Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (Kushoto) akikagua ujenzi wa Vivuko katika barabara ya
Namelock-Loltepes-Sunya yenye urefu wa Km 88 iliyopo katika Wilaya ya
Kiteto.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (Kulia) akiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa Vivuko katika
barabara Namelock-Sunya wakati wa ziara yake Wilayani Kiteto.
Huu
ni muonekano wa baadhi ya Kivuko kinachojengwa katika barabara ya
Namelock – Loltepes – Sunya ambavyo Waziri Jafo amesimamisha ujenzi wake
kutokana na dosari zilizojitokeza.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa
barabara ya Namelock – Loltepes – Sunya yenye urefu wa Km 88 wakati wa
ziara yake Wilayani Kiteto.
Nteghenjwa Hosseah, Kiteto
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amesimamisha ujenzi wa vivuko vyote katika ujenzi wa
barabara ya Namelock-Loltepes Sunya yenye urefu wa Km 88.1 inayojengwa
katika Wilaya ya Kiteto na Mkandarasi Deniko Constraction Ltd.
Waziri
Jafo ametoa agizo hilo mapema jana wakati wa ziara yake Wilayani humo
kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kubaini mapungufu makubwa
katika ujenzi wa vivuko zaidi ya kumi alivyovipitia ndipo alipoagiza
kusitisha ujenzi huo mara moja hadi hapo Wataalamu wa Wakala wa barabara
Mijini na Vijijini (TARURA) watakapofika kukagua barabara ma
kuwasilisha ripoti.
Aidha
kutokana na hali hiyo ya aligiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa
barabara hiyo Deniko Construction sambamba na Mhandisi Mshauri Luptain
Consult Ltd, Mhandisi Consulting Engineers pamoja na ACE Consultant
kufika Ofisini kwake mara moja kutoa maelezo ya kina ya mapungufu hayo
yaliyojitokeza katika ujennzi wa barabara hiyo.
“Ni
mara ya tatu sasa nakuja kukagua Barabara hii na kila mara nabaini
changamoto tofauti sjui kuna tatizo gani nahitaji kusikia zaidi kutoka
kwa wataalamu wa pande zote ili tutafute suluhisho kwa pamoja”Alisema
Jafo.
Aliongeza
kuwa hapo awali Barabara hii iligawanywa kwa wakandarasi wajenzi wawili
ambaye ni huyu Deniko alikuwa anajenga upande mmoja wenye Km 44 na Km
44 zilizobakia alipewa Maginga Construction ambaye alishindwa kabisa
kazi hii ndipo nilipoagiza taratibu zifuatwe ili kuvunja mkataba wa
awali na kazi ile apewe Mkandarasi mwingine.
“Kazi
hiyo aliongezewa Deniko Construction ambaye kwa sasa ndiye anayejengwa
barabara hii yote yenye Km 88. Hapo awali kazi yake ilionekana nzuri
sana na ya kuridhisha lakini baada ya mvua za msimu huu mapungufu
makubwa yamebainika hasa katika vivuko vyote vilivyojengwa haviendani na
mahitaji ya barabara hii” Alisema Jafo.
Naye
Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kiteto Elias Paul alisema kuwa tatizo
lililobainika katika ujenzi wa vivuko hivyo ni Vivuko hivyo haviendani
na wingi wa maji ya maji yanayopita na vipenyo vya vivuko ni vidogo
hivyo havina uwezo wa kuhimili maji na takataka zingine zinazotakiwa
kupita hapo na ni rahis sana kuziba na hata kivuko chote kubebwa na maji
ndani ya kipindi kifupi.
Mradi
wa ujenzi wa barabara ya Nmelock – Loltepes – Sunya unatekelezwa na
Serikali kupitia Fedha za wafadhili kutoka Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) chini ya mpango wa (FEED FOR
FUTURE) unaotekelezwa katika Wilaya Nne Nchini ambazo ni Kilombero,
Mvomero, Kongwa na Kiteto.
Wilaya
ya Kiteto kupitia kwa Wakala wa Babarabara za Mijini na Vijiji (TARURA)
inahudumia mtandao wa barabara zenye jumla ya urefu wa Km 1,088.35 kati
ya barabara hizo km 2.8 ni za Lami, Changarawe Km 132 na Udongo Km 955.
No comments:
Post a Comment