Monday, September 1, 2014

TAHA YAADHIMISHA SIKU YA WAKULIMA SHAMBANI KILIMANJARO

picha 1
Afisa ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

Wakulima wakimsikiliza Mtaalamu wa masuala ya mbolea na viuatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi. Baby Nkossa wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viuatilifu kwenye mazao
Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa  wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
picha3
Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Giliard Daniel katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

picha 6
Shamba mfano lililotumika kuwafundishia wakulima siku hiyo
picha 4
Shamba mfano namba 1
picha 5
Shamba mfano namba 2
1
Mzee Shabani Shoo akizungumza na wakulima (hawapo pichani)kuhusu mbinu alizofundishwa na wataalamu 
wa TAHA na kuweza ukuaji bora wa zao lake la kabeji ikiwa ni pamoja na ongezeko la idadi ya mazaokutoka kabeji 4000-18000
picha7
Wakulima wa Kijiji cha Silversand-Machame wakifuatilia mafunzo ya namna bora ya uandaaji wa udongo kwa ajili ya kuotesha miche ya mbogamboga
picha8
Wakulima waliohudhuria mafunzo ya kilimo cha mboga katika siku ya wakulima shambani wakifuatilia hotuba kutoka kwa mgeni rasmi
picha9
Wakulima wakifatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga mboga kutoka TAHA Bw.Collins Okiyawakati wa mafunzo hayo

Asasi ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na mbegu zake imehadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
 
Maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya ‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo biashara.

PONGEZI KWA JWTZ KWA KUTIMIZA MIAKA 50 TOKEA KUANZISHWA KWAKE

 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa kwenye maonyesho Katika Uwanja wa Taifa.Picha na Maktaba.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa mazoezini.
Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog. 

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1/09/1964. JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa Ni Jeshi lenye weredi wa hali juu Duniani kutokana na Operesheni ambazo wamewahi kuzifanya na linalotumia Silaha za Kisasa. Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23 nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa Mataifa (UN).

Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23 nchini Congo.

Jukumu kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea Nchini.

Kwa kifupi Sahivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa 

TAASISI ISIYO YA KISERIKALI YA NKWAMIRA YAANDA HAFLA YA KUCHANGIA VITABU 2500 KWA SHULE ZA SEKONDARI NA ZA MSINGI JUMLA YA MILIONI 218 ZINAHITAJIKA

 Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda , akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena wapili kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla, Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana na Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia)
 Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana wapili kutoka (kulia) akisistiza jambo kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena. Wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla, ni Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda , Afisa Uhusiano wa NSSF Anna Nguo, Meneja wa  Kampuni ya Dun &Bradstreet Credit Bureua ( T) LTD Adebowele Atobatele (Kushoto) kulia ni Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar .
 Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia) akiongea kwa waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena. Wapili kushlia ni Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana. Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla, ni Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda , Afisa Uhusiano wa NSSF Anna Nguo, Meneja wa  Kampuni ya Dun &Bradstreet Credit Bureua ( T) LTD Adebowele Atobatele (Kushoto)
 Meneja wa  Kampuni ya Dun &Bradstreet Credit Bureua ( T) LTD Adebowele Atobatele akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani juu umuhimu wa kusaidia kupatikana elimu bora nchini  ambapo taasisi isiyo ya kiserikali ya Nkwamira  Oktoba 3 mwaka huu wataakuwa na hafla ya kutafuta uwezo wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena  wapili kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa NSSF Anna Nguo, Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda, Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla , Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana na Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia) 

 Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana akisistiza jambo kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena. Wapili kutoka kulia ni Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla, ni Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda , Afisa Uhusiano wa NSSF Anna Nguo, Meneja wa  Kampuni ya Dun &Bradstreet Credit Bureua ( T) LTD Adebowele Atobatele (Kushoto)
 Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena  katikati ni Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana na Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia)  kwa wale ambao hawatafika katika hafla hiyo wanaombwa kuchangia  mradi huo kupitia namba 777777 yenye jina la Nkwamira.
 
 Mkurugenzi  Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena. Kushoto ni Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda ,Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana na Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia). 
UCHANGIAJI WA VITABU: Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nkwamira ,Noreen Mazalla akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya hafla ya kutafuta uwezo  wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari  za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.Hafla hiyo itafanyika usiku wa Oktoba 3 mwaka huu kwenye hoteli ya serena. Kushoto ni Afisa  Mkuu Ugawaji Rasmaiali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mozes Nyirenda ,Mkurugenzi  Mauzo na Masoko wa Hoteli ya Serena  Seraphin Midana na Mkurugenzi wa Seaforth General Angencis Ltd Anver Rajpar (kulia).(Picha na Albart Jackoni) 

TAMASHA LA FIESTA 2014 LILIVYOSAMBAZA UPENDO KWA WAKAZI WA MJI WA MOSHI MWISHONI MWA WIKI

 Msanii Mkongwe wa muziki wa Hip hop nchin Farid Kubanda a.k.a FQ pichani shoto wakilishambulia jukwaa na msanii mwenzake Stamina jukwaani huku wakiwa na shabiki wao,juu ya jukwaa la tamasha la Fiesta 2014 lilofanyika katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
 Msanii wa Bongofleva pichani kulia wakimuimbisha shabiki wao jukwaani,kushoto ni Fid Q
 Mkali mwingine wa hip hop Roma pichani shoto wakilishambulia jukwaa la Fiesta 2014 mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Moshi na vitongoji vyake,lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya uwanja wa majengo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro
 Ana majina kibao ya kisanii lakini hapa mwite Dully Sykes akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi
 Mmoja wa mashabiki wa tamasha la Fiesta pichani akitazama kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
 Mashabikii wakishangilia jambo wakati wasanii mbalimbali wa tamasha la Fiesta 2014 wakiendelea kutumbuiza jukwaani.
 Mwanadada Feza Kessy akiimba jukwaani wakati wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyka mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi.
 MKali wa kusugua ngoma,kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwa kwenye mashine yake ya kazi
 Mashabiki wakisambaza upendo wa kutosha kabisa kwa wasanii wao waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
 Sehemu ya umati wa mashabiki wa tamasha la fiesta wakiwa wamemezwa vilivyo na jicho la samaki
 Wakazi wa jiji la Moshi walisambaza upendo wa kutosha ndani ya tamasha hilo ambalo hukusanyisha watu kutoka vitongoji mbalimbali ndani na nje ya mji wa Moshi.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiimba kwa hisia jukwaani.
 Rachael na madansa wake wakilishambulia jukwaa la fiesta mwishoni mwa wiki jijini Moshi.
 Mkali mwingine wa muziki wa Bongofleva,Ali Kiba akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa hip hop nchini,Fid Q akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani) ,mwishoni mwa wiki kwenye tamasha la fiesta lililofanyika katika viwanja vya Majengo.
 Msanii Shaa akilishambulia jukwaa.
 Msaniii Shaa na Madansa wake kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta 2014
 Mashabikii wakishangilia jambo wakati wasanii mbalimbali wa tamasha la Fiesta 2014 wakiendelea kutumbuiza jukwaani.

MRADI WA MAJARIBIO WA KUFUNDISHA MASOMO YA SAYANSI WA UNESCO WANEEMESHA TANZANIA

DSC_0018
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini Dar.

Na Mwandishi wetu
MRADI wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya kuendeleza mradi huo.

Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.

Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza mazuri ya mradi.

Mradi huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.

Aidha ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa, tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuendelezwa kwake.
DSC_0015
Mradi huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja na vitabu vya kufundishia.

Aidha mradi huo ulizingatia pia kuongeza upendo wa masomo ya sayansi kwa jamii na kuwafanya wanafunzi wapende na wawe na hamu na masomo ya sayansi.

Mradi huo ambao umefanyika kwa kuzingatia pia mahitaji ya taifa na kimataifa chini ya dhana ya kuendeleza masomo ya sayansi duniani unaendeshwa na UNESCO kwa kujenga uwezo wa shule za sekondari na msingi kufanya mazoezi ya utambuzi wa nadharia mbalimbali kimaabara hutoa masanduku maalumu ambayo yanakuwa ni kama maabara ndogo zinazotembea.

Maabara hizi hutoa uwezo wa kufanyika kwa majaribio ya msingi na yale makubwa kwa kuzingatia madaraja mbalimbali ya mafunzo kuanzia ngazi za chini kati na juu.

Katika ufungaji wa mradi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti washiriki walielezwa maendeleo ya mradi hadi mwisho wake na changamoto zilizokuwa zinakabiliwa.

Unesco imesema kutanuka kwa kasi kwa elimu ya msingi kumesababisha changamoto za ubora wa elimu katika mfumo wa elimu nchini na mradi wa majaribio ulionesha kwamba ubora unaweza kurejeshwa kwa kuwa na mpango kama MSKs.
DSC_0021  
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa juma.

Kutokana na changamoto za raslimali kushindwa kuhakikisha kwamba kila darasa, mwalimu na mwanafunzi wanakuwa na zana zinazotakiwa kufundisha na kujifunza,walimu na wanafunzi walielemewa na hivyo kuathiri ufundishaji wa masomo ya sayansi ya baiolojia, kemia na fizikia.

Mathalani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011 wastani wa matokeo ya masomo ya sayansi kitaifa uliporomnoka chini ya asilimia 50.

Fizikia ilikuwa aislimia 43.2, kemia 43.3 na baiolojia 43.4 na katika takwimu hizo zilionesha kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi.

Utafiti ulionesha wazi kwamba udhaifu huo umetokana na kukosekana kwa maabara, vifaa vya kufundishia na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.

Pamoja na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa masanduku haya ya maabara, tathmini iliyiofanywa ilionesha kwamba mradi ungeliweza kuunganishwa na miradi kama ya JICA na pia kutengenezewa mfumoi wa wa kuweza kuwa endelevu kutokana na umuhimu wake na ufanisi.

Changamoto kama za masanduku machache kuliko yalivyokusudiwa katika mradi , muda mfupi wa kufunza walimu na pia kutekeleza yote yaliyopangwa na suala la ukaguzi bado mradi huu kutokana na asili yake ungelikuwa na maana zaidi kuendelezwa ili kufikia zaidi shule zilizo pembezoni.
DSC_0009
Aidha ili kuendelea na mradi huo tathmini iliyofanywa na kuelezwa na Ellen Binagi katika kikao cha wadau ilishauriwa serikali kufikiria kuanzisha vituo na taasisi za kutengeneza maabara hizo ndogo nchini badala ya kuagiza kutoka nje kutokana na gharama zake na hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi kubwa na yenye shule nyingi.

Binagi alisema kwamba kuanzishwa kwa mtindo huo kumeleta muonekano mpya katika upenzi wa masomo ya sayansi na katika shule za majaribio ufanisi wake ulikuwa mkubwa na ipo haja ya kuangalia namna ya kuendeleza.

Mtathmini huyo pia amesema ipo haja kwa UNESCO na serikali ya Tanzania pamoja na mradi kumalizika kuona namna ya kuuendeleza na kuondoa changamoto zilizoonekana wakati wa utekelezaji wake.
DSC_0012

UTAFITI WAIBUA MAKUBWA NGONO ZA UTOTONI DAR

DSC_0140
Mratibu wa mradi wa PREPARE ambaye pia ni Mwanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili, Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono mwishoni mwa wiki kwenye kituo cha maelezo ya afya Muhimbili katika idara ya magonjwa ya akili. Kulia ni Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo.

Na Mwandishi wetu
SAMPULI tathmini ya matokeo ya mradi wa PREPARE uliokuwa na lengo la kuangalia uwezekano wa vijana kupunguza ngono, imebainisha haja ya elimu ya afya ya uzazi kukabili hali ya sasa ya tabia hatarishi zinazowakabili vijana wadogo.

Matokeo ya awali ya mradi yalionesha kuwa asilimia 10 ya vijana wenye umri wa miaka 12 mpaka 14 ambao ni darasa la tano na sita waliofanyiwa utafiti walikuwa wameshawahi kufanya ngono na asilimia kubwa ikiwa ni kwa kutumia njia ya haja kubwa.

Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa watafiti wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili,Kitengo cha magonjwa na afya ya akili, Lusajo Kajula.

“Vijana wengi walionekana wakifanya ngono ya uke na ya mdomo ikifuatiwa na ngono ya njia ya haja kubwa Kwa wale ambao wameshawahi kufanya ngono, asilimia 6.3 wamefanya ngono ya njia ya haja kubwa wakati asilimia 93.7 hawajawahi.”

Aidha alisema utumiaji wa kondomu ulionekana kuwa mdogo kwa vijana wadogo ambao wameanza kufanya ngono.

“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajawai kutumia kondomu kabisa wakati asilimia 32 wamewahi kutumia kondomu.”

Alisema utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa miaka minne ulioshirikisha Vyuo Vikuu vya Makerere cha Uganda, Cape Town na Limpopo vya Afrika Kusini, Bergen na Oslo vya Norway, Maastricht cha Uholanzi na Sussex cha nchini Uingereza.
DSC_0154
Mtathmini kiongozi wa mradi huo, Mrema Kilonzo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema utafiti umeonesha haja ya kutolewa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wadogo ambao bado hawajaanza ngono ili kuchelewesha kuanza ngono kwa mfumo wa kisaikolojia ili waweze kujitambua na kuacha kufuata nadharia za kisayansi pekee ambazo ndizo zinazotumika katika shule mbalimbali kuwaeleza mabadiliko ya miili yao.

Katika utekelezaji wa utafiti huo idadi ya wanafunzi 5,099 walichaguliwa mwanzoni mwa mradi kufanyiwa utafiti huo ambapo wanafunzi 4783 (asilimia 93.9) walifuatiliwa kwa miezi 6 na wengine 4370 (asilimia 85.8) walifuatiliwa kwa miezi 12.

Utafiti ulionesha elimu inayojishughulisha na masuala ya ujinsia na afya ya uzazi kwa vijana wadogo itumie mtazamo mpana utakaoleta mabadiliko ya msingi kwenye misingi ya virekebisho vya mabadiliko ya tabia.

Mradi huo wa PREPARE ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka manispaa ya Kinondoni zilizochaguliwa kwa kutumia taratibu sampuli mtawanyiko zilizopangwa katika makundi mawili ya shule za mwingilio yaani ilikotolewa elimu hiyo zilizokuwa 19 na za kulinganisha zilizokuwa 19.

Ili kuweza kupata matokeo yaliyokusudiwa mradi ulitoa mafunzo kwa walimu watano wakufunzi wa wakufunzi; ulitoa mafunzo kwa walimu watekelezaji 76, na waelimishaji rika wanafunzi 132 na kuelekeza watoa huduma 8 wa afya katika kliniki za huduma rafiki kwa vijana ili kutekeleza muingiliano.

Tathmini iliyotoa majibu ya jinsi utendaji unavyoendelea na ya matokeo ilihusisha shule zote na wanafunzi zaidi ya 6,000 waliowekwa kwenye muingiliano, huku uchambuzi wa tathmini ukihusisha wanafunzi wenye umri wa miaka 12-14, wenye kujua kusoma na kuandika.

Matokeo yaliyotathminiwa ni Mabadiliko katika masuala ya ngono (kuanza ngono) na Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa wale waliokwisha anza ngono.

Kwa wastani mradi uliona kwamba mwingilio wa PREPARE ulipunguza uwezekano wa vijana wadogo (wavulana na wasichana) kuanza ngono na kuongeza uwezekanao wa kutumia kondomu kwa wale walioanza.
DSC_0148
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo. Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro akiuliza swali kwenye mkutano huo.

Hata hivyo, katika utekelezaji wa mradi mabadiliko katika uchukuaji wa hatua yalionekana zaidi miongoni mwa wasichana waliopata mwingilio ukilinganisha na wale ambao hawakupata mwingilio.
Uchukuaji wa hatua ulisababisha tabia ya kutumia kondomu miongoni mwa wanafunzi wa kiume lakini siyo miongoni mwa wanafunzi wa kike.

“Kimsingi tunataka kuwaambia wanahabari kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya mradi wa PREPARE ni kuchelewesha kuanza ngono miongoni mwa wanafunzi wa kiume na wa kike wenye umri wa miaka 12-14 katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania;

“Kuongeza uchukuaji wa hatua ulio chanya katika kutumia kondomu kwa jinsia zote na taarifa za ongezeko la utumiaji wa kondomu miongoni mwa vijana wa kiume. “

Mradi huu uliofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya, Programu ya utafiti wa afya umelenga kuangalia mwingilio ulio katika misingi ya utamaduni na jinsia, endelevu, kijamii ili kukuza ujinsia na afya ya uzazi miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 12-14 kwa kutumia shule kama njia ya kufundishia.