Wednesday, November 4, 2015

VYUMBA VYA KUPIMIA NGUO KABLA YA KUNUNULIWA KATIKA SOKO LA MCHIKICHINI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM VILITUMIKA KUDHALILISHA WANAWAKE

Wawezeshaji wa Sheria katika soko la Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa na mabango ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na waaandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo kuona maendeleo ya vita ya  kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika masoko hayo baada ya Shirika la Equality for Growth linaloendesha mradi huo kutoa mafunzo kwa Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na wafanyabiashara katika vita hivyo.
Mwezeshaji wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Charles Beatus akichangia kuhusu mwongozo wa kutoa adhabu kwa wanaobainikwa na makosa ya udhalilishaji. Kushoto ni Mtaalamu wa kujitolea wa  masuala ya kijinsia kutoka nchini Canada, Ashley Ekelund.
Mwezeshaji wa kisheria katika soko hilo, Domitila Ngwada akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala, Zainabu Namijojo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao wapo katika ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshai wa Sheria katika soko hilo, Nechi Omar.
Mfanyabiashara wa vitenge na magauni, Sophia Kizinga akichangia jambo kuhusu kupungua kwa ukatili wa jinsia katika soko hilo.
Mfanyabiashara, Ikram Zubery (katikati), akizungumza na waandishi wa habri kuhusu ukatili wa kijinsia katika soko hilo.
Mama Lishe katika soko hilo, Edwiga Assenga (wa pili kulia), akizungumza na wanahabari waliotembelea soko hilo.

Na Dotto Mwaibale

VYUMBA vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha wateja hasa wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko hilo Zainabu Namijojo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).

"Katika soko letu tulikuwa na changamoto kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya wauza nguo kuu kuu (Mitumba), kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya kujaribishia nguo kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na kuwawekea kioo chini ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.

Alisema hivi sasa vitendo hivyo vimekoma baada ya shirika hilo kufanya matamasha na semina mbalimbali na kutoa mafunzo kwa baadhi yao ambao sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko hilo ambao wamekuwa karibu na wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya udhalilishaji.

Mwezeshaji wa Sheria Domitila Ngwada alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya nguono yalishamiri sana lakini hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo hivyo vimepungua kwa asilimia 70 ukilisha na hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG.

"Tangu kuwepo na wawezeshaji wa Sheria katika soko letu vijana wengi waliokuwa na vitendo vya kudhalilisha wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa kupigwa faini zilizowekwa kuanzia kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.

Mfanyabiashara katika soko hilo, Ikram Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo hilo ingawa kwa kiasi kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.

Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika na makosa ya udhalilishaji wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo uliopo na kesi zote zinaanza kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana upelekwa ngazi nyingine ikiwemo polisi.

Tuesday, November 3, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI


Mfuko wa taifa wa bima ya afya waelezwa kujenga vituo mbalimbali vya afya katika mikoa mbalimbali nchini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya nchini.https://youtu.be/ZIJyCjDDuCU

Jeshi la polisi nchini lawataka wananchi kuendelea kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya aina yeyote ile vyenye lengo la kuvuruga amani.https://youtu.be/xwt9tkZRMck
Muungano wa taasisi 172 za uangalizi wa uchaguzi kutoka ndani watoa taarifa yake ya awali kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika nchini. https://youtu.be/DWR6PgSNn6E
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam awataka viongozi wa dini kendelea kuwaasa waumini wao kuendelea kutunza na kuenzi amani katika kipindi hiki baada ya uchaguzi mkuu. https://youtu.be/AHo89d2KZlQ
Wahamiaji haramu 60 kutoka nchini Ethiopia waliongia nchini kinyume cha sheria wahukumiwa kwenda jela huku gari lililotumika kuwaingiza nchini limetaifishwa.https://youtu.be/jb7HAvPhJkg
Wakazi wa Tabora mjini wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kukithiri kwa uchafu mjini hapo. https://youtu.be/Q9tGozvliFQ
Hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar imeathiri sana sekta ya utalii kuvuatia mvutano wa kisiasa unaoendelea hivi sasa. https://youtu.be/YxPQ6t6MnIY

Kiongozi wa kanisa la Church of All Nations TB Joshua amewasili nchini kushuhudia kuapishwa kwa Dr.Magufuli huku akimtembelea pia Edward Lowassa.https://youtu.be/LjTpCIxU_hI

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu waendelea kuutesa mji wa Arusha huku ikibainika licha ya uwepo taarifa za ugonjwa huo bado juhudi za makusudi hazijachukuliwa kujikinga. https://youtu.be/65U10Mhax_I

Jeshi la polisi nchini limeawataka wananchi kupuuza habari zinazosambaa katika mitandao ya kijamii huku likiwataka kuviamini vyombo vya habari.https://youtu.be/GXPKwUxjduo

Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali mkoani Rukwa yaelezwa kusababisha maafa makubwa katika maeneo mabalimbali ya mkoa huo.https://youtu.be/iRS5dTkbZ7U

Watu wawili wauawa kikatili mkoani Tabora katika matukio mawili tofauti ikiwa ni muendelezo wa mauaji yanayojitokeza mara kwa mara mkoani humo.https://youtu.be/8dXlQjcmDNw
TEMCO yatoa taarifa yake ya awali kuhusu Uchaguzi na kubainisha kwamba kabla ya uchaguzi hakukuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani.https://youtu.be/9VC6XWVNOhI

CCM Zanzibar kimetoa rai kwa wananchi wa kisiwani Zanzibar kuwa watulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi; https://youtu.be/M4xIihvwzA4

Idara ya afya ya wilayani kahama, Shinyanga imefikia hatua ya kuifunga zahanati ya NK kwa kukiuka kanuni za tiba; https://youtu.be/XOf3acpw16I

Serikali imeunda kamati ya mahakama wilayani kinondoni ili kusaidia wananchi kupata haki zao kwa haraka; https://youtu.be/hhnu2uAJ0bw

Teknolojia  ya matofali maalumu iliyotumika katika ujenzi wa kipande cha barabara katika mamlaka Ngorongoro yaleta tija; https://youtu.be/KC_qzKSVrqE

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI NOVEMBA 3, 2015.

Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu November 3, 2015.

Watu 6 wamefariki dunia na 1 kujeruhiwa katika matukio 4 tofauti yaliyotokea mkoani Singida toka oktoba 31 na November 1.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa nchini Peter Mziray avishauri vyama vya siasa kutumia baraza hilo kutatua Migogoro kwa Njia ya Mazungumzo. https://youtu.be/Z90lI_ga7Mg

Wahamiaji Haramu raia Wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa ndani ya lori wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 6 jela au faini ya laki 5  https://youtu.be/xc637Ykh6Mw

Halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imefanikiwa kutatua baadhi Ya changamoto zinazoikabili sekta ya Kilimo kwa kuongeza idadi ya Afisa Ughani. https://youtu.be/nqk4rGU6hvE

Kamati kuu Ya Chama Cha Mapinduzi CCM imetangaza kurudiwa kwa zoezi la kura za maoni katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Handeni. https://youtu.be/RVTSjWOxPGc

Aliyekuwa mgombea Uraisi CCK aliyeenguliwa na NEC Dkt. Godfrey Malisa akusudia kuwania nafasi ya Spika wa Bunge. https://youtu.be/m4gnvAcUJn4

Kukusekana kwa Umeme na Huduma za Maji kumetajwa kukwamisha maendeleo ya wanafunzi wa mchepuo wa sayanzi katika Shule Ya Wel Wel. https://youtu.be/PcmWUOA-v-o
Raisi Jakaya Kikwete azungumzia ushindi wa ccm kuwa umetokana na kazi kubwa iliofanywa na vijana katika kuhakikisha ushindi wa Kishindo kwa Dkt. Magufuli huku akiviponda baadhi ya Vyombo vya Habari kuegemea Upande wa wapinzani na kunyima Fursa ya wananchi kusikia Sera za Chama Cha Mapinduzi. https://youtu.be/OoQicJcNJAI

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WILLIAM LUKUVI AAGA RASMI SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea kadi ya pongezi ya Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Baadhi ya mameneja wa Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia mazungumzo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Fatma Chillo akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo kumshukuru Waziri huyo wakati Waziri alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.

Waziri wa ArdhiNyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ameiagiza Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaendeleza kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara bila kusahau misingi iliyoliunda shirika hilo.

Akizungumza leo wakati akiaga rasmi Shirika hilo alisema amejifunza mengi katika uwepo wake ndani ya Wizara na hasa dhamira na utendaji wa kasi wa Shirika hilo na akaiagiza menejimenti ya Shirika hilo kufanya kazi bila kuchoka likihakikisha linapigania makazi bora kwa kila mtanzania.

"Kabla ya kuingia katika Wizara , na hata nilipoingia sikuwa nafahamu kwa kina kwamba Shirika la Nyumba limebadilika kutoka lile la kuangalia nyumba za msajili wa majumba na kuwa sasa limejenga nyumba nyingi na kuziuza kwa Watanzania, sasa nimefahamu kwa kujifunza kwamba Shirika letu hili limebuni utaratibu unaolifanya lifanye kazi kwa kasi kubwa kibiashara lakini pia likibakia na 'human face', "alisema Lukuvi.

Alisema Serikali inafahamu changamoto linazokabiliana nazo Shirika hilo za ulipaji wa VAT mara mbili na gharama za miundombinu kama maji, umeme na barabara ambazo mara kadhaa zimekuwa zikirudi kwa mnunuzi wa mwisho na kwamba zinafanyiwa kazi pia akaliagiza Shirika na mamlaka hizo kukaa pamoja na kuweka mipango yao pamoja ili angalau kuliwezesha Shirika kuwafikia Watanzania wengi.

Waziri Lukuvi alisema kuwa Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, alilihimiza Shirika hilo liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba.

Alisema wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Akiungumzia Serikali ya awamu ya Tano ijayo alisema kama kuna watumishi wa umma ambao walikuwa wakifanya mambo kwa mazoea katika awamu zilizopita basi awamu hii wahakikishe wanakuwa mguu sawa kwani Serikali ya Magufuli ambayo inaingia madarakani ni serikali isiyotaka mchezo wala lele mama na kwamba wala rushwa, na wazembe watatafuta mlango wa kutokea.

Akimkaribisha Waziri Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu alisema Shirika hilo linatekeleza miradi yake ili kuhakikisha linaweka makazi bora kwa Watanzania
Alisema kwa shirika hilo lonafanya hivyo kwa kuwa sekta ya nyumba ni sekta mtambuka katika maendeleo ya uchumi.

 Sekta ya nyumba husaidia kuleta maendeleo ya haraka ya sekta zinginena kutoa ajira. Taifa linalozingatia sekta ya nyumba huwezesha nchi yao kuwa na amani, kwani mtu mwenye makazi bora, huthamini uwepo wa amani.

FAINI ZILIVYOSAIDIA KUPUNGUZA MAKOSA YA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI

 Katibu wa Soko la Gezaulole lililopo Kiwalani Bomubomu Manispaa ya Ilala, Salum Yusuf (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo za kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia sokoni hapo baada ya kuwezeshwa mafunzo ya kupinga ukatili huo na Shirika la Equality for Growth. Kushoto Mwenyekiti wa Soko hilo, Muhidin Waziri.
 Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika hilo, Samora Julius akitoa ushauri kwa Serikali hasa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika masuala mbalimbali yakiwemo ya ukatili wa jinsia. Kushoto ni mtaalamu wa kujitolea wa masuala ya kijinsia kutoka nje ya nchi, Ashley.
 Mwezeshaji wa Sheria, Khadija Mohamed (kulia), akielezea mafanikio waliyoyafikia ya kukabiliana na vitendo hivyo katika soko hilo baada ya kuwezeshwa na EfG.
 Mwezeshaji Asha Abbas akichangia katika mkutano huo.
 Mfanyabiashara wa samaki katika soko hilo, Asha Mohamed akihojiwa na wanahabari kuhusu namna wanavyo pambana na ukatili katika soko lao hilo la Gezaulole.
Mfanyabiashara Amina Mussa akilishukuru Shirika la EfG kwa kusaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia katika soko hilo.

Na Dotto Mwaibale

FAINI zinazotolewa kwa watu wanaobainika na makosa ya unyanyasaji wa kijinsia katika soko la Gezaulole lililopo Kiwalani Bomubomu Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam zimesaidia kupunguza vitendo hivyo kwenye soko hilo.

Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo asubuhi na Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Khadija Mohamed wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari waliotembea soko hilo kujua ni kwa kiwango gani vitendo hivyo vimepungua katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa elimu ya kupinga unyanyasaji katika masoko ya Manispaa ya Ilala.

"Faini tunazo watoza wafanyabiashara wanaobainika na makosa ya kutumia lugha chafu, kupigana na kuwadhalilisha wenzao kwa kuwakamata  maunguni na unyanyasaji mwingine zimesaidia kupunguza makosa hayo katika soko letu" alisema Mohamed.

Alisema mara zote matusi katika masoko yamekuwa yakichangia kuwakimbiza wateja na ndio maana wana lishukuru shirika la EfG kwa kuwapa elimu iliyowasaidia na kuwafanya waendelee na biashara zao kama kawaida.

Mwezeshaji wa Sheria Amina Mussa alisema hapo awali wanaume walikuwa wamekubuhu kwa kutukana tusi la mama jambo ambalo lilikuwa linawakera lakini hivi sasa wanashukuru mungu baada ya wanaume hao kujitambua na kuacha matusi hayo.

Mwenyekiti wa soko hilo, Muhidin Waziri alilipongeza shirika hilo kwa kuwasaidia wafanyabiashara katika masoko mbalimbali ya Manispaa ya Ilala na kujitambua hivyo kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia masokoni.

Katibu wa soko hilo, Salum Yusuf alisema changamoto kubwa waliyokuwa nayo hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG ilikuwa ni kutojua maana ya unyanyasaji ambapo mtu aliyekuwa akishikwa mwilini au kutukanwa alikuwa hachukui hatua yoyote.

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika hilo, Samora Julius alitoa ushauri kwa Serikali hasa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika masuala mbalimbali yakiwemo ya ukatili wa jinsia.

Julius aliomba serikali kuyaunga mkono mashirika yanayofanya vizuri kwa kuyapa ruzuku itakayosaidia kuwafikia wananchi kwa wingi na jamii kwa ujumla.

\(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

Monday, November 2, 2015

Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC

Jumamosi,Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.
Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios
Ratiba kamili ya vipindi kutoka Swahili Media Network, 
itawajia hivi karibuni
Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza
Steven Mghaza akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi, na mwakilishi wa balozi kwenye hafla hiyo, Swahiba Mndeme
Kushoto ni Meneja mauzo wa CBC Radio R.J Trzaska, mratibu wa Mis Congo na msanii toka congo
Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni
Wasanii Adele na Frank wakiimba nyimbo za taifa za Marekani na Tanzania, wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo
Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho
Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska
Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali
Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake

MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC

Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC
Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi
 Wanafamilia

WATAALAM WA TAKWIMU KUTOKA OFISI ZA TAKWIMU BARANI AFRIKA

Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga Maluleke akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
 (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

VIONGOZI wa Ofisi za Takwimu barani Afrika leo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.

Wakizungumza katika mkutano wa wataalam wa takwimu ulioanza leo Jijini Dar es Salaam, viongozi hao wamesema ili takwimu bora zipatikane kwa wakati, ni lazima kuwepo na mfumo bora wa uongozi pamoja na wataalamu waliobobea katika fani ya takwimu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la mkutano huo ni kujadili mfumo wa uongozi bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na namna ya kuboresha mitaala ya ufundishaji wa masomo ya takwimu barani Afrika.

“Leo tupo hapa wataalamu wa takwimu kutoka zaidi ya mataifa 25 barani Afrika ili kujadili namna ya kuboresha mifumo yetu ya uongozi katika Ofisi za Takwimu pamoja na kujadili mbinu bora za kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa watakwimu vijana hasa kupitia upya mitaala ya ufundishaji,” amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema kuimarishwa kwa mfumo wa uongozi pamoja na kuboresha mafunzo kwa wakwimu kutasaidia katika ukusanyaji wa takwimu bora zitakazotumika katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wa Afrika ya Kusini, Risega Maluleke amesema mataifa mengi ya Afrika yanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uwezo wa kujitegemea kifedha kitu ambacho hukwamisha upatikanaji wa takwimu kwa wakati.

Amesema licha ya changamoto hiyo, kwa kiasi kikubwa kazi ya ukusanyaji wa takwimu imekuwa ikifanyika kwa ufanisi mkubwa kutoka kwa watalaam hao wa takwimu na hivyo kupitia mkutano huu, wataweza kujadili namna ya kuboresha uimarishaji wa Ofisi za Takwimu.

Maluleke amesema ni vyema Serikali zikaziwezesha ofisi za ukusanyaji wa takwimu ili ziweze kujitegemea kibajeti na kuboresha utendaji kazi wake katika kuhakikisha takwimu bora zinapatikana kwa wakati muafaka.

Mkutano huo wa siku tano unatarajia kumalizika tarehe 06 Novemba, 2015 ambapo wataalam takribani 30 wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKUTANA

Msajili wa vyama vya siasa nchini,Jaji Mstaafu ,Francis Mtungi akiarisha mkutano wa vyama vya siasa ulioandaliwa kwa ajili ya kumuaga Rais Dk.Jakaya Kikkwete leo jijini Dar es Salaam.

.Mchambuzi wa wa Masuala ya Siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.Benson Bana akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya siasa nchini leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP,Maxmillian Lymo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula( Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Labour Patry (TLP), Agustino Lyatonga Mrema  (kulia ) na katikati Mgombea Urais, Maxmillian Lymo  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  Taifa  wa chama cha  (AFD)  Said Soud Said akifafanua jambo kwa wandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya Jamii

WAKAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy. Kushoto ni Bw. Slyvester Kibona, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Morogoro. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa umakini mafunzo  ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akizungumza na wanahabari kuhusu mafunzo hayo.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaohudhuria mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na wanahabari kuhusu mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuhakikisha uhuru wa CAG unapatikana.


Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi wa umma nchini wenye fani ya ukaguzi, wametakiwa kutumia weledi katika utendaji kazi zao hali itakayoongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.

Bibi Massoy amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri ili kuwezesha mkaguzi mwengine kuweza kufikia hitimisho moja kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi mwengine.

“Programu ya TEAMMATE hutoa fursa kwa wakaguzi kwa kuwawezesha  kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi Kimataifa vya ukaguzi,” alisema Bibi Massoy.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi yao ya ukaguzi.

“Nawasihi muweze kutumia fursa hii kujiendeleza na kutekeleza utaratibu wa kaguzi wa mwongozo kwa vile wengi wa hatua na taratibu wamekuwa umeboreshwa katika Teammate Programu.

Akizungumzia mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuiboresha Ofisi ya CAG, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na uamuzi wa dhati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha taasisi za utawala bora, maadili na udhibiti, ikiwemo NAOT.

Bw. Mwanilwa aliongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria, kuongeza uhuru wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa za Ofisi hiyo kwa kupeleka Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.

“Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliitisha vikao mbalimbali, kwa nyakati tofauti na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa kusisitiza umuhimu wa kuzipitia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hii imeleta mwamko mpya katika kuona umuhimu wa ripoti hizi na kutumika katika kufanya maamuzi mbalimbali serikalini,” alisema.

Bw. Mwanilwa aliongeza Katika Uongozi wa Awamu ya Nne NAOT ilishuhudia uanzishwaji wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali ilitunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009. Sheria hii iliongeza wigo na uhuru wa Ofisi hii katika kutekeleza majukumu yake Kikatiba.

Kuhusu Bajeti ya uendeshaji wa NAOT, Bw. Mwanilwa aliongeza: “Rais Kikwete aliongeza Bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi ambapo Serikali iliboresha utaratibu na mchakato mzima wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliowezesha bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuongezeka kwa asilimia 306% katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/9 hadi 2013/14.”

Jumla ya wakaguzi 65 kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kutoka 25 Wizara ya Fedha wanahudhuria mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro.