Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar .
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza bidhaa zilizopitwa na wakati.
Waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali, amesema
kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi juu ya tabia ya
baadhi ya wafanyabiashara kuwauzia vitu vilivyopitwa na wakati.
Amefahamisha
kuwa, udanganyifu huo unaofanywa na wafanyabiashara huwasababishia
wananchi kupata maradhi mbalimbali ikiwemo saratani.Akiwa
katika ziara ya kukagua maghala mbalimbali ya chakula kisiwani Unguja
kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani, Balozi Amina amesema serikali
imechoka kuona wananchi wanauziwa vyakula visivyokuwa na kiwango
kutokana na kumalizika muda wao wa matumizi.
Waziri
huyo amekemea vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara kuuza vyakula
vilivyokaa maghalani kwa muda mrefu hata kupindukia miaka mitano, hali
aliyosema ni kuwaathiri na kuwadhulumu wananchi.“Wazanzibari
tumechoka kulishwa michele mibovu. Tunasema sasa imetosha na
hatutawafumbia macho wafanyabiashara watakaoendeleza vitendo hivyo,”
alisema Waziri Amina.
Amesema
serikali inakusudia kuweka bei elekezi kwa wafanyabiashara wote ili
kuzuia upandaji bei kiholela hali inayowapa usumbufu wananchi hasa wa
kipato cha chini.Aidha
Balozi Amina amesema kila mwaka ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani,
serikali imekuwa ikipunguza kodi za bidhaa muhimu kwa wafanyabiashara
ili kutoa punguzo kwa wananchi.
Amezitaja bidhaa hizo kuwa ni unga wa ngano, sukari na mchele.
Hata
hivyo, ameeleza kusikitishwa kwake kwamba bei za bidhaa hizo zimebakia
palepale au kuongezeka zaidi licha ya nia nzuri ya serikali.Ili
kuandaa mazingira ya kuwapa unafuu wananchi, amesema serikali
inakusudia kukaa na wafanyabiashara wote ili kujadili na kupanga mipango
mizuri kwa itakayowaletea maendeleo wafanyabiashara hao na taifa kwa
jumla.
Kwa
upande wao, wafanyabiashara waliotembelewa na Waziri huyo,
wamemuhakikishia kuwa chakula kipo cha kutosha katika kipindi hiki cha
kuelelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani.Aidha wamesema chakula hicho kimeagizwa miezi mitatu kabla ya mwezi huo.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake, mfanyabiashara Abdulghafar Ismail Mohammed wa
kampuni ya Evergreen Ltd, ameiomba serikali kukaa pamoja nao pale
inapotaka kufanya maamuzi yoyote yanayowahusu ili kuweka uwiano kwa
upande wao, serikali na wananchi.
Ziara
ya Balozi Amina ilihusisha maghala ya kampuni za Yassir Provision,
Akhtar Enterprises Malindi, Evergreen Ltd Saateni, Sub Sahara Maruhubi,
Azam Mtoni, Vigor Turkey Group na Bopar Enterprises zote za Mombasa
mjini Unguja.
Pamoja
na kujua akiba ya chakula iliyopo nchini kupitia ziara hiyo, Waziri
Amina pia alitaka kujua hali ya mfumko wa bei kuelekea mwezi mtukufu wa
Ramadhani unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo.
MENEJA
Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed akimfahamisha
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu ya hali ya
chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saaeteni mjini Zanzibar.
WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.
WAZIRI
wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akisaini kitabu cha
wageni alipotembelea kiwanda cha Zanzibar Milling Corporation kilichoko
Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
MENEJA
Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Khalid Ali Yussuf,
akimpa maelezo Waziri Amina Salum Ali juu ya uzalishaji wa chakula
alipotembelea ofisini kwake Mtoni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
WAZIRI
wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika maeneo ya
kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya ziara maalum
kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa kuelekea
mwezi mtukufu wa Ramadhan.
WAZIRI
wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa ngano na
Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni Zanzibar
Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea kiwanda
hicho.
MENEJA
Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said, akizungumza na
Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake
Mombasa mjini Zanzibar.PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment