Wednesday, June 1, 2016

DKT SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI WILAYA MJINI LEO, ZANZIBAR

Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza na kuwashukuru wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi wa marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani 
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Kichana Bi,Fatuma Shomari Juma alipokuwa akisoma risala ya Chama Wilaya ya Mjini Kichama wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanywa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Chama cha Mapinduzi kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Kichana Bi,Fatuma Shomari Juma (kushoto) wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum akiwasalimia wanachama cha mapinduzi waialaya hiyo wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Kichama Bw. Juma Fakih Choum wakati wa mkutano wa kuwashukuru na kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi Wilaya hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama Bi.Rukia Omar kutoka jimbo la Kikwajuni alipokuwa akitoa mchango wake wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,alipowapongeza na kuwashukuru Wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani
Mwanachama cha Mapinduzi wa umoja wa Vijana UVCCM Ashrak Saleh Zingo katika shehia ya kiponda mji Mkongwe wa Zanzibar alipokuwa akitoa mchango wake uliogusia zaidi uvunywaji wa katiba ya Zanzibar unaofanywa na Wanachama cha Upinzania,mchango huo aliuotoa leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati wa Mkutano wa Kuwashukuru Viongozi wa Mashina,wenyeviyi wa Matawi na Maskani uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
Wanachama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama,wakinyoosha mikono juu kuunga mkono hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,wakati alipokua akiwashukuru kuwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,katika mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Kichama, wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani,[Picha na Ikulu.] 01/06/2016.

WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO ZANZIBAR ATEMBELEA MAGHALA YA KUHIFADHIA VYAKULA KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN.

Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar .
          
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza bidhaa zilizopitwa na wakati. 

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi  Amina Salum Ali, amesema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi juu ya tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuwauzia vitu vilivyopitwa na wakati.

Amefahamisha kuwa, udanganyifu huo unaofanywa na wafanyabiashara huwasababishia wananchi kupata maradhi mbalimbali ikiwemo saratani.Akiwa katika ziara ya kukagua maghala mbalimbali ya chakula kisiwani Unguja kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani, Balozi Amina amesema serikali imechoka kuona wananchi wanauziwa vyakula visivyokuwa na kiwango kutokana na kumalizika muda wao wa matumizi.

Waziri huyo amekemea vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara kuuza vyakula vilivyokaa maghalani kwa muda mrefu hata kupindukia  miaka mitano, hali aliyosema ni kuwaathiri na  kuwadhulumu wananchi.“Wazanzibari tumechoka kulishwa michele mibovu. Tunasema sasa imetosha na hatutawafumbia macho wafanyabiashara watakaoendeleza vitendo hivyo,” alisema Waziri Amina.

Amesema serikali inakusudia kuweka bei elekezi kwa wafanyabiashara wote ili kuzuia  upandaji bei kiholela hali inayowapa usumbufu wananchi hasa wa kipato cha chini.Aidha Balozi Amina amesema kila mwaka ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani, serikali  imekuwa ikipunguza kodi za bidhaa muhimu kwa wafanyabiashara ili kutoa punguzo kwa wananchi.

Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni unga wa ngano, sukari na mchele.
Hata hivyo, ameeleza kusikitishwa kwake kwamba bei za bidhaa hizo zimebakia palepale au kuongezeka zaidi licha ya nia nzuri ya serikali.Ili kuandaa mazingira ya kuwapa unafuu wananchi, amesema serikali inakusudia kukaa na wafanyabiashara wote ili kujadili na kupanga mipango mizuri kwa itakayowaletea maendeleo wafanyabiashara hao na taifa kwa jumla.

Kwa upande wao, wafanyabiashara waliotembelewa na Waziri huyo,  wamemuhakikishia kuwa chakula kipo cha kutosha katika kipindi hiki cha kuelelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.Aidha wamesema chakula hicho kimeagizwa miezi mitatu kabla ya mwezi huo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mfanyabiashara Abdulghafar Ismail Mohammed wa kampuni ya Evergreen Ltd, ameiomba serikali kukaa pamoja nao pale inapotaka kufanya maamuzi yoyote yanayowahusu ili kuweka uwiano kwa upande wao, serikali na wananchi.

Ziara ya Balozi Amina ilihusisha maghala ya kampuni za Yassir Provision, Akhtar Enterprises Malindi, Evergreen Ltd Saateni, Sub Sahara Maruhubi, Azam Mtoni, Vigor Turkey Group  na Bopar Enterprises zote za Mombasa mjini Unguja.

Pamoja na kujua akiba ya chakula iliyopo nchini kupitia ziara hiyo, Waziri Amina pia alitaka  kujua hali ya mfumko wa bei kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saaeteni mjini Zanzibar.
WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kiwanda cha Zanzibar Milling Corporation kilichoko Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
MENEJA Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Khalid Ali Yussuf, akimpa maelezo Waziri Amina Salum Ali juu ya uzalishaji wa chakula alipotembelea ofisini kwake Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika maeneo ya kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya ziara maalum kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan. 
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa ngano na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni Zanzibar Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea kiwanda hicho.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said, akizungumza na Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar.PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

MKUTANO WA 5 WA MWAKA WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE WAFANYIKA JIJINI ARUSHA.


 Prof. Magimba (Kulia)akifungua mkutano wa 5 wa mapitio wa Mpango wa Taifa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambao unapitia na kupanga mikakati ya utekelezaji wa kutoa elimu,kukinga na kutibu magonjwa hayo nchini ambayo ni usubi,vikope(trakoma), kichocho, minyoo ya tumbo pamoja na matende na mabusha.
 Baadhi ya mdau wa mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele toka nchi mbalimbali akichangia mada kwenye mkutano huo.
 Waratibu wa mpango huo kutoka halmashauri mbalimbali wakijiandaa Kuwasilisha mada jinsi walivyofanikiwa kutekeleza mipango hiyo kwa mwaka 2015/2016,wa kwanza kulia ni dkt.Mabai Leonard(Mwanza) katikati dkt.Faraja Lyamuya(Dodoma) na Dkt.Ida Ngowi(Ruvuma).
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi akiwa na watumishi toka wizara ya afya,waratibu wa halmashauri na wadau toka mataifa mbalimbali.
 Mgeni rasmi wa mkutano huo Prof.Ayoub Magimba(Kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR)Dkt.Mwele Malecela(kulia)katikati ni Mratibu wa mpango huo Dkt.Upendo Mwingira.
Prof. Magimba akiwa pamoja na watumishi wa wizara ya  afya na wa mpango wa Taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini.
Prof.Magimba mwenye tai nyekundu(aliyekaa katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja wadau wa maendeleo toka mashirika mbalimbali toka Tanzania na nje ya nchi.
 Prof.Ayoub Magimba akisalimiana mshauri wa kitaalam wa shirika la RTI international toka Washington DC.

SPEECH BY
CHIEF MEDICAL OFFICER  MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER, ELDERLY AND CHILDREN, 
PROF. MOHAMMAD BAKARI KAMBI 
ON THE OFFICIAL OPENING OF FIFTH NTD ANNUAL JOINT PLANNING MEETING ON 
31th MAY, 2016.
AT KIBO PALACE HOTEL, ARUSHA CITY

Representatives, World Health Organization, 
Distinguished Representatives of Development Partner Agencies,
Director of Preventive Services-Dr. Neema Rusibamayila
Distinguished guests, 
Delegates from Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children and its Institutions
Ladies and Gentlemen.

Let me take this opportunity on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania, to warmly welcome you all to the fifth (5th) Annual Joint Planning Meeting for the Control of Neglected Tropical Diseases in Tanzania. I wish to thank every one of you who made this important meeting happen. The attendance shows how committed you are, and you are much eager to support the control and elimination of NTDs in the endemic countries, Tanzania being one them. For those coming from outside of this country, I would like to assure you that, Tanzania is a country of peace and I hope you will enjoy the hospitality of Tanzanians, specifically the Arusha City, “the Geneva of Africa” during your stay here. Please spare time to visit our national parks and world’s wonders of Ngorongoro crater as well as the rift valley and the famous Serengeti National Park. 

Ladies & Gentlemen 
With support of Development Partners, Tanzania has undertaken a move to integrate vertical programs back in 2009, in attempting to control and eventually to eliminate the disease impacts on individuals, families and the society in general. The implementation of the Integrated control of NTDs has been in stepwise approach due to funding availability. We started with 36 councils of 6 regions in 2009 and by  2015, we reached all  186 councils in the current 26 regions .This is a great achievement and I would like to congratulate those who made this possible. May GOD bless you. 

Ladies & Gentlemen 
Currently, the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children (MoHCDGEC) through the National Neglected Tropical Diseases Control Program (NTDCP) is responsible for coordination of the implementation of interventions stipulated in the Strategic Master Plan for the Neglected Tropical Diseases Control Program (2012 – 2017). The strategic plan is the roadmap by which, the vision of “Tanzania free of NTD’s” can be achieved. NTDs are included into the Health Strategic Plans and its budget tools, these are the HSSP (IV)   2015-2020 and the comprehensive Council Health Plans (CCHPs).The plan is based on the principles of organizational integration of health services as well as, a wider intersectoral integration between other Ministries.

The NTD Master-plan  is prioritizing 4 areas: (i) Strengthen Government Ownership, Advocacy, Coordination and Partnership, (ii) Planning for results, Resource mobilization and Financial sustainability, (iii) Scale up access to interventions, treatment and system capacity building and (iv)  NTD monitoring and evaluation, surveillance, Information, Education and Communication (IEC) and operational research 

 Ladies & Gentlemen 
I would like to share with you the key activities implemented in 2015/2016. 
First and foremost, there has been a strong in-country collaboration between partner’s organizations including IMA-World Health, Sight Savers –Tanzania Office, World Health Organization Country Office, Helen Keller International, Kongwa Trachoma Project, Kilimanjaro Center for Community Opthalmology,  and  many others.

With this collaboration, in this year 2015/16, we have achieved the full (100%) geographical coverage in Mass Drug Administration (MDA). This was also attained in a stepwise approach as all councils that need MDA for onchocerciasis were reached by 2009, for Lymphatic Filariasis  in 2014 and for Soil Transmitted Helminthiasis and Schistosomiasis in 2015/16. In terms of treatments in 2013, over 19 million people were treated with 45 million treatments of Ivermectin, Albendazole, Praziquantel and Zithromax, and in 2014; over 23 million people were reached with 55 million treatments of Ivermectin, Albendazole, Praziquantel and Zithromax.

On morbidity management, we are delightful for the continuation support of the DFID and TRUST Fund in 6 regions with highest Trachomatous Trichiasis (TT)  backlog namely Manyara, Pwani, Lindi , Mtwara, Dodoma and Arusha. DFID-TRUST  are working in collaboration with in-country Grantee partners: IMA-world health, Sight Savers TZ Office, Kongwa Trachoma Project (KTP), and Kilimanjaro Center for Community Ophthalmology (KCCO), and not forgetting their coordinating partner- Helen Keller International TZ office. 

This project has a purpose of scaling up TT surgery in the country on efforts to reduce TT backlog in Tanzania.  During the year 2015/2016 TT surgical camps continued in the 6 regions; and also under the support of Sight Savers -TZ in Tanga, Ruvuma, and Pwani regions, a total of 2,598 TT surgeries were done. 

On Lymphatic filariasis morbidity management, we are very delightful for the support of  208 hydrocele surgeries  in Pangani  district from End-Fund and 1,160 hydrocele surgeries in Mtwara and Lindi regions from IMA World Health in 2015/2016.

Ladies and Gentlemen,
In Progress to reach 2020 World Health Assembly (WHA) goals, Tanzania has made a profound achievements  since the inception of the integrated NTD program: Some of the achievements include; stopping of MDA in a  number of implementation councils  countrywide, i.e., 166 council to 63 councils by this year.
For Trachoma, 22 districts have met the criteria of stopping Zithromax MDA for Trachoma, thus further shrinking the Tanzania trachoma map. By end of 2015, only 18 councils needed Zithromax MDA. Many more districts are expected to achieve the Trachomatous Foliculitis (TF) level of <5 .="" i="">

The country has also reached, received and adopted  the new WHO guidelines on onchocerciasis elimination which stipulates that, before stopping ivermectin MDA for onchocercias, new serological tests together with entomological evaluations need to be conducted to all districts.

 Ladies and Gentlemen,
The NTD program has made a significant progress during 2015/2016 in the areas of strengthening M&E systems which includes development of NTD Data-base and Web-site. The MDA data is all being entered directly into the program database. This has been a remarkable achievement for the program. 
However, the program still faces a big challenge on the funding gap which is mostly reflected in areas of: Database roll out and electronic data collection, Entomological survey funding for Onchocerciasis elimination, and Lymphatic Filariasis morbidity control, just to mention the few.  

Ladies and Gentlemen,
It is my hope that, through this forum, you will continue to foster the partnership which will enable you to share experiences, best practices, information and approaches to preventing and controlling NTDs. In our health sector strategic plan III as well as  plan IV, we have strategy which addresses Public Private Partnership (PPP) in health care that aim at promoting quality health services through networking and strengthening partnership.  It is my hope that, this forum will continue to address these issues with the aim of improving the health of our Nation. Your efforts combined with ours will make a difference.

Ladies & Gentlemen 
The Government of United Republic of Tanzania will continue to collaborate with Development Partners and other stakeholders in addressing all challenges facing the Strategic Master Plan for the Neglected Tropical Diseases Control Program through development of sustainable program, with a key notion that Government is the steering wheel. This is important especially for creation of government ownership and transparency. Please always have a confidence in our Government that it will support you.

On this occasion I am delighted that Tanzania delegation participated in the closure of African Program for Onchocerciasis Control (APOC) in Kampala Uganda on December 2015. Tanzania also has been in the forefront to support and hence launch of the new entity ‘Expanded  Special Project  for Elimination of NTDs (ESPEN)  to be hosted at AFRO-HQ. It’s a major step indeed, and I urge partners to support  African endemic countries in a more coordinated manner  which will make us  attain our desired goals of countries free of NTDs.

Ladies & Gentlemen 
At this juncture, I would like to wish you fruitful deliberations throughout these 2 days, and I do hope the meeting will come out with tangible plans for NTD implementation for the year 2016/17.
With these few remarks, I would like to declare that the meeting is officially opened. 
                           Thank you for your kind attention.

Usajili Azania Kids Run 2016 wapamba moto

MCHAKATO wa usajili wa washiriki wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, umezidi kushika kasi, huku siku tatu zikiwa zimesalia kabla ya kufanyika kwake Juni 5 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, alisema kufikia jana mchana, mchakato wa usajili ulikuwa ukiendelea vema, ambako wazazi na walezi wamejitokeza kusajili watoto wao.

Gidabuday alisema kuwa, matarajio ni kusajili watoto wapatao 2,000 walio na umri chini ya miaka 16, ambao watashiriki Azania Bank Kids Run 2016, mbio zilizogawanywa katika kategori tano za kilomoita 5, km 2, km 1, mita 100 na mita 50.
Alibainisha kuwa, fomu za ushiriki zinapatikana katika Matawi ya Azania Bank popote jijini Dar es Salaam, pamoja na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji. Aliwataka wazazi na walezi ambao hawajachukua fomu za ushiriki wa watoto wao, kuchangamkia mchakato huo kwa kufika katika vituo husika na kununua fomu hizo kwa shilingi 2,000 tu, ili kuwawezesha watoto kushiriki na kushinda zawadi.

Naye, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank inayodhamini mashindano hayo, Othman Jibrea, alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kusajili watoto wao katika Azania Bank Kids Run, ili kufikia lengo lao la kuibua vipaji vipya vya riadha.

Jibrea alibainsiha kuwa, Azania Bank imejitosa kudhamini mbio hizo kutokana na mlengo wake wa kuibua vipaji vichanga katika riadha, hivyo ili kufikia lengo, wazazui na walezi hawana budi kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao.

Alizitaja zawadi za mbio za Kilomita tano kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu, wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo (track suit).

Jibrea alibainisha kuwa, mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 2 atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh. 50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.

Katika mbio za kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh. 75,000 kwa mshindi wa kwanza, 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.

"Pia, washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh. 15,000, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo. Nia ni kuwafanya watoto watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano," alisema Jibrea.

FOUNDING FIRST LADIES ADDRESS EALA, CALL ON EAC TO FORTIFY INTEGRATION

East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: June 1, 2016: In a memorable occasion for the East African Legislative Assembly, founding First Ladies of the EAC late yesterday delivered motivating addresses at a Special Sitting held in Arusha.

Looking graceful yet resplendent, Kenya’s Mama Ngina Kenyatta and Uganda’s Mama Miria Obote brought back the good old memories of the first EAC and challenged EALA Members to ensure the future of integration is both guaranteed and realised.  The United Republic of Tanzania’s Mama Maria Nyerere sent her apologies. Her family was however represented at the occasion of the Special Sitting by Hon Makongoro Nyerere, who is an elected Member of EALA.

First to take the podium was Mama Miria Obote who was emphatic that the EAC must re-energise itself and strive to be a fully functioning integration bloc.   The former First Lady called for prioritisation of economic investment projects including oil refineries, the Standard Gauge Railway, agricultural research, food security and climate change.
A birds eye view of the proceedings

The founding First Lady called for creation of employment opportunities especially for the youth in the region.

“This can be achieved through joint or common East African Community investments such as the ongoing projects between Uganda and Tanzania for the proposed pipeline, Uganda, Rwanda, Tanzania and Kenya for the Standard Gauge Railway; Kenya, Ethiopia and the new South Sudan for the Lamu Port. The clear call should be an intensification of efforts across various fields to make our region more integrated”, H.E. Mama Obote said.

She further called for the region to move faster to have an integrated syllabus and curriculum to stabilise the labour market within the EAC.
H.E. Mama Miria Obote delivers her remarks as H.E Mama Ngina Kenyatta pays attention at the Special Sitting in Arusha.

“For instance, a majority of Ugandans have never learnt proper Swahili. We are now learning proper Swahili in schools and in the public engagement. This is the best way towards integration”, Mama Obote said.

Mama Miria Obote was full of praise for the EALA for recognising the contribution of the founding families.

“We are very grateful for EAC and EALA for recognising the contribution of our founding Fathers, Comrade Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Jomo Kenyatta & Comrade Dr. Apolo Milton Obote and we are also thankful to the Almighty God for having kept us alive as former First Ladies of the Independent East African Community, Mama Miria Nyerere, Mama Ngina Kenyatta and I”, Mama Obote said. 
EALA Speaker presents a plaque to Hon Makongoro Nyerere, Member of EALA and son of the founding father of the United Republic of Tanzania, H.E. Mwalimu Julius Nyerere and H.E. Mama Maria Nyerere.

She further appreciated the Governments of the United Republic of Tanzania, Kenya and their people who as the original Members of the East African Community, understood the social-political challenges of Uganda.

“They welcomed, sheltered and catered for our people as political refugees. This spirit of togetherness was extended to Rwanda, Burundi, the Democratic Republic of Congo and the new South Sudan. Not only for receiving and hosting refugees but also for walking the extra mile and facilitating peace talks, for example”, H.E. Mama Obote said.

Mama Ngina Kenyatta informed the Sitting that EAC’s founding fathers had “walked and worked tirelessly” in anticipation of unity of the region. 
EALA Speaker presents a plaque to H.E. Mama Ngina Kenyatta.

“In 1967, all three of us were witness to the establishment of a Community that spoke to that shared sentiment. The East African Community was built on the understanding that our nations and our peoples were stronger together.  I request you to keep the hope of the founding fathers alive and to ensure that unity in the region is achieved”, Mama Ngina said.

“It is a credit to your hard work and persistence—and the hard work and persistence of your respective Governments—that today, that Community is more vibrant and active than ever”, the former First Lady added.

