Friday, January 1, 2016

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WA MKESHA WA MWAKA 2016 KATIKA PICHA

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake, wakishangilia baada ya kutimia saa sita kamili usiku juzi, Kwenye Uwanja wa Uhuru, walipokuwa wakisherehekea mwaka mpya. (Picha na Francis Dande)
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akipongezana na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, akiwa na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape NnauyeWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakiwa katika mkesha wa mwaka 2016.
 Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyakea wakiwa katika mkesha wa mwaka mpya.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na mkewe wakicheza kwa furaha wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa na furaha wakati wa mkesha wa mwaka 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akicheza nyimbo za injili wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha wa Kuliombea Taifa (Dua maalum), Mchungaji Godfrey Mallassu akizungumza katika mkesha huo.
 Brass Band ikitoa burudani wakati wa mkesha huo.
 Watu wa dini mbalimbali wakitoa sadaka katika mkesha huo.
 Kwaya ikiimba.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye alimwakilisha Rais Dk. John Magufuli akitoa hotuba yake.
DJ Timber akifanya vitu vyake wakati wa mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye Ukumbi wa Club Bilz, Posta jijini Dar es Salaam. 

DAR ES SALAAM, Tanzania


WAKATI Rais Dk. John Magufuli akizidi kuwaomba waumini wa dini mbalimbali nchini kumuombea katika mchakato wake wa kupambana na mafisadi, amewataka Watanzania kutumbua majipu madogo wanayoishi nayo mitaani likiwamo la uhujumu uchumi ili taifa liweze kusonga mbele.

Tangu Serikali ya Awamu ya Nne iingie madarakani imekuwa ikiwachukulia hatua mbalimbali wala rushwa na wakwepa kodi ambao walichangia serikali kupoteza mapato.

Akizungumza katika mkesha wa kuliombea taifa pamoja na kuukaribisha mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Rais Dk. Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema kwa kipindi kirefu taifa limekabiliwa na vigogo wanaouza dawa za kulevya, wakwepaji wa kodi, walaji wa fedha za maendeleo pamoja na wizi wa dawa katika hospitali nchini.

Lukuvi alisema kuwa Watanzania hawapaswi kumuachia mzigo huo Rais Magufuli peke yake bali wawe tayari kukabiliana na majipu hayo kutokana na idadi kubwa ya wabadhirifu hao wanaoanzia ngazi za chini, wakiwamo watumishi wa halmashauri ambao wanaweza kuwajibishwa na  wananchi kabla ya kumsubiri rais.

“Kazi iliyopo hivi sasa ni kwa viongozi wa dini na Watanzania kulivalia njuga suala hili na kila mtu aweze kuyatumbua majipu hayo ambayo yanakwamisha mafanikio ya kimaendeleo,” alisema.
Waziri huyo alisema viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea taifa hasa kwa wale wasiopenda maendeleo ili waweze kubadilika, hatua itakayosaidia kuweza kupiga hatua.

Alisema ubadhirifu wa mali za umma umechangia kuzorotesha maendeleo ya Watanzania kutokana na watu wachache wasiokuwa waaminifu serikalini kuendekeza vitendo vya rushwa.

“Viongozi wa dini wanapaswa kuwahubiria waumini wao kuwa wafanye kazi kwa bidii kwani hata vitabu vya dini vinaeleza kwamba asiyefanya kazi na asile, hivyo kutokana na kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ ni lazima ifanywe kwa vitendo,” alisema.

Lukuvi aliwataka Watanzania waendelee kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli kutokana na hatua mbalimbali anazozichukua dhidi ya watumishi wa umma, kukabiliana na wizi wa dawa katika vituo vya afya na watumishi wazembe ambao hawafanyi kazi kama inavyohitajika.

Kuhusu suala la amani, Lukuvi alibainisha kuwa inatakiwa kuendelezwa kwa ushirikiano bila kujali itikadi za vyama na dini zao ili kutunza umoja, mshikamano na amani iliyopo ambayo imedumu tangu taifa lipate uhuru.

“Kama yalivyo malengo ya serikali hii ya Awamu ya Tano kwamba tutafanya kazi chini ya misingi ya haki bila ubaguzi wa dini, rangi wala kabila, hivyo hata wananchi nao wanatakiwa kulifanya hilo,” alisema.

No comments: