Sunday, November 6, 2011

VODACOM TANGA CYCLE CHALLENGE 2011

Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa  akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja  na nusu Mshindi wa kwanza wa mbio za  Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 140,Hassan Sharif (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo kwa kutumia  muda wa masaa 4:13.07 wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.
Mwaandaaji wa Mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge Sophy Wakati akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  kushoto kabla ya mbio hizo kuanza,wa pili kutoka kushoto Buruhani Yakub ambae ni  Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communication na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Washiriki mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa walemavu wakimaliza mbio hizo hapo jana mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana mjini Tanga ambapo Hassan Sharif aliibuka mshindi kwa kutumia masaa 4:13.07 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja na nusu.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu ,afya na uchumi,  Seleboss Mustafa, (kushoto)akimkabidhi  shilingi 75,000.mshindi wa  tatu wa mbio za Vodacom Tanga cycle  Challenge kwa upande wa Kilomita 140 Revocatus Sebastian, aliyetumia  Masaa 4: 15.52 mashindano hayo yaliyoanzia katika uwanja wa Mkwakwani  mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo ,wanaoshuhudia wapili kutoka kushoto ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude,Michael Kasun ambae ni msimamizi wa mawakala wa Vodacom kanda ya Kaskazini.
Washindi wa kwanza na wapili wa mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa kilometa 80 wakimaliza mbio hizo,ambapo Kudushi Nkandi  kushoto aliibuka mshindi na Mohamed Bundala akawa mshindi wa pili.
Mshindi wa  kwanza  wa Kilomita 140 wa mbio za  baiskeli za “Vodacom Tanga cycle Challenge “  Hassan Sharif akimaliza mbio hizo kwa kwa kutumia masaa 4.13.07 .ambapo mbio hizo zilianzia katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo  hapo jana. 
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja Mshindi wa kwanza wa mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 80,Kadushi Nkandi (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.

HASSAN Shariff ametwaa ubingwa wa mashindano ya Mbio za baiskeli ya (Vodacom Tanga Cycle Challenge 2011)baada ya kumaliza mwendo wa umbali wa kilomita 140 akiwa mbele ya washiriki wengine.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Wakati Sports Promoter na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania yalishirikisha makundi matatu ambayo ni ya baiskeli zilizotengenezwa maalumu kwa michuano ambapo washiriki walipita Wilaya za Muheza na Korogwe na kurejea Tanga mjini umbali wa kilomita 140.

Sharrif alitwaa ubingwa huo akiwa katika kundi la baiskeli maalumu za mbio hizo ambapo alimaliza michuano hiyo akiwa amekimbia kwa saa 4.13.07 na kufuatiwa na Juma Kashinde aliyetumia muda wa saa 4.14.52 wakati mshindi wa tatu alikuwa Revecatus Sebastian aliyemaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.15.30.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Hamis Milikioni aliyekimbia kwa saa 4.28.08, Mathew Alberto alimaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.35.06 huku Athumani Muya akikimbia kwa saa 4.38.07.

Kundi la baiskeli za kawaida lilianzia Tanga mjini kupitia Tanganyika Wilaya ya Muheza umbali wa kilomita 80 ambapo Kadushi Nkandi aliongoza kwa kutumia muda wa saa 1.56.00,Issa Kashinde alishika nafasi ya pili kwa kumaliza akiwa ametumia muda wa saa 1.57.12 huku Mohamed Bundala alitumia saa 2.15.13.

Baiskeli za miguu mitatu zilikuwa za kulizunguka jiji la Tanga ambapo aliyeongoza ni Jackson Kinyusa aliyekimbia kwa dakika 30.20 akifuatiwa na Mohamed Balozi dakika 32.16 huku Medrin Sabuni akishika ushindi wa tatu kwa kukimbia kwa dakika 45.02.

Mgeni rasmi ,Mohamed Mustapher ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nguvumali na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Tanga,aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuukumbuka mchezo wa baiskeli na kuwaomba kuboresha zaidi mwakani kwani Tanga ni mkoa wenye vipaji vingi.

Mgeni huyo ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Tanga alimkabidhi Shariff kiasi cha sh 150,000, Kashinde sh 100,000,Revocatus sh 75,000 wakati washindi wa kwanza katika makundi ya baiskeli za miguu mitatu na za kawaida walizawadiwa sh 100.000,wa pili sh 75,000 wa tatu sh 50,000 huku washiriki wengine wakipewa kifuta jasho cha sh. 10,000 kwa kila mmoja.

Afisa Udhamini wa Vodacom,Ibrahim Kaunde alisema huu ni mwaka wa pili kwa Kampuni yake kudhamini mashindano ya baiskeli kwa Mkoa wa Tanga na Mwanza lengo likiwa ni kuimarisha mchezo huo katika maeneo hayo kwa kuwa unaonekana kupendwa zaidi.

“Kimsingi Vodacom imejikita kudhamini michuano ya baiskeli Tanga na Mwanza kutokana na ari na mwamko uliopo kama ambavyo tunavyodhamini riadha mkoani Kilimanjaro”alisema Kaunde.

Friday, November 4, 2011

Kiota cha kisasa cha Msemo Hotels and Tours LTD mjini Mtwara

Mama balozi wa finland hapa nchini Tanzania Ms Sinikka Antila aliandaa chakula cha jioni katika hotel ya Msemo mjini Mtwara na kuhudhuliwa na watu wapatao 80 akiwemo Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Joseph Simbakalia na viongozi wengine waandamizi wa mkoa wa mtwara,waliohudhuria wengine ni maafisa waandamizi toka wizara ya mambo ya nje na ushurikiano wa kimataifa Tanzania pamoja viongozi wa finaland waliokua katika msafara.

Wageni walifurahi sana na hawakuamini kama wapo Mtwara kwa huduma bora ya kiwango cha hali ya juu na mandhari ya eneo husika. Msemo Hotels and Tours LTD ni hotel pekee ya kitalii ya kujivunia kwa mkoa wa Mtwara.

Chakula kilikua na mchanganyiko wa kiafrika na kimagharibi kwa kuzingatia afya ya mlaji. Fatilia picha utaona unadhifu wa fanyakazi na mazingira safi ya hoteli kwa mapumziko ya kifamilia au jumuiya.














Thursday, November 3, 2011

Dr.Kimei azungumzia hali ya uchumi wa nchi na mafanikio ya Benki ya CRDB kwa muhula wa mwisho wa mwaka

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB,Dkt. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kuhusu maendeleo na mafanikio ya Benki ya CRDB na hali ya uchumi wa nchi.Kushoto ni katibu wa Benki ya CRDB Bw. John Baptist Rugambo

============  ======  ==============

Utangulizi

Wakati tunakaribia mwishoni mwa mwaka 2011 nimeona ni bora kukutana nanyi ndugu zangu waandishi wa habari ili tupate kuzungumza mawili matatu kuhusu Benki yetu. Hivi Karibuni tumemaliza robo ya tatu ya mwaka wa fedha wa Benki hivyo nimeona  niwashirikishe kuhusu hali ya CRDB Benki ili nanyi  muweze kuwafikishia habari hizi watanzania wenzetu ambao ni wateja wetu, wanahisa na pia wawekezaji.

Kwanza kabisa ni nianze kwa kusema kwamba kwa ujumla kuwa hali ya kifedha na kibiashara ya CRDB Benki ni nzuri sana. Pamoja na changamoto za kiuchumi zilizoikumba nchi yetu ambazo ni:
  • Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 6.4 mwanzo wa mwaka wa 2011 hadi asilimia 17.4 mwishoni mwa mwezi Septemba 2011.
  • Kushuka kwa thamani ya shillingi ya kitanzania kwa karibu ya asilimia 20 dhidi ya fedha za kigeni hasa hasa dola ya Marekani tokaShilingi 1,512 kwa dola moja January 2011 hadi shilingi 1,830 kwa dola moja mwishoni mwa mwezi Oktoba 2011.
  • Kutotabirika kwa soko la fedha, ambapo riba zimekuwa zikishuka na kupanda kwa kasi katika kipindi kifupi (interest rate volatility).
  • Mgawo wa umeme unaosababisha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, na kupungua kwa uwezo wa wateja wetu wakopaji kuzalisha na kulipa mikopo yao;
  • Serikali kuchelewesha malipo kwa wakandarasi tunaambiwa TANROADS yenyewe inadaiwa zaidi ya bilioni 400….. hii inamaanisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizi zinadaiwa mabenki.
 
Hali ya biashara ya CRDB Benki - Robo Tatu ya Mwaka
Pamoja na hayo yote ni fahari yangu kuu kusema tena kwamba CRDB Benki imefanya vizuri sana. Hadi mwisho wa mwezi Septemba 2011 Benki ilikuwa na amana toka kwa wateja zifikiazo Trilioni 2.3. Ikumbukwe kuwa wakati tunafunga robo ya pili ya mwaka mwezi Juni; Benki ilikuwa na amana za wateja zipatazo shilingi trilioni 2.1. 

Hapa kuna ongezeko la shillingi bilioni 200. Hili ongezeko linaonyesha kuwa wateja wetu wanaongeza kuwa na imani na CRDB Benki licha ya hali ya uchumi ikiwa tete. 

Pamoja na imani ya wateja wetu waletao fedha zao CRDB Benki kama amana, nasi kama Benki tumeongeza imani kwa wateja wetuwakopaji licha ya changamoto zinazowakabili kutokana na hali ya uchumi. 

Mpaka kufikia mwisho wa robo ya tatu ya mwaka 2011, Benki imeshatoa mikopo ya shilingi za kitanzania TRILLIONI 1.3, ikiwa tumeongeza utoaji wa mikopo kwa shilingi bilioni 80 katika robo ya tatu ya mwaka. Kama mnavyoona imani inazaa imani; mwisho maendeleo kwa jamii yetu wote. 

Baada ya kutoa taarifa kidogo kuhusu hali ya Mizania ya CRDB Benki, sasa nitazungumzia faida ambayo Benki imepata mpaka mwisho wa mwezi Septemba. Benki katika mipango yake ilikuwa imedhamiria kuongeza faida kwa asilimia 5 ikilinganishwa na matokeo ya robo kama hii mwaka jana.

Mpaka tunazungumza hapa, matokeo yaliyopo ya kifedha ni kuwa CRDB Benki imeshapata faida ya shillingi bilioni 63 kabla ya kodi.Shilingi bilioni 63 ni zaidi ya bilioni 10.5 ya faida ambayo Benki ilikuwa imepatikana katika kipindi kama cha Januari mpaka Septemba 2010. 

Hizi BILIONI 63 ni zaidi ya ongezeko la asilimia 22 ukifananisha na matokeo ya mwaka jana. Kama nilivyosema hapo awali hali ya kibiashara na kifedha ya CRDB Benki ni ya fanaka. Mimi naamini Mungu yuko na CRDB Benki 

Tunavyozungumza hapa, bado mwaka haujaisha. Sisi kama Benki bado tunaendelea kuweka bidii na kuongeza matumizi ya maarifa ili wateja wetu, wanahisa wetu na watanzania kwa ujumla wafaidike na Benki yao. CRDB Benki iko kwa ajili yao. 
Hali ya usoni ya kibiashara ya Benki

Baada ya kuzungumzia hali ya uchumi wa nchi na hali ya fedha ya CRDB Benki, naona ni sawia sasa tukazungumzia hali ya usoni ya kibiashara ya Benki hii. 

Mpango Mkakati wa Benki

Kwanza kabisa Benki imeendelea na utaratibu wake wa  kuhakikisha kuwa inawapatia wateja wake wote huduma na bidhaa za kivumbuzi (Innovative), za kisasa (Modern) na kwa gharama nafuu. Benki yetu huhakikisha kuwa ni “DAIMA YA KWANZA, KUWAWEKA WATEJA WETU KWANZA”. 

Wote mnafahamu kuwa tumeuletea umma wa watanzania kadi ya TemboCardMasterCard ambayo ni “chip card” (EMV Compliant)tukiwa wa kwanza kuuwezesha umma mkubwa wa watanzania kuweza kunufaika na bidhaa hii maarufu dunia nzima. Kama mnakumbuka tulikuwa wa kwanza kuutambulisha umma wa watanzania chapa ya Visa kwenye  kadi za malipo.

Hivi sasa ukiwa na akaunti na Benki yetu unaweza kupata huduma ulimwenguni kote ukiwa na chapa hizi mbili. Haijalishi akaunti uliyonayo ni ya shilingi au fedha zingine za kigeni. Mpaka tunavyoongea muda huu tumeshafikia na kuzidi lengo ambalo tulikuwa  tumekubaliana na MasterCard International.

CRDB Benki inatambua umuhimu wa wateja wadogo katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu. Hivyo mbali ya mikakati mingi ambayo benki imetekeleza katika kuinua sekta hii; sasa imewaletea katika soko akaunti maalum ijulikanayo kama akaunti ya BIDII. Bidii akaunti ni akaunti mahususi kwa wafanya biashara wa kati na wadogo (SME). Itawasaidia sana kupata unafuu wa kuendesha shughuli zao za biashara na pia mikopo ya kuendeshea biashara hizo. 

Ni mahususi sana kwa wale wafanyabiashara wenye biashara mbalimbali ndogo au za kati  na wakati  mwingine wakiwa pia na ajira. Hapa nawazungumzia wenye biashara za maduka, mahoteli, biashara za usafiri (daladala au/na malori), Kilimo biashara (agribusiness) au ufugaji biashara  n.k. Bidii akaunti ni ya kipekee kwa kuwa ni akaunti ya hundi (Current) ambayo wakati huo huo inatoa faida, yaani riba kwa fedha ambazo zinakuwa kwenye akaunti.

 Hii pia ni mara ya kwanza kwa umma wa  watanzania kupata akaunti ya hundi ambayo pia inatoa riba.

Muda mfupi ujao pia CRDB Benki itazindua huduma mpya na ya kipekee kwenye sekta ya Kilimo-biashara (agribusiness) na ufugaji-biashara (livestock business) ambayo itajulikana kama Kilimo na Ajira Loans. 

Hii huduma nawahakikishia itawakosha wengi na kufuta machozi ya vijana wengi hapa nchini. Nadhani wote mnafahamu kuwa CRDB Benki inakopesha zaidi sekta ya kilimo kuliko sekta  nyingine zote. Asilimia 28% ya mikopo yetu yote inaenda kwenye sekta ya kilimo. 

Hili litakuwa na siku yake, hivyo kwa leo mnivumilie kwa kuwa naishia hapa. 
Wakati tunashughulikia hilo pia tuko kwenye hatua za mwisho katika kuboresha huduma yetu ya SimBanking. Kama mnavyofahamu hii ni huduma ambayo inamuwezesha mteja wa benki kupata huduma za Benki kwa njia ya simu ya mkononi. 

Nitawaeleza kwa undani zaidi tutakapokutana tena karibuni. 

Nikiendelea kuzungumzia hali usoni ya biashara, kama mnavyofahamu baada ya sekta ya kilimo, sekta inayofuata kwa ukuaji  ni sekta ya ujenzi. Hii sekta inakua sana, na sisi kama Benki tuliliona hilo na tumekuwa mstari wa mbele kwa miaka mingi kukopesha sekta hii.  

Hivi majuzi kulikuwa na tukio moja jema lililowahusisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na benki kadhaa, kusaini mkataba wa kutoa mikopo kwa wanunuzi wa nyumba za NHC. Benki yetu haikuwa moja kati ya watia saini wale. Kitendo hiki kiliwapatia simanzi watanzania wengi na kuwapa shaka pamoja na maswali mengi kulikoni???. Tumekuwa tukipata simu nyingi, barua na barua pepe watanzania wakiulizia jambo hilo. 

Napenda nilizungumzie hili katika sehemu tatu tofauti:
  • Kwanza, Nitaanza na suala la Benki na biashara  ya kukopesha wateja binafsi (Personal Customers) mikopo ihusuyo nyumba kama vile kujenga, kukarabati, kuongeza  au kununua. Benki imekuwa ikitoa mikopo ihusuyo suala zima la nyumba kwa wateja binafsi kwa miaka takribani kumi hadi sasa. Imekuwa ikitoa mikopo ya kukarabati  au/na kuongeza nyumba , kujenga na kununua nyumba. Biashara hii imekuwa ikikua na kukubalika sana na wateja.
Changamoto kubwa ya mikopo hii imekuwa ni gharama kubwa za viwanja, ujenzi au ununuzi wa nyumba ambazo zimekuwa zikiongezeka sana.

Nadhani hili si geni kwa watanzania wengi. Gharama za viwanja zipo juu zaidi kwa viwanja vilivyopimwa. Si ajabu leo hii kusikia fulani amenunua kiwanja kwa bei ya zaidi ya shilingi milioni 200. Hili limefanya nyumba ziwe na bei ya juu sana na hivyo kuwafanya watanzania hata wenye bidii sana kushindwa kumudu.

Pia CRDB Benki imekuwa ikikopesha wateja wafanyao biashara za kati na kubwa. Hapa  Benki imekuwa ikikopesha katika nyanja zote, ununuzi wa majengo, ujenzi wa majengo, na pia ukarabati wa majengo ya biashara kama hoteli, shule na kadhalika. Haya majengo marefu maarufu kama “skyscappers” ni baadhi tu ya majengo hayo.   
Hali ya usoni ya Uchumi wa nchi

CRDB Benki imefurahishwa na kitendo cha serikali yetu kupitia Benki kuu kuingilia kati kuanguka kwa thamani ya shilingi yetu dhidi ya fedha za kigeni pia juhudi zake za kupunguza mfumuko wa bei. Tumefarijika pia na kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme nchini.

Hivi vyote vinaashiria kuwa hali ya uchumi itaendelea kuimarika na biashara ya wateja wetu kwa minajili hiyo, biashara ya benki itaimarika zaidi. 

Nimalize kwa kuwashukuru sana kwa kuja kwenu hapa, kuuitikia mwito wa CRDB Benki. Nimefarijika sana kukutana nanyi tena baada ya kitambo kidogo kupita. 
Nawaona mna siha njema. Kwa wale ambao hatutaonana hivi karibuni, nawatakia Idd njema.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Wednesday, November 2, 2011

JOB VACANCIES

Dodoma Urban Water supply and Sewerage Authority (DUWASA) was established under section 3(I) of Cap. 272 of 1997 as repealed by section 60 of Watersupply and Sanitation Act No. 12 of 2009. DUWASA is charged with the overall responsibility of operations and management of Watersupply and sanitation services in Dodoma urban within the Municipality. Applications are invited from suitably qualified, dynamic, experienced and performance driven Tanzanians, male and female, to fill in excellent carrier opportunities.
  1. MAINTENANCE AND LOGISTICS ENGINEER – One post


    1.1 Required Qualifications:
    Holder of a Degree in Electromechanical/Electrical/Mechanical Engineering or its equivalent from a recognized institution with at least three (3) years of working experience on the same capacity from a reputable organization. Those with either high managerial interpersonal skills and Registered with the Engineers Registration Board (ERB) will be highly considered. Computer skills are essential.
    1.2 Duties and Responsibilities
        1.2.1 Carry out regular/routine inspection of pumps, machines, motor vehicles and equipment according to the laid down proceeds, time schedule and established official check list.
        1.2.2 Ensuring that plants, machines, equipments and motor vehicles are repaired professionally.
        1.2.3 Liaise with TANESCO to ensure constant power supply to the water production and distribution systems and ensure immediate repair and restoration of power whenever failure occurs.
      1.2.4 Assess and recommend replacement needs for plants, machines, motor
      vehicles or their parts whenever their respective performances have
      decreased.
      1.2.5 Performing any other duties as may be assigned by the Technical Manager.
2.0 PLANNING AND DESIGN ENGINEER II– One post
    2.1 Required Qualifications
      Holder of a Degree/Advance Diploma in Civil/ Sanitary Engineering from recognized institution and registered as professional engineer with Engineers Registration Board (ERB) of Tanzania with at least three (3) years working experience as an engineer in water sector.Computer literate in Network design by using CAD, Microsoft Windows is an added advantage.
    2.2 Duties and Responsibilities.
      2.2.1 Investigate priority areas in need of Watersupply distribution networks.
        2.2.2 Timely preparation of monthly, quarterly, semi-annually and annually progress as per signed Memorandum of Understanding between DUWASA and Ministry of Water and EWURA.
      1. Supervise construction of watersupply projects and document all projects implemented by the Authority.
      2. Supervise implementation of construction works and ensure that such works comply with design parameters and set standards.
      3. Perform any other duties as may be assigned by the Planning and Design Engineer (PDE).



    3.0 WATER PRODUCTION ENGINEER II (MZAKWE STATION) -One post
3.1 Required Qualifications
      Holder of a Degree/Advanced Diploma in Civil Engineering/Sanitary/ Electrical/Mechanical Engineering and registered as a professional engineer with Engineer’s Registration Board of Tanzania with at least three (3) years working experience as an engineer in water production and treatment works.
    3.2 Duties and Responsibilities
        3.2.1 Monitoring water quality and quantity from boreholes and water distribution system and ensuring compliance with the prescribed standards for drinking water.
      1. Ensuring that the water laboratory adequately equipped with water testing equipment and reagents and is manned by qualified and experienced staff.
      2. Conducting daily analysis of operation and working conditions of surface pumps, submersible pumps and associated electromechanical equipment to identify necessary changes to achieve and maintain optimal operations and assess the replacement needs for pumps and electromechanical equipment.
      3. Ensuring that there is adequate and proper storage of chemicals and other stocks related to water production.
      4. Performing any other duties as may be assigned by the Water Production Engineer.



4.0 PUBLIC RELATIONS OFFICER II - One post
4.1 Required Qualifications
    Holder of a Degree in Journalism, Mass Communication, International Relations, Marketing Communication, Public Relations & Advertising, or any other approved equivalent qualification by recognized institution with at least one (1) year working experience as Public Relations Officer from a reputable organization. Knowledge in Web Design and strong command of both spoken and written English and Swahili is essential.
4.2 Duties and Responsibilities:
    4.2.1 Taking minutes during meetings between Board of Directors and all staff.
      4.2.2 Reading bulk flow water meters and pressure gauges daily, compiling information/data and present them to Head of Public Relations Unit including the detection of major points where water is lost and advice accordingly.
      1. Disseminating notices of interruptions of Watersupply for maintenance purposes and information concerning water tariffs, water consumption and conservation, demand management, hygiene education, and utility performance to customers, recording and following up on customers’ complaints.
      2. Making sure that the image of Duwasa to the public is always positive
      3. Performs any other duties as may be assigned by the Head of Public Relations Unit.


5.0 LEGAL ASSISTANT-One post
      5.1 Required Qualifications
      Holder of an ordinary Diploma in Law from a recognized college with at least two years working experience in legal practice in any reputable legal firm within Tanzania. Should posses’ attributes of managed person utility and behavior, problems solving/leadership/ planning skills and organizing skills.
5.2 Main Duties and Responsibilities:
        5.2.1 Plan and formulates legal defense and prosecution strategies for cases in which DUWASA has interest.
      1. Combating all illegal issues pertaining to the improper use of water by customers.
      2. Handles administers and advises on leases, tenancies and general countersigning matters.
      3. Drafting and enforcing all legal contracts between DUWASA and customers
      4. Assist the Management to liaise with the High Court and Courts subordinate, various institutions, Government Ministries and Department on legal matters.
      5. Performs any other duties as he/she may be assigned by Supervisor.



6.0 CIVIL TECHNICIAN - One post
    6.1 Required Qualifications
      Holder of FTC or a Diploma in Civil/Sanitary/Water resources engineering from a recognized Technical College with three (3) years working experience as Technician in Watersupply and Sewerage works. Considerable technical knowledge of drafting techniques, surveying and related engineering practices, procedures, materials and tools, including working knowledge of computer assisted drafting (CAD) principles and techniques. Should have supervisory skills/qualities. Should be ready to work in extra hours under minimum supervision.
    1. Duties and Responsibilities:
        6.2.1 Planning, design and supervising construction of watersupply and Sewerage structures and buildings.
        6.2.2 Preparing bills of quantities and estimates for water and Sewerage structures and buildings.
      6.2.3 Draft by hand and using computer-aided drafting/mapping software.
      6.2.4 Organize, prepare layout, prepare complete project plans for water and
      Sewer Works.
        6.2.5 Performing any other duties as may be assigned by the Head of planning and design unit.
7.0 ELECTRICAL TECHNICIAN-One post
    7.1 Required Qualifications
      Form IV/VI Certificate with FTC/Diploma in Electrical Engineering from a recognized Technical College with at least one (1) year working experience as a Technician in the Operation and maintenance of electrical works.
    7.2 Duties and Responsibilities
        7.2.1 To carry out regular electrical inspection and maintenance for all electrical motors and control circuits for all booster stations.
      7.2.2 To prepare weekly report for pumps and motors in all booster stations.
        7.2.3 To carry out inspection and testing for new installed electrical equipment as well as making addition installation to the existing one where necessary.
      7.2.4 Ensuring that all pump motors are equipped with protection device to protect motors from being damaged with electrical shock or fluctuation.
        7.2.5 Performing any other duties as may be assigned by the Maintenance and Logistic Engineer.
8.0 MECHANICAL TECHNICIAN (MZAKWE STATION)-One post
    8.1 Required Qualifications
      Form IV/VI Certificate with FTC/Diploma in Mechanical/Motor Vehicles Maintenance Engineering from a recognized Technical College with at least three (3) years working experience as a Technician in maintenance of mechanical works and motor vehicles.
    1. Duties and Responsible:
      1. Carrying out preventive maintenance of both submersible and surface pumps according to the schedule.
      2. Carrying out all repairs (including emergencies) of submersible and surface pumps as the breakdown occurs.
      3. To ensure all electromechanical equipment at all pumping stations are in good and proper operative condition all the time.
      4. Performing any other duties as may be assigned by the Maintenance and Logistic Engineer.


9.0 PUMP MECHANICS-One post
    9.1 Required Qualifications
      Form IV/VI Certificate with FTC/Diploma in pump mechanics from a recognized Technical College with at least one (1) year working experience as a Technician in the Operation and maintenance of pump works.
    9.2 Duties and Responsible:
        9.2.1 Carrying out maintenance and repair of submersible pumps, surface pumps and motors professionally.
      1. Ensuring that preventive maintenance schedule for all pumps and motors is prepared and followed accordingly.
      2. Completing job cards for every maintained and repaired submersible pumps, surface pumps and motors
      3. Using established official checklist when carrying out Mechanical Inspection.
      4. Proper keep of pumps and motors.
      5. Making sure that all pumps and motors are in good working condition all the time.
      6. Performing any other duties as may be assigned by the Mechanical Technician.



    ADDITIONAL COMPETENCIES FOR MAINTENANCE AND LOGISTICS ENGINEER,PLANNING AND DESIGN ENGINEER II,WATER PRODUCTION ENGINEER II,PUBLIC RELATIONS OFFICER II AND LEGAL ASSISTANT.
    • Strong relationship building, communication, and problem solving/analytical skills.
    • Must be able to articulate ideas clearly and concisely to staff at all levels
    • Must have strong advising skills, comprehensive understanding of HR principles, in – depth knowledge of employment laws and experience in resolving employee relations issues.
    • Excellent interpersonal, organizational, oral and written communication skills.
    • Ability to work independently and collaborate in a team.
    • Able to work under pressure and in extra hours
    • Knowledge in ICT is essential.



10.0 TERMS OF EMPLOYMENT FOR THE POSTS
    Permanent and pensionable.
11.0 AGE LIMIT FOR THE APPLICANTS
    Applicants preferably are between 25 – 40 years of age.
12.0 REMUNARATIONS:
    The posts carry attractive remunerations package subject to work professional experience and qualifications.
13.0 MODE OF APPLICATION
    Letter of application accompanied by a detailed CV, Photocopies of relevant certificates; names and addresses of three referees, day contact telephone numbers and postal address should reach the under mentioned address before or on November 15, 2011:
    The Managing Director,
Dodoma Urban Water Supply and Sewerage Authority,
P.O. Box 431,
Tel: 026 – 2324245. Fax: 026 – 2320060,
DODOMA
    NB: ONLY SHORTLISTED CANDIDATES WILL BE CONTACTED FOR INTERVIEW; AND THOSE WHO WILL NOT HEAR FROM US SHOULD CONSIDER THEMSELVES UNSUCCESFUL CANDIDATES.

libeneke la taswirazz enzi za mwalimu