The first lady informed the August House that the region was on the verge of realizing the dream of integration.  She challenged EALA and the current EAC to strive to ensure disunity and mistrust was removed in a bid to strengthen integration

Hon Miria Obote was accompanied by her son, Hon James Akena while H.E. Mama Ngina Kenyatta’s entourage consisted of her family members including Mrs Wambui, Kristina Pratt, Selina Renee Pratt, Members of the Parliament of Kenya, women leaders from Central Kenya and representatives of the Mount Kenya University.
The EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Fred Kidega receives H.E. Mama Miria Obote and H.E. Mama Ngina Kenyatta earlier today

Welcoming the founding First ladies of Independence, Speaker of EALA, Rt. Hon Daniel Fred Kidega, lauded them for their contribution to the integration process.“We are happy that you still show leadership in your own rights and continue to be involved in numerous humanitarian causes throughout the EAC region much akin to your active and prolific years when you worked for political and social justice and advocated for a wide range of human rights issues”, the Speaker said.

“Today, we celebrate you. You are walking encyclopedias in your own rights and repositories of information, who despite ageing gracefully, still credit, follow developments of this great region, and are supportive of the EAC unto this day. Late last year for example, Mama Ngina Kenyatta met with the EALA Kenya Chapter in Gatundu, Kenya, while in August 2014, a group of EALA Women Members paid a courtesy call on Mama Maria Nyerere in Dar Es Salaam. Mama Obote on her part, is still involved in the political spheres in Uganda and continues to follow developments at the EAC closely from Uganda House in Kampala”, the Speaker added.

The Speaker remarked that the integration process was on course and that it was stronger.  “Indeed, in retrospect, the collapse of the Community in 1977 was a sad and catastrophic affair, a great loss in opportunities and setback for the region.   But today, I stand here convinced that the steps we have taken as a Community since its re-establishment are fundamentally underpinned on the Treaty for the Establishment of the EAC and we are on course for full integration of the region”.

The Assembly at its Sitting 5th Meeting of the 4th Session on March 16th, 2016, passed a Resolution recognizing the role you all continue to play in galvanizing East Africa in the integration process and in the service of East Africans as “informal Institutional Memory”. The Resolution was moved by Hon Mumbi Ngaru.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MRADI WA UZALISHAJI WA NG'OMBE WA MAZIWA GEREZA MTEGO WA SIMBA NA GEREZA KUU LA WANAWAKE KINGOLWIRA, MKOANI MOROGORO

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea salaam kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, ACP. Shaban Kitolo mara tu baada ya kuwasili katika Gereza Mtego wa Simba katika ziara yake ya kikazi Mei 31, 2016, Mkoani Morogoro(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projest Rwegasira akionja chakula cha Wafungwa katika Jiko la Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya kikazi ili kujionea Uendeshaji wa Magereza hapa nchini(kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira, ACP. Loyce Ruhembe(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP. John Casmir Minja.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, CGP, John Casmir Minja(kulia) akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Projest Rwegasira kuelekea katika Shamba la uzalishaji wa ng'ombe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba.
Sajini Taji wa Jeshi la Magereza, Sarah Kabunda ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ufugaji Kuku katika Gereza Kuu la Wanawake Kongolwira akitoa maelezo ya Kitaalam kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira namna Ufugaji kuku unavyofanyika.
Wafungwa wa Kike katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira(walioketi) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(meza Kuu) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo ili kujionea uendeshaji wa Magereza hapa nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia kundi la ng'ombe wa maziwa katika shamba la uzalishaji wa ng'ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba, Mkoani Morogoro. Gereza hilo hivi sasa linafuga ng'ombe wa maziwa 496.
Kundi la ng'ombe wa maziwa wanaofugwa katika shamba la uzalishaji Mifugo Gereza Mtego wa Simba, Kingolwira Mkoani Morogoro wakiwa malishoni kama wanavyoonekana katika picha. (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA TING KUBORESHA MAPATO YA UWANJA WA TAIFA.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.(Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM)


Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.

Akizungumza hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.

“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.

Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.

Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.

Kampuni ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika miundombinu na wataalam.Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.

Akizungumza hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.

“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.

Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.

Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.

Kampuni ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika miundombinu na wataalam.