Thursday, April 5, 2018

KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha Skurani kutoka Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo, wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 63 ya Umoja wa Wazazi Tanzania, lililoandaliwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, leo 
MWANZO⤋
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akishuka katika gari lake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, kuadhimisha miaka 63 ya kuzaliwa Umoja wa Wazazi Tanzania.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutan wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisalimiana na Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akisindikizwa na viongozi kwenda ukumbini baada ya kuwasili eneo la Ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, na kutoka kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa huo Lugano Mwafongo na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Kate Kamba 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akipata maelezo ya awali kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha baada ya kuwasili katika chumba cha Wageni maarufu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo (kushoto) akiwa na Katibu wa CCM mkoa huo Saad Kusilawe wakati wa mazungumzo hayo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwaunga mkono wajumbe waliokuwa wakimshangilia baada ya kuwasili ukumbini kwenye Kongamano la miaka 63 ya kuzaliwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoandaiwa na Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa dar es Salaam Frank Kamugisha.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, tayari kushiriki kongamano hilo
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Mwinyimkuu Sangaraza akifungua pazia la kongamano hilo kwa kufanya utambulisho
 "Jamani sare maalum ya sherehe hizi ilichelewa kidooogo, lakini ninayo imeshafika hii hapa" akasema Sangaraza na kuwaacha wajumbe na mgeni rasmi wakicheka
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala akisalimia baada ya kutambulishwa
 Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam wakisalimia baada ya ktambulishwa. Kutoka Kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha habib Nasser, Mwafongo na Kamugisha
 Wazee wa Jumuiya ya Umoja wa wazazi mkoa wa Dar es Salaam (mstari wa mbele) wakiwa kwenye kongamano hilo
 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Lugano Mwafongo akizungumza kwenye kongamano hilo.
 Wajumbe wakimshangilia Mwanfongo wakati akifanya utambulisho
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jumiya ya Umoja huo Mzee Mkali akisalimia baada ya kutambulishwa
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha akitoa nafasi ya kufanywa dua na maombi kabla ya kongamano kuanza rasmi
 Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza
 Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akiomba dua kabla ya kongamano kuanza
 Wajumbe wakipokea dua ya Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) kabla ya kongamano kuanza
 Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira wa Jumiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Wilson Tobola akisoma maombi kabla ya kongamano hilo kuanza
 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akisoma taarifa ya maadhimisho ya miaka 63 ya Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania wakati wa Kongamano hilo
 Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo akimkabdhi taarifa hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuisoma
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Beatrice Mandia akizungumzia maadili wakati wa kongamano hilo
 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Habib Nasser akitangaza Wajumbe wa Baraza la Uchumi na fedha kwenye kongamano hilo  
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana mkoa wa Dar es Salaam akisalimia  
 Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam ndugu Busolo akizungumza kwenye kongamano hilo 
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mkali akizungumza kwenye kongamano hilo
 Vijana wa Vyombo vya Habari vya CCM Jumanne Gude wa Gazeti la Uhuru na mwenzake kutoka Uhuru FM wakiwa makini wakati wakichukua taarifa kwenye kongamano hilo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate kamba akizungumza  katika kongamano hilo
 Mwenyekiti wa Jumuiya wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamugisha akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza kwenye kongamano hilo
 Baadhi ya wajumbe ukumbini
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akizungumza na wajumbe wakati wa kongamano hilo
 Baadhi ya wajumbe ukumbini
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo, wakati wa Kongamano hilo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akimkabidhi Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) Cheti cha pongezi kutoka Jumuiya ya Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kongamano hilo
 Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba) akifurahia baada ya kupewa Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akimkabidhi Doto Msawa Cheti cha Skurani kutoka Jumuiya ya Umoja huo Wilaya ya Kigamboni kutambua mchango mkubwa wa hali na mali ambao amekuwa akiutoa kwa jumuiya hiyo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali, anayekabidhiwa ni katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akiendelea kukabidhi tuzo za shukrani na pongezi kwa viongozi mbalimbali, Anayekabidhiwa ni Ndugu Busoro
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam akimpongeza Busoro
 Frank Nkinda (kulia) ambaye ni Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiwa ukumbini
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akizungumza kutoa neno la shukurani mwishoni mwa kongamano hilo
PICHA ZA PAMOJA⇩


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akiagana na wajumbe baada ya kongamano hilo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo  akiagana na Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania, mkoa wa Dar es Salaam, Abdulkadir Sharif (Scaba Scuba)  mwishoni mwa kongamano hilo.
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe (kushoto) akiondoka ukumbini mwishoni mwa kongamano hilo la Maadhimisho ya miaka 63 ya kuanzishwa kwa  Umoja wa Wazazi Tanzania, lilioandaliwa na Jumuiya ya Umoja huo mkoa wa Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

PROF KABUDI ATAJA HATUA INAZOCHUKUA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

Prof.Kabudi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 : kwanini ushindani ni muhimu.

Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani ,ukiongozwa na viwanda , pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

akizungumza  baada ya ufunguzi wa washa hiyo Profesa Kabudi ametaja hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini na kufafanua kinachoendelea ni kuangalia jinsi gani kufanya bidhaa za Tanzania kuwa na ushindani kwenye soko la Dunia.

"Kuna mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini .Nikumbushe tu wakati tunapata uhuru tulikuwa na viwanda viwili , hivyo jukumu la wakati ule ikawa ni kuanza kujenga viwanda na vilijengwa na kutoa ajira kwa wananchi.

"Hata hivyo ilipofika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tukarudi nyuma kidogo na baadae tukaingia kwenye vita dhidi ya Uganda ambapo tulitumia dola za Marekani milioni 5 kwenye vita.Hivyo tukawa hatuna fedha za kuendeleza viwanda.

"Pamoja na magumu ambayo tumeyapitia bado leo hii tunavyo viwanda vingi ingawa jukumu la Serikali ni kujenga viwanda zaidi ili kuboresha maisha ya wananchi wake katika kuleta maendeleo,"amesema Profesa Kabudi.

Amefafanua kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina hatua ambazo zinatakiwa kuchukuliwa katika kufikia malengo la kujenga viwanda na kuboresha maisha ya wananchi na kutumia nafasi hiyo kueleza tayari Serikali  imeanza kuchukua hatua kadhaa na baadhi ni elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari ambayo inatoa fursa ya kuandaa wasomi kwa maendeleo ya nchi.

Pia amesema jitiahada nyingine zinaendelea katika ujenzi wa miundombinu ya barabara reli na bandari na kwamba miundombinu hiyo ni muhimu katika kujenga msingi imara wa kukuza na kuimarisha uchimi wa Tanzania.

Prof.Kabudi amezungumzia namna ambavyo Serikali imejikita katika kuboresha sekta ya afya ili kuwa na wananchi wenye afya imara watakaoshiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya Taifa letu.Pia amegusia hatua zinazochukuliwa katika kuongeza nishati ya upatikanaji wa umeme kwa kuanzisha miradi mikubwa ya umeme na jana Rais John Magufuli amezindua mradi wa umeme wa Kinyerezi II.

Hata hivyo amesisitiza umuhimu wa ujenzi wa viwanda na kueleza huko nyuma wakati kukiwa na viwanda vya kutosha wanawake na wasichana wengi walipata ajira na kuondoa wale ambao wanaonekana wanazurula mtaani.Hivyo viwanda vikijengwa vitatoa ajira ikiwamo kwa wanawake.

Kuhusu malalamiko ya kodi kubwa , Profesa Kabudi amesema tayari Rais Magufuli ameshatoa maelekezo ya kuhakikisha kodi inakuwa yenye unafuu na juzi juzi amekutana na wafanyabishara kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya biashara na uwekezaji nchini ,hivyo kwenye eneo hilo mambo yanakwenda vizuri.

Kwa upande wa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Amina Salim Ali amesema warsha hiyo imekuja wakati muhimu kwani yapo mambo ya kiseria ambayo yanajadiliwa na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kuinua uchumi wa wananchi na kwa Zanzibar kuna hatua mbalimbali ambazo wamezichukua katika kuboresha maisha ya wananchi.

Amesema kwenye eneo la ujenzi wa viwanda, bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa Zanzibar imejikita pia katika kufufua viwanda vya zamani  na ujenzi wa viwanda vipya kulingana na bajeti ya fedha ambayo wameitenga.

Pia wameamua kuimarisha kilimo cha bahari na katika hilo kuna baadhi ya vijana wapo nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo ya uvuvi hasa kwa kuzingati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenunua meli ya uvuvi kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi.

Amesema wameimarisha kilimo cha mbogamboga kwani wanatambua kuna nchi za Uarabuni ambazo zinanunua mbogamboga kutoka Zanzibar huku akielezea hatua kadhaa ambazo zinachukuliwa na Serikali katika kuinua uchumi wa wananchi.

Kuhusu sera ya viwanda, amesema Zanzibar wameweka mikakati ya kuhakikisha wanaondoa changamoto zilizopo katika sekta ya viwanda na kuelezea namna ambavyo wameondoa urasimu kwa wanaotaka kufanya bishara na kuwekeza huku akizungumzia hatua ambazo wamechukua katika kuimarisha sekta ya utalii visiwani huo kwa kuhakikisha watalii wakienda wanakaa muda mrefu.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk.Donald Mmari amesema pamoja na kushuhudia ukuaji mzuri wa uchumi wa Tanzania kwa miaka 15 iliyopita, tafiti zinaonesha viwango vya tija katika sekta nyingi bado ziko chini na ushindani wake kulinganisha na nchi nyingine duniani bado haujaridhisha.

"Hata hivyo Tanzania ina uwezo wa kujiweka katika nafasi kubwa zaidi katika uchumi wa dunia  kwa kujenga uwezo wa ushindani ukiinuliwa na uwepo wa faida za kipekee ikiwemo eneo la kijiografia , wingi wa rasilimali za asili na utulivu wa kisiasa na kijamii.

"Lengo la warsha hii ni kujadili na kupata maoni yatokanayo ma tafiti na uzoefu wa nchi nyingine ili yatuongoze katika kushiriki na kuchangia zaidi kwenye juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi wa viwanda ikizingatiwa kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitato(2021/22-2025/26) utajikita katika kuimarisha uwezo wa Tanzania kushindana na kuongeza ukuaji wa uchumi kupitia mauzo ya nje ya nchi,"amesema Dk.Mmari.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti ya REPOA leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
 Mtoa mada Mkuu wa Warsha hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika katika mausuala ya forodha(SACU), Paulina Mbala Elago akitoa mada yake juu kwanini Ushindani na jinsi ya kuufikia katika maendeleo ya viwanda katika nchi hizo.
 Mkurugenzi Mkuuu wa Tasisi  ya utafiti nchini Repoa Dk Donald Mmari akizungumza kabla ya kumkaribisha msemaji mkuu katika warsha hiyo ya kwanini ushindani juu ya viwanda kufikia 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Infotech Investment Group LTD , Ali Mufuruki akiongoza majadiliano ya hali ya biashara kwa sasa katika Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Repoa nchini.
 Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
  Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi  watatu kushoto akiwa katika picha ya  pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya utafiti nchini Repoa pamoja na wadau wa utafiti

SERIKALI KUIMARISHA MASOKO YA MAZAO MAKUU MATANO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha vyama vya msingi vya ushirika vya mazao ya kilimo na masoko vinavyozalisha mazao ya kimkakati ya biashara ya pamba, kahawa, korosho, chai na tumbaku. 
Amesema katika mwaka 2018/2019, Serikali inalenga kuimarisha masoko ya mazao hayo kwa kuhamasisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambapo mazao hayo yatazalishwa na kuuzwa kupitia vyama vya ushirika kwa njia ya minada. 

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 4, 2018) Bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019 kwenye mkutano wa 11 wa Bunge.

Waziri Mkuu amesema pamoja na hatua hizo, Soko la Bidhaa ambalo limeshaanzishwa, litasaidia sana kuimarisha masoko ya mazao kwani yatakuwa yanauzwa kwa njia ya ushindani mkubwa huku wakulima wanaozalisha kwa ubora wakinufaika na bei ya juu zaidi.

“Serikali imeamua kuweka mkazo maalum wa kuyaendeleza kwa kasi mazao matano ya biashara ambayo ni chai, kahawa, korosho, pamba na tumbaku. Lengo ni kuongeza mapato ya wakulima, kuwa chanzo cha kuaminika cha malighafi katika uchumi wa viwanda, na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira na fedha za kigeni. 

Amesema uamuzi wa kuongeza usimamizi katika uzalishaji wa mazao hayo makuu ya biashara unatokana na ukweli kwamba, kwa kipindi kirefu uzalishaji ulishuka kutokana na changamoto kadhaa. 

“Miongoni mwa changamoto hizo ni kupungua tija katika uzalishaji, baadhi ya wakulima kuacha kulima mazao hayo kutokana na kukata tamaa kwa sababu mbalimbali zikiwemo vyama vya ushirika kutotekeleza vema wajibu wao, wizi, dhuluma na pia ushiriki mdogo wa maafisa kilimo katika kusimamia kilimo cha kitaalamu,” alisema. 

Alizitaja sababu nyingine za kushuka uzalishaji wa mazao hayo kuwa ni huduma zisizoridhisha za ugani na utafiti, ukosefu wa pembejeo bora, utitiri wa tozo na wingi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika. 

Akitolea mfano, Waziri Mkuu alisema uzalishaji wa pamba ulipungua kutoka tani 456,814 mwaka 2013/2014, hadi tani 282,809 mwaka 2015/2016. Kwa upande wa tumbaku, Waziri Mkuu alisema uzalishaji katika kipindi cha miaka minne ulishuka kutoka tani 126,624 mwaka 2010/2011 hadi kufikia tani 60,929 mwaka 2015/2016.

“Serikali imechukua hatua za kuimarisha utawala bora kwenye vyama vya ushirika kwa kusimamia chaguzi za vyama 2,537, chaguzi za viongozi wa bodi za vyama vya ushirika 532 na kufanya kaguzi katika vyama vya ushirika 2,896 vikiwemo vyama vikuu. Kazi za kusimamia vyama vya ushirika zinaendelea,” alisema. 

Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema Serikali inasimamia uendelezaji wa mazao hayo moja kwa moja kupitia maafisa kilimo na Bodi za Mazao na kwamba imechukua hatua za kufuta baadhi ya tozo zilizokuwa kero katika mazao makuu ya biashara pamoja na kuhakikisha kwamba mauzo yanafanyika kwa njia ya wazi na inayoleta ushindani. 

“Kutokana na hatua zinazochukuliwa na Serikali kusimamia mazao makuu ya biashara, tayari tumeanza kuona matokeo chanya kwa kuongezeka uzalishaji wake. Kwa mfano, hadi mwezi Machi 2018, uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara ulifikia tani 804,025. Uzalishaji huu unaashiria ongezeko la mavuno ikilinganishwa na mwaka 2016/2017. Ongezeko hilo la uzalishaji wa mazao ya biashara linakwenda sambamba na kuimarika kwa mwenendo wa bei za mazao hayo hususan korosho na kahawa,” alisema.

Waziri Mkuu aliliomba Bunge likubali kupitisha sh. 143,618,762,698 zikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2018/2019 ambapo sh. 74,527,321,698 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 69,091,441,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. 

Vilevile, Waziri Mkuu aliliomba Bunge liidhinishe sh. 125,521,100,000 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge ambapo sh. 117,205,487,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh. 8,315,613,000 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.

JUMATANO, APRILI 4, 2018

Wednesday, April 4, 2018

WAUGUZI,WAKUNGA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI SEHEMU ZAO ZA KAZI.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi vyeti vya kufanya vizuri baadhi ya wawakilishi wa  mashirika yanayoshirikiana na Wizara ya Afya wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau,wakunga na wauguzi wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.

 Baadhi ya Wauguzi na Wakunga wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo akiongea na wauguzi na wakunga hawapo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha uuguzi na Ukunga Dodoma wakiwakilisha salamu zao kwa kutumia wimbo kwa  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini lililofanyika leo mkoani Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA DODOMA.

 
 NA WAMJW-DODOMA.
 
Serikali imewataka Wauguzi na Wakunga nchini kufuata na kusimamia misingi ya maadili ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi la Uuguzi na Ukunga nchini.

Najua kuwa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga inalishughulikia suala la maadili kwa wauguzi na wakunga hivyo nitoe msisitizo tena huduma za Uuguzi na Ukunga zinapimwa zaidi na uadilifu wa mtoa huduma hivyo muendelee kusimamia kwa ukaribu misingi ya maadili ya taaluma zenu amesema Dkt Ndugulile.

Aidha, Dkt Ndugulile amewataka Wauguzi na Wakunga kupitia vyama vyao vya kitaaluma kushirikiana na Baraza la Uuguzi na Ukunga kuendelea kuwakumbusha mara kwa mara wauguzi kuhusu maadili ya taaluma yenu.

Mteja anapokuja kwenye vituo vya kutolea huduma anategemea kupata huduma ya upendo na huruma, anategemea kupewa maneno ya faraja na matumaini hivyo basi, wale wote wanaoichafua taaluma yenu kwa kutotekeleza wajibu wao kwa wakati, kuwadhalilisha, kuwashambulia au kutowasikiliza wateja wenu wabainishwe na wahimizwe kujirekebishaamefafanua Dkt Ndugulile.

Ninawapongeza sana kwa kuweka msisitizo kwa mambo yanayohusiana na kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga hiyo ni moja ya agenda muhimu ya Serikali ya  Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuliameongeza Dkt. Ndugulile.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa serikali inazifanyia kazi changamoto zinazowakumba Wauguzi na Wakunga kwa namna mbalimbali ambapo hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuongeza kiwango cha bajeti kwa ajili ya kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, na vitendanishi katika Bohari ya Dawa.

kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Bw. Gustav Moyo amesema kuwa kongamano hilo limeandaliwa ili kuwakumbusha wauguzi na wakunga maadili ya taaluma yao pindi wanapokuwa sehemu zao za kazi.

Aidha Bw. Moyo amesema kuwa Akizungumzia Kongamano hilo limebeba kauli mbiu isemayo isemayo Kuelekea Huduma za Uuguzi na Ukunga Zinazozingatia Ubora, Utu, Huruma na Usalama wa Wagonjwa; Katika Kupunguza Vifo vya Akinamama na Watoto.

JAFO ASIMAMISHA UJENZI WA VIVUKO BARABARA YA NAMELOCK-LOLTEPES-SUNYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akikagua ujenzi wa Vivuko katika barabara ya Namelock-Loltepes-Sunya yenye urefu wa Km 88 iliyopo katika Wilaya ya Kiteto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Vivuko katika barabara Namelock-Sunya wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.
Huu ni muonekano wa baadhi ya Kivuko kinachojengwa katika barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya ambavyo Waziri Jafo amesimamisha ujenzi wake kutokana na dosari zilizojitokeza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya yenye urefu wa Km 88 wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.



Nteghenjwa Hosseah, Kiteto

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesimamisha ujenzi wa vivuko vyote katika ujenzi wa barabara ya Namelock-Loltepes Sunya yenye urefu wa Km 88.1 inayojengwa katika Wilaya ya Kiteto na Mkandarasi Deniko Constraction Ltd.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa ziara yake Wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kubaini mapungufu makubwa katika ujenzi wa vivuko zaidi ya kumi alivyovipitia ndipo alipoagiza kusitisha ujenzi huo mara moja hadi hapo Wataalamu wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (TARURA) watakapofika kukagua barabara ma kuwasilisha ripoti.

Aidha kutokana na hali hiyo ya aligiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo Deniko Construction sambamba na Mhandisi Mshauri Luptain Consult Ltd, Mhandisi Consulting Engineers pamoja na ACE Consultant kufika Ofisini kwake mara moja kutoa maelezo ya kina ya mapungufu hayo yaliyojitokeza katika ujennzi wa barabara hiyo.

“Ni mara ya tatu sasa nakuja kukagua Barabara hii na kila mara nabaini changamoto tofauti sjui kuna tatizo gani nahitaji kusikia zaidi kutoka kwa wataalamu wa pande zote ili tutafute suluhisho kwa pamoja”Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa hapo awali Barabara hii iligawanywa kwa wakandarasi wajenzi wawili ambaye ni huyu Deniko alikuwa anajenga upande mmoja wenye Km 44 na Km 44 zilizobakia alipewa Maginga Construction ambaye alishindwa kabisa kazi hii ndipo nilipoagiza taratibu zifuatwe ili kuvunja mkataba wa awali na kazi ile apewe Mkandarasi mwingine.

“Kazi hiyo aliongezewa Deniko Construction ambaye kwa sasa ndiye anayejengwa barabara hii yote yenye Km 88. Hapo awali kazi yake ilionekana nzuri sana na ya kuridhisha lakini baada ya mvua za msimu huu mapungufu makubwa yamebainika hasa katika vivuko vyote vilivyojengwa haviendani na mahitaji ya barabara hii” Alisema Jafo.

Naye Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kiteto Elias Paul alisema kuwa tatizo lililobainika katika ujenzi wa vivuko hivyo ni Vivuko hivyo haviendani na wingi wa maji ya maji yanayopita na vipenyo vya vivuko ni vidogo hivyo havina uwezo wa kuhimili maji na takataka zingine zinazotakiwa kupita hapo na ni rahis sana kuziba na hata kivuko chote kubebwa na maji ndani ya kipindi kifupi.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Nmelock – Loltepes – Sunya unatekelezwa na Serikali kupitia Fedha za wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) chini ya mpango wa (FEED FOR FUTURE) unaotekelezwa katika Wilaya Nne Nchini ambazo ni Kilombero, Mvomero, Kongwa na Kiteto.

Wilaya ya Kiteto kupitia kwa Wakala wa Babarabara za Mijini na Vijiji (TARURA) inahudumia mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa Km 1,088.35 kati ya barabara hizo km 2.8 ni za Lami, Changarawe Km 132 na Udongo Km 955.

KITUO CHA DALADALA JAMATINI KUENDELEA KUTUMIKA, MABASI YA MIKOANI YAONYWA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge alipozungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda ya Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na wadau wa usafishaji katika Stendi Kuu ya muda Mabasi ya Mikoani iliyopo eneo la Nanenane jana Aprili 3, 2018 alipofanya ziara fupi katika stendi hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi (katikati) akifafanua jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) alipofanya ziara fupi kukagua maeneo yanayoweza kuwekewa miundombinu muhimu na kutumika kama kituo cha daladala cha Mjini, jana Aprili 3, 2018. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Ludigija Ndwata. 


Na Ramadhani Juma,Ofisi ya Mkurugenzi

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ameelekeza matumizi ya kilichokuwa kituo Kikuu cha Mabasi madogo maarufu kama Daladala cha Jamatini Mjini Dodoma kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya Manispaa hiyo yaendelee kama kawaida wakati Manispaa ikiandaa eneo mbadala.

Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza ‘ruti’ za Daladala zifupishwe kama ilivyokuwa awali, na kwamba upangaji wa ‘ruti’ ndefu ujadiliwe upya na wadau wote wanaohusika na endapo utakubaliwa na wengi ndipo utekelezaji wake uanze.

Dokta Mahenge ametoa maelekezo hayo leo Aprili 3, 2018, alipokuwa akizungumza na wadau wa usafirishaji katika kituo kikuu cha mabasi ya Mikoani cha muda kilichopo Nanenane Manispaa ya Dodoma baada ya kituo hicho kufungwa wiki iliyopita kwa ajili ya kupisha mradi wa Reli ya Kisasa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano na wadau wote ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMTRA), Manispaa, Jeshi la Polisi, na Shirika la Reli ambao ndio wamiliki wa eneo hilo, na kwamba matumizi ya stendi hiyo yataendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia sasa, kipindi ambacho Manispaa itatakiwa kuwa imeshapata na kuandaa stendi mbadala.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema Manispaa imepokea maagizo yote na itahakikisha inaandaa eneo kwa ajili ya Stendi ya Mabasi madogo Mjini katika kipindi cha miezi miwili kama ilivyoelekezwa na Mkuu wa Mkoa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza mabasi yote yanayosafirisha abiria Mikoa mbalimbali Nchini kupakia na kuanzia safari zao katika kituo Kikuu cha mabasi ya muda kilichopo Nanenane na Kampuni itakayokiuka itachukuliwa hatua kali za Kisheria.

“Namuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani wa Mkoa kuwa, kuanzia kesho mabasi yote yauze tiketi na kuanza safari zao hapa katika kituo hiki Kikuu cha mabasi cha muda cha Nanenane…hakuna Mkubwa wala mdogo katika kutoa huduma kwa Wananchi” alisisitiza Dkt. Mahenge.