro Mkoani Manyara, wameandamna hadi kituo cha polisi Mirerani, wakipinga kitendo cha maofisa biashara wa wilaya hiyo kuwataka walipe sh22,000 za tozo la Mamlaka ya usafirishaji wa vyombo vya majini na nchi kavu nchini (Sumatra).

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, ASP Lwitiko Kibanda, waendesha bodaboda hao walidai kuwa wamechoshwa kunyonywa na maofisa biashara hao kwani tozo hizo hutolewa eneo hilo peke yake hivyo wao wanagoma kulipa kwani wanaonewa na hawapo yatari kulipa kiasi hicho.

Mmoja kati ya madereva hao Rashid Omary alisema maofisa biashara hao waliwaeleza suala hilo siku moja na kesho yake wakaanza zoezi la kukamata pikipiki zao ili hali hawakupatiwa elimu wala kushirikishwa kwenye suala hilo, hivyo hawapotayari kulipa kiwango hivyo kwani wamechoka kunyonywa kila mara.

“Tunashangazwa kuambiwa tutoe sh22,000 za Sumatra ili hali maeneo mengine ya Arusha, Kilimanjaro au wilaya ya Simanjiro kule Landania, Orkesumet na Naberera hawalipishwi, kama sheria ya kunyoa nywele watu wote imepitishwa kwanini sisi tuwe na vipara wengine wawe na nywele, hatukubali kulipa hizo fedha,”  alisema Omary.

Naye, Geofrey John alisema wabunge walifuta tozo za pikipiki za kubebea abiria hivyo wanashangazwa na maofisa biashara wa wilaya hiyo kuwataka walipe fedha hizo, hivyo watagoma kutoa fedha hizo kwani hivi sasa kila mmoja anatambua haki zake na hawatakubali kuburuzwa tena.

Kwa upande wake, Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, ASP Lwitiko Kibanda aliwaeleza waendesha bodaboda hao kuwa wanatakiwa wakutane tena na maofisa biashara hao ili kuzungumzia suala hilo kwani kodi ya Serikali ni lazima ilipwe.'

“Tatizo ni kutotolewa kwa elimu juu ya suala hili kwani wengine waendesha bodaboda siyo mali zao ni  waajiriwa hivyo, tujipange upya kwa maofisa biashara na ninyi bodaboda tukutane na viongozi wenu ili mueleze ipasavyo na mshirikishwe kutokana na jambo hili,” alisema Kibanda.

Hata hivyo, Ofisa biashara wa wilaya ya Simanjiro, Peter Sanga alisema wanatoza sh22,000 za Sumatra wilayani humo, kwa pikipiki inayosafirisha abiria  yenye magurudumu mawili na pikipiki za magurudumu matatu (bajaji) na texi kwa mujibu wa sheria ya Bunge.

“Tozo  hiyo ni halali kulipwa na hudumu kwa muda wa mwaka mmoja na endapo mtu akilipia mwezi Mei au Julai mwaka huu, atatakiwa kulipa tena mwakani mwezi Mei au Julai na siyo vinginevyo, hivyo waendesha pikipiki za kubebea abiria ni lazima walipie pikipiki hiyo,”alisema Sanga.



Alisema Bunge halikufuta tozo hizo, kwani waliziachia na pia ada ya zimamoto kwenye pikipiki zinazolipiwa sh10,000, bima ambayo hutozwa wastani wa sh50,000 na sh22,000 ya ada ya Sumatra na ombi la kukatiwa tozo hiyo, hivyo pikipiki za kubebea abiria zinatakiwa kulipa fedha hizo za Serikali.

YATIMA KITUO CHA MWANDALIWA WAWEZESHWA KUANZISHA MRADI WA KUJIPATIA KIPATO

  Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Bunju, jijini Dar es salaam. Vodocom ilitemebela kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondeshwa na kituo hicho. 
 Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Jamii wa Vodafone Laura Turkington akiwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Mwandaliwa wakifurahia picha kupitia simu ya mkononi ya Laura. Wafanyakazi wa Vodacom  walitembelea kituoni hapo kukakidhi hundi ya Sh. 20 kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji unaondehswa na kituo hicho
 Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano ya Vodacom Rosalyn Mworia akigawa vitabu vya kujifunzia mambo mbalimbali vilivyochangwa na wafanyakazi wa Vodacom kusaidia watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa. Mbalina vitabu na vifaa vya kuchezea, Vodacom Foundation nayo ilikabidhi Sh 20 Milioni kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.
 Mkurugenzi wa Kituo cah mwandaliwa Islami cha Bunju jijini Dar es salaam Halima Ramadhan akiipitia kwa umakini mfano wa hundi mara baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa Vodacom. Fedha hizo zimetolewa na Vodacom Foundation   kusaidia mradi wa ushinjai na ufugaji wa kituo hicho.


 Mmoja wa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania akiwagawia vifaa vya kuchezea watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwemo pia  vitabu. Mbali na vitu hivyo, wafanyakazi ho walikabidhi hundi ya Sh 20 Milioni iliyotolewa na Vodacom Foundation kusiadia mradi wa ushonaji na ufugaji kituoni hapo. 
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Monalisa Jovin akiwagawia vitabu watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwemo pia  vifaa mbalimbali vya kuchezea Mbali na vitu hivyo, wafanyakazi ho walikabidhi hundi ya Sh 20 Milioni iliyotolewa na Vodacom Foundation kusiadia mradi wa ushonaji na ufugaji kituoni hapo.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Mariam Abdallah akiwafundisha kusoma baadhi ya watoto wa kituo cha yatima cha Mwandaliwa vilivyotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwemo pia  vitabu. Mbali na vitu hivyo, wafanyakazi ho walikabidhi hundi ya Sh 20 Milioni iliyotolewa na Vodacom Foundation kusiadia mradi wa ushonaji na ufugaji kituoni hapo.
 =======  =======  =======
Yatima Kituo cha Mwandaliwa wawezeshwa kuanzisha mradi wa kujipatia kipato
Dar es Salaam, Julai 1, 2014 … Kituo cha Kiislamu cha kulelea watoto yatima na ushauri  cha Mwandaliwa Islamic Orphans Home and Counseling Support (MIOCA’S) kilichopo Mbweni jijini dar es salaam kimepokea Sh 20 Milioni kutoka Vodacom Foundation kusaidia mradi wa ushonaji na ufugaji ili kujijenga kiuchumi.
Fedha hizo zimekabidiwa kituoni hapo wakati na wafanyakazi wa Vodacom waliotembelea kituo hicho kwa lengo la pmaoja na mambo mengine kuwaislisha pia Zawadi mbalimbali walizozikusanya wka ajili ya watoto wanaelelewa kituoni hapo.
Akikabidhi hundi ya fedha hizo kwa niaba ya Vodacom Foundation, mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Angela Mwakasege amesema Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation wakati wote inaguswa na changamoto zinazoizunguka jamii ikiwemo suala la watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu.
Amesema hatua ya kukabidhi fedha hizo pamoja na zawadi za vitabu na vifaa mbalimbali vya kuchezea watoto ni kielelezo cha jinsi ambavyo wafanyakazi na kampuni kwa ujumla inayoguswa na kusukumwa kusaidia jamii na kuweka mbele ajenda ya kusaidia kukabiliana na changamoto hizo
“Leo tunafuraha sana kufika hapa, tunawapenda sana na tunaimani kwamba hiki tunachpowakabidhi kitawasaidia kutimiza lengo lenu la kujijengea uwezo wa kiuchumi kupitia miradi mnayokusudia kuianzisha ya ushonaji na ufugaji.”Alisema Mwakasege
“Kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Vodacom kipekee tunawpongeza sana walezi na viongozi wa kituo hiki kwa namna mlivyokubali kujitoa kuwalea watoto hao. Sisi tunatambua kuwa hiyo sio kazi rahisi, tunawatia moyo mzidi kujitoa kwa ajili ya akzi hii.”Alisema 
Kituo hicho chenye watoto 94 kinatarajia kuanzisha miradi ya ushonaji na ufugaji itakayotumika kukiwezesha kituo kuwa na vyanzo vya mapato na pia kuwa na fursa ya kuwajengea uwezo wa stadi za kazi na kujiajiri watoto ili kuwapa uwezo wa kujitegemea katika siku za usoni.
Kwa sasa kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea misaada ya wahisani mbalimbali, lakini kuanzishwa kwa mradi huo wa ufugaji kuku wa nyama na ushonaji kutawezesha kituo hicho kuounguza utegemezi wa wahisani.
Akisoma maelezo ya kituo na shukrani kwa Vodacom Foundation na wafanyakazi wa Vodacom kw akile walichowawezesha, Katibu wa kituo hicho Omary Ramadhan amesema watoto walio wengi hupatikana kwa kuletwa kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni na husomeshwa na wengi wao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu kuanzia ya chekechea.
Akizungumzia msaada huo, xx alisema “ Tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu na baadae kukubalika kwa ombi letu ka kusaidia fedha kufadhili mradi wa ufugaji na ushonaji. Tunajua haikuwa kazi nyepesi, tulihataji kuwa wavumilivu lakini hatiame tuanshukuru sana kuona leo tunaelekea kutimzia ndoto yetu ya kuwa na miradi ya kiuchumi.”

UZINDUZI RASMI WA FARIDAS FOUNDATION WAFANA

Mkurugenzi  Farida A. Sekimonyo wa Faridas Foundation Akiomba Sala ya  Uzinduzi Rasmi wa Foundation
 Mshehereshaji wa Shughuli ya uzinduzi wa Faridas Foundation Taji Liundi
 Elias Masaki katibu mkuu 'CHAWATA' na pia Mweka Hazina Shirikisho la watu wenye ulemavu akichangia  mawazo kuhusiana na jinsi Farida Foundation Inavyofanya kazi zake kwa Jamii
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia maada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa Faridas Foundation
Kassim  Kibwe Katibu wa "SHIVYAWATA" Temeke na Mwenyekiti wa Albino  akichangia maada Iliyokuwa ikiendelea katika uzinduzi wa Faridas foundation
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini Uzinduzi wa Faridas Foundation
Afisa Miradi wa Faridas Foundation Bw.Lumanus  akijadiliana Jambo Na Mkurugenzi Wa Faridas Foundation Bi Farida A.Sekimonyo
 Wasanii walemavu wajulikanao kama Mabaga Fresh waliojitokeza kutumbuiza kwenye uzinduzi wa Faridas Foundation wakifurahia mada zilizokuwa zinatolewa
 Kikundi  cha Mabaga Fresh Wakitoa Burudani kwenye uzinduzi wa Faridas Foundation
 Mkurugenzi wa Faridas Foundation Akimkabidhi zawadi ya pointer  Mshehereshaji wa Shughuli hiyo Bw.Taji Liundi
 Afisa Miradi wa Faridas Foundation akikabidhiwa cheti cha Uadilifu na Mkurugenzi wa Foundation hiyo
Mkurugenzi wa Faridas Foundation(kulia) Akiwakabidhi cheti cha  Ushirikiano wawakilishi wa Global Publisher
 Mwakilishi wa mtandao wa Dj Sek Blog akipokea Bw.Geofrey Adroph Cheti Kwaniaba ya Mkurugenzi wa mtandao huo

 Keki ya maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa Faridas Foundation
 Mkurugenzi wa Faridas Foundation Bi Farida A,Sekimonyo akimlisha keki mama yake mzazi kwa niaba ya wageni wote walioalikwa kwenye uzinduzi huo
Shampeni ikiandaliwa kufunguliwa
 Shampeni ikiwa imefunguliwa kwa ajili ya uzinduzi Wa Faridas Fondation
 Wakigonga glass kiitakia Heri Faridas Foundation
 Mshehereshaji wa Uzinduzi wa Faridas Foundation akipiga mnada picha kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Foundation
  Mshehereshaji wa Uzinduzi  akipiga mnada fulana yenye nembo ya Faridas Foundation kwa ajili ya kuchangia mfuko wa Foundation
 Mmoja ya wageni akichangia Kiasi cha pesa katika mnada wa picha iliyokiuwa ikizungushwa katika ukumbi huo
Burudani ikitolewa ndani ya ukumbi katika kupamba uzinduzi wa Faridas Foundation
Mmoja wa wafanyakazi wa Faridas Foundation akifurahia Burudani zilizokuwa zikitolewa ndani ya ukumbi katika uzinduzi Rasmi