Friday, January 1, 2016

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WA MKESHA WA MWAKA 2016 KATIKA PICHA

Mhandisi Mohamed Millanga akiongoza msafara wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TBIII).
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa TBIII kutoka kwa mhandisi Mohamed Millanga (kulia).
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
 Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
Waziri waWizara ya Ujenzi,. Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prtof Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni katika jingo la kikosi cha zimamoto cha kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


 DAR ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh.Prof.  Makame Mbarawa ameagiza  watumishi wa Tassisi  zote  zinazotoa  huduma katika viwanja vya ndege  hapa nchini kuwajibika kwa Mameneja  wa Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege  (TAA)  wanaosimamia  viwanja  ambavyo  watumishi hao wamepangiwa  kufanya  kazi. 

Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu  ya  TAA  ambapo  pamoja na mambo mengine  alikagua  ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria (TBIII), na  kituo cha Zimamoto na Uokoaji. Pia  alitembelea mradi  wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding  Bridges) na  usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa dharura (Standby Generators) iliyopo katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza  na menejimenti ya TAA ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi  Suleiman S. Suleiman  katika Ofisi  za TAA  ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa aliwapongeza TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan  katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja. Hata hivyo alisema pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine zote  zinazofanyakazi katika viwanja vya  ndege hapa nchini kama njia ya  kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.

“ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani  wakati umefika sasa kwa taasisi zote zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini  ziwe chini ya TAA”,  alisema  Prof. Mbarawa  huku akisisitiza umuhimu wa  taasisi hizo kufanya kazi  kwa kushirikiana  kama timu moja. 
 “Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria, watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,” alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na Wizara zote zinazohusiana  na taasisi hizo ili kupanga utaratibu muafaka.
Mbali na idara ya uhamiaji,  taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili,  afya, kilimo, mifugo, madini,  polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya.  
Mh. Mbarawa  pia  ameiagiza  TAA kubuni  mikakati  ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia ihakikishe kuwa inaepukana  na matumizi yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA  kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji wao wa kazi na kuhudumia wateja  ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.
“Nisingependa taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza Mh. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi S.S.Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake, likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya mamlaka na wizara kwa ujumla. 
“Kuhusu mapato tunauhakika wakati wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni mbinu nyingi zaidi, ili  tuwe na vyanzo vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.
Awali Mh. Mbarawa alipotembelea ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hususan  magari ya zimamoto ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine  kulazimika pia kusaidia  jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga ya  moto.
        Imetolewa na kitengo cha 
Habari na Mahusiano na Sheria TAA.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WA MKESHA WA MWAKA 2016 KATIKA PICHA

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake, wakishangilia baada ya kutimia saa sita kamili usiku juzi, Kwenye Uwanja wa Uhuru, walipokuwa wakisherehekea mwaka mpya. (Picha na Francis Dande)
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akipongezana na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akiwa na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakiwa katika mkesha wa mwaka 2016.
 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyakea wakiwa katika mkesha wa mwaka mpya.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mkewe wakicheza kwa furaha wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa na furaha wakati wa mkesha wa mwaka 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akicheza nyimbo za injili wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha wa Kuliombea Taifa (Dua maalum), Mchungaji Godfrey Mallassu akizungumza katika mkesha huo.
 Brass Band ikitoa burudani wakati wa mkesha huo.
 Watu wa dini mbalimbali wakitoa sadaka katika mkesha huo.
 Kwaya ikiimba.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye alimwakilisha Rais Dk. John Magufuli akitoa hotuba yake.
DJ Timber akifanya vitu vyake wakati wa mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye Ukumbi wa Club Bilz, Posta jijini Dar es Salaam. 

DAR ES SALAAM, Tanzania


WAKATI Rais Dk. John Magufuli akizidi kuwaomba waumini wa dini mbalimbali nchini kumuombea katika mchakato wake wa kupambana na mafisadi, amewataka Watanzania kutumbua majipu madogo wanayoishi nayo mitaani likiwamo la uhujumu uchumi ili taifa liweze kusonga mbele.

Tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani imekuwa ikiwachukulia hatua mbalimbali wala rushwa na wakwepa kodi ambao walichangia serikali kupoteza mapato.

Akizungumza katika mkesha wa kuliombea taifa pamoja na kuukaribisha mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Rais Dk. Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema kwa kipindi kirefu taifa limekabiliwa na vigogo wanaouza dawa za kulevya, wakwepaji wa kodi, walaji wa fedha za maendeleo pamoja na wizi wa dawa katika hospitali nchini.

Lukuvi alisema kuwa Watanzania hawapaswi kumuachia mzigo huo Rais Magufuli peke yake bali wawe tayari kukabiliana na majipu hayo kutokana na idadi kubwa ya wabadhirifu hao wanaoanzia ngazi za chini, wakiwamo watumishi wa halmashauri ambao wanaweza kuwajibishwa na  wananchi kabla ya kumsubiri rais.

“Kazi iliyopo hivi sasa ni kwa viongozi wa dini na Watanzania kulivalia njuga suala hili na kila mtu aweze kuyatumbua majipu hayo ambayo yanakwamisha mafanikio ya kimaendeleo,” alisema.
Waziri huyo alisema viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea taifa hasa kwa wale wasiopenda maendeleo ili waweze kubadilika, hatua itakayosaidia kuweza kupiga hatua.

Alisema ubadhirifu wa mali za umma umechangia kuzorotesha maendeleo ya Watanzania kutokana na watu wachache wasiokuwa waaminifu serikalini kuendekeza vitendo vya rushwa.

“Viongozi wa dini wanapaswa kuwahubiria waumini wao kuwa wafanye kazi kwa bidii kwani hata vitabu vya dini vinaeleza kwamba asiyefanya kazi na asile, hivyo kutokana na kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ ni lazima ifanywe kwa vitendo,” alisema.

Lukuvi aliwataka Watanzania waendelee kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli kutokana na hatua mbalimbali anazozichukua dhidi ya watumishi wa umma, kukabiliana na wizi wa dawa katika vituo vya afya na watumishi wazembe ambao hawafanyi kazi kama inavyohitajika.

Kuhusu suala la amani, Lukuvi alibainisha kuwa inatakiwa kuendelezwa kwa ushirikiano bila kujali itikadi za vyama na dini zao ili kutunza umoja, mshikamano na amani iliyopo ambayo imedumu tangu taifa lipate uhuru.

“Kama yalivyo malengo ya serikali hii ya Awamu ya Tano kwamba tutafanya kazi chini ya misingi ya haki bila ubaguzi wa dini, rangi wala kabila, hivyo hata wananchi nao wanatakiwa kulifanya hilo,” alisema.

Dar Live na Shangwe za Kuukaribisha Mwaka Mpya 2016

Bella d (74) Christian Bella akipanda jukwaani kuwasalimia mashabiki.Bella d (1) Mashabiki wakijiachia kwa kucheza muziki dakika chache kabla ya kuanza mwaka mpya 2016Bella d (2) Ni full kufurahia. Bella d (5)Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za mkononi, Airtel Tanzania na wafanyakazi wa Dar Live wakiandaa maputo kwa ajili ya shamra shamra za kuukaribisha mwaka mpya 2016. Bella d (7) Bella d (8)Maputo yakipeperushwa hewani kuashiria kuanza mwaka mpya 2016. Bella d (73) Bella akitoa kionjo wakati wa kuukaribisha mwaka mpya. Bella d (27)Christian Bella (mwenye kofia nyekundu) na Mama Tunu wakitikisa chupa za shampeni. Wanaoshuhudia tukio hilo ni mashabiki pamoja na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo (katikati mwenye shati la dratfi). Bella d (29)Zoezi la kufungua shampeni likishika kasi. Bella d (31) Bella d (32)Shampeni ya mama Tunu hiyooooo ikafunguka. Bella d (34)Bella naye akakazana. Bella d (37)Dakika zikatimia.... mwaka 2016 huoooo ukafika. Bella d (44)Bella akaanza kuwaonjesha shampeni mashabiki zake. Bella d (47)Mashabiki wakichukua picha za ukumbusho wa tukio hilo kwenye simu zao. Bella d (75) Bella d (76) Bella d (77)Bella akaanza kutoa vionjo vya nyimbo zake kali.Bella d (78)Bella acha kabisaaaaa Bella d (84)Mashabiki wakifuatilia shoo hiyo.
PICHA NA MUSSA MATEJA/GPL