Thursday, October 2, 2014

UZINDUZI WA REDIO JAMII UVINZA: MKUU WA MKOA AHIMIZA WELEDI, UADILIFU NA AMANI

DSC_0177
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo (kulia) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia) kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Uvinza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM mkoani Kigoma. Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
 
Na Mwandishi wetu, Uvinza - Kigoma
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya amesisitiza uadilifu katika vyombo vya habari jamii kwa kutangaza habari zisizoumiza hisia kwa wananchi wengine na kuepuka migogoro.
Akizindua kituo cha redio jamii cha Uvinza FM, Luteni Kanali Mstaafu Machibya alisema kuwa vyombo vina wakati mgumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Changamoto hii inaweza kuepukika kwa kuhakikisha habari zinazotolewa zinalenga kuendeleza utamaduni wa amani, upendo, utulivu na uvumilivu na kuepuka viashiria vinavyoweza kusambaza chuki kwa lengo la kufanikisha chaguzi salama.

Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza umuhimu wa kuutumia uhuru wa kutoa na kupata habari vizuri kwa kusema kwamba uhuru huo usitumike kutoa habari zinazopendelea upande mmoja na kukandamiza mwingine kwa kuwa hali kama hiyo husababisha machafuko.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 18 (b) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi, lakini haki hiyo iende sambamba kwa kuzingatia Sheria za nchi na kuhakikisha habari hizo haziumizi hisia za wananchi wengine,”
DSC_0206
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM ambapo alilipongeza shirika la UNESCO kwa juhudi kuwaweka karibu wananchi na serikali kupitia mawasiliano ya redio.

Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameitaka redio jamii Uvinza kuonyesha uwezo wao ili waweze kujitangaza na kujijengea imani kwa wanajamii wao kuwa wanaweza. “Ni kwa hali hiyo tu mtaweza kujulikana, kutambulika na kupata udhamini na matangazo ya kutosha.”
Amewataka wanajamii kukitumia vyema kituo chao cha redio ili kiwe chachu ya kuleta na kukuza maendeleo katika vijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa ameitaka redio jamii ya Uvinza kutangaza habari zenye kuonyesha madhara ya mila potofu na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mila hizo hususan mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kufichua wagonjwa wanaohofia kuwa na dalili za ugonjwa wa ebola na uharibifu wa mazingira.

Amelipongeza shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kutoa msaada wa vifaa vya kituo hicho na kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanahabari jamii, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuruhusu matangazo ya Uvinza FM Redio yarushwe kupitia mnara wake na waanzilishi wa kituo hicho.
DSC_0120
Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii, Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM uliofanyika wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
“Ninayapongeza mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa na Airtel kwa ufadhili wao, Ruchugi Salt Works na Asasi za kiraia (EHENA) kwa ushirikiano wao kwa jambo hili”.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo amewakumbusha waandishi wa habari kuepuka kutangaza habari zinazoleta hofu katika jamii kwa kutangaza habari zinazotoa maelezo ya ufafanuzi kutoka chombo husika.

Amekemea matumizi ya lugha isiyo sahihi na kutoeleweka kwa wasikilizaji kwa kusema kwamba redio inalenga makundi yote ya umri kwa hiyo Matangazo yalenge wananchi wote.

“Redio Uvinza isiwe chombo cha propaganda, zingatieni mojawapo ya madhumuni ya kuanzishwa kwa redio zenu ambayo yanalenga kuhamasisha mshikamano, Amani, upendo, utulivu, umoja na utaifa, alisema Mwalimu Nyembo.”

Chombo cha habari jamii Uvinza FM Redio ni cha kwanza kuanzishwa mkoani Kigoma katika halmashauri mpya ya Uvinza.
DSC_0153
"Hongereni sana UNESCO serikali inatambua mchango wenu",...... Ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akimpongeza Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio jamii Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu kwa niaba ya UNESCO. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
Chombo hicho kimetakiwa kutumika kuwaunganisha wanajamii, kuepuka kutangaza hisia au uvumi kwa kueleza ukweli na kuwatunzia heshima wasikilizaji wao kwa kuwa wana haki ya kuheshimiwa na kutoumbuliwa masuala yao binafsi.
Uzinduzi huo umeshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mheshimiwa Mwalimu Hadijah Nyembo, viongozi wa chama na serikali, viongozi wa dini, Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Kampuni ya simu za mkononi AIRTEL, wanakijiji na wananchi wa halmashauri ya Uvinza.
Wengine ni wanahabari 30 wanaohudhuria mafunzo ya maadili, jinsia na habari za migogoro kijijini Uvinza, kutoka redio jamii za wilaya 8 ambazo ni Karagwe, Bunda, Mwanza, Kahama, Sengerema, Maswa, Simanjiro, Loliondo, Mpanda, Ngara. Kutoka Zanzibar ni Unguja North, na Southern Pemba (Pemba).
DSC_0082
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, akitoa salamu kwa wakazi wa wilaya ya Uvinza kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao wametoa udhamini wa mnara wao kurusha matangazo ya kituo cha redio jamii Uvinza FM ili kupanua wigo wa usikivu kwa redio hiyo.
DSC_0257
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa mkoa na wadhamini wa kituo hicho cha redio jamii Uvinza FM.
DSC_0054
Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akishiriki kutoa burudani na kikundi cha wakinamama wachimba chumvi Uvinza.
DSC_0164
Baadhi ya viongozi wa dini na jeshi la polisi waliohudhiria uzinduzi huo...Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hassan Hamisi, OCD wa Wilaya ya Uvinza S.P Nobert Mahala, Mchungaji wa SDA, Pius Mutani, Mchungaji wa EAG Uvinza, Daniel Magunge na Diwani wa kata ya Ngumka, Abdallah Masanga.
DSC_0333
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali za jamii waliokuwa wakihudhuria warsha ya siku nane iliyokuwa ikiendelea kwenye kituo cha redio jamii Uvinza FM na wakazi wa wilaya hiyo waliohdhuria sherehe za uzinduzi wa kituo hicho.
DSC_0231
DSC_0226
DSC_0264
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM chini ya ufadhili wa Shirika la UNESCO na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mwalikishi wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambaye pia ni mshauri na mkufunzi wa redio jamii Bi Rose Haji Mwalimu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.
DSC_0267
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0285
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akifanyiwa mahojiano mafupi ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM na Mtangazaji wa kituo hicho, Kadisilaus Simon mara baada ya kuzindua rasmi redio hiyo.
DSC_0304
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisaini kitabi cha wageni ndani ya studio za redio jamii Uvinza FM.
DSC_0308
Mtangazaji wa kituo cha redio jamii Uvinza FM, Kadisilaus Simon akitekeleza majukumu yake kwa furaha kabisa mara baada ya kupewa baraka na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya.

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akiwa na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakati wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya serena jijini Dar es Salaam kuzungumzia Wiki ya Wateja wa Benki hiyo itakayoanza Oktoba 6-11. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akiingia katika mkutano huo akiongozana na maofisa wa Benki hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (katikati) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei muda mfupi kabla ya kuanza mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa jkatika mkutano huo.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia) akiwa na maofisa wa Benki hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza na waandishi wa habari kjuhusu Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB.



Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB itakayoanza Oktoba 6-11.
 
Na Mwandishi Wetu


WATANZANIA wametakiwa kutumia huduma za kibenki katika kukuza na kujiongezea uchumi wa maisha yao.



Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu wiki ya wateja wa benki hiyo itakayoanza Oktob 6,hadi 11,mwaka huu.



Alisema wiki hiyo ni maalum kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wateja ikiwemo kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa.



"Azma kubwa ya maazimisho hayo ni kuwasikiliza wateja na kutimiza mahitaji yao kwa wakati ...lengo la CRDB ni kuboresha na kuinua uchumi wa kila mtanzania kupitia mikopo, kutunza na kukuza amana pamoja na kutoa ajira kwa vijana na misaada kwa jamii"alisema Dk. Kimei.

Akifafanua zaidi alisema kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa watanzania kwa CRDB, wanatumia wiki hiyo kutoa huduma bora na kusikiliza kero zao.

Wednesday, October 1, 2014

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA SHAMBANI KIJIJI CHA KWEMNYEFU

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima na kupanda mahindi katika shamba kijijini Kwemnyefu Kata ya Mpapayu wilayani Mheza mkoani Tanga pamoja na wananchi wakati alipotembelea shamba hilo na kukagua shughuli za kilimo cha mkono, Katika shughuli hiyo katibu mkuu huyo ameshirikiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katibu Mkuu huyo kesho anaelekea wilayani Pangani baada ya kumaliza ziara yake wilayani Muheza leo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MUHEZA-TANGA)3Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi naye akishiriki pamoja na vijana kulima shambani katika kijiji cha Kwemnyefu wilayani Muheza leo.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi shambani pamoja na vijana wa kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu5Vijana nao wakiendelea na kazi ya kilimo shambani6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana wakirejea huku majembe yao yakiwa begani baada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi shambani7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana wakirejea wakirejea huku majembe yao yakiwa beganibaada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi shambani8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kilulu wilayani Muheza.9Jengo la Kituo cha habari za kilimo lililojengwa na serikali katika kata ya Songa wilayani Muheza ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amelitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili. 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa I. M. Matovu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati alipotembelea kituo cha Afya Muheza na kukagua ujenzi wa miundo mbinu kadhaa kabla kituo hicho hakijapandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Mbaramo Ubwari wilaya ya Muheza.14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee mjini Muheza.16Peter John Jambele Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na wananchi wa Muheza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Jitegemee mjini Muheza Tanga.17 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongeza na wananchi wa Muheza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Jitegemee mkoani Tanga.

Mkutano sekta ya mawasiliano 'Connect to Connect Summit' waendelea Dar

Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge (kulia) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge (kulia) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa katika mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa tatu kulia) viongozi hao pamoja na maofisa kutoka sekta hiyo walikutana kimazungumzo ya kuangalia namna ya kushirikiana katika utendaji kazi. Mkutano huo umeandaliwa na TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa tatu kulia) viongozi hao pamoja na maofisa kutoka sekta hiyo walikutana kimazungumzo ya kuangalia namna ya kushirikiana katika utendaji kazi. Mkutano huo umeandaliwa na TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa pili kulia). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (wa pili kulia). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (katikati). Wa kwanza kulia Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (katikati). Wa kwanza kulia Mkuu wa Kitengo cha Ufundi cha TTCL, Senzige Kisenge.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (mwanamama pichani) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao juu ya ushirikiano kikazi. Wengine ni maofisa waandamizi kutoka pande zote wa sekta ya mawasiliano. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura na Waziri wa Mawasiliano na Huduma za Posta wa Sudan Kusini, Rebecca Okaci (mwanamama pichani) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao juu ya ushirikiano kikazi. Wengine ni maofisa waandamizi kutoka pande zote wa sekta ya mawasiliano.Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.

YES Tanzania yaanzisha darasa kwa walioathirika na dawa za kulevya

Katibu wa Shirika la YES Tanzania Lusajo Mwamakura akizungumza na waathirika wa dawa za kulevya mara baada ya kuanza kutolewa elimu kwa vijana hao ambao wengi wao wanatoka katikati ya mji wa Moshi.
Mwenyekiti wa Shirika la YES Tanzania,Laurance Mwonyony akizungumza na waathirika wa dawa za kulevya hawapo pichani.(kulia) kwake ni mweka hazina wa shirika hilo John Mmbando.
Baadhi ya vijana walioathirika na dawa za kulevya wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na walimu,(hawapo pichani)
Baadhi ya vijana walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya wakijitambulisha wakati wa darasa hilo.
Vijana wengi wameudhuria katika darasa hilo lengo likiwa ni kuachana kabisa na matumizi ya dawa za kulevya.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kasikazini.