Tuesday, March 1, 2016

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AKIKABIDHI MICHANGO YA TWIGA STARS.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). 
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga akitoa shukura kwa Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia wadhamini Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura(wapili kutoka kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” (Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. 
Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”  Bibi. Nasra Juma  wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM.
 Naibu Waziri wa  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimweleza jambo   Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha hizo  katika Benki ya NMB Bank House akaunti  namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”. 
 Naibu Waziri wa  Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi  Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka  jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Fedha hizo zimewekwa  katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Picha na Anna Nkinda.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKAMILISHA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI TANGA

 Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga Mwanakombo Mwakuru akimvisha Skafu Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais  amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga. Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe.Henri Shikifu.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliangalia vijana wa kikundi cha sanaa cha Tanga kwanza alipowasili Ofisi  ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.       
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01.2016.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Tanga katika Ofisi ya CCM Nkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01,2016.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na vijana wa kikundi cha wasanii cha Tanga kwanza alipokua akiondoka katika Ofisi ya Chama cha  Mapinduzi CCM Mkoa Tanga baada ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016.
  (Picha na OMR).               

MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA (TCAA), HAMZA JOHARI.AANZA KAZI RASMI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (katikati) akimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa Mamlaka hiyo , Vallery Chamulungu wakati alipokuwa akimkaribisha rasmi ofsini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).Hamza Johari (watatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa Mamlaka hiyo , Vallery Chamulungu (watatu kutoka kulia) wakati alipokuwa akimkaribisha rasmi ofisini Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam. Wengini ni maofsa wa mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari (KUSHOTO)akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uongozaji ndege na Huduma za ufundi , Bw. Nyello Abeid ,wakati wa kumkalibisha rasmi kuanza kazi TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiwa katika kikao na menejimenti ya Mamlaka hiyo mara baada ya kukaribishwa rasmi kuanza kazi Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akiwa rasmi ofini kwake kuanza majukumu yake kama Mkurugenzi Mkuu TCAA ,baada ya kukaribishwa rasmi TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akipokea Shada la maua kutoka kwa mmoja wa wafanyaakzi wa Mamlaka hiyo ,Evelyne Ngachengo ,wakati alipokuwaakikaribishwa na wafanyakazi wenzake rasmi kuanza kazi ,rasmi ofisini Makao Makuu ya TCAA, Banana Ukonga Dar es Salaam

Mahakama ya Tanzania yakutana na Wadau wa Haki jijini Dar es salaam, yasisitiza utoaji wa Haki kwa wakati

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza.
Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akitoa mchango wake kuhusu uboreshaji wa huduma ya Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza akizungumza na Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam.
Washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.

Na Aron Msigwa – Dar es salaam.

Mahakama ya Tanzania imesema kuwa inaendelea na mkakati wa kufanya maboresho ya miundombinu yake ili kurahisisha utoaji wa huduma ya mahakama kwa wadau na wananchi kwa wakati. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Katanga wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi mmoja, jijini Dar es salaam.

Bw. Katanga amewaambia wadau hao kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya mabadiliko ya huduma zake kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka Serikalini pia kutoka kwa wadau wa Haki wanaoiwezesha Mahakama kufanya maboresho hayo kwa lengo la kukuza Utoaji wa Haki nchini.

Amesema ili kusogeza huduma karibu na wananchi Mahakama itatekeleza Mpango mkakati wa miaka 5 wa kuiwezesha kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau na Taasisi za utoaji Haki katika masuala yanayohusu shughuli za kila siku za utendaji wa Mahakama nchini.

“ Mahakama tutaanzisha mpango wa miaka 5 ambao utaanzisha mfumo wa wa kushirikiana na wadau wetu kwa karibu katika mambo yanayohusu shughuli zetu ili kuwaondolea wananchi usumbufu na upotevu wa muda pindi wanapofuatilia huduma” Amesema.

Amefafanua kuwa Mahakama imeshaanza kujenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama za Mwanzo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya mwanzo Kigamboni jijini na Kawe zote za jijini Dar es salaam, Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga na Kibaha mkoani Pwani ili kurahisisha utoaji wa Haki.

“ Mahakama sasa tuko katika mwelekeo mzuri wa kufanya mabadiliko, kwa kushirikiana na wataalam wetu wa ndani wakiwemo Chuo Kikuu Ardhi , tunaendelea kujenga majengo mapya ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Kigamboni, Mkuranga, Kibaha na Kawe ambayo yatakamilika ifikapo Juni mwaka huu” Amesisitiza.

Bw. Katanga ameongeza kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa majengo yaliyopo yanakarabatiwa sanjali na ujenzi wa majengo mapya katika Mahakama zote 133 nchi nzima.

Aidha, amebainisha kuwa Mahakama inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa watumishi wake ikiwemo ununuzi wa mabasi ya kusafirishia watumishi, magari madogo na Pikipiki ili kuwawesha watumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Solanus Nyimbi akizungumza na wadau hao amewataka wafanye kazi kwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza imani yao kwa Mahakama.

Amezitaka Taasisi na wadau wanaohusika na utoaji wa Haki kujikita katika kushughulikia matatizo ya wananchi ili kufanikisha dhana ya Utoaji Haki kwa Wakati ili kwenda na mpango uliowekwa na Mahakama wa kuondoa mrundikano wa mashauri mahakamani na ule wa kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu. 

Naye Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Lugalema Kahyoza ametoa wito kwa Taasisi za Utoaji wa Haki kukutana mara kwa mara ili kujdili na kutatua changamoto zinazoukabili Utoaji wa Haki nchini.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI


Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral 
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo.
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi.
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).

UNCDF YAWAKUTANISHA WATAALAMU WA FEDHA KUTOKA NCHI MBALIMBALI KUJADILI JINSI YA KULETA MAENDELEO KWA KUTUMIA VYANZO VYA NDANI

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Benki ya TIB, Jaffer Machano, akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
 Mtoa Mada, Suzane Ngane kutoka Cameroun,  akitoa mada kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shemumoyo, kitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
Na Beda msimbe
Wataalamu  wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza mkutano wa siku mbili jijini Dare s Salaam kuangalia namna ya  kuwezesha fedha za kusaidia maendeleo endelevu  kwa kutumia vyanzo vya ndani.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro umelenga kuja na maelezo muafaka ya namna ya kupata fedha za kuendesha na kujenga miundombinu mbalimbali kwa ajili ya miji inayotanuka.

Katika mahojiano na mwandishi wa Mo Blog kuhusu mkutano huo , mmoja wa wakurugenzi wa UNCDF kutoka makao makuu anayeshughulikia uendelezi wa fedha, David Jackson alisema kwamba wataalamu walioalikwa wanatarajiwa kutoka na msimamo unahusu uwezeshaji wa fedha wa ndani.

Alisema wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya wananchi kutoka vijijini kwenda mijini uwezo wa majiji mengi duniani ikiwamo manispaa ni mdogo kuwezesha kutengeneza miundombinu na pia kuwezesha ajira.

Alisema  kwa sasa kutokana na uwingi wa watu wanaofurika katika miji, halmashauri  na uhaba wa fedha kutoka katika vyanzo vya mapato kumesababisha kushindwa kuendelezwa mifumo endelevu ya miundombinu na ajira na kulazimisha wataalamu kuanza kuangalia namna nyingine ya kupata fedha.

Alisema mpango wa kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwa kuunganisha nguvu nje ya mfumo rasmi umewezekana Tanzania hasa kutokana na manispaa kama ya Kibaha kuwezeshwa kupata fedha za miradi mbalimbali na wengine nao watatoa uzoefu wao.

“Zamani ilikuwa rahisi sana kwa manispaa nyingi kutengeneza mipango ya maendeleo, lakini kwa sasa kutokana na uwingi wahamaji vyanzo vya kawaida vimezidiwa na kuonekana haja ya kutafuta vyanzo vingine ili kuwezesha maendeleo na ajira,” alisema Jackson.

Alisema mataifa yanahitaji sasa kuangalia mifumo yao ya kuwezesha maendeleo endelevu kwa kutumia vyanzo vya ndani ambavyo vinawezekana kupatikana.

Aliongeza kuwa miradi mikubwa ya maendeleo haiwezi kufanywa na vyanzo vya zamani na kutolea mfano mradi wa maji wa Abu Dhabi ambao umewezeshwa kwa kutumia vyanzo vya ndani lakini kwa namna ambayo inasaidia mji huo kuwa na maji ya uhakika pamoja na kwamba vyanzo vyake havifai.

Alisema ni matumaini yake kwamba baada ya kusikiliza mada mbalimbali wataalamu hao watakuwa na nafasi ya kutoa tamko la namna bora ya kushirikisha wadau wa maendeleo wa ndani kutengeneza miradi mikubwa ya huduma kwa jamii.

Pia alisema kwamba washiriki katika mkutano huo wa siku 2 ni pamoja na wadau wa maendeleo kutoka Uswisi, Sweden na Denmark wapo pia wataalamu wa masuala ya fedha, miradi kutoka Afrika Kusini, Ethiopia, Benin, Rwanda, Mali, Senegal,Uganda, Msumbiji, india, Bangladesh , Marekani na Tanzania.

Mkutano huo wa mashauriano uliandaliwa na UNCDF ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio la AddisAbaba kuhusu maendeleo endelevu na umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kifedha wa manispaa mbalimbali.
Mchumi Daniel Platz kutoka Umoja wa Mataifa akiwasilisha mada kwa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo waliokutana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala
 Washiriki wa mkutano wa kimataifa wa siku mbili wa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo wakifuatilia mada ikliyorushwa kwa njia ya video na Profesa Paul Smoke kutoka Chuo Kikuu Cha New York, nchini Marekani.
 Mchumi, John Boex, akitoa mada kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili ulioanza Februari 29, 2016
 Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala, akiongoza mkutano wakati wa asubuhi
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa(UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala
 Baadhi yawashiriki wakifuatilia kwa makini yanayoendelea katika mkutano
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akiwa kwennye mahojiano na Mjumbe kutoka nchini Uganda, Naibu Mkurugenzi wa usimamizi wa mikakati na maendeleo ya biashara, jiji la Kampala, Patrick Musoke, pembezonimwa mkutano wa siku mbili wa wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016
Wajumbe wakibadilishana mawazo.(Picha zote na Khalfan Said na Geofrey Adroph.)

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AZINDUA MRADI WA MAJI MKOANI KILIMANJARO

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.

Mhe. Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.

Vilevile, Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha. 

Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
Jiwe la msingi likiashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga (kulia) na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akiwa na viongozi na wataalamu aliombatana nao kwenye ziara yake kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Inj. Ruth Koya akimuonyesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge moja ya miradi ya maji inayotekelezwa na mamlaka hiyo, Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru.