Friday, January 1, 2016

Christian Bella Aweka Rekodi Mpya Dar Live!

Bella d (80)Christian Bella akipagawisha mashabiki waliofika Dar Live kwenye shoo ya mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2016.Bella d (81)Malaika Band wakifanya yao.Bella d (82)Mashabiki wakiserebukaBella d (83)Bella d (84)...wakichukua matukio muhimu ya shoo hiyo kwa simu za mkononiBella d (85)Bella d (86)Bella d (87)Ni hatariBella d (88)Bella d (89)Bella akiwaongoza Malaika Band kutumbuiza ukumbini hapo Bella d (93)Bella d (94)Bella d (95)Bella d (96)Bella d (97)...shoo si ikanoga sasaBella d (98)Bella d (99)Bella akitamba jukwaani Bella d (48) Bella d (52)Mashabiki wakinogewa na shoo ya Malaika Band Bella d (55) Bella d (59) Bella d (65) Bella d (67)Bella d (68) Bella d (70) Bella d (73) Bella d (75)Bella d (76)Bella d (77)Bella na jukwaa, Bella na mashabiki Bella d (81)Kama kawaida yao Malaika Band wakikinukisha jukwaaniBella d (82)Bella d (83)Mashabiki wakifuatilia shoo hiyobella (1)Shabiki akipanda jukwaani kucheza na Bella bella (2) Dada huyu akikata mauno wakati wa shoo hiyobella (7) bella (9) bella (10) bella (15) Shabiki na Bella jukwaanibella (16) Bella akiendelea kuwasha motobella (19) bella (20)Shabiki akimzawadia Bella bella (24) Zawadi zikimiminikabella (56) bella (57)Shoo ikibamba bella (58) bella (59) Shangwe za mwaka mpyabella (60) bella (61) bella (62) bella (63) bella (64) Mashabiki wakipanda jukwaanibella (65) bella (66) bella (67) bella (68) Shoo ikinogabella (69)Bella akicheza na mashabiki wake bella (71) bella (72) bella (73) Shoo ikinogabella (74) Bella na mashabiki jukwaanibella (75)Mashabiki wakizidi kupagwa.
PICHA NA MUSA MATEJA/GPL

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAKE ELO IKULU JIJINI DAR.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Jaji Meja Jenerali Projest A.Rwegasira akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora,Dkt.Laurian Ndumbaro akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Waandishi mbalimbali wa Vyombo vya Habari wakifuatilia kwa umakini hafla ya kuwaapisha kwa Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Amina H.Shaban akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa,Balozi Ramadhan  Muombwa Mwinyi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Immaculate Peter Ngwale akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wake iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Profesa Simon S.Msanjila akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wake iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Epifani Mdoe akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,James Dotto akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Amon Mpanju akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wake iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Makatibu Wakuu na manaibu wao kabla ya kuapishwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Pichani kuliani ni Makamau wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao Ikulu jijini Dar,wa tatu kulia ni Mke wa Rais,Mama Janeth Magufuli pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bwa.George Masaju.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa amembatana na  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakiwasili kwenye hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu wao iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR AONGOZA BONANZA LA MAZOEZI YA VIUNGO KITAIFA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza Matembezi ya wanamichezo katika Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo kwa kuwanzia Uwanja wa Tumbaku Mjini Unguja na kumalizia Uwanja wa Amaan Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanamichezo wa Vikundi mbali mbali kama ishara ya kuyapokea maandamano ya vikundi hivyo katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Wamamichezo wa Vikundi vya mazoezi wakipita mbele ya jukwaa kubwa Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa yaliyofanyika leo ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Wanakikundi cha Amakweli Fitness Club ya Welezo Grinada wakibeba bango la Chama cha Mchezo wa Maziezi ya Vuingo Zanzibar (ZABESA) linalosema "JIKINGE DHIDI YA MARADHI YA KISUKARI PRESHA NA SARATANI KWA KUFANYA MAZOEZI"wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi Mwera Fitness Club kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi Chumbuni Studio kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi wakati wa Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Kikundi cha Mazoezi kutoka Kisiwani Pemba kikipita mbele mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipoyapokea matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.

Kikundi kutoka Dar es Salaam ni miongoni mwa vikundi vilivyojumuika katika matembezi ya Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Miongoni mwa Vikundi vya Mazoezi hapa Mjini Unguja nacho kikionesha manjonjo ya aina ya mazoezi mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika kilele cha Bonanza la mazoezi ya viungo kitaifa lililofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguji.

Wananchi watakiwa kuwa nje ya mita 60 kutoka vyanzo vya maji vinavyopeleka Mtera

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Chimwenga wilaya ya Mbeya vijijini ambapo Naibu Waziri aliwaeleza wananchi hao umuhimu wa kukaa mbali na vyanzo vya maji ili kutoviharibu na kusababisha upungufu wa maji unaopelekea bwawa la uzalishaji umeme la Mtera kukauka.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa wakiwa katika kijiji cha Makwenji wilaya ya Mbeya vijijini ambapo Naibu Waziri alikagua vyanzo vinavyotiririsha maji kwenye mito inayopeleka maji katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mwenye tai nyekundu) akikagua moja ya miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji inayofanyika katika wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya ambayo hutumia maji kutoka katika mapitio yanayopeleka maji katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mbele) akiwa katika ukaguzi wa vyanzo vinavyotiririsha maji kwenye mito inayopeleka maji katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.Nyuma yake ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Maendeleo ya Nishati, James Andilile.
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimwangalia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akikagua mapitio ya maji yanayoelekea katika bwawa la uzalishaji umeme la Mtera.

Na Teresia Mhagama, Mbeya

Wananchi wanaozunguka vyanzo  vinavyotiririsha maji katika mito inayomwaga maji kwenye bwawa la uzalishaji umeme la Mtera wametakiwa kuhakikisha kuwa hawafanyi shughuli zozote za kiuchumi au ujenzi wa makazi ndani ya eneo la mita 60 kutoka kilipo chanzo cha maji.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati alipofanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji katika wilaya ya Mbeya vijijini ambavyo vinachangia upatikani wa maji katika bwawa la Mtera lenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 80.

Licha ya kuagiza kwamba eneo hilo la mita 60 lisifanyike shughuli zozote zikiwemo za kilimo na ufugaji, Dkt. Kalemani pia aliiagiza Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mbeya kufanya tathmin ili kufahamu idadi ya watu wanaoishi ndani ya eneo hilo katika vyanzo vyote vya maji ili kuona uwezekano wa kuwahamisha kwa kufuata utaratibu. 

Vilevile Naibu Waziri aliagiza kuwa vyanzo vyote vya maji viwekewe alama ili kuepusha wananchi kuingilia maeneo hayo na kufanya shughuli zitakazoathiri upatikanaji wa maji katka mabwawa ya uzalishaji umeme.

" Zuio hili ni lazima liende sambamba na suala la Halmashauri zetu kuwa na mipango ya matumizi ya ardhi, bila hivyo hakutakuwa na matumizi endelevu ya maji na matokeo ni kama haya ambapo wananchi wanaamua kufanya shughuli kama za kilimo na ufugaji katika vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu," alisema  Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani pia aliwaagiza watendaji wa Wilaya na Halmashauri zinazozunguka vyanzo hivyo, kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi bora ya maji katika vyanzo na mapitio ya maji yanayopeleka maji katika bwawa la mtera ambalo sasa limesimamisha uzalishaji wa umeme kutokana na upungufu wa maji.

Kuhusu suala la wananchi wenye vibali kutumia maji hayo kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, Naibu Waziri alisema kuwa wananchi hao wanapaswa kutumia maji kwa kiwango walichoruhusiwa tu na si vinginevyo na yeyote atakayebainika kuharibu chanzo cha maji atachukuliwa hatua kali za kisheria.

" Wadau mbalimbali wanaosimamia sheria zinazoongoza sekta ya maji ikiwemo Wizara zinazohusika na maji, Kilimo, Mifugo, Nishati  na Madini na Mamlaka za Mabonde, lazima wahakikishe kuwa wanasimamia sheria hizo kikamilifu, kila mtu atimize wajibu wake na kama kuna yeyote ataonekana  anafanya hujuma atachukuliwa hatua kali," alisema Dkt. Kalemani.

Naibu Waziri pia  alitoa wito kwa wananchi kuvilinda vyanzo vya maji nchini kwa kushirikiana na serikali katika ngazi za vijiji, wilaya na mikoa ili  kuhakikisha kuwa uharibifu wa vyanzo vya maji nchini unafikia tamati.

MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI KWA MWAKA 2015

BENDI MPYA
•Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
•Tarehe 21-Feb-2015,  JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
 •Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
•Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho. Bendi hii inaundwa pia na mpiga solo Alain Kisomundele na Mao Santiago aliyekuwa Machozi Band.
•Dec-2015, bendi mpya itakayojumuisha Mule Mule FBI, Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende” ipo katika maandalizi ya kuundwa na kuzinduliwa huku Mule Mule FBI akiwa rais (prezidaa) wa bendi hiyo huku Losso Mukenga, mpiga solo wa Ally Kiba, akiipigia pia bendi hiyo.

UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Tarehe 27-Dec-2015, Milimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae”, ndani ya TCC Chang’ombe, yazindua album ya “Jinamizi la Talaka” sambamba na kufanya sherehe za miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978

KILI MUSIC AWARD
•Tarehe 23-Mar-2015, Kililimanjaro Music Award 2015 yazinduliwa rasmi
•Tarehe 25-Apr-2015, Academy ya Kili Music Award yakutana kuchagua majina ya washiriki wa kila kipengele.
•Tarehe 29-Apr-2015, majina ya washiriki wa kila kipengele yatangazwa rasmi
•Tarehe 13-Jun-2015 (Jumamosi), sherehe za washindi wa Kili Music Award 2015 zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 6  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Bendi Bora ya Mwaka- FM Academia
2. Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi-Jose Mara (Mapacha Watatu)
3. Rapa Bora wa Mwaka Bendi- Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo wa Kiswahili Bendi- ”Wale Wale” (Vijana Ngwasuma)
5. Mwimbaji Bora wa Kiume Bendi- Jose Mara (Mapacha Watatu)
6. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo Bendi-Amoroso Sound

NB: Mwaka huu hakukuwa na Mwimbaji Bora wa Kike Bendi

WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Tarehe 04-Jan-2015 (Jumapili), mwanamuziki  Flowin aka “Kachumbari” aliyekuwa mpiga drums na tumba wa Chuchu Sound afariki dunia.
•Tarehe 30-Jan-2015, mwanamuziki Peter Kanuti afariki dunia kwa ajali ya gari akiwa Zanzibar. Huyu anatokea familia ya wanamuziki Gaspar Kanuti, Fred Kanuti na Joseph Kanuti.
•Tarehe 28-Feb-2015, mwanamuziki, mwanasiasa, mwanajeshi mstaafu, mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, Mkurugenzi wa kundi la sanaa za maonesho la Tanzania One Theatre (TOT Plus) Captain John Damian Komba afariki dunia.
•Tarehe 16-Apr-2015, mwanamuziki Joseph Chigwele “Che” Mundugwao afarikia dunia.
•Mwanamuziki Mutombo Lufungula “Audax”, mmoja ya waanzilishi na wamiliki wa bendi ya Maquis du Zaire (ambayo baadaye ikaitwa Maquis Original) afariki dunia alfajiri ya Alhamis tarehe 23-Apr-2015 na kuzikwa Jumapili ya tarehe 26-Apr-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 17-Jul-2015 (Ijumaa), mwanamuziki Ramadhan Ally Masanja aka “Banza Stone” afariki dunia siku ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Azikwa Jumamosi tarehe 18-Jul-2015 sikukuu ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika makaburi ya Sinza.
•Tarehe 01-Nov-2015, Mkurugenzi wa bendi ya FM Academia, Martin Jotham Kasyanju, afariki dunia akiwa hospitali ya Aga Khan. Alizikwa Ijumaa ya tarehe 06-Nov-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 09-Nov-2015, mwanamuziki mkongwe Captain  John Simon afariki dunia katika hospitali ya Muhimbili. Alizikwa tarehe 11-Oct-2015 katika makaburi ya Tabata Kimanga.
•Tarehe 19-Nov-2015, aliyepata kuwa mtangazaji maarufu wa radio na TV Prince Baina Kamukulu hususan wa vipindi vya muziki wa dansi (kama Radio Free Africa na Star TV) afariki dunia. Aliwahi pia kuwa mtangazaji wa Kipindi cha “Afrika Bambataa” cha Clouds FM.
•Tarehe 20-Nov-2015, aliyepata kuwa rapa wa bendi ya Mashujaa “Kama Simba” afariki dunia.
•Tarehe 28-Nov-2015, muasisi wa Safari Trippers aliyekuwa mtunzi, mwimbaji, mpuliza sax na mpiga solo David Bernard Gordon aka “David Musa” afariki dunia. Azikwa tarehe02-Dec-2015 katika makaburi ya Kinondoni.
•Tarehe 02-Dec-2015, mwanamuziki Kasongo Mpinda “Clayton” afariki dunia. Azikwa tarehe 03-Dec-2015 katika makaburi ya Kisutu.

WANAMUZIKI WAKUBWA WALIOHAMA BENDI
•Feb-2015, mwanamuziki Badi Bakule “Mkandarasi” aondolewa katika bendi ya Twanga Pepeta.
•Tarehe 08-Apr-2015, Ally Choki na Super Nyamwela watangazwa rasmi kujiunga (kurejea) Twanga baada ya kuivunja rasmi bendi ya Extra Bongo. Hii ilitanguliwa na kitendo cha Ally Choki kusalimia kisanii kwenye jukwaa la Twanga Leaders Club 17-Jan-2015, tukio ambalo halijawahi kufanyika kwa miaka 8. Pia tarehe 30-Jan-2015, Ali Choki na Mama Asha Baraka walipatanishwa rasmi chini ya usuluhishi uliofanywa na Global Publisher. Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), ndio ilifanyika show ya kwanza ya Ally Choki na Super Nyamwela baada ya kurejea Twanga Pepeta yafanyika Mango Garden.
•May-2015, Wanamuziki Bob Kissa na Grayson Semsekwa wajiunga na Double M Sound wakitokea Extra Bongo iliyovunjika baada ya kundoka kwa Ally Choki.
•Tarehe 08-May-2015 (Ijumaa), Mashujaa Band imetambulisha wanamuziki wawili wapya Roggart Hegga Katapila na Dady Dipirone “Rais wa Masauti ya Chini”. Hiyo ilifanyika wakati Mashujaa Group wakizindua ukumbi wao wa Mashujaa Lounge ambao zamani ulikuwa unaitwa Business Park uliopo maeneo ya Victoria, Dar-es-Salaam.
•Jul-2015, mwanamuziki Janeth Kushaba aka AK47 ajiengua katika bendi ya Skylight Band na kuanzisha bendi mpya ya Stars Band.
•Tarehe 29-Jul-2015, mwanamuziki Elyston Angai awasili nchini na kujiunga na Mashujaa Band japo baadaye akarudi Afrika Kusini ambako inasemekana amekwenda kujiandaa ili aweze kurudi Tanzania moja kwa moja.
•Jul-2015, Wanamuziki Polepole Bahogwerhe “Papy Catalogue”, Chims Kamanyola na Ben Bievang wahama bendi ya Vijana Ngwasuma. Chims Kamanyola na Ben Bievang warejea FM Academia.
•Aug-2015, mwanamuziki Roggart Hegga Caterpillar ajiunga na Twanga Pepeta akitokea Mashujaa Band.
•Nov-2015, wanamuziki Salehe Kupaza, Dogo Rama na Jojo Jumanne kutoka Twanga Pepeta wahamia bendi ya  Double M Sound iliyo chini ya uongozi wa Prince Mwinjuma Muumin ambayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuitwa Double M Plus.
•Nov-2015, mwanamuziki Jaddo Field Force ahama Mashujaa Band na kuhamia bendi ya Dar Musica.
•Nov-2015, mwanamuziki Eddo Sanga aihama Dar Musica na kurudi bendi ya Msondo Ngoma ambayo alipata kuwepo hapo awali. Kabla ya hapo, mwanzoni mwa mwaka alikuwa Victoria Sound kabla ya kuhamia Mlimani Park Orchestra “Sikinde” ambapo baadaye alielekea Dar Musica.
•Nov-2015, mwanamuziki Karama Regesu ahama bendi ya Dar Musica na kurejea bendi ya Mlimani Park Orchestra. Mwanamuziki mwingine aliyerejea Mlimani Park ni mpiga solo Adolph Mbinga.
•Dec-2015, mwanamuziki Mulemule FBI ahama bendi ya FM Academia. Aenda kuanzisha bendi mpya inayoundwa pia na Totoo Ze Bingwa, Alain Mulumba Kashama, Montana Amarula na Didi “Number” Kayembe (Numero) aka “Dume la Mende”.
•Dec-2015, mwimbaji Dispatch arejea Mashujaa Band.
•Dec-2015, mwimbaji Tarsis Marsela yupo katika sintofahamu ya kuendelea kubaki au kuondoka Akudo Impact baada ya likizo yake ya muda mrefu huku uongozi wake wa bendi akipewa Zagreb Butamu.

MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Tarehe 24-Jan-2015 (Jumamosi), tamasha linaloitwa TIGO KIBOKO YAO Concert lafanyika Leaders Club. Bendi za muziki wa dansi zilizoshiriki ni Msondo Ngoma, Mlimani Park Orchestra, Christian Bella & Malaika Music Band, Yamoto Band. Kila bendi ilipiga kwa dakika 45.
•Tarehe 25-Jan-2015 (Jumapili), tamasha la miaka 10 ya CDS lafanyika TCC Chang’ombe na kushirikisha bendi za muziki wa dansi za Msondo Ngoma, Mapacha Watatu, Malaika Music Band na FM Academia.
•Tarehe 07-Feb-2015 (Jumamosi), tukio la “Miaka 16 ya Luizer Mbutu” ndani ya Twanga Pepeta lafanyika Mango Garden.
•Tarehe 28-Mar-2015 (Jumamosi), wafanyika mpambano kati ya FM Academia na Twanga Pepeta katika ukumbi wa Escape One.
•Tarehe 18-Apr-2015 (Jumamosi), Christian Bella afanya tukio la “Usiku wa Masauti” ndani ya ukumbi wa Escape One. Christian Bella atumia tukio hilo kutambulisha/kuzindua audio na video ya wimbo wake mpya wa “Nashindwa”.
•Tarehe 25-Apr-2015 (Jumamosi), kundi la Les Wanyika kutoka Kenya latumbuiza katika kiwanja cha Escape One.
•Tarehe 26-Apr-2015, Bendi ya Cuban Marimba watunukiwa nishani ya Muungano kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya ikulu. Waliopokea nishani kwa niaba ya bendi ni Waziri Nyange (mpiga solo) na Mzee Juma Sangura (mpiga bass).
•Tarehe 08-May-2015 (Ijumaa), Mashujaa Group wazindua ukumbi wao wa Mashujaa Lounge ambao zamani ulikuwa unaitwa Business Park uliopo maeneo ya Victoria, Dar-es-Salaam. Katika tukio hilo, Mashujaa Band imetumia nafasi hiyo pia kutambulisha wanamuziki wawili wapya Roggart Hegga Katapila na Dady Dipirone “Rais wa Masauti ya Chini”. Pia Mashujaa Band walitambulisha nyimbo 2 mpya. Ikumbukwe pia kuwa Mashujaa Group mwaka huu wamefanikiwa kuanzisha radio ya Mashujaa FM mkoani Lindi.
•Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika siku ya Idd Mosi (Eid al Fitr) katika ukumbi wa TCC Chang’ombe kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment.
•Bendi ya African Stars Band-Twanga Pepeta yafanya tukio lililopewa jina la “Usiku wa Juzi, Jana na Leo” katika siku na sehemu 3 tofauti za Escape One (31-Jul-2015), Dar West Tabata (01-Aug-2015) na TCC Chang’ombe (02-Aug-2015)
•Tarehe 08-Aug-2015, bendi ya African Stars Band-Twanga Pepeta ndani ya ukumbi wa Mango Garden wafanya tukio lililoitwa “Usiku wa Dream Team” ambapo walizindua vyombo vipya, walishiriki wanamuziki kadhaa wa zamani wa bendi hiyo, walifanya show moja na bendi ya Mapacha Watatu na walipiga baadhi ya nyimbo zao bora kabisa tokea bendi kuanzishwa.
•Tarehe 06-Aug-2015, Rais JM Kikwete ahudhuria hafla maalum ya kumuaga iliyoandaliwa na Muungano wa Wasanii Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
•Tarehe 21-Aug-2015, bendi ya FM Academia wafanya sherehe ya birthday ya 18 katika ukumbi wa Arcade, Mikocheni.
•Tarehe 28-Nov-2015, bendi za Twanga Pepeta na Mapacha Watatu zafanya onyesho moja katika ukumbi wa Mango Garden katika tukio la “Usiku wa Kuachwa” ambapo wanamuziki Chaz Baba, Khalid Chokora, Kalala Juniour na Jose Mara walipanda jukwaa moja .
•Tarehe 27-Dec-2015, Mlimani Park Orchestra “Sikinde-Ngoma ya Ukae” wafanya tukio la kuadhimisha miaka 37 tokea bendi ianzishwe mwaka 1978. Siku hiyo pia walizindua album ya “Jinamizi la Talaka”. Siku moja kabla, yaani Boxing Day 26-Dec-2015, walitembelea hospitali ya wagonjwa wa saratani ya Ocean Road kuwajulia hali na kuwapa msaada wagonjwa.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA KUWAIT NCHINI


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Dkt. Kolimba kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait. 
Mhe. Balozi Al Najib akimkabidhi Mhe. Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.
Mhe. Dkt. Kolimba nae akimshukuru Balozi Al Najib kwa kuwasilisha salamu hizo za pongezi na kwamba amezipokea na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kuwait katika masuala mbalimbali ya maendeleo. 
Sehemu ya ujumbe kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Kolimba na Balozi wa Kuwait hapa nchini (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Batholomeo Jungu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw. Tahir Bakari, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri. 
Picha ya pamoja.

WAZIRI PROF. MBARAWA AWATAKA TAA NA TCAA KUBORESHA HUDUMA NA KUONGEZA MAPATO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo ya uboreshaji unaoendelea kufanyika wa kiwanja cha Ndege Terminal Two kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Eng. Suleiman Suleiman jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Waziri Prof. Mbarawa ujenzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three), ambapo jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka.
Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Prof. Makame Mbarawa eneo ambalo limefanyiwa ukarabati kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), wakati alipotembelea eneo hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), na kuagiza Mamlaka hiyo kuongeza mapato ili kuweza kupanua fursa za uwekezaji na kuendeleza uchumi wa nchi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametembelea Mamlaka ya Viwanja  vya ndege (TAA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) jijini Dar es salaam na kuagiza Mamlaka hizo kuboresha huduma na kuongeza mapato ili kupanua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi.

Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa mapato yatakayokusanywa yawe yanatoka kwa makampuni ambayo yapo chini ya mamlaka hizo na si kwa kuwabana wananchi.

‘Nataka msiongeze mapato kwa kuwaathiri wananchi na badala yake  mtafute vyanzo vingine vya mapato ambavyo vitasaidia katika kuchochea fursa za uwekezaji’, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ametaka huduma zote katika viwanja vya ndege kama zima moto,uhamiaji,polisi na huduma za afya, ziwe chini ya mamlaka ya viwanja vya ndege  ili kurahisisha uharaka na ukaribu wa huduma kumfikia mteja kwa urahisi.

‘Ninyi ndio kioo cha jamii, hivyo basi haipaswi kuchukua zaidi ya dakika kumi kumhudumia mteja mmoja au kuwa na tabia ya kumsumbua mteja pindi anapohitaji huduma’, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Ameitaka TAA kufanya utaratibu wa kujenga jengo kubwa la ofisi kwa ajili yao na kukodisha kwani kufanya hivyo kutaongeza mapato katika Mamlaka hiyo.

Awali wakati akitoa taarifa kwa Waziri Mbarawa Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman Suleiman amesema kuwa Mamlaka hiyo imeweza kuhakikisha kuwa huduma za usafirishaji  kama za ufundi na zimamoto na uokoaji zinaridhisha.

Katika hatua nyingine wakati akiwa katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa uharaka katika uendaji kazi wao ili kuendana na kasi ya mabadiliko anayoitaka Rais John Pombe Magufuli

“Najua ni waadilifu katika kazi zenu ila nawaomba muongeze, pasiwe na usumbufu kila mtu ana haki ya kupata huduma stahiki anayohitaji na kwa wakati unaotakiwa” amesisitiza Waziri Mbarawa.

Ameitaka TCAA kujitathmini wao binafsi, wateja na huduma wanazozitoa kwa wateja wao ili kuhakikisha sekta yao inakuwa. 

Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Chacha ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo kuwa ni uwekaji wa mitambo ya kisasa ya kuongoezea ndege na kufuatilia safari za ndege nchini iitwayo ‘Automatic Dependent Surveillance’. 

Ameainisha kuwa mradi mwingine ni ununuzi wa rada mbili za kuongozea ndege za kiraia ambazo zitafungwa katika viwanja vya Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam na KIA mkoani Kilimanjaro.

IMETOLEWA NA 
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO 
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

KAMATI ZA MAAFA NGAZI ZA MIKOA, WILAYA NA VIJIJI ZASHAURIWA KUOMBA MBEGU BADALA YA CHAKULA CHA MSAADA

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly akimkabidhi mkazi wa kijiji cha Kiegea, Bibi Sarah Matereka mbegu za mtama kwa ajili ya shamba lake kama mpango wa wilaya hiyo kuhamasisha wananchi wilayani humo kulima mazao yanayohimili ukame ili kukabili maafa ya njaa , wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Idara ya uratibu maafa Ofsi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya na katikati ni mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mhe. George Lubeleje tarehe 31 Desemba, 2015.
Mmiliki wa shamba la Uzalishaji Mbegu bora za Muhogo aina ya Mumba katika Kijiji cha Choka wilayani Mpwapwa, Edward Kusenha akieleza ubora wa mbegu ya muhogo huo kuwa tangu apande mbegu hiyo mwaka 2014 anaouhakika wa chakula kwa kipindi chote cha hali ya ukame kijijin hapo anayemsikiliza ni Dereva Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu maafa, Nuru Gagu wakati ofisi hiyo ilipokuwa ikifuatilia hali ya upungufu wa chakula kijijini hapo tarehe 31 Desemba, 2015.
Kufuatia ziara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa katika Wilaya za Mpwapwa na Kondoa mkoani Dodoma tarehe 30 Desemba, 2015, iliyolenga kufuatilia hali ya upungufu wa chakula katika wilaya hizo hususan katika maeneo yote yaliyoathirika na ukame. Ofisi ya waziri mkuu, Idara ya Uratibu wa maafa imetembelea wananchi wa Wilaya hizo na kufanikiwa kuona baadhi yao wanayo mashamba ya mbegu na mazao yanayohimili ukame suala linalowezesha familia zao kuwa na uhakika wa chakula kwa  kutohitaji chakula cha msaada kutoka Ofisi ya waziri mkuu. 

Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa inazishauri Kamati za Maafa za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji ambazo ndizo zenye jukumu kubwa la kusimamia masuala ya maafa katika ngazi hizo ziombe mbegu za mazao yenye kuhimili ukame katika Halmashauri zao na kuzigawa bure kwa wananchi badala ya kuwa wanawaombea chakula cha msaada kila mwaka. 

Hivyo;“Nashauri watendaji wakuu wa Halmashauri na  mikoa  kupitia kamati za maafa  maombi yanayokuja ofisini kwangu kuanzia sasa wasiombe chakula cha msaada tu bali waombe na mbegu zinazo himili ukame kwa kuwaorodhesha wananchi wote wanaohitaji mbegu hizo na kuwasilisha katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa  na Ofisi yangu itatuma fedha za kununua mbegu kutoka kwa wananchi  wenye mashamba ya  mbegu hizo ili zigawiwe bure kwa wananchi  wengine wenye upungufu  wa chakula. tunahitaji wananchi wote wawe na uhakika wa chakula .” amesema Brig. Jen. Msuya 

Katika kuhakikisha ushauri huo unatekelezwa Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa, ili wananchi walime wanahitaji chakula hivyo tayari ofisi yake imeshapeleka tani, 1,396 za mahindi ya chakula cha msaada mkoani Dodoma kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba 2015, ikiwa tani 200 za mahindi zimepelekwa wilayani Mpwapwa na tani 150 za mahindi wilayani Kondoa. 

Awali akiongea katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu Maafa kwa kufuatilia hali ya upungufu wa chakula wilayani humo pamoja na kuahidi kutoa mbegu pamoja na chakula cha msaada kingine wilayani humo kwa kuwa wilaya hiyo imeshaanza mipango endelevu wa kukabili njaa wilayani humo na kuvitaka vyombo vya habari kuripoti taarifa sahihi za hali ya chakula wilayani humo.

“Napenda kwanza kukanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa wananchi wa wilaya yangu wanapika mawe hilo sio kweli bali sisi chakula tumeshaletewa na Ofisi ya waziri Mkuu lakini tatizo la wananchi wetu ni uwezo wa kununua mahindi hayo yanayouzwa kwa bei nafuu hivyo kimsingi tunaendelea kuwashauri wananchi walime zao la muhogo kwani linahimili ukame katika wilaya hili kwa ajili ya chakula na biashara lakini pia na ufugaji wa kuku na mbuzi utawawezesha wananchi wangu kukabili athari za ukame kama njaa” amesisitiza Utaly.

Mbunge wa jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje alifafanua kuwa, kama kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ataendelea kuwahamasisha wananchi kulima mazao yanayohimili ukame ambayo yatawawezesha kuwa na uhakika wa chakula na uchumi.

 “Kimsingi Ofisi ya Waziri Mkuu kuamua kutoa mbegu bure zinazohimili ukame litakuwa jambo jema kwa kuwa wananchi kipindi cha upungufu wa chakula huacha shughuli zao na badala yake kutafuta vibarua ili waweze kupata pesa na kununua chakula lakini kwa mpango huu watakuwa wanalima mashamba yao” amesema Lubeleje.
Aidha; Sheria Na. 7 ya Mwaka 2015 ya Menejimenti ya Maafa inamtaka kila mdau kutekeleza wajibu wake katika suala zima la menejimenti ya maafa ikiwa pamoja na Kuzuia, Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali baada ya maafa kutokea. 

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
OFISI YA WAZIRI MKUU
31 DESEMBA 2015