Monday, November 2, 2015

WAKAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy. Kushoto ni Bw. Slyvester Kibona, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Morogoro. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa umakini mafunzo  ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akizungumza na wanahabari kuhusu mafunzo hayo.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaohudhuria mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na wanahabari kuhusu mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuhakikisha uhuru wa CAG unapatikana.


Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi wa umma nchini wenye fani ya ukaguzi, wametakiwa kutumia weledi katika utendaji kazi zao hali itakayoongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.

Bibi Massoy amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri ili kuwezesha mkaguzi mwengine kuweza kufikia hitimisho moja kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi mwengine.

“Programu ya TEAMMATE hutoa fursa kwa wakaguzi kwa kuwawezesha  kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi Kimataifa vya ukaguzi,” alisema Bibi Massoy.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi yao ya ukaguzi.

“Nawasihi muweze kutumia fursa hii kujiendeleza na kutekeleza utaratibu wa kaguzi wa mwongozo kwa vile wengi wa hatua na taratibu wamekuwa umeboreshwa katika Teammate Programu.

Akizungumzia mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuiboresha Ofisi ya CAG, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na uamuzi wa dhati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha taasisi za utawala bora, maadili na udhibiti, ikiwemo NAOT.

Bw. Mwanilwa aliongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria, kuongeza uhuru wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa za Ofisi hiyo kwa kupeleka Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.

“Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliitisha vikao mbalimbali, kwa nyakati tofauti na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa kusisitiza umuhimu wa kuzipitia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hii imeleta mwamko mpya katika kuona umuhimu wa ripoti hizi na kutumika katika kufanya maamuzi mbalimbali serikalini,” alisema.

Bw. Mwanilwa aliongeza Katika Uongozi wa Awamu ya Nne NAOT ilishuhudia uanzishwaji wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali ilitunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009. Sheria hii iliongeza wigo na uhuru wa Ofisi hii katika kutekeleza majukumu yake Kikatiba.

Kuhusu Bajeti ya uendeshaji wa NAOT, Bw. Mwanilwa aliongeza: “Rais Kikwete aliongeza Bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi ambapo Serikali iliboresha utaratibu na mchakato mzima wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliowezesha bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuongezeka kwa asilimia 306% katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/9 hadi 2013/14.”

Jumla ya wakaguzi 65 kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kutoka 25 Wizara ya Fedha wanahudhuria mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro.

UWANJA WA KAITABA BUKOBA WAANZA KUWEKWA NYASI RASMI LEO.

Na Faustine Ruta, Bukoba.

Uwanja wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu. 

Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. Uwanja huu umejengwa kwa 
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.

Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.
Taswira ya Nyasi zenyewe za Bandia zikiwa zimetandazwa katika Uwanja huo wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini ambao hutumiwa na Timu ya Hapa Bukoba Kagera Sugar ambayo kwa sasa inaendelea kutumia Viwanja vya Ugenini.
Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi Nchini akizungumzia swala zima la Uwanja huo wa Kaitaba na Waandishi wa habari leo jumatatu 02 Novemba, 2015. Chama ameeleza kutokana na kasi iliyopo na kama Mafundi hawatakwama Uwanja huo utamalizika ndani ya Wiki mbili tuu.
Taswira kamili
Uwanja huo umeanza kuwekwa nysi rasmi leo na ndani ya siku 14 utamalizika na taratibu nyingine zitafuata na Timu ya Kagera itaanza kuutumia Uwanja huo. Uwanja huu sasa utakuwa umeongezeka katika Viwanja vilivyowekwa nyasi hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

Vijana moro wachangamkia mradi wa Airtel Fursa wiki hii

Afisa Masoko wa kampuni ya simu mkoa wa Morogoro, Aminata Keita akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Mkufunzi kutoka Veta kanda ya mashariki na kati, Marthin Mollel akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo ya ujasiliamali wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.

vijana zaidi ya 200 mjini Morogoro wamehudhuria warsha ya siku nzima  ya 'Airtel FURSA Tunakuwezesha. Airtel Fursa ni mpango unaowalenga vijana wemye umri kati ya miaka 18 -24 na wanamiliki biashara ndogo ndogo  kwa kuwapatia ujuzi na nyenzo muhimu kwa mafanikio ya biashara zao na kuweza kujenga fursa kwa wengine.

Akizungumza katika warsha hiyo, mmoja wa washiriki bw. Musa Ndauka alisema;"napenda kuwashukuru Airtel kwa kutambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na kutusaidia sisi vijana wa Morogoro"

"Leo hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja zaidi. Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha yangu. "aliongeza Ndauka

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha hiyo afisa masoko wa  Airtel Tanzania, Aminata Keita, alisema "tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira. Nchini Tanzania, vijana wapatao milioni moja kila mwaka huwa wanapata matatizo ya ajira. 

Tunahitaji kuwawezesha na kubadili  mawazo ya kutaka kuajiriwa kwa kuwasaidia kuwa wabunifu na kuweza kujiajiri. Mpaka sasa Airtel FURSA Tunakuwezesha imewawezesha vijana zaidi ya 1200 kupitia warsha hii na tuna mpango wa kufikia  vijana wapato 2000 mwaka huu peke yake. 

Tunatambua na kuwapongeza hawa vijana ambao ni wafanyabiashara wadogo wadogo  kwa juhudi walizofanya na kuweza kufikia hapa walipo licha ya changamoto hizi zote. Nami  nawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi na kuomba kuwezeshwa kupitia mradi wa  “Airtel FURSA Tunakuwezesha”, "alisema Keita

Alitoa wito kwa vijana katika mkoa wa Morogoro kutumia nafasi hii ya “Airtel FURSA Tunakuwezesha” kwa kuweza kujiendeleza kibiashara na kuhakikisha kuwa wanapanuka kibiashara. Morogoro ina mambo mengi mazuri sana kwahiyo vijana watumie mji wao kuweza kujiendeleza na vile vile kupanua uchumi wa Morogoro. 

Huu sio muda wa kukaa bila kazi wakati kuna fursa inayokuwezesha kupata maarifa ya bure. Vijana wetu lazima wajishughulishe na vitu tofauti vitakavyowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazowafanya wafaidike na kuweza kujikomboa na umasikini, "alisema Keita

Alisisitiza kwamba mpango wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unawalenga wale vijana  ambao tayari wanabiashara na walio katika umri kati ya miaka 18-24,  na anayeishi Tanzania na kuendesha biashara zake hapa nchini. Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 au barua pepe kwa airtelfursa@tz.airtel.com au kutembelea mtandao wa  Airtel  na kurasa za kijamii kwa maelezo zaidi.

Keita alihitimisha kwa kusema Airtel imedhamiria kufanya kazi na Serikali ili kusaidia kuwajenga vijana na kuwaweka kuweza kuamini kwamba Airtel FURSA Tunakuwezesha' ipo kwa ajili yao na kuleta  mabadiliko na msisimko kwa vijana mkoani Morogoro na maeneo mengine ya hapa nchini.

TAMASHA LA UTALII NA AMANI KUFANYIKA NOVEMBA 22 ARUSHA


 mkurugenzi wa kampuni ya  Arusha Media  ambaye ni mmojawapo wa waandaaji wa tamasha hili Musa Juma katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo
 Akizungumzia tamasha hilo na kutaja michezo itakayokuwepo  , Mkurugenzi wa  Alfredo Shahanga  Sports Promotion ,Alfredo Shahanga katika kati
 baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole   katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani

 Na Woinde Shizza,Arusha
TAMASHA la Utalii na amani, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 22 katika jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari  Golden Rose hotel , Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alisema, tamasha hilo limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media na Alfredo Shahanga Sports  Promotion.

Alisema katika tamasha  hilo, kutakuwa na michezo michezo mbali mbali, ikiwepo soka, mashindano ya riadha ya Tourism Marathon, maonesho ya utalii na kongamano la utalii na amani.
"kauli mbiu ya tamasha hili ni Utalii wa ndani na amani sasa tunatoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza kushiriki"alisema

Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi Alfredo Shahanga alisema, maandalizi yote muhimu yamekamilika.

Hata hivyo, alitoa wito kwa wadhamini zaidi kujitokeza  kudhamini ili kuhakikisha wakazi wa Arusha wanashiriki kuhamasisha utalii wa ndani na kuhubiri amani.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya Arusha media ambaye pia ni mmoja wapo wa waandaaji wa tamasha hilo alitaja michezo ambayo itakuwepo ni pamoja na kukimbiza kuku,kuruka kamba,kukimbia na magunia ,riadha ambapo alisema kuwa kutakuwa na mbio za kilometa tano,half marathoni pamoja na full marathoni ambapo alieleza kuwa mbio za full marathoni zenyewe zitafanyika siku  december 13.

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAABIKA NA MAFURIKO KUTOKANA NA MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA.

Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua zinapoanza kunyesha.

Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika mdogomdogo.

Picha na Loyce Nhaluke
Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii .Whatsupp +255 (0) 757 43 26 94

Sunday, November 1, 2015

SIKU YA MARUHANI DUNIANI

Na Swahilivilla blog.  Washington D.C
Jana ililkuwa ni "Siku ya Maruhani" nchini Marekani. Siku hii ijulikanayo kama "Halloween" husherehekewa kila tarehe 31 Oktoba, na ina historia ndefu.
Siku ya Maruhani ilianzia huko barani Ulaya kiasi miaka 2,000 iliyopita ikifungamana na imani za kishirikina. Wazungu walipoyavamia mabara ya Amerika walihamia pia na utamaduni mila, desturi, dini, na silka zao - na sema upendavyo. Miongoni mwa hayo ilikuwa ndiyo hii siku ya Maruhani ambayo jina lake la asili ni "Samhein".
Sherehe za Maruhani  Photograph by treasuredragon/iStock.

Tuyaachie ya historia kwa wanahistoria, lakini kwa ufupi hii iliaminika kuwa ni siku ambayo pepo, majini, maruhani, mazimwi na mizimu au mizuka ya watu waliokufa hurejea hapa duniani katika maeneo yao ya asili na kujichanganya na watu waliohai.
Maudhui kuu ya siku hii ni kutisha, kuadhibu na mauti, ingawaje katika enzi zetu za leo imekuwa ni siku kuu ya watoto zaidi kuliko watu wazima. Sherehe zake hufanyika kuanzia familia, mitaa, makazini na hadi kufikia Ikulu yenyewe. Rejea kwenye toleo la jana la Swahilivilla uone Ikulu ya Marekani ilivyoadhimisha siku hii akiwepo rais Obama na familia yake.
 Wana maruhani wakiwa katika kwaride. (Photo Jefferson Siegel/New York daily news)

Kama ambavyo kila siku kuu au sherehe huwa zinaaambatana na ada maalum ambazo zikikosekana basi siku hiyo huwa kana kwamba haijatimia, Siku ya Maruhani nayo pia ina ada na desturi zake. Na kama zilivyo sherehe nyingi hapa Marekani siku hii pia nayo imekuwa fursa ya wafanyabiashara kujipatia rizki zao.
Mapambo: Shamra shamra za Siku ya Maruhani huanza mapema, pengine tangu mwezi wa Septemba kwa kuweka mapambo kwenye majumba, mabarabara na hata sehemu za kazi na biashara. 
Na kama tulivyotangulia kusema, mapambo yote huwa yanalenga kwenye hali ya kutisha, kuadhibu na mauti. Miongoni mwa mapambo hayo ni buibui na nyumba zao, popo wakining'inia, mifupa na mabufuru ya vichwa vikiashiria watu waliokufa, panga, paka weusi, masanamu ya mizuka au mazombi na vimbwanga vyengine. Almradi kuonesha kuwa nyumba zimesibiwa na maruhani (haunted house). Si hasha ukapita vichochoroni ukakutana na kitu ukashtuka. Kwa ufupi ni kama vile tunavyoona kwenye picha za kutisha (scary movies).

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI November 1, 2015.

Wanachama Wa Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu THDRC walaani vikali kitendo cha jeshi la polisi Kuvamia Kituo chao cha TACCEO.https://youtu.be/eDFOxahaEMc

Viongozi na Wachangaji Wa kanisa La AICT Geita wawataka viongozi walioshindwa uchaguzi kushirikiana na walioshinda ili kuleta Maendeleo. https://youtu.be/KNZQ-NAVT7Y

Shirika la Mazingira ENVIRO CARE lapongeza Ushindi wa Dkt. Magufuli kama ishara ya kuendeleza juhudi za kutunza na kulinda mazingira.  https://youtu.be/MiSp_JpurBw

Ligi kuu soka Tanzania Bara imeendelea Leo kwa michezo 3 huku Azam FC yazidi kuchomoza na ushindi baada ya Kuifunga Toto Afrika Bao 5 kwa 0.https://youtu.be/sSVw0PmdPN8

Bunge la Tanzania limewataka wabunge wote kuhakikisha wanapatiwa vyeti vya kuteuliwa kuwa wabunge vinavyotolewa na Msimamizi Wa Uchaguzi.https://youtu.be/ExH0V9jqWps

Wananchi wanaonufaika na Mpango wa TASAF katika Manispaa ya kigoma Ujiji waipongeza serikali kuanzisha mpango huo kwa ajili ya maendeleo ya taifa.https://youtu.be/1l7uDquTLRM

Jeshi la Polisi Zanzibar limewataka wakazi wananchi kuwa wavumilivu wakati taratibu za kutafuta ufumbuzi wa kisiasa ukiendelea. https://youtu.be/CqpJREF5TLM

Mvua Kubwa ilioandamana na upepo mkali iliyonyesha leo mchana mkoani Rukwa yasababisha kuharibika kwa miundombinu ya barabara.https://youtu.be/K7G8wDCrrV4
Timu ya Taifa, Taifa Stars imeingia kambini jijini Dar tayari kujiandaa na mchezo wa kiufuzu kombe la Dunia dhidi ya Algeria. https://youtu.be/zYUe1PgARvg

Kocha Wa Chelsea Jose Morihno adai kubaki kuendelea katika wadhifa wake kama kocha wa Chelsea na kufufua Kiwango cha klabu hiyo. https://youtu.be/HJw_6nfASFE

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yawatoa wananchi wake wasiwasi kuhusiana na uhalali wa raisi wa Zanzibar kuendelea kubaki madarakani;https://youtu.be/SKbpRIJDvzo

Pande zinazohasimiana Zanzibar zatakiwa kukaa meza moja kwa mazungumzo ya msitabali wa visiwa hivyo; https://youtu.be/ZFstFQ77joU

Imetwaja kuwa matofali yanayo tengenezwa kwa udongo    saruji yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutunza hifadhi ya msitu wa Ngorongoro; https://youtu.be/3SQTq_p7bKs

Wananchi mkoani shinyanga  waiomba serikali ya awamu ya tano kuboresha zaidi sekta ya michezo hususani timu ya taifa; https://youtu.be/MBd4E1AxwGA

Timu ya taifa ya New Zealand ya Rugby imefanikiwa kutetea ubingwa wake waduania kwa kuifunga timu ya taifa ya Rugby ya nchini Australia;https://youtu.be/GVdQnPmrfgM

AZAM FC YAIFUNGA TOTO AFRICAN 5-0

 Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kumtoka veki wa Toto African,  Hamis Seleman katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)

Beki wa Toto African, Salum Chuku (katikati) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Azam ilishinda 5-0. 
 Kipre Tchetche akimiliki mpira huku beki wa Toto African akijaribu kumzuia.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kupata bao.
 Kocha Mkuu wa Toto African, Martin Grelics (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na kikosi cha kwanza cha timu hiyo kilichoanza kucheza na Azam FC kwenye Uwanja wa Chamazi. Kocha huyo amevunja mkataba na kuwaaga wachezaji wa timu hiyo.
Wachezaji wa Toto African  wakiwa wamebeba ujumbe uliokuwa unasomeka 'Asante Sana Kocha Martin' 
 Kocha Mkuu wa Toto African, Martin Grelics akiagana na wachezaji wake baada ya mchezo na Azam FC kwenye Uwanja wa Chamazi. Kocha amevunja mkataba na timu hiyo.
 Wachezaji wa Toto African wakiomba dua katika mchezo wao dhidi ya Azam FC.

MBUNGE MTEULE KATIKA JIMBO LA MANONGA MKOANI TABORA , SEIF KHAMIS GULAMALI (CCM) AWASHUKURU WANANCHI KWA KUMCHAGUA

 
 Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwashukuru wananchi wa Kata ya Ndebezi katika jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na Dkt. John Magufuli aliyekuwa anawania kiti cha urais.
 
 Wananchi wa Kata ya Ntobo wakishangilia kwa furaha mara baada ya  Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alipowasili eneo hilo kwa kutoa shukrani kwa wananchi hao kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza na wakazi wa Kata ya ChomaMbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alisema ushindi wa kura 31,485 sawa na asilimia 67. 65 aliopewa na wana Manonga dhidi ya Ally Nguzo wa Chadema aliyepata kura 14,420 sawa na asilimia 30.96. Amesema atahakikisha anawapa wananchi hao ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi. 
Mke wa Mbunge Mteule Bi Sarah Abdallah akitoa shukrani kwa wananchi wa kata ya Choma kwa kazi nzuri waliyoifanya.
 Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwapungi amkono pamoj a na kuwashukuru wananchi wa kata ya Mwashiku kwa kuonesha upendo wa dhati baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo ilo
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa wakazi wa jimbo la Manonga