Saturday, November 3, 2012

JK azindua Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia jijini Arusha

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kuaindua rasmi Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha  Sayansi na Teknolojia  jijini Arusha akiongozana Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo  hicho
 Rais Kikwete akipata maelezo juu ya utafiti mbalimbali unaofanywa na wanafunzi Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha  Sayansi na Teknolojia  jijini Arusha

Maelezo ya utafiti
Mdau akielezea utafiti wake






Meza ya Serikali ya Chuo


Maua kwa mgeni rasmi
Kukata utepe
Rais Kikwete akifunua pazia kuzindua sanamu ya Mzee Nelson Mandela
Sanamu ya Mwalimu Nyerere ikizinduliwa
Mgeni rasmi akisindikizwa kuelekea meza kuu
Ni siku ya furaha na fahari kwa mdau Pallangyo
Uzinduzi wa plaque ya Taasisi
Maelezo ya utafiti wa vyakula na madawa asilia
Wageni Mashuhuri wakiwa jukwaa kuu
Wakuu wa Mifuko ya Taifa ya Jamii
Viongozi mbalimbali
Wageni mashuhuri jukwaa kuu
Kwaya ya Chuo ikiwa kazini
Burudani toka bendi ya Polisi
Ngoma ya wasanii wa JKT Oljoro
Kwaya ya JKT Oljoro ikitumbuiza
Dr Frannie Leautier, ACBF Executive Secretary  speaks
Rais Kikwete akipokea zawadi toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Burton Mwamila huku Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na Mkuu wa Chuo akishuhudia
Maelezo ya utafiti wa DNA
Rais Kikwete akiongea na waalikwa
Rais Kikwete akikabidhi hati ya kiwanja cha chuo

Wageni wakishangilia
Sauti na muziki toka Clouds FM Arusha
Rais Kikwete akisalimiana na Mzee Edwin Mtei
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari
Ni wakati wa picha za pamoja na wadau







Picha ya mgeni rasmi na wanafunzi waliokuwa ushers wa siku hiyo




Friday, November 2, 2012

sherehe ya kumuaga luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo

Askari wa kikosi cha bendera kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwa mwendo wa haraka mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.

Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakitoa heshima kwa mwendo wa pole mbele ya Luteni Jenerali Mstaafu A Shimbo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiangalia kwa furaha funguo za gari aina ya Toyota landcruiser alilopewa zawadi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo alilitumikia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 41 huku Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimuangalia. Sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi hilo Mgulani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meja Generali Grace Mwakipunda.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange akimkabidhi hati ya utumishi Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (aliyesimama kwenye gari) akisindikizwa maafisa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiwa ni kuhitimisha sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiangalia gwaride la sherehe za kumuaga Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (hayupo pichani) zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.
Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo akikagua kikosi cha askari wa kike kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa sherehe za kumuaga rasmi zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam. Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo amelitumikia jeshi hilo kwa zaidi ya miaka 41 kwa kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na mnadhimu mkuu wa Jeshi.
Ndugu, jamaa na marafiki wa Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (wan ne mstari wa mbele kulia) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe za kumuaga zilizofanyika leo katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mgulani jijini Dar es Salaam.Wa katikati mstari wa mbele ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Davis Mwamnyange. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Wednesday, October 31, 2012

Ligi kuu ya Vodacom sasa kwenye mtandao

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom,Rene Meza
· Wateja kupata taarifa kupitia SMS, Facebook na Twitter.
·Yatoa pongezi kwa vyombo vya habari na timu.

Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata taarifa na matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia njia ya simu za kiganjani na intanet.

 Kupitia mifumo mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata matokeo ya mechi mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na ujumbe mfupi wa maneno na mitandao ya kijamii. Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema, Mtandao wa Vodacom una miundombinu ya kutosha na unaongoza katika masuala ya teknolojia.
 
Hivyo itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya nchi kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom. “Licha ya ligi yetu kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super Sport.

 Tumejipanga sasa kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda wote kwa kila mchezo na kila tukio katika soka, Mashabiki watapata taarifa za ligi popote watakapokuwa,” alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet matukio haya yatapatikana kupitia Facebook na Twitter na mitandao mingine ya kijamii.” 

“Ili kupata matokeo na taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha atachagua VODACOM FLAVA na akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa na matokeo ya mechi mbalimbali” Aliongeza kuwa, 

“ Kwa wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani huduma hizo zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka watatembelea Ukurasa wetu wa facebook na Twitter na kupata taarifa mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia zawadi kwa kujibu maswali mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,” 

Aidha Mkurugenzi huyo alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa inayofanya katika kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali hususani ligi kuu ya Vodacom kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na Mitandao ya kijamii.

 “Vyombo vya habari ni wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa taarifa hizi wanastahili pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga mkono kwa namna moja ama nyingine katika jitihada za kukuza soka la Tanzania na tunaamini tutafika mbali.” 

Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki katika ligi kwa kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa ni ishara ya ukuaji wa soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo kuu la Vodacom. 

“Ligi sasa imekuwa na msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mechi,hadi sasa timu zote zimeonesha kiwango kikubwa na soka la kuvutia tunatarajia maendeleo haya yataleta tija hata kwa timu yetu ya Taifa kufanya vizuri. 

Vipaji vingi vinaonekana na ajira kwa vijana imeongezeka kupitia michezo,” alihitimisha Meza. Kampuni ya Vodacom katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa ofa mbalimbali msimu huu kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50, Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB 50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki. 

Pamoja na mambo mengine kampuni hiyo inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji tiketi kwa wateja wake kutumia huduma ya M - pesa kununua tiketi za mechi mbalimbali